Shirika la Nyumba la Taifa lakabidhi mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana Kigoma

September 30, 2014

 Meneja wa Mkoa NHC, Nistas Mvungi akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya mashine 32 za kufyatulia matofali ya kufungamana.
  
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji akishukuru Shirika kwa kuwapatia vijana mashine ya hydraform.
  
Wafanyakazi wa NHC na kikundi cha Vijana Kwanza Group  na wageni waalikwa wakisubiria Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Mhe Kanali Issa Machibya.
 Meneja wa Shirika la Nyumba Kigoma Ndg Nistas Mvungi akijadiliana na Mkuu wa Mkoa Mhe Issa Machibya jambo kuhusiana na Mashine ya matofali ya kufungamana kuhusu ufanisi wake na ajira kwa vijana.
 Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Shirika Mkoa wa Kigoma na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Mhe Kanali Issa Machibya.
 Meneja wa Shirika la Nyumba Ndg. Nistas Mvungi akihutubia wananchi wa Kigoma kuhusu mradi wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana 32 zilizotolewa na Shirika kwa vikundi vya  vijana wa Mkoa wa Kigoma
 Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno akikabidhi mashine za kufungamana kwa Kikundi cha Vijana Kwanza Group. Mwenyekiti wa kikundi Ndg Daniel George  na Katibu wake wakipokea mashine.
 
  Picha ya pamoja ya kikundi cha vijana kwanza group na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa. 
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ramadhani Maneno kwa makini kuhusiana na maelekezo yake kuhusu umuhimu wa kutumia matofali ya kufungamana na kuondokana na nyumba za matope.

SERIKALI MKOANI TANGA YACHUKUA TAHADHARI MLIPUKO WA UGONJWA WA EBOLA

September 30, 2014


Afisa Afya kutoka Hospitali ya Bombo Bw. Said Ibrahim akifundisha kwa vitendo jinsi ya uvaaji wa mavazi na vifaa maalumu wakati wa kutoka huduma ya kitabibu kwa mgonjwa wa Ebola . Aliyevaa mavazi maalumu ni Dr Nakiete Mchomvu.
SERIKALI  imetoa rai kwa wananchi kutoa taarifa kwa mgonjwa yeyote mwenye  dalili ya ugonjwa wa Ebora ili aweze kupati msaada wa kitabibu hali ambayo itapunguza maambuzi kwa watu wengi .
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga wakati akifungua kikao cha maelekezo huhusu ugonjwa hatari wa Ebola na dhana ya ushirikiano baina ya Sekta binafsi na Sekta ya Umma kwa madaktari na wauguzi kutoka serikalini na sekta binafsi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Rodasaksa Hospiali ya Mkoa wa Tanga (Bombo).
Kikao hicho ni moja ya jitihada ambazo zinachukuliwa na Mkoa wa Tanga katika kutoa uelewa  wa ugonjwa huo hatari ambao sasa  umekuwa tishio katika baadhi ya maeneo ya Afrika.  Vile vile ametoa wito kwa sekta ya umma na sekta binafsi kuweka nguvu zao pamoja katika kuhakikisha wanachi wanapata huduma bora za afya.
Akielezea mkakati wa Mkoa dhidi ya jinsi gani Mkoa umejiandaa endapo atapatikana mgonjwa wa Ebola katika Mkoa wa Tanga,Mganga  Mkuu wa Mkoa  wa Tanga Dr Asha Mahita amesema kuwa tayari maeneo mbalimbali yenye vifaa maalumu yametengwa ili kutoa huduma ya kitabibu kwa wagonjwa wa aina hiyo. Maeneo hayo ni pamoja na eneo la Masiwani lilipo jengo la Hospitali ya Wilaya ya Tanga na kituo kingine kipo Mpakani Horohoro.
Serikali pia imekuchukua tahadhali katika maeneo ya mpakani hasa eneo la Horohoro  mpaka wa Tanzania na Kenye na uwanja wa ndege kwa kuweka kifaa maalumu cha kuweza kupima na kutambua msafiri mwenye maambukizi ya  Ugonjwa wa Ebola. Hatua ambayo imefikiwa baada ya kusikia kuwepo mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi za jirani na hasa Afrika.
Akifafanua dhana ya ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kutoa huduma za afya, Dr.Samweli Ogillo ambaye ni Mtendaji Mkuu kutoka Chama cha Watoa huduma Binafsi za Afya Nchini ( APHFTA)amesema ni jambo la msingi iwapo Serikali na Sekta binafsi zitaweka nguvu ya pamoja ili kudhibiti na kuzuia ebola kuingia nchini kwa sababu upande mmoja peke yake hauwezi.
Hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote mwenye dalili ya ugonjwa wa Ebola ambaye ameripotiwa kupatikana katika nchi ya Tanzania.  Historia inaonyesha mwaka 2012  Mwezi wa Julai ulitokea mlipuko wa ugonjwa wa Ebola  magharibi mwa Uganda eneo linaitwa Kabaale ambapo zaidi ya watu 14 walipoteza maisha.
Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalamu “Ebola Virusi na husambaa kwa haraka sana . Dalili zake ni pamoja na homa kali inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama pua, njia ya haja kubwa na ndogo, mdomoni, machoni kutapika na kuharisha damu.

