MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE NA MATUKIO YA PICHA KATIKA ZIARA YA RAIS DR. JAKAYA KIKWETE NCHINI CHINA

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE NA MATUKIO YA PICHA KATIKA ZIARA YA RAIS DR. JAKAYA KIKWETE NCHINI CHINA

October 22, 2014

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa mfanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai iliyoko Beijing mara baada ya kuwasili hotelini hapo. Mama Salma ameambatana na mumewe Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambaye amewasili nchini China tarehe 21.10.2014 kwa ziara ya kiserikali. 2 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai ya mjini Beijing mara baada ya kuwasili nchini China kwa ziara ya kikazi tarehe 21.10.2014. 3 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Bwana Yang Hua, Mmoja wa viongozi wakuu wa China National Offshore Oil Corporation (CNOOC), wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa Shirika hilo Bwana Wang Yilin kwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea makao makuu ya Shirika hilo yaliyoko Beijing nchini China tarehe 22.10.2014. Shirika hilo hujishughulisha na utafiti wa mafuta na gesi baharini, uchimbaji na uuzaji wa maliasili hizo. 4 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa China National Offshore Oil Corporation Bwana Wang Yilin wakizindua rasmi mtambo mpya wa utafutaji wa mafuta na gesi baharini, Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014. 5 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania unaozuru nchini China wakiangalia vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na Shirika la  CNOOC la China katika kazi ya utafutaji wa mafuta na gesi baharini wakati walipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014. 6 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akishirikiana na Mkewe Mama Salma Kikwete na Professa Li Songshan (kushoto kwa Rais Kikwete), Mwanzilishi wa Kijiji cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe 22.10.2014. 7 8 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia baadhi ya ngoma za asili ya Afrika zilizokuwa zikipingwa na vijana wa kichina mara baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha sanaa za Afrika huko Songzhuang tarehe 22.10.2014. 9 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama. 10 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama. 11Waanzilishi wa Kijiji cha Sanaa za Afrika Professa Li Songshan na Mke wake Dkt. Han Rong wakimkabidhi zawadi ya picha Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mke wake mara baada ya ufunguzi rasmi wa kijiji hicho tarehe 22.10.2014.
unnamed 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiandika kumbukumbu yake kwenye kijiji cha sanaa za Afrika mara baada ya Rais Dkt. Kikwete kuandika kumbukumbu yake.
PICHA NA JOHN  LUKUWI.

JE UNAMJUA MKE WA MSANII JB BONGE LA BWANA? BASI MCHEKI HAPA.

October 22, 2014


Katika pita pita mtandaoni tumekutana na picha hizi za JB a.k.a Bonge la bwana akiwa ameziweka katika akaunti yake ya Instagram na kuonyesha ni jinsi gani anajivunia kuoa na kuwa na
mke mzuri kama huyu. Tazama picha hapo chini uone ni jinsi gani jamaa anajiamini na anampenda mke wake na haoni shida kumuweka mtandaoni ili mashabiki zake wamfahamu shemeji na wifi yao.



Po

KOCHA PRISONS: SIMBA HAWATOKI SOKOINE JUMAMOSI

October 22, 2014

                         
                       Na Bertha Lumala, Mbeya

Wakati Kocha wa Tanzania Prisons, David Mwamwaja ameelekeza nguvu zote katika mechi inayofuata ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba, mashabiki wa soka jijini Mbeya wamesema mwaka huu ni
wa tabu kwa mkoa wao kisoka.
Baada ya Prisons kukubali kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya JKT kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini hapa jana huku Mbeya City ikilala 1-0 dhidi ya Azam FC Jumamosi, kauli iliyotawala mitaa mbalimbali ya mji huu ni ‘mwaka wa tabu Mbeya’.
Magoli ya Najim Magulu dakika ya 27 na Jabir Aziz aliyefunga kwa penalti dakika ya 51 yaliipa ushindi wa kwanza msimu huu JKT Ruvu inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Felix Minziro.
Akizungumza na mtandao huu mjini hapa jana, Mwamwaja alisema kikosi chake kilirejea kambini juzi kuanza maandalizi ya mechi yao dhidi ya Simba ambayo alidai itakuwa ngumu kwa kuwa Simba watakuwa wanasaka
ushindi wa kwanza msimu huu.
“Kikosi changu cha ni kizuri kuzidi cha msimu uliopita, mechi ya jana (juzi) tuliponzwa na kipa (Beno Kakolanya). Magoli yote yametokana na makosa yake, tumeshaanza kurekebisha kasoro hiyo, kufikia Jumamosi tunaamini atakuwa sawa,” alisema Mwamwaja.
“Mechi yetu ya Jumamosi itakuwa ngumu, pengine kuzidi mechi zote nne tulizocheza msimu huu hadi sasa. Ninatambua Simba wataingia uwanjani kusaka ushindi wao wa kwanza msimu huu baada ya kuambulia sare katika mechi zote walizocheza, lakini hata sisi tunahitaji ushindi ili tujiweke pazuri na kulinda heshima ya uwanja wetu wa nyumbani,”
alisema zaidi kocha huyo wa zamani wa Simba.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA RAIS WA MMI BINGWA WA MASUALA YA UTAWALA NA UONGOZI KUTOKA BAHAMAS, DKT. MYLES MUNROE

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA RAIS WA MMI BINGWA WA MASUALA YA UTAWALA NA UONGOZI KUTOKA BAHAMAS, DKT. MYLES MUNROE

October 22, 2014

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akigana na Rais wa MMI Bingwa wa Masuala ya Utawala na Uongozi kutoka Bahamas, Dkt. Myles Munroe, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR 3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa MMI Bingwa wa Masuala ya Utawala na Uongozi kutoka Bahamas, Dkt. Myles Munroe, na ujumbe wake baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam. Picha na OMR 2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais wa MMI Bingwa wa Masuala ya Utawala na Uongozi kutoka Bahamas, Dkt. Myles Munroe, wakati alipofika ofosini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, juzi Oktoba 20, na kufanya mazungumzo. Picha na OMR 1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha, Rais wa MMI Bingwa wa Masuala ya Utawala na Uongozi kutoka Bahamas, Dkt. Myles Munroe, na ujumbe wake wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, juzi Oktoba 20, 2014 akiwa na ujumbe wake na kufanya mazungumzo. Picha na OMR
MAOFISA WA UN WAHAMASISHA WANAFUNZI WA JANGWANI KUTEKELEZA AJENDA ZA UMOJA WA MATAIFA

MAOFISA WA UN WAHAMASISHA WANAFUNZI WA JANGWANI KUTEKELEZA AJENDA ZA UMOJA WA MATAIFA

October 22, 2014

DSC_0132 
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani akiwa ameambatana na maafisa wenzake wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa unazishwe. Kushoto kwa Bi Ledama ni Albert Okal (ILO).
Shamrashamra za maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa uanzishwe zimeanza nchini, na leo jumatano maofisa waandamizi wa UN walitembelea shule ya sekondari ya Jangwani na kuwahabarisha wanafunzi hao juu ya shughuli za Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Mjadala kati ya maofisa hao Phillemon Mutashubirwa, Programme Manager wa UN Habitat, Usia Nkhoma Ledama, Afisa habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Albert Okal (ILO),Greta Sayungi (UNICEF), ulijikita katika masuala ya HIV/AIDS, EBOLA, Usafi na umuhimu wakuosha mikono ili kujikinga na maradhi, elimu ya ujasiriamali, ajira kwa vijana, kazi za kujitolea, malengo ya Milenia na malengo ya Umoja wa Mataifa kwa ujumla wake.
Ijumaa wiki hii Umoja wa Mataifa utaadhimisha mkiaka 69 toka uanzishwe na kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
DSC_0106
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule yasekondari Jangwani jijini Dar. Kutoka kushoto ni Phillemon Mutashubirwa (UN Habitat), Greta Sayungi (UNICEF) pamoja na Dr Bwijo Bijo (UNDP)
DSC_0094 
Pichani juu na chini ni Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani wakiwasiliza maafisa wa Umoja wa Mataifa waliowatembelea shuleni hapo.
DSC_0083

Shirika la ndege la Flydubai lenye makao yake makuu Dubai lazindua njia mbili mpya za ndege

October 22, 2014

Makamu wa Rais mwandamizi katika shughuli za kibiashara wa shirika la ndege la FlyDubai ,Bwa.Sudhir Sreedharan akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wana habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) katika hafla fupi ya uzinduzi wa njia mbili mpya za shirika la ndege hiyo kutoka Dubai kuja jijini Dar es salaam na Zanzibara (nchini Tanzania). Bwa.Sudhir amesema kuwa shirika hilo la Flydubai liliingia katika soko la kibiashara kuanzia mnamo mwaka 12009,ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kuongeza njia mpya sita (six new routes ) .
Mgeni rasmi,Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Mh Samia Suluhu akizungumza mapema leo katika uzinduzi wa njia mbili mpya za ndege ya FlyDubai aina ya Boieng 737-800,uliofanyika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar.

Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo wa njia mpya ya shirika la ndege la Flydubai lenye makao yake makuu Dubai..

 Wageni waalikwa wakishangilia jambo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo .