February 09, 2014

MTOTO WA MGIMWA ASHINDA KURA ZA MAONI KUGOMBEA UBUNGE WA KALENGA

 Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu Dkt William Mgimwa, akiongea kwa niaba ya familia wakati wa mazishi ya baba yake kijijini Magunga jimbo la Kalenga mkoani Iringa.

Na Francis Godwin, Iringa

Mtokeo  ya  kura  za maoni  ndani ya  CCM yametangazwa usiku wa kuamkia leo  huku mtoto wa aliyekuwa mbunge  wa  jimbo hilo Godfrey Mgimwa akishinda kwa  kishindo  katika  nafasi hiyo, akifuatiwa na Jackson Kiswaga katika matokeo hayo.

Godfrey Mgimwa amepata  kura 342 huku Kiswaga  akipata kura 170 na mkuu wa wilaya ya Pangani Hafsa Mtasiwa akiambulia  kura 42 .
February 09, 2014

CHADEMA YAIBURUZA CCM KILIMANJARO

MGOMBEA wa Udiwani kata ya Kiboriloni kwa tiketi ya Chadema,Frank Kagoma ameibuka Mshindi katika uchaguzi huo uliuohusisha vyama vitatu, Chadema, CCM na UDP.
akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Msimazi wa Uchaguzi, Shaban Ntarambe alisema uchaguzi huo ulikuwa huru na haki ambapo kutokana na kura zote zilizopigwa 1288, Kagoma ambaye ni Mwenyekiti wa kata ya Mnazi alipata kura 1019 dhidi ya kura 255 alizopata mpinzani wake wa karibu mgombea wa CCm, Willy Aidano.
Mgombea mwengine, Aidan Muganga Mnzava alijipatia kura 2 ambapo jumla ya kura halali zilikuwa ni 1276 na zilizoharibika ni 12.
Kulikuwa na vituo vikuu vitatu vya kupiga kura pamoja na vingine vidogo 11 na kufanya jumla ya vituo kuwa 14.

HIVI NDIVYO MNYAMA ALIVYOUWAWA MKWAKWANI.

February 09, 2014
MENEJA WA HOTELI YA TANGA BEACH RESORT MR.JOSEPH NGOYO  KATIKATI AKIWA NA MR JOHSON KUSHOTO ALIYEVAA MIWANI AMBAYE PIA NI KIONGOZI KWENYE HOTEL HII NA KATIBU MKUU WA COASTAL UNION KASSIM EL SIAGI LEO WAKIFUATILIA MECHI YA MGAMBO NA SIMBA AMBAPO MGAMBO ILIIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0 MCHEZO ULIOCHEZWA DIMBA LA CCM MKWAKWANI

 MENEJA WA HOTELI YA TANGA BEACH RESORT MR.JOSEPH NGOYO  KATIKATI AKIWA NA MR JOHSON KUSHOTO ALIYEVAA MIWANI AMBAYE PIA NI KIONGOZI KWENYE HOTEL HII NA KATIBU MKUU WA COASTAL UNION KASSIM EL SIAGI LEO WAKIFUATILIA MECHI YA MGAMBO NA SIMBA AMBAPO MGAMBO ILIIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0 MCHEZO ULIOCHEZWA DIMBA LA CCM MKWAKWANI
MENEJA WA KLABU YA COASTAL UNION YA TANGA,AKIDA MACHAI AKIFUATILIA MCHEZO HUO LEO AKIWA NA MASHABIKI WENGINE WA SOKA  MKOANI TANGA



KOCHA MKUU WA MGAMBO SHOOTING,BAKARI SHIME AKISITIZA JAMBO NA WACHEZAJI WAKE WAKATI MECHI YAO NA SIMBA IKIENDELEA LEO.

SHEHENA YA MWISHO YA MABOMBA KWA AJILI YA UJENZI WA BOMBA LA GESI YAWASILI DAR

February 09, 2014


 Katibu mkuu wizaraya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (Watatu kushoto), akizungumza jambo na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa (Wanne kushoto), wakati kamati hiyo ilipotembelea bandari ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kujionea kazi ya upakuaji vifaa vya ujenzi na kupokea shehena ya mwisho ya mabomba ya kupitishia gesi. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, Raha Mohammed (Kulia), Richard Ndasa (Wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Yonah Kilagane.
 Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (Wapili kushoto), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ikiongozwa na mwenyekiti wake, Victor Mwambalaswa (Wakanza kushoto) kuhusu kazi ya upakuaji vifaa vya ujenzi na kupokea shehena ya mwisho ya mabomba ya kupitishia gesi bandarini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Yonah Kilagane
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Victor Mwambalaswa (Wapili kulia) na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Mhe Richard Ndasa, wakiangalia kazi ya upakuaji saruji kutoka kwenye meli bandarini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamati hiyo ilitembelea ili kujionea kazi hiyo na ile ya kupokea shehena ya mwisho ya mabomba ya kupitishia gesi kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, akiwaeleza wajumbe wa kamati ya bunge ya Nishati na Madini (Hawapo pichani), kuhusu kazi ya upakuaji saruji kutoka kwenye meli, bandarini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Saruji hiyo itakayotumika kujengea mabomba ya kupitishia gesi, iliwasili sambamba na shehena ya mwisho ya mabomba hayo.
February 09, 2014

MASHABIKI WA AZAM FC WAKISHANGILIA WAKATI WA MCHEZO WA KOMBE LA SHIRIKISHO DHIDI  YA FERROVIARO YA MSUMBIJI ULIOCHEZWA KWENYE UWANJA WA AZAM FC CHAMAZ, DAR ES SALAAM JANA. AZAM ILISHINDA 1-0

MFUNGAJI WA GORI , KIPRE AKIAMBA NA MPIRA

MASHABIKI WA AZAM FC WAKIISHANGILIA TIMU YAO
February 09, 2014

SIMBA SC YAKALISHWA NA MIGAMBO MKWAKWANI 

Na Oscar Assenga, Tanga 

SIMBA SC imelala bao 1-0 jioni ya leo mbele ya Mgambo Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kwa mara nyingine leo kipa Ivo Mapunda amefungwa bao rahisi, baada ya kumtemea mpira mshambuliaji Fully Maganga dakika ya 29 kufuatia mpira wa adhabu.
Wachezaji wa Simba SC walipambana sana kujaribu kusawazisha bao hilo tangu hapo, lakini Mgambo Shooting leo walisimama imara kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu.


Kwa matokeo hayo, Simba SC inabaki na pointi zake 31 baada ya kucheza mechi 17, wakati Mgambo inatimiza pointi 12 na inaendelea kushika mkia.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dk57, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Awadh Juma/Uhuru Suleiman dk62, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amisi Tambwe na Ali Badru/Haroun Chanongo dk46.
Mgambo Shooting; Saleh Tendega, Bashir Chanache, Salim Kipaga, Bakari Mtama, Novaty Lufunga, Mohamed Samatta, Peter Mwalyanzi, Bolly Ajali, Fully Maganga Malima Busungu.