DSCO4681Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dedengo akifungua rasmi kikao hicho .Kulia  ni Mganga Mkuu Mkoa waTanga Dr Asha. Mahita na Mtendaji Mkuu kutokaChama cha Watoa Huduma binafsi za Afya Nchini, Dr. Samweli Ogillo.

Afisa Afya Mkoa wa Tanga Bw. Magoma akitoa maelezo juu ya ugonjwa wa Ebola
 
Wajumbe wa Kikao wakisikiliza kwa makini
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita akizungumza na wajumbe muda mchache  kabla ya Mgeni rasmi kufungua kikao rasmi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dedengo na kulia na Mtendaji Mkuu Kutoka Chama Cha Watoa Huduma Binafsi za Afya, Dr Samweli Ogillo
Mtendaji Mkuu kutoka Chama Cha Watoa Huduma Binafsi za Afya Dr Samweli Ogillo akitoa dhana ya ushirikiano baina ya sekta Binafsi na Sekta ya Umma katika kuboresha huduma za afya. Kushoto ni Mganga Mkuu Mkoa wa Tanga Dr Asha Mahita  na Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dendego.
Picha ya pamoja ya wajumbe na mgeni rasmi,Picha na Stori kwa hisani ya tovuti ya mkoa wa Tanga.
 UPIGAJI KURA WA RASIMU INAYOPENDEKEZWA WAENDELEA LEO BUNGENI MJINI DODOMA.

UPIGAJI KURA WA RASIMU INAYOPENDEKEZWA WAENDELEA LEO BUNGENI MJINI DODOMA.

September 30, 2014

PICHA 1Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 2 
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Hassan Suluhu akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 3 
Makamu wa Pili wa Zanzibar ambaye pia Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Seif Ali Idd akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 4Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Andrew Chenge akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 5 
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati namba Tano ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Asha-Rose Migiro akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 6 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fenella Mukangara akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 7 (2) 
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Juma Nkamia akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
8 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Ummy Mwalimu akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
9Waziri wa TAMISEMI ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Hawa Ghasia akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
10 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Shymar Kwegir akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

NSSF YATOA FURSA KWA WAKAZI WA MBEYA NA SONGEA

September 30, 2014

Kupitia Semina za Fursa zinazoendelea kufanyika katika mikoa mbali mbali hapa nchini, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imekuwa ikitoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi na kuwahamasisha kujiunga na mfuko huo ili waweze kunufaika na mafao ya NSSF hususani matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi wake pamoja na mikopo kupitia SACCOS.

Fursa nyingine kutoka NSSF ambazo mwanachama anaweza kunufaika nazo ni pamoja na Pensheni ya uzeeni, Pensheni ya Ulemavu, Pensheni ya Urithi, msaada wa Mazishi, Mafao ya Uzazi, mafao ya Kuumia Kazini.

Semina hizi zinatoa fursa kwa wajasiriamali, wakulima pamoja na watu mbalimbali waliojiajiri wenyewe na kuuliza maswali mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na NSSF na wengi hujiuga na NSSF baada ya kuona faida zake.

"Katika semina za Fursa NSSF inafanya uandikishaji wa wanachama wapya na pia inatoa nafasi kwa wananchi kuuliza na kufahamu mambo mbali mbali yanayohusu mfuko huo" alisema Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba.

Mpaka sasa NSSF imeshiriki katika Semina ya Fursa  katika mikoa ya Geita, Ruvuma, Mbeya na Morogoro. 
 Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba akitoa mada katika semina ya Fursa kuhusu Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi na kuwahamasisha wajiunge na mfuko huo ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa na NSSF hususani Matibabu Bure kwa mwanachama na wategemezi wake pamoja na mikopo kwa wanachama kupitia Saccos. Semina hiyo ilifanyika mkoani Mbeya hivi karibuni.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba (katikati), Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba (wa tatu kutoka kulia) wakiwa meza Kuu pamoja na wageni wengine wakati wa Semina ya Fursa iliyofanyika mkoani Mbeya.
 Baadhi ya umati wa wakazi wa Mbeya mjini wakifuatilia kwa makini Semina ya Fursa iliyofanyika katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa mjini Mbeya.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba akitoa mada katika semina ya Fursa Mbeya iliyodhaminiwa na NSSF kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi wakazi wa Mbeya.
Afisa Matekelezo wa NSSF, Ally Mkulemba akitoa mada kuhusu faida za kujiunga na NSSF kwa wakazi wa mjini Songea wakati wa Semina ya Fursa iliyofanyika mkoani Ruvuma.
Msanii wa Bongo Fleva Mwasiti Almasi akiwasihi wakazi wa Songea wajiunge na NSSF ili waweze kupata Fursa ya kujikwamua kimaisha kupitia mafao mbali mbali ya NSSF kama Mikopo kupitia Saccos, Matibabu Bure, Pensheni ya uzeeni, pensheni ya ulemavu, pensheni ya urithi, msaada wa mazishi, mafao ya uzazi, mafao ya kuumia kazini. 
Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba (kushoto) wakifuatilia kwa makini semina ya Fursa iliyofanyika Songea mkoani Ruvuma.

STAND UNITED YAPANIA KUBAKI LIGI KUU MSIMU UJAO.

September 30, 2014

TIMU ya Stand United imesema kuwa malengo yake makubwa msimu huu katika Michuano ya Ligi Kuu soka Tanzania bara ni kuhakikisha wanapambana vilivyo ili kuweza kubaki kwenye ligi hiyo.
Mkurugeni wa Ufundi wa timu hiyo, Muhibu Kanu aliyasema hayo mara baada ya kumalizika mechi yao na Mgambo Shooting ya Tanga ambapo Stand United iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 bao likifungwa na Mussa Said dakika ya 13.

Kanu alisema kuwa kilichopelekea wao kupata ushindi kwenye mechi hiyo ni kutokana na kufanyiwa kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi yao dhidi ya Ndanda ya Mtwara ambapo timu hiyo ilifungwa mabao 4-1.

Alisema hivyo walipoingia kwenye mechi hiyo walikuwa na umakini mkubwa wa kuhakikisha wanafanya vizuri kwa ajili ya kuipeperusha vyama bendera ya mkoani kwao Shinyanga na viongozi wao ambao wamekuwa wakiwasapoti mara kwa mara.

Hata hivyo alisema kuwa wanatarajia kufanya vizuri kwenye mechi yao inayofuata ambapo wao watacheza na Coastal Union kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni muendelezoi wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

Kwa upande wake, Kocha wa Mgambo Shooting, Bakari Shime amesema kuwa kilichopelekea wao kushindwa kuutumia vema uwanja wao wa nyumbani ni makosa madogo madogo yaliyofanywa na wachezaji wake.

Shime alisema kazi kubwa aliyopo mbele yake ni kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mechi yao inayofuata.

WAWILI WANUSURIKA KIFO AJALI YA LORI LA MIZIGO”

September 30, 2014
Picha namba moja mpaka sita ni Gari aina ya Scania lenye namba za usajili T.545 ANG lililokuwa limebaba chokaa ikipelekwa nchini Kongo likiwa limepiduka karibu na eneo na Mizani Majani Mapana jijini Tanga
juzi,ajali hiyo ilitokea  wakati wa gari hilo likitaka kuingia mizani ambapo dereva alipotaka kurudi nyuma akaingia kwenye mtaro baada ya tela kuyumba dereva na utingo wake walisalimika katika tukio hilo
ambalo lilitoka jana saa kumi na moja jioni,



