MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA MTANDAO WA VYAMA VYA WAZEE TANZANIA

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA MTANDAO WA VYAMA VYA WAZEE TANZANIA

April 30, 2016

wa1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake  bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
wa3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake  bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)wa2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake jijini bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MWENYEKITI WA MTAA ATAKAYESHINDA KWA KUFANYA USAFI KATIKA MTAA WAKE KUIBUKA NA MILIONI 50.000.000

MWENYEKITI WA MTAA ATAKAYESHINDA KWA KUFANYA USAFI KATIKA MTAA WAKE KUIBUKA NA MILIONI 50.000.000

April 30, 2016

????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mwanamuziki Diamond Plutnamz pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Clods FM Bw. Ruge Mutahaba wakati wa matembezi ya mshikamano kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya usafi wa jiji la Dar es salaam itakayofanyika kwa siku 90 ikishirikisha wenyeviti wa mitaa,  wananchi katika maeneo yao, Taasisi za Serikali na Mashirika Binafsi ili kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa safi kabisa.
Makonda amewaambia wananchi mara baada ya matembezi hayo kwamba Dar es salaam bila uchafu inawezekana na amenzisha shindano kwa wenyeviti wa mitaa iliyopangwa na isiyopangwa mwenyekiti atakayeshinda kwa usafi katika eneo lake atajishindia shilingi milini 50.000.000 na mwenyekiti atakayekuwa wa mwisho katika eneo lake atapata nafasi ya kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na uchafu uliopo katika eneo lake na wananchi wake na pia mazingira hayo machafu yataonyeshwa yakiambatana na picha za mwenyekiti huyo.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Radio Clods Bw. Ruge Mutahaba na Mwanamitindo Millen Magesse ambaye pia ameshiriki kikamilifu katika kampeni hiyo
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti Radio Clods Bw. Ruge Mutahaba na Mwanamitindo Millen Magesse ambaye pia ameshiriki kikamilifu katika kampeni hiyo
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiongozana na Diamond Plutnamz huku ulinzi ukiwa umeimarishwa wakati wa matembezi hayo yaliyofanyika leo kwa ajili ya kuhamasisha wakazi wa jiji la Dar es salaam kufanya usafi katika maeneo yao.???????????????????????????????????? 
Haya ni miongozi mwa matukio yaliyojiri wakati wa matembezi hayo ya kuhamashiwa wakazi wa jiji kufanya usaifi ambapo kampeni maalum ya siku 90 za kufanya usafi zimezinduliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Wapiga picha waliendelea na ubunifu wa kutafuta picha nzuri kama wanavyoonekana hapa kwenye picha wakiwa kwenye pikipiki wakipiga picha katika matembezi hayo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya washiriki wa matembezi hayo wakifanya mazoezi mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambako ndiko kampeni hiyo ilikozinduliwa.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akishiriki katika mazoezi hayo mara baada ya mtembezi hayo kuwasili katika viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akisalimiana na viongozi wa dini waliofika katika uzinduzi wa kampeni hiyo ambao ni Sheikh Mkuu wa Dar es salaam Sheikh  Alhadi Mussa Salim na  Askofu  David  Mwasota kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally  Hapi????????????????????????????????????Kikundicha ngoma kikitumbuia katika uzinduzi huo
12 
Kundi la Yamoto Band likitumbuiza katika zunduzi huo.
13
14 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo wakiwa katika viwanja vya Leaders Kinondoni.
15 
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema, Askofu David Mwasota, Sheikh Mkuu wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi wakiwa katika uzinduzi huo.
16 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika kwenye viwanja vya Leaders mara baada ya matembezi ya kuhamasisha wananchi kufanya usafi katika maeneo yao.
IMG_6078 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wa pili kutoka kushoto na wenyeviti wa wenyeviti wa mitaa kutoka wilaya zote tatu wakifanya ishara ya kufangia ikiwa ni uzinduzi rasmi wa siku 90 za kufanya usafi katika jiji la Dar es salaam kutoka kulia ni Juma Ngemwa Kinondoni, Mbayo Chuma Ilala na Bakiri Makere Temeke.
IMG_6086 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi akizungumza katika uzinduzi huo na kutoa maagizo kwa watendaji na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha wanazingatia na kutimiza malengo kuhakikisha Kinondoni inakuwa safi.
RAIS Dk.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI KATIKA TAASISI MBALI MBALI

