RED BRIGADE WA CHADEMA, WALA KIAPO MBELE YA MBOWE, MWANZA

March 01, 2015

Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, almaarufu kama RED BRIGADE, wakila kiapo cha utii, mbele ya Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, jijini Mwanza leo Jumamosi Februari 28, 2-015. Kiapo hicho kinafuatia kkamilika kwa mafunzo ya kiulinzi na usalama kwa vijana hao, ambapo nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu 2015.
Vijana hao wakila kiapo mbele ya Mbowe, (kulia).
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatare (kulia), kiasoma taarifa ya mafunzo ya vijana wa chama hicho 'Red Brigedi' huku mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto) akisikiliza kwa makini.
Vijana hao wakitoa heshima mbele ya Mwenyekiti wao Mbowe.PICHA KWA HISANI YA KIVIS BLOG

TIMU MPYA ZITAKAZOLETA UPINZANI LIGI KUU BARA

March 01, 2015



Hatimaye wiki moja iliyopita Mwadui ya Shinyanga ilitwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza na kuzipiku timu nyingine tatu zilizofanikiwa kupanda ligi msimu ujao. Timu zingine zilizorejea Ligi Kuu ni African Sports ya Tanga, Majimaji FC ya Songea na Toto Africans ya Mwanza.
Timu hizo zilimaliza kwenye nafasi mbili za juu za makundi mawili (Kundi A na B) katika mechi za Ligi Daraja la Kwanza kwani kila kundi lilitakiwa kutoa timu mbili zitakazopanda daraja.
Kwa upande wa Kundi A, African Sport na Majimaji zilifuzu wakati kwenye Kundi B zilifuzu timu za Mwadui FC na Toto Africans.
Timu hizo zinazomilikiwa na wakazi wa maeneo timu zinapotokea, siyo ngeni kwenye Ligi Kuu kwani kwa miaka ya nyuma timu zote zilishawahi kushiriki Ligi Kuu kabla ya kushuka. Hivi sasa timu hizo zinatarajiwa kutoa upinzani mkubwa kwenye Ligi ikiwamo kuwania ubingwa wa ligi. Timu hizo ziko kama ifuatavyo:
Majimaji FC ‘Wanalizombe’
Ni miongoni mwa timu ambazo zilikuwa tishio nchini katika miaka ya 1980 hadi iliposhuka daraja mwaka 2000. Kisha ikarejea tena mwaka 2009 na kushuka mwaka 2010. Mashabiki wengi wa soka nchini wanaikumbuka Maji Maji ya Songea maarufu kwa jina la Wanalizombe.
Maji Maji ambayo ilianzishwa mwaka 1977 ilipata umaarufu mkubwa mwaka 1980, mwaka ambao timu hiyo ilipata nafasi ya kushiriki kwa mara ya kwanza Ligi Daraja la Kwanza ambayo kwa sasa ni Ligi Kuu.
Uwezo wa timu hiyo
Kocha Mkuu wa Majimaji, Hassan Banyai anasema, “Mafanikio ya timu yangu yalitokana na kufanya kazi kwa umoja, nilishirikiana na wachezaji, pia umoja uliokuwapo kati ya viongozi, benchi la ufundi, wafadhili na mashabiki ulitufanya twende vizuri na tufanikiwe.”
Mipango kwenye Ligi Kuu
Kocha wa Majimaji, Banyai anasema kuwa ndoto zake kwa timu hiyo ni kuchukua ubingwa wa ligi ndani ya muda mfupi. “Tuliwahi kuchukua ubingwa wa Muungano miaka ya nyuma, hivi sasa tunataka kurudisha heshima yetu ya hapo awali kwa kuchukua ubingwa mapema,” alisema kocha huyo.
African Sport ‘Wanakimanumanu’
Hii ni moja ya timu ambazo ziliwahi kufanya vizuri miaka ya nyuma na kujiwekea heshima. Mpinzani wake mkubwa ni Coastal Union iliyopo Ligi Kuu. African Sport iliwahi kutwaa ubingwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku ikitamba kati ya miaka ya 80 na 90.
Ilitwaa kombe hilo mwaka 1988, lakini ikateremka daraja miaka mitatu baadaye, mwaka 1991.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Joseph Lazaro ambaye ni beki wa kushoto wa zamani wa Coastal Union na Yanga anasema katika mpango wao wa kutengeneza timu mpya amepanga kuongeza wachezaji saba tu kwenye usajili.
“Tuna imani kubwa na uwezo wa hawa vijana wetu, yatakuwapo maboresho kidogo tu, Tunajua Ligi Kuu ina ugumu wake, kikubwa kwetu kitakuwa ni maandalizi ya mapema,” anasema.
Nguvu ya timu yake
Kocha wa timu hiyo, Joseph Lazaro anasema kuwa kilichowabeba zaidi ni umri mdogo wa wachezaji ambao uliwawezesha kucheza vizuri. Pia ushirikiano na nidhamu ya mazoezi.
“Pia tulijiandaa vyema kwa kufanya zaidi mazoezi na kucheza kama timu,” anasema Lazaro.
Uongozi ulivyojipanga
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Khatibu Enzi anasema,”Tunataka kurudisha historia ya nyuma kwa kupanda ligi na kuchukua ubingwa kama tulivyofanya mwaka 1988, hakuna kinachoshindikana kwetu. Tuna nguvu na umoja katika timu yetu, ugumu ulikuwa kupanda, lakini sasa tumefika.”
Toto Africans ‘Wanakishamapanda’
Toto Africans imepanda Ligi Kuu baada ya juhudi za muda mrefu. Klabu hiyo ilishuka daraja kutokana na ukata ulioikabili mwaka 2013. Kabla ya kushuka daraja miaka miwili iliyopita, Toto ilikuwa imecheza misimu sita mfululizo kwani ilikuwapo kwenye ligi tangu msimu wa 2007/08. Hivi sasa timu inaongeza utamu wa soka kwa Kanda ya Ziwa baada ya Kagera Sugar, Stand United na Mwadui nao kuwa na nafasi kwenye ligi.
Nguvu za timu hiyo
Kocha Mkuu wa Toto, John Tegete anasema, “ Kilichotubeba kupanda Ligi Kuu ni usajili mzuri, licha ya umaskini wa timu yetu tulitafuta wachezaji bora wenye viwango na uzoefu mzuri.”
Mipango kwenye ligi
Kocha Tegete anasema watafanya marekebisho kwenye nafasi mbalimbali ili kuhakikisha ligi ya msimu ujao wanafanya vyema na kuleta ushindani.
Mwadui FC
Kifedha wako vizuri na wako chini ya udhamini wa mgodi wa almasi wa Petra Diamonds -Wiliamson uliopo Mwadui Shinyanga. Timu hii ilitamba msimu uliopita kwenye Ligi Daraka la Kwanza, lakini ikashindwa kwa pointi mbele ya majirani zao Stand United.
Mwadui FC ni moja ya timu kongwe nchini, Ilicheza Ligi kuu kati ya miaka ya 70 na kisha kushuka kwenye miaka ya 80.
Moja ya mafanikio ya timu hiyo ni kufika nusu fainali ya kusaka ubingwa wa Tanzania kwa kuitoa Yanga kwa mikwaju ya penalti.
Nguvu ya timu
Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ anasema, “ Timu yangu ilikuwa bora kwenye idara zote hasa kwenye idara ya ushambuliaji kwani ilifunga mabao mengi zaidi kuliko timu zingine zilizocheza na sisi.
“Usajili wa wachezaji wazoefu kama Athumani Iddi ‘Chuji’, Uhuru Selemani, Razack Khalfani uliisaidia timu, kimsingi usajili ndiyo uliochangia Mwadui kupanda Ligi Kuu,” anasema Julio.
Mipango kwenye Ligi
Kocha Julio anasema,”Mimi na timu yangu tumekuja kusaka ubingwa wa Ligi Kuu na kama siyo hivyo basi nikichemka sana niwe kwenye nafasi ya tatu.

