WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTNO WA ALAT.

April 09, 2016

 Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Edwin  Rutageruka wakati alipotembelea abanda la maonyesho  la TANTRADE kabla ya kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala  za Mitaa (ALAT) kwetuo cha Mikutano cha Dodoma  Aprili  8, 2016.
 Wasanii wa kikundi cha Nyota cha Dodoma  wakitumbuiza katika Mkutano Mkuu Malum wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma  mjini Dodoma Aprili  8,2016. 
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jafo kizungumza kabla ya kumakribisha Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kufungua Mkutano Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Dodoma Aprili 8, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Akizungumza wkati alipofungua mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania  (ALAT) kwenye  Kituo cha Mikutano cha Dodoma Aprili 8, 2016.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa  Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma Aprili 8, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT), Gulam Mkadam Taarifa ya Utafiti  kuhusu Sekta ya Umma na Binafsi kwenye serikali za Mitaa wakati alipoizindua baada ya kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi wa Jumuiya ya Tawla za Mitaa Tanzania (ALAT) kwenye Kituo cha  Mikutano cha Kimataifa cha  Dodoma  Aprili 8, 2016. Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawla za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAASISI YA KUFUNDISHA LUGHA YA "INTERNATIONAL LANGUAGE TRAINING CENTRE" YABORESHA ZAIDI MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA.

April 09, 2016
Charles Mombeki ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kufundisha Lugha mbalimbali ikiwemo za Kitaifa na Kimataifa Jijini Mwanza ya "International Language Training Centre" akiwa amesimama katika jengo la taasisi hiyo iliyopo Isamilo (barabara ya Mediacal Reseach) Jijini Mwanza.

Mombeki anasema taasisi hiyo imeboresha zaidi mazingira ya kujifusia ili kukidhi mahitaji wasomaji. Pia anaongeza kwamba taasisi hiyo imeboresha mazingira kujifunzia kwa ajili ya Kituo chake cha Elimu ya Makuzi kwa Watoto Wadogo (Day Care Centre) ambapo anawasihi wananchi kutembelea taasisi hiyo ili kunufaika na fursa iliyopo hivi sasa kabla haijafikia ukomo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kufundisha Lugha mbalimbali ikiwemo za Kitaifa na Kimataifa Jijini Mwanza ya "International Language Training Centre" akitoa ufafanuzi kwa wanaohitaji kusoma katika taasisi yake. Pembeni ni eneo rafiki kwa ajili ya mapumziko mafupi baada ya masomo au majadiliano baada ya masomo. 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kufundisha Lugha mbalimbali ikiwemo za Kitaifa na Kimataifa Jijini Mwanza ya "International Language Training Centre" akionyesha baadhi ya maeneo kwa ajili ya michezo ya watoto.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kufundisha Lugha mbalimbali ikiwemo za Kitaifa na Kimataifa Jijini Mwanza ya "International Language Training Centre" akionyesha baadhi ya maeneo kwa ajili ya michezo ya watoto.

Wasiliana na International Language Training Centre kwa nambari 0784 66 49 33 au 0754 66 49 33
Bonyeza HAPA Ili Usipitwe.
Waziri Ummy Mwalimu atembelea Hospitali za Mkoa wa Mbeya

Waziri Ummy Mwalimu atembelea Hospitali za Mkoa wa Mbeya

April 09, 2016

8e796dee-b674-43f7-97f8-3bad1046087d
Na Catherine Sungura, Mbeya
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara katika hospitali zilizopo Mbeya na kuzitaka hospitali zinazotumia mfumo wa ukusanyaji mapato wa kieletroniki wasibweteke na mapato wanayoyakusanya kila siku.
Rai hiyo imetolewa na aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali ya rufaa ya kanda ya mjini Mbeya.
Ummy alisema ukusanyaji wa mapato kwa mfumo huu unasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo ununuzi wa dawa, vifaa na vifaa tiba pamoja na utoaji wa motisha kwa watumishi.
"Bado tunatambua hali ya uhaba wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kuanzia ngazi zote, tukiweza kusimamia vizuri hili tutafanikiwa," alisema.
Aidha alisema wanatarajia katika serikali ya awamu hii bajeti ya dawa itaongezeka zaidi ya mara tatu kulinganisha na bajeti za nyuma, hivyo wameishauri Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wanunue dawa toka kwa wawekezaji wa hapa nchini ambapo itakua na bei nafuu na itaongeza tija na upatikanaji wa dawa kwa haraka.
Waziri Ummy Mwalimu aliutaka Mkoa kufuatilia, kuwafichua na kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na wizi wa dawa.
"Tunao watumishi wachache wa afya ambao wanahujumu na kuiba dawa na kuzipeleka kwenye maduka ya dawa binafsi, hao hatutowafumbia macho na kuwapeleka mahakamani"
Kuhusu upungufu wa watumishi wa kada ya afya nchini, Waziri wa afya alisema, nchi ina upungufu wa asilimia 52, hivyo serikali inatarajia kuajiri watumishi takribani elfu kumi hivi karibuni ambao watatawanywa nchi nzima ikiwemo mikoa iliyo pembezoni.
Katika hospitali ya uzazi ya Meta, waziri huyo ameguswa na ufinyu wa wodi za wazazi na kupelekea mama wajawazito na waliojifungua kulala chini na wawili wawili kwenye kitanda kimoja na hivyo kuwataka kufanya haraka ujenzi wa jengo jipya litakaloondoa mrundikano wa mama wajawazito na watoto njiti.
Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya inakusanya kwa mwezi kiasi cha shilingi Milioni mia tano na pia inahudumia mikoa saba nchini na kuhudumia zaidi ya watu milioni mbili.
46e02c3a-bc41-4fed-9ff6-a180f42fa264
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisalimia na watumishi mara alipofika kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mbeya.
afc64d2e-46a1-49a8-be9b-59340b6d8a8a
Waziri Ummy akimsalimia mtoto Jenifer Joel (9) mkazi wa Chunya aliyelazwa hospitalini hapo.
5f7ab771-5109-4c0c-95e6-83931c8ec108
Waziri wa afya akimjulia hali mtoto Baraka Jekonia (1) mkazi wa Chunya aliyelazwa wodi ya watoto, Waziri Ummy ameitaka hospitali hiyo kuwachaji pesa wagonjwa wote wanaofika hospitali ya rufaa moja kwa moja bila kupatiwa rufaa kutoka vituo vya afya vilivyopo jirani na wananchi ili kupunguza msongamano kwenye hospitali za rufaa nchini.
8e796dee-b674-43f7-97f8-3bad1046087d
Katika hospitali ya uzazi ya Meta, Waziri Ummy Mwalimu alimsalimia Binti Kanisia Komba aliyejifungua mtoto wa kike katika hospitali hiyo mama wajawazito wote wanatibiwa kwa kadi ya bima ya afya inayodhaminiwa mpango wa kusaidia akina mama wajawazito wa KFW toka Banki ya Ujerumani.
9518e21d-3e1e-43ad-a96a-c9b85ce91018
Hospitali ya Meta tayari imetekeleza maagizo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ya kutoa kipaumbele kwa wazee wote nchini wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma.
974627cc-137b-436b-996a-f364952f7580
Waziri Ummy akiwasalimia wazazi waliolazwa kwenye moja ya wodi Hospitali ya Meta kutokana na ufinyu wa wodi inawalazimu akinamama wengine kulala chini hospitali hiyo inatarajia kuanza ujenzi wa jengo jipya ambalo litaondoa msongamano wa wazazi hospitalini hapo.
5b44d003-a727-495c-bde5-dea332ef407f
Waziri wa Afya akiwasalimia wagonjwa waliofika Hospitali ya Uzazi ya Meta kupata matibabu.