RAIS Dk.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI KATIKA TAASISI MBALI MBALI

April 30, 2016

Z1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Salmin Amour Abdalla  kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,
Z3 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Asaa Ahmada Rashid kuwa   Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi
Z6 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw, Mzee Ali Haji  kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi
Z7 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi,Mwanahija Almasi Ali  kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi
Z4 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi,Raya Issa Msellem  kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar  katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Z2  Washauri wa Rais wa Zanzibar ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa kwa Viongozi wa Taasisi mbali mbali Serikali ya Mapinduzi leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. Z5   
Baadhi ya Viongozi mbali mbali Serikali na wananchi waliohuria katika hafla ya kiapo kwa Watendaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi, Z8  
Baadhi ya Viongozi mbali mbali Serikali na Wananchi waliohuria katika hafla ya kiapo kwa Watendaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi walipoapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Alo MOhamed Shein,
[Picha na Ikulu.]

MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ,JAMES MBATIA AKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA WAHANGA WA MAFURIKO.

April 30, 2016
Diwani wa kata ya Kahe ,Rodrick Mmanyi akizungumza baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini,Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya kutembelea kata hiyo kutizama athari zilizotokana na mafuriko.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Kahe wakiwa katika kikao na ujumbe wa Mbunge wa jimbo la Vunjo uliofika katika kata hiyo kwa ajili ya kutoa msaada wa chakula.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya  Moshi,Michael Kilawila akizungumza na kutoa pole kwa wakazi wa kata ya Kahe waliofikwa na maafa yaliyotokana na mafuriko.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini,Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya akizungumza na wakazi wa kata ya Kahe baada kutembelea maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mafuriko.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika kikao hicho kilicho fanyika ofisi ya kata ya Kahe ,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini ,Brigedia Jenerali,Mbazi Msuya,kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila.
Mbunge wa Viti maalum Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Lucy Owenya akitoa salamau za pole kwa wakazi wa kata za Mabogini na Kahe walioathirika na mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.
Sehemu ya Msaada uliotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila akikabidhi mfuko wa Unga kwa baadhi ya wazee katika kata ya Kahe walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akikabidhi Chumvi kwa baadhi ya wazee walioathirika na mafuriko .
Wananchi katika kata ya Kahe wakifurahia pamoja na Wabunge James Mbatia na Lucy Owenya msaada uliotolewa kwa ajili ya kusaidia wananchi walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MAZISHI YA MZEE PIUS MKUNJA YAFANYIKA MKOANI MOROGORO.

April 30, 2016
Mazishi ya Marehemu Mzee Pius Joseph Mkunja (90), aliefariki April 25,2016 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Mkoani Mwanza yamefanyika Mkoani Morogoro. 

Marehemu Mzee Pius amezikwa jana nyumbani kwake Mpanga Kilombero. Alifariki kutokana na tatizo la vidonda vya tumbo lililokuwa likimsumbua. Enzi za Uhai wake alikuwa mfanyabiashara maarufu Mkoani Morogoro.
Katikati pichani juu ni Idda Adam ambae ni mmoja wa Watoto wa Marehemu Mzee Pius, akiwa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika mazishi hayo.

MBATIA AMUONGOZA MKURUGENZI WA IDARA YA MAAFA NCHINI KUTEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA KWA MAFURIKO.

April 30, 2016
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya wakati wakitembelea kijiji cha Mandaka Mnono kujionea athari ya mafuriko,katikati ni Mbunge wa viti Maalum (Chadema)  mkoa wa Kilimanjaro Lucy Owenya. 
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya akimweleza jambo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila (wa tatu kutoka kushoto) wengine ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia,Diwani wa kata ya Mabogini Emanuel Mzava .
Baadhi ya wananchi katika kjiji cha Mandaka mnono ambao mashamba yao yameathirika kwa mafuriko.
Sehemu ya barabara inayounganisha vijiji vya Miwaleni na Mandaka Mnono ikiwa imeharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko.
Usafiri wa pikipiki pekee ndio unatumika kuvusha watu kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.
Hivi ndivyo hali inavyoonekana.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu,Mbazi Msuya akizungumza na wananchi katika eneo hilo lililoharibika vibaya.
Madereva wa bodaboda wakijaribu kupita katika eneo hilo kwa umakini mkubwa.
.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.