KHADIJA KOPA NDANI YA MAJONZI

March 01, 2015


 Khadija Kopa (kulia) akiwa kwenye majonzi makubwa ya kuondokewa na Jabali la muziki wa kwaya nchini na kiongozi wa TOT Kapteni John Komba.
 Khadija Kopa akilia kwa uchungu baada ya kukutana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye msiba wa kiongozi wa TOT na Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba.
 Khadija Kopa (kulia) akilia kwa uchungu na wasanii wenzake wa TOT wakati wa kuhani msiba wa Kapteni John Komba

WASHINDI WA TIGO KILI HALF MARATHON WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

WASHINDI WA TIGO KILI HALF MARATHON WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

March 01, 2015

TI1 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 2, mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon Ismail Juma baada ya kushinda katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mkoani Moshi, katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mchezo wa Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
TI2 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kulia) akifurahia jambo na Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano wakati wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi.
TI3 
Washindi wa kwanza mpaka wa tatu wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, kwa upande wa wanaume, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Leonidaz Gama (kushoto), kulia ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage pamoja na na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
TI4 
Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano (wa pili kushoto) akisoma risala katika mashindano ya fainali ya mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa kwanza kushoto ni Ofisa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama pamoja na Makamu Mwenyekiti wa RT William Kalage na Mwenyekiti wa KAA Liston Metacha.
TI5Mkurugenzi wa Kampuni ya simu ya Tigo Diego Gutierez (kushoto) akizungumza na Kaimu wake Cecile Tiano (katikati) pamoja Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini David Charles kabla ya kuanza kwa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon yaliyofanyika juzi Mkoani Moshi.
Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano (wa pili) kushoto, akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo kabla ya kuanza kwa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi.
TI02 
Washindi wa mashindano ya Tigo Kili Marathon, kwa upande wa Wanawake, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
TI03 
Washindi wa mashindano ya Tigo Kili Marathon, kwa upande wa Wanawake, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
TI04 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. 500,000 mshindi wa tatu Vicoty Chepkemei, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa wanawake katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage.
TI05 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 1 mshindi wa pili wa mashindano Tigo Kili Half Marathon, Eunice Echumba, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage.
TI06 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh.500,000 mshindi wa tatu Theophil Joseph, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa Wanaume, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.

TASWIRA YA MKUTANO WA PAMOJA WA VYAMA VINAVYOUNDA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI UKAWA JIJINI WASHINGTON DC, MAREKANI

March 01, 2015

Viongozi wa Vyama vya CUF na CHADEMA wakiwa pamoja katika mkutano jijini Washington DC.
Mbunge wa Mji Mkongwe Zanzibar Mh Ismail Jussa akiwa katika mkutano wa Pamoja wa Vyama vinavyounda umoja wa Katiba UKAWA jijini Washington DC.
Viongozi wa CUF na CHADEMA DMV wakiwa na Mgeni rasmi Mh Ismail Jussa.
Kutoka Kushoto ni Mbunge wa Mji Mkongwe Zanzibar Mh Ismail Jussa, wa pili ni Mh Shamis ambaye ni Mwenyekiti wa CUF DMV, wa tatu ni Mwenyekiti wa CHADEMA DMV Kalley Pandukizi na wa nne ni Katibu wa Tawi la CHADEMA DMV Liberatus Mwang’ombe.
 
Katibu wa Tawi la CHADEMA DMV Liberatus Mwang’ombe akiongea katika Mkutano wa pamoja unaunganisha vyama vya CUF na CHADEMA.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA DMV Kalley Pandukizi akiongea kabla ya Kumpisha Mgeni Rasmi Mh Ismail Jussa.
 
Mh Jussa akiwa na Mwenyekiti wa Tawi la CHADEMA DMV Kalley Pandukizi.
Viongozi wa CHADEMA na CUF DMV wakiwa na Mh Jussa katika Picha ya Pamoja kuonyesha Mshikamano wa Vyama vyao.
Kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa Tawi la CHADEMA DMV Ndugu Hussein Kauzela, katikati ni Mh Ismail Jussa na Kulia ni Katibu wa CHADEMA DMV katika picha ya pamoja kuonyesha mshikamano.
Mwenyekiti wa CUF DMV Ndugu Shamis akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Ndugu Baybe Mgaza.
Katibu Mwenezi wa CHADEMA DMV Ndugu Hussein Kauzela akiwa na Mweka Hazina wa Tawi la CHADEMA DMV Ndugu Ludigo Mhagama.
Mh Ismail Jussa akiwa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Salma Moshi.

