RAIS AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA ALBINO TANZANIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

March 05, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo. Walioketi kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Mcheche Masaju Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabirika Mushi na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bw. Emmanuel Achayo 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua jambo wakati akiongea na viongozi Wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi Wa Chama Cha Albino Tanzania baad ya kukutana nao pamoja na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Mcheche Masaju Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabirika Mushi na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bw. Emmanuel Achayo Ikulu jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU
Matatizo ya Maji kwenye maeneo ya Ziwa Victoria kuwa historia

Matatizo ya Maji kwenye maeneo ya Ziwa Victoria kuwa historia

March 05, 2015

MA1 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda wilaya za Igunga,Nzega Uyui mpaka Tabora.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Jumanne Maghembe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.Kulia kwake ni Mbunge wa Tabora Mjini Alhaji Ismail Aden Rage na kushoto ni Mbunge wa Igalula Mhandisi Athumani Mfutakamba. MA3 
Mbunge wa Tabora Mjini Alhaji Ismail Aden Rage, akizungumzia mradi huo unaotarajia kunufaisha vijiji 68 na watu karibu watu 385,280 katika maeneo yanayozunguka mradi huo. MA4 
Mbunge wa Igalula Mhandisi Athumani Mfutakamba, akieleza kufurahishwa kwake na ujenzi wa mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 30.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri Maji na Umwagiliaji Profesa Jumanne Maghembe (hayupo pichani). MA6 
Baadhi ya waandishi wa habari na watendaji wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakimsikiliza Waziri Prof. Maghembe.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO.
MWANAHABARI AJITOLEA KUPAMBANA NA MAUAJI YA ALBINO

MWANAHABARI AJITOLEA KUPAMBANA NA MAUAJI YA ALBINO

March 05, 2015
Balozi wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya jhabari. Kampeni hiyo inajulikana kwa jina la Imetosha. Balozi wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya jhabari. Kampeni hiyo inajulikana kwa jina la Imetosha.Mchoraji maarufu na mmoja wa wanakamati wa kampeni za imetosha Masoud Kipanya (kulia) akizungumza na DW. Mchoraji maarufu na mmoja wa wanakamati wa kampeni za imetosha Masoud Kipanya (kulia) akizungumza na DW.Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kulia)  akihojiwa na DW mara baada ya mkutano wao. TBN imeunga mkono kampeni hizo zinazoongozwa na balozi wa kujitolea wa mapambano hayo, Henry Mdimu. Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akihojiwa na DW mara baada ya mkutano wao. TBN imeunga mkono kampeni hizo zinazoongozwa na balozi wa kujitolea wa mapambano hayo, Henry MdimuBaadhi ya wajumbe wa kampeni za imetosha wakipata picha za ukumbusho mara baada ya kuzungumza na wanahabari. Baadhi ya wajumbe wa kampeni za imetosha wakipata picha za ukumbusho mara baada ya kuzungumza na
.Mkutano na wanahabari ukiendelea.  
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