MCHEZAJI KANU WA NIGERIA AMBAYE NI BALOZI WA KAMPUNI YA STARTIMES ATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WA SHULE YA MSINGI YA MAJI MATITU MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

April 09, 2016
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu (wa pili kushoto), akitoka kusaini  kitabu cha wageni katika Shule ya Msingi ya Majimatitu baada ya kufika shuleni hapo leo asubuhi kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu wanao soma kwenye shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi. Wengine ni walinzi wake.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi, akimkaribisha mchezaji huyo shuleni hapo. Kutoka kulia ni Mwalimu Shabani Msabaha wa shule hiyo, Mchezaji Kanu na Makamu Rais wa Kampuni ya StarTimes, Zuhura Hanif.
Mchezaji Kanu akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kukabidhi msaada huo.
Hapa Kanu akimkabidhi msaada wa sabuni ya unga Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi.
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wazazi wa watoto wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Kanu akitoa msaada wa magodoro.
Kanu akitoa msaada wa vyombo vya jikoni kwa wanafunzi hao.
Hapa Kanu akikabidhi unga wanafunzi hao. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha watoto hao, Rehema Lemway na kulia kwake ni Mlezi wa watoto hao, Somoe Said Omary.
Kanu akiwakabidhi wanafunzi hao Luninga.
Kanu akiwa katika picha ya pamoja na watoto hao.
Kanu akishiriki kucheza na watoto hao wakati wakitoa burudani.
Kanu akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa watoto hao.
Hapa Kanu akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule hiyo.

(
Waziri Ummy Mwalimu azindua Duka la Dawa la MSD Kanda ya Mbeya

Waziri Ummy Mwalimu azindua Duka la Dawa la MSD Kanda ya Mbeya

April 09, 2016

0f5c4672-9fd5-4bcf-87cc-9862e000a1c2
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amefanya uzinduzi wa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa Kanda ya Mbeya.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema uzinduzi wa duka hilo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Magufuli kuwatia wananchi huduma bora na kwa gharama nafuu.
“Neema hii imekuja kwa kipindi cha Rais Magufuli, sasa amekidhi matakwa na shauku ya wananchi wa Mbeya kwa kuwapa duka la dawa,
“Sera ya huduma ya afya inataka wananchi wachangie isipokuwa wazee, watoto na wajawazito na kupitia duka hili wananchi wataweza kupata dawa kwa gharama nafuu,” amesema Mhe. Mwalimu.
Duka hilo la dawa la Kanda ya Mbeya limetumia Shilingi Milioni 13 kwa ukarabati wa jingo na vifaa vyake.
0f5c4672-9fd5-4bcf-87cc-9862e000a1c2
Mh.Ummy Mwalimu akionesha moja ya dawa inayouzwa dukani hapo kwa shilingi 7,000 ambapo kwenye maduka binafsi inauzwa shilingi 25,000,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurine Bwanakunu na kulia ni Mfamasia wa duka hilo, Cornel Mkeng'e
2ff7c78a-1555-486b-93f6-19118e784a78
Mfamasia wa Duka la Dawa, Cornel Mkeng'e akitoa maelezo kwa Mh.Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua duka hilo
7a1d5446-ae11-4b37-946b-337d47d8e85c
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiangalia jinsi ya ufungashaji wa dawa kwenye ghala jipya la Kanda ya Mbeya.ghala hilo limelozinduliwa leo jijini Mbeya
18f8ebf2-a48e-4f8d-ae8a-99ce5c23f6ac
Duka la Dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Kanda ya Mbeya ambalo litahudumia mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi.
e38d5120-d82d-496e-85f2-e82f53d9dcbb
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelezo jinsi ya utunzaji dawa kwenye ghala hilo.