WAFANYE WATABASAMU WATABASAMU NA WATOTO MUHIMBILI

March 01, 2015

 Mratibu wa programu ya Wafanye Watabasamu na mchora vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala, akimwonesha mtoto Maurine jinsi ya kuchora katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita. Mpangala na wenzake walitembelea watoto wanaotibiwa saratani ili kuchora nao na kuwapa zawadi mbalimbali. Zaidi kuhusu programu hii tembelea: https://www.facebook.com/wafanyewatabasamu
 Nguvu ya sanaa tiba kama inavyooneshwa na Clara.
 Sanaa tiba ikawasahaulisha maumivu, wakajihisi wako nyumbani. Baadhi ya watoto wakijiachia na marafiki wa Wafanye Watabasamu waliokwenda kuwatabasamisha katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita.
 Mtoto Nico akienda sambamba na marafiki wa Wafanye Watabasamu. Kutoka kulia ni Sia Marupa, Masoud Junior na Cloud Chatanda.
 Sanaa tiba ikapandisha mzuka, viganja vikazungumza kama inavyoonekana kwa mtoto Heri. Wafanye Watabasamu inakuombea upate nafuu ya mapema.
 Ha ha ha haaaaaa. Hili ndilo lengo hasa la Wafanye Watabasamu. Mungu akupe nafuu ya mapema Nico.
 “Tukikosea je?!” Swali alilouliza mtoto Clara na kuzua kicheko. Aliliuliza baada ya mchoraji Paul Ndunguru aliyeipa kamera mgongo kusema kuwa wachore huku wamefumba macho. Kutoka kushoto: Tatu Bendera, Mama Pili Mtambalike na Beatrice Makelele.
 Baadhi ya watoto na marafiki wa Wafanye Watabasamu wakionesha kazi zao.
 Kulikuwa na aina mbalimbali za sanaa tiba. Komediani Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga (kulia) alikuwa kivutio kwa watoto.
 Mtoto Clara (kulia) akiwa na rafiki wa Wafanye Watabasamu, Arafa Salim.
 Rafiki wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni gwiji la uchoraji nchini, Paul Ndunguru, akiangalia umahiri wa uchoraji wa mtoto Clara wakati wa zoezi la sanaa tiba.
Hakika sanaa tiba ni dawa. Mtoto Henry alidhihirisha kuwa hata naye komedi iko damuni. Toka kulia; Abdul Kingo, Faiza Ally, Fred Halla, Wakuvwanga, Amani Abeid na Lute Mwakisopile. (Picha zote na Wafanye Watabasamu).
Links:

TAMASHA KUBWA LA MICHEZO LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI NA TAASISI ZAKE LAFANYIKA, LAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

March 01, 2015

 Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (kushoto) akimsalimia mtumishi wa Wizara hiyo, Said Ngovi ambaye ni mvuta kamba wa timu ya Utawala wakati Mkurugenzi huyo alipokuwa anazikagua timu mbalimbali za wizara hiyo katika Tamasha la Michezo la kwanza lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kapteni wa timu ya wanaume (Utawala) ya kuvuta kamba, Ally Lubuva.
 
 Kapteni wa Timu ya Utawala ya kuvuta kamba wanaume, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Neema Chilipweli (kushoto) akiimasisha timu yake kuivuta timu ya Uhamiaji (haipo pichani) wakati timu hizo zilipokuwa zikishindana katika Tamasha kubwa la Michezo lililoandaliwa na wizara hiyo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi wake na kuwawezesha kufanya mazoezi ya viungo. Tamasha hilo ambalo la kwanza kufanywa na wizara hiyo lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
 
 Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mary Nyegazeni akiishangilia timu yake ya Utawala ya kuvuta kamba wanaume baada ya kunyakua pointi mbili kwa kuivuta timu ya Uhamiaji katika mashindano maalumu ya Tamasha la Michezo la wizara hiyo ambalo lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
 
 Mtumishi wa Idara ya Uhamiaji, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Amina Mavengero (katikati) akicheka kwa furaha baada ya kushinda mchezo wa kufukuza kuku kwa kuwapiku wenzake wa Timu ya Utawala, Mary Nyegazeni (kushoto) na Consalva Nagamchonga wa Timu ya Jeshi la Magereza. Mchezo huo ulishirikisha watumishi wenye umri zaidi ya miaka 55 katika timu zote zilizoshiriki.  Wizara hiyo pamoja na Taasisi zake za Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zilifanya mashindano ya michezo mbalimbali yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam, ambapo Tamasha hilo lilifunguliwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lilian Mapfa.
 
 Timu ya Utawala ya kuvuta kamba wanawake, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiivuta timu ya Uhamiaji (haipo pichani) wakati timu hizo zilipokuwa zikishindana katika Tamasha kubwa la Michezo lililoandaliwa na wizara hiyo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi wake na kuwawezesha kufanya mazoezi ya viungo. Tamasha hilo ambalo la kwanza kufanywa na wizara hiyo lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
 
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akizungumza na wanamichezo wa timu za Utawala, Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) walioshiriki katika michezo ya Kuvuta kamba, mpira wa miguu, riadha, Netiboli na kufukuza kuku katika Tamasha kubwa la Michezo lililoandaliwa na Wizara hiyo kwa ajili ya kuwakutanisha watumishi wake na kuwawezesha kufanya mazoezi ya viungo. Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Probesheni na Huduma kwa Jamii, Fidelis Mboya, na kulia ni Jesuad Ikonko, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (kushoto), Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa (wapili kushoto) wakijumuika kulisakata rumba na wanamichezo wa Wizara na Taasisi zake katika Tamasha la Michezo la kwanza lililofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo lilijumuisha timu za Utawala, Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida).
Katibu wa Michezo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jarahi Kilemile akimshukuru Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (hayupo pichani) kwa kulifungua na kufunga Tamasha kubwa la michezo la wizara hiyo lililofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo lilijumuisha timu za Utawala, Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.