 Na Mwandishi Wetu  

MMOJA wa watu wenye ulemavu wa ngozi, albino na mwanahabari shupavu kutoka kampuni ya Mwananchi Communication, Henry Mdimu amejitolea kuwa balozi wa hiyari kupinga mauaji ya kikatili ya watu wenye albino yanaoendelea nchini. Bw. Mdimu ambaye ameungwa mkono na baadhi ya marafiki na watu wanaokerwa na vitendo hivyo, ikiwemo Chama cha Bloggers nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) amesema ameamua kufanya hivyo baada ya kushuhudia ndugu zake wakiteseka kwa muda mrefu dhidi ya mauaji hayo. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Balozi Mdimu amesema lengo lake kuu ni kuhakikisha anazunguka pamoja na marafiki watakao muunga mkono na kutoa elimu kwa kuanzia Kanda ya Ziwa ili tatizo hilo lisiendelee kuenea nchi nzima. Akifafanua zaidi alisema mauaji ya watu wenye albino yanaichafua Tanzania hivyo atahakikisha anaisaidia Serikali kupambana na watu wenye imani hizo za kipuuzi ili kuondoa doa linaloichafua nchi yetu ambayo imekuwa na sifa ya amani dunia nzima. "...Nimeamua kufanya hivi baada ya kushuhudia ndugu zangu wakiteseka kwa muda mrefu. Awali nilishindwa kuanzisha harakati hizi nikiamini kuna vyombo vinavyohusika na utetezi wa watu wenye ulemavu wa ngozi." "...Hivyo nimeamua niweke jitihada zangu binafsi niisaidie Serikali yangu katika kuondoa doa hili linaloichafua Nchi yetu yenye sifa ya Amani duninia nzima. Hivyo nawaomba Watanzania wenzangu mniunge mkono tukishirikiana na Serikali ili mauaji haya yakome," alisema Mdimu. "Kutokana na ushawishi nilionao kama Mwandishi, Mtangazaji wa redio na Blogger naamini nitaleta mabadiliko makubwa katika kuhakikisha haki ya kusihi kwa ndugu zangu inaheshimiwa na kubaki historia. Salamu zangu ziwafikie wanyanyasaji, wauaji na wenye kufanya dhihaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kuwa IMETOSHA." Akifafanua zaidi alisema kwa uchunguzi wake wa awali umebaini ukosefu wa elimu juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi ndio chanzo cha tatizo hilo kukua na hatimaye kuuana kwa imani za kishirikina. "...Hivyo basi, silaha ya Elimu ni sehemu kubwa ya haraki hizi," alisisitiza Balozi huyo wa kujitolea. Aidha alisema kuendesha harakati hizo alizozipa jina la 'IMETOSHA' elimu itatolewa kwa njia ya sanaa, na washauri nasaha pamoja na kundi la wanamuziki ambao pia wataandaa nyimbo mbalimbali za kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili huu. Alisema wasanii ambao hadi sasa wamejitokeza kuunga mkono kampeni hizo ni paoma na Jhikoman, Kassim Mganga, Profesa J, Ray C, Fid Q, Roma Mkatoliki na Dami Msimamo. Hata hivyo alisema bado pia anaamini nguvu ya vyombo vya habari ikiungana na kampeni hizo wanaweza kufanikiwa zaidi hivyo kuomba ushirikiano katika kuhakikisha vinapaza sauti kutokomeza mauaji hayo ya kikatili. *Imeandaliwa na www.thehabari.com _____________________________________________________
 Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE JIMBO LA KIBAKWE WILAYANI MPWAPWA.