DEREVA wa Lori na Utingo wake wamenusurika kifo baada ya lori aina ya Scania waliliokuwa wamepanda kupinduka eneo la Mizani jijini Tanga wakati likitoka na kuelekea nchini Kongo likiwa limepakia Chokaa baada ya kumaliza kupima.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai alithibtihisha kutokea tukio hilo ambapo alisema kuwa baada ya kumaliza kupima uzito wakati lori hilo lilirudi nyuma lilipitiliza na hatimaye kuingia mtaroni mkubwa wa kupitisha maji uliopo pembezoni mwa reli na kupinduka.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa kumi na moja jioni ambapo
alisema kutokuwa makini kwa dereva huyo ndio kulipelekea ajali hiyo ambapo utaratibu lori hiyo kupelekwa kwenye kituo cha Polisi Mabawa kwa ajili ya taratibu nyengine unaendelea.

Alimtaja utingo wa lori hilo kuwa ni Emanuel Kwai ambaye aliweza
kunusurika kwenye ajali hiyo yeye pamoja na dereva wake ambaye jina lake halikuwepo kupatikana mara moja.

Aidha, Kamanda Kashai alitoa wito kwa watu wanaotumia vyombo vya moto kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani ili kuweza kuepuka ajali zisizo za ulazima ambayo wanaweza kukutana nazo.

Hata hiyo aliwaonya madereva hao kuacha kuendesha magari mwendokasi kasi kwa sababu hali hiyo huchangia asilimia kubwa ongezeko la ajali ambazo wakati mwengine hupelekea kupoteza maisha ya wananchi pamoja na mali zao

26 WAITWA TAIFA STARS KUIVAA BENIN

September 30, 2014

Wachezaji 26 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kocha Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Wachezaji walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).

Mabeki ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).

Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba).

Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).


BONIFACE WAMBURA
MKURUGENZI WA MASHINDANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

WAWILI WAFARIKI DUNIA TANGA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI”

September 30, 2014



WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Tanga ambapo tukio la kwanza lilitokea kijiji cha Katurupesa kata ya Kwemkwazu wilayani Lushoto mkoani hapa kwa mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 ambaye hakufahamika jina wala mahala anapoishi amegundulika amefariki dunia na mwili wake ukiwa umesogezwa kwenye kalvati la Daraja ikiwa baadhi ya viungo vyake sehemu ya kichwani sehemu za siri vikiwa vimeondolewa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai alithibitisha kutokea tukio hilo ambapo alisema limetokea Septemba 26 mwaka huu saa nane mchana eneo ha Katurupesa Kwemkwazu wilayani Lushoto mkoani Tanga ambapo mwili huo uligunduliwa na baadhi wa wasamaria wema.

Alisema baada ya polisi kupata taarifa hizo walifanikiwa kufika eneo la tukio ambapo waliuchukua mwili na kwenda kuuzikwa na wananchi baada ya uchunguzi wa daktari kufanyika.

Kamanda Kashai alisema kuwa chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na watuhumiwa kuhusiana na tukio hilo bado hawajakamatwa wakati juhudi za upelelezi ukiwa unaendelea ili kuweza kuwabaini wahusika.

Tukio la pili lilitokea Kijiji cha Kwangahu Kata ya Mkata Tarafa ya Mazingira wilayani Handeni lilihusisha mwendesha pikipiki Kiduo Rajabu (35) Mzigua akiwa anaendesha pikipiki yenye namba T.813 CAM aina ya Fekon akiwa amempakia Amiri Bakari (65) Mzigua mkulima wote wakiwa ni wakazi wa Mkonga wakielekea porini kuwinda wanyama na kila mmoja akiwa amebeba silaha yake aina ya Gobole.

Alisema kuwa walipofika kilima cha Lugala pikipiki ilishindwa kupanda mlima huo na kuanza kurudi nyuma na kuanguka chini ambapo katika tukio hilo silaha aliyokuwa ameibeba dereva alifyatua na kwa kuwa ilikuwa na baruti gololi na ilimjeruhi abiria Amiri Bakari ubavu wake wa kushoto na kusababisha kifo chake.

Kamanda Kashai alisema kuwa mtuhumiwa katika tukio hilo amekamatwa na upelelezi wa kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea.