UZINDUZI WA KITABU CHA WEKEZA AFRIKA 2014, WASHINGTON, DC

May 20, 2014


Scott Eisner (kulia)vice President of African Affairs, US Chambers of Commerce akifungua sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza Afrika 2014 iliyofanyika US Chambers of Commerce Washington, DC siku ya Jumatatu May 19, 2014 wengine katika meza ni Balozi wa kudumu wa African Union Mhe. Amina Salum Ali na Paul Duffen ambaye ni News Desk Media. 
Sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza afrika 2014 ".invest in africa 2014" kitabu kinachotolewa na ubalozi wa umoja wa afrika ilifanyika Jumatatu May 19, 2014 kama kuanzia wiki ya kusherehekea siku ya afrika tarehe 27 mwezi mei .
Katika sherehe hizi zilizoandaliwa kwa pamoja baina ya ubalozi wa afrika washington na jumuia ya wafanya biashara wa marekani US chamber of commerce
Kulikuwa na majadiliano yaliyofanywa na viongozi wanao wakilisha Mabalozi wa kanda 5 za afrika zikiwemo East.West .South Central na North.viongozi hao walizungumzia rasilmali zilizopo Afrika na kuwaalika wawekezaji wawekeze afrika kwani kuna faida kubwa zinapatikana. Kwa upande wa serikali ya marekani ilihudhuriwa na mwakilishi wa msaidizi katibu wa ofisi ya mambo ya nje ya marekani na mgeni mwengine wa heshima ni muwakilishi wa umoja wa matIfa united nation global compact.kitabu kilichotoka mwaka huu pia kimeelezea mafanikio yaliyopatikana afrika na muelekeo katika miaka ijayo.


 Sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza Afrika 2014 ikiendelea.
 Meza upande wa wawekezaji
 Meza waliokaa wawekezaji na wawakilishi wa Mabalozi na baadhi wa wahemimiwa Mbalozi/

TAZAMA PICHA JINSI MAREHEMU ADAM KUAMBIANA ALIVYOAGWA VIWANJA VYA LEADERS CLUB LEO

May 20, 2014





BREAKIN NEWZZZ:- CHATU MKUBWA WA AJABU ANASWA MBEYA ONA HAPA LIVE!!

May 20, 2014

SIKU chache baada ya wakazi wa Jiji la Mbeya kupewa tahadhari  juu ya uwepo wa nyoka mkubwa aina ya Chatu katika maeneo ya Rift Valley pembezoni mwa mto Meta uliopo jijini hapa juhudi za kumsaka zaanza kuzaa matunda.

 Juhudi za kumsaka Chatu huyo zilianza juzi kwa ushirikiano wa Wataalamu wa Wanyamapori pamoja na waganga wa jadi ambao walikuwa wakimsaka pembezoni mwa mtu huo.
 Hata hivyo jitihada za klumsaka Nyoka huyo zilianza kuzaa matunda baada ya jana asubuhi Waganga hao kufanikiwa kumnasa Chatu mdogo pembezoni mwa Mto Meta karibu na Hoteli ya Rift Valley.

MBEYA CITY FC YAENDELEA KUJIWINDA NA CECAFA NILE BASIN CUP JIJINI DAR

May 20, 2014
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEigcsIp6D6P7odVk_aoxH5JzvwopDBcZQJGNHLDXKccCGO0V8D3xK7tXPCPc2kXzBtOTriPhQNslDP7QyYaPcuYqZZnuSZZchQIbEDUZQDnoha170k_Z0GqaF_wBCxhWOuDL3F7Tcah4JE/s1600/IMG_1150.JPG
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City fc bado ipo jijini Dar es salaam kujiandaa na safari ya kwenda Sudan kushiriki michuano mipya ya CECAFA Nile Basin inayotarajia kuanza mei 22 mpaka juni 4 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Maka Mwalwisyi ameuambia mtandao huu kuwa asubuhi hii wanaendelea na mazoezi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.
“Ninavyozungumza na wewe muda huu tupo hapa Karume. Tunaendelea vizuri na mazoezi yetu. Na mambo yakikaa sawa muda wowote tutaanza safari ya kwenda Sudan”. Alisema Mwalwisyi.
Kocha huyo aliongeza kuwa wachezaji wote wapo katika morali kubwa na wanahamu kubwa ya kwenda kushiriki michuano hii mikubwa.
“Wachezaji wetu siku zote wanapenda kucheza. Hii ni nafsi nyingine nzuri ya kupata uzoefu wa michuano ya kimataifa. Najua itakuwa changamoto kwetu, lakini tutapambana kwa kila mechi”.
“Sisi bado ni wachanga katika soka. Michuano kama hii ni msingi mzuri kwetu”
“ Tutaitumia vyema nafasi hii kuhakikisha tunafanya vizuri, tumekuwa tukitumia muda mwingi kuwapa mbinu  za kimpira wachezaji wetu”. Aliongeza Mwalwisyi.
Mwalwisyi aliwaomba mashabiki wao na watanzania wote kuwaombea mafanikio katika mashindano hayo kwasababu kufanya vizuri itakuwa sifa kwa taifa zima.
Mbeya City fc waliopo kundi B wataanza kampeni zao mei 23 kwa kukabiliana na El Merreikh Al Fasher .