March 05, 2015


Pichani Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Abdulrahman Kinana ukielekea jimbo la Kimbakwe  Wilayani Mpwapwa mapema leo asubuhi kuendelea na ziara yake ya siku 9 mkoani Dodoma ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua nakuhimiza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 pamoja na kusikiliza kero za Wananchi ikiwemo na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya vijana waliopo katika kituo cha mradi wa Wanyama kazi ndani ya kijiji cha Kibakwe,wilayani Mpwapwa.
Mmoja wa Vijana waliopo katika kituo cha mradi wa Wanyama kazi ndani ya kijiji cha Kibakwe,wilayani Mpwapwa wakitoa maelezo mafupi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana namna zana hizo za kilimo zinavyotumiwa na wanyaka katika suala zima la kilimo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhusiana na uoteshaji wa mbegu za miti ya mikorosho  katika kituo cha mradi wa Wanyama kazi ndani ya kijiji cha Kibakwe,wilayani Mpwapwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua shamba la mfano la Wanaushirika waitwao Mkombozi,lililopo karibu na kituo cha mradi wa Wanyama kazi ndani ya kijiji cha Kibakwe,wilayani Mpwapwa.
Mwenyekiti wa kikundi cha Mkombozi,Bwa.Athanas Kigosi akitoa maelezo mafupi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,kuhusiana na shamba la mfano ambalo limepandwa mahindi,lililopo katika kijiji cha Kibakwe,Wilayani Mpwapwa.Bwa.Athanas alieleza changamoto wazipatazo katika maandalizi yao ya kilimo kuwa suala la pembejeo limekuwa tatizo kubwa kwao,kwani zimekuwa zikiletwa kinyume na wakati,hali inayowapelekea ugumu wa kuendelea na kilimo kwa wakati,mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo sambamba na mazao yao kutopandishwa bei,Hivyo Bwana Athanas ameiomba serikali kuwasaidia wakulima kupelekewa pembejeo kwa wakati ili kuhakikisha maandalizi ya kilimo yanakwenda kwa wakati.
Katibu Mkuu wa  CCM,Ndugu Kinana akifafanua jambo kwa Wanahabari katika shamba la mfano ambalo limepandwa mahindi,lililopo katika kijiji cha Kibakwe,Wilayani Mpwapwa.Pichani kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa darasa la shule ya sekondari Ikuyu katika kijiji cha Luhundwa,wilaya ya Mpwapwa.Ndugu Kinana alikagua na kushiriki  mradi wa ujenzi wa darasa la shule hiyo na kuwasalimia wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Luhundwa mapema leo,alipokwenda kushiriki ujenzi wa darasa la shule ya sekondari Ikuyu katika kijiji cha Luhundwa,wilaya ya Mpwapwa.
Wananchi wa kata ya Rudi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kukagua na kushiriki ujenzi wa ofisi ya Mtendaji Kata.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akishiriki mradi wa ujenzi wa ofisi ya Mtendaji Kata ya Rudi,Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.Mwisho kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Mh.Addam Kimbisha pamoja na Diwani wa kata hiyo,Mh.Nyaulingo Bulamlete.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiweka jiwe la msingi katika ofisi ya CCM tawi la Mtamba,wilaya ya Mpwapwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakifurahia jambo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya CCM tawi la Mtamba,wilaya ya Mpwapwa.
 Wakazi wa jimbo la Kibakwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibakwe stendi,Katibu Mkuu aliwataka viongozi wanaosimamia sheria kuzingatia wananchi wa kawaida na kuwashirikisha kwenye jambo linalowagusa kwenye shughuli zao za kila siku kwani kufanya hivyo kutawasaidia wananchi hao kuishi maisha yao na pia kuinua uchumi wa eneo husika.
 Wakazi wa jimbo la Kibakwe wakimshangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibakwe stendi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe wilayani Mpwapwa.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wakazi wa Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe na kuwataka wana CCM kuchagua viongozi wanaowataka na kusema wilaya au mkoa hawataka jina la mtu yeyote aliyechaguliwa na wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Kibakwe,jimbo la Kibakwe wilaya ya Mpwapwa,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama mkoa wa Dodoma akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Wakazi wa jimbo la Kibakwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibakwe stendi,Katibu Mkuu aliwataka viongozi wanaosimamia sheria kuzingatia wananchi wa kawaida na kuwashirikisha kwenye jambo linalowagusa kwenye shughuli zao za kila siku kwani kufanya hivyo kutawasaidia wananchi hao kuishi maisha yao na pia kuinua uchumi wa eneo husika.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

March 05, 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kamishina Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya, wakati walipokutana baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Burn Ltd, Malaczynski Burn, baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia alipokuwa akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015. Picha na OMR.
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo yatoa zawadi kwa wateja bora wa Tigo wa mwaka 2014

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo yatoa zawadi kwa wateja bora wa Tigo wa mwaka 2014

March 05, 2015

Tigo Mteja bora 2014, Anta Ramadhani (kulia) akipokea zawadi ya simu kutoka kwa Mtaalamu wa Habari katika Mitandao ya Kijamii ya Tigo Samira Baamar, katikati ni Meneja Uendeshaji na Msaidizi wa Mifumo ya Mawasiliano wa Tigo Halima Kasoro
TI2 
Tigo Mteja bora 2014, Hamin Halfani (kulia) akipokea zawadi ya simu kutoka kwa Meneja Ubora Mwangaza Matotora TI3 
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja na Tigo Wateja bora 2014, katika hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi wateja hao iliyofanyika leo katika Makao Makuu ya Tigo Tanzania, Makumbusho Dar es Salaam.

Mh. Lowasaa akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini

March 05, 2015

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose aliyefika ofisini kwake leo kwa mazungumzo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose ofisini kwake,jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

BARAZA LA USHAURI SUMATRA LAZINDUA VILABU VYA WANAFUNZI

March 05, 2015

 Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Ayoob Omary akizindua vilabu vya wanafunzi vya Sumatra. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Oscar Kikoyo na kulia ni Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatan.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano akizungumza.
 wanafunzi wakifuatilia hotuba za uzinduzi kutoka kwa viongozi.
 Mgeni rasmi pamoja na meza Kuu ikipiga picha na Vilabu mbalimbali kutoka shule za sekondari na msingi.
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo (kulia) akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay, Dar es Salaam jana baada ya uzinduzi wa klabu za wanafunzi watumiaji wa huduma za usafiri mkoa wa Dar es salaam jana. Wengine ni  Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano na Mwenyekiti wa Baraza hilo Ayoob Omary. Picha na Sori: mrokim.blogspot.com