USAJILI WA WACHEZAJI KUANZA JUNI 15

May 20, 2014
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2014/2015) unaanza Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.

Kipindi cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai 30 mwaka huu. Kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Agosti 4 na 11 mwaka huu. Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni Agosti 12 hadi 14 mwaka huu.


Usajili hatua ya pili utakuwa kati ya Agosti 14 na 29 mwaka huu. Kupitia na kutangaza majina ya pingamizi hatua ya pili ya usajili ni kuanzia Agosti 30 hadi Septemba 4 mwaka huu. Uthibitisho wa usajili hatua ya pili ni Septemba 5 na 6 mwaka huu.

Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka huu, na ratiba inatarajiwa kutoka mwezi mmoja kabla (Julai 24 mwaka huu).

MECHI YA TAIFA STARS YAINGIZA MIL 63/-

May 20, 2014
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe iliyochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 63,345,000.

Mapato hayo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Taifa Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 yametokana na washabiki 11,079 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000.

Mgawo wa mapato hayo ni asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 9,662,796.61, gharama za kuchapa tiketi sh. 6,000,000, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 7,152,330.51, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 9,536,440.68 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa pamoja wamepata sh. 30,993,432.20.

Katika hatua nyengine,Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaandaa utaratibu utakaowawezesha washabiki kwenda jijini Harare, Zimbabwe kushuhudia mechi ya Taifa Stars.

Mechi hiyo ya marudiano ya Kombe la Afrika kwa ajili ya fainali zitakazochezwa Morocco mwakani itafanyika Jumapili (Juni 1 mwaka huu) jijini Harare.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilishinda mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0.

Usafiri huo utakuwa wa basi ambapo washabiki wanatarajiwa kuondoka siku ya Ijumaa na kuwasili Jumapili mchana jijini Harare ambapo watashuhudia mechi na kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo.

Washabiki wanatakiwa kuwa na hati za kusafiria (pasipoti), nauli ya kwenda na kurudi itakuwa sh. 300,000.

TIMU YA U15 YAWASILI GABORONE

May 20, 2014


Timu ya Tanzania ya umri chini ya miaka 15 imewasili salama jijini Gaborone, Botswana kwa ajili ya michezo ya Afrika ambapo itacheza mechi yake ya kwanza Mei 22 mwaka huu dhidi ya Mali.

Kikosi hicho cha wachezaji 16 chini ya Kocha Abel Mtweve kimetua jijini Gaborone jana (Mei 19 mwaka huu) jioni kwa ndege ya South African Airways. Michezo hiyo itamalizika Mei 30 mwaka huu.

Wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.

Nchi nyingine zinazoshiriki michezo hiyo kwa upande wa mpira wa miguu ni Afrika Kusini, Botswana, Nigeria, Mali na Swaziland.

Gabon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ambazo nazo zilikuwa zishiriki kwenye michezo hiyo katika dakika za mwisho.

NGORONGORO HEROES YAENDA NIGERIA

May 20, 2014
Kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) chenye watu 25 kinaondoka kesho alfajiri kwenda Nigeria kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).

Mechi hiyo itachezwa Jumamosi (Mei 24 mwaka huu) katika Jiji la Kaduna kwenye Jimbo la Kaduna ambalo lipo katikati ya Nigeria. Msafara wa timu hiyo unaoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi unaondoka kwa ndege ya Ethiopian Airlines.

Ngorongoro Heroes inayonolewa na Kocha John Simkoko ilipoteza mechi ya kwanza iliyofanyika nyumbani jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0.

Mwamuzi Alhadi Allaou Mahamat wa Tchad ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Atasaidiwa na Issa Yaya, Alfred Madjihoudel na Idriss Biani wote kutoka Tchad. Kamishna ni Aboubakar Alim Konate wa Cameroon.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MILIONI 10 KWA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA KIBOSHO

May 20, 2014

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisaini kitabu cha wageni alipofika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibosho, wakati wa mahafali ya Kidato cha Sita. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Mhandisi Aloyce Peter Mushi. 
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibosho, Sista Anna akimpeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa mahafali ya Kidato cha sita yaliyofanyika Shuleni hapo. Benki ya CRDB ilitoa msaada wa shs. milioni 5 na katika harambee iliyofanyika shuleni hapo jumla ya sh.milioni 10 zilipatikana. 
 Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Sita wakiimba ngojera wakati wa sherehe za mahafali ya kidato cha sita.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiwasili Shuleni hapo.

MAKANGE AWASHAURI WANAVYUO KUACHANA NA MIGOMO

May 20, 2014
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM),Abdi Makange amewataka wanafunzi katika vyuo mbalimbali hapa nchini kuacha kufikiria masuala ya migomo na maandamano badala yake waone namna ya watakavyo jiajiri wakati watakapokuwa wamemaliza kwenye vyuo hivyo.

Makange alitoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya Chuo cha  kujiendeleza kielimu cha  Noverty kilichopo  mjini Tanga ambapo alisema masuala hayo hayana faida yoyote kwao zaidi ya kuwaharibia malengo yao waliyojiwekea kwenye maisha yao ya baadae.

Alisema ni vema wakamua njia za busara kuiepuka migomo na maandamano yasiyo na tija kwenye vyuo vyao lengo likiwa kukaa chini na kuzungumza ili kuweza kupata muafaka badala ya kujichukulia hatua za aina hiyo kwani sio suluhu ya kile wanachokuwa wakikitaka zaidia ya kuwapa  hasara jamii zao wanazotoka.

Alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa chuo hicho kwa kutoa elimu kwenye jamii ndio maana wamekuwa wakiwaalika kwenye matamasha na vikao mbalimbali ikiwemo baadhi ya misaada wanayoipeleka.

Aidha alisema chuo hicho kimekuwa mkombozi mkubwa wa vijana kwa kuwawezesha kupata ajira kwenye sekta mbalimbali mkoani hapa kitendo ambacho kinachangia kukuza maendeleo yao na jamii zinazowazunguka.

Akilizungumzia suala la Katiba,Makange alisema nchi imeingia kwenye mchakato wa katiba mpya ambapo itakayoandikwa leo itaishi miaka 59 ijayo na walengwa ni vijana hivyo wahakikisha wanakataa mambo ambayo yanaweza kuwagawa watanzania na mshikamano wao.

Mwenyekiti huyo aliwataka pia wahitimu hao kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri kwenye jamii wanazoishi pamoja ikiwemo kuwaasa wanafunzi wa kike kujiadhari na mafataki ambao wanaweza kuwaharibia maisha yao hali itakayowafanya kushindwa kufikia malengo yao.

  “Hakikisheni mnakuwa mabalozi wazuri kwenye jamii zenu lakini kwa upande wa wasichana napenda kuwaasa mjihadhari na mafataki wanaoweza kuwaharibia malengo yenu ikiwemo wanafunz mnaobaki tilieni mkazo elimu kwani ndio njia pekee itayowaletea maisha bora “Alisema Makange.

KAMISHNA WA NCCR MAGEUZI MKOA WA TANGA NA MSHAURI MWELEKEZI WA MASUALA YA UCHUMI WAFUNGUKA KUHUSU SERA YA ASILIMIA 10 YA MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI

May 20, 2014
KAMISHNA WA CHAMA CHA NCCR MAGEUZI MKOA WA TANGA,RAMADHANI MANYEKO AKISISITIZA JAMBO WAKATI AKIUZNGUMZA KATIKA KIPINDI CHA AMKA NA MWAMBAO KINACHORUSHWA KILA SIKU NA RADIO MWAMBAO YA TANGA KUHUSU ASILIMIA 10 YA MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI KUTUMIKA KUWASAIDIA VIJANA NA WANAWAKE

HAPA RAMADHANA MANYEKO AKISISITIZA JAMBO KWENYE KIPINDI HICHO AMBACHO KILIKUWA KIKIENDESHWA NA MTANGAZAJI NGULI WA RADIO HIYO,BENEDICT KAGUA JUMAPILI ILIYOPITA.


MSHAURI MWELEKEZI WA MASUALA YA UCHUMI NA UWEKEZAJI STEVEN KIAMA MWAIMU AKIZUNGUMZA KWENYE MJADALA HUO AMBAO ULICHUKUA TAKRIBANI MASAA MATATU,KULIA KWAKE NI KAMISHNA WA NCCR MAGEUZI MKOA WA TANGA,RAMADHANI MANYEKO.