MGODI WA BUZWAGI WAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 700 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KAHAMA KAMA MALIPO YA HUDUMA.

August 10, 2016
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya mji wa Kahama, hafla hiyo ilifanyika baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi madarasa ya shule ya msingi Budushi na nyumba za walimu Mwime.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakishuhudia wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi
Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 700
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu wakati wa makabidhiano ya hundi ya malipo ya huduma. 
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma
Baadhi ya wananchi katika wilaya ya Kahama wakishuhudia makabidhiano hayo.

Na Dixo Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.


Mgodi wa Buzwagi umekabidhi wa halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba na kumi na saba (717,276,055/=) ikiwa ni sehemu ya malipo ya kodi ya huduma(service levy) ambayo hulipwa kwa halmashauri hiyo.
 
Akizungumzia malipo hayo ya hundi Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema kiasi hicho ni malipo ya kuanzia mwezi januari hadi juni mwaka huu.
Mwaipopo ameongeza kuwa licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali na kujishughulisha katika kufadhili miradi ya Maendeleo, amesema ipo haja ya Jamii kuilinda na kuitunza miradi hiyo ili iwe na manufaa kwa Jamii nzima.
“Acacia kupitia Mgodi wetu wa Buzwagi tunajivunia kuwa wadau muhimu wa maendeleo wa halmashauli ya mji wa Kahama na serikali kwa ujumla, na tunafarijika sana kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata, ombi letu kwa Jamii zinazonufaika na miradi yetu kuilinda na kuitunza kwa manufaa ya Jamii nzima.”
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea hundi ya kodi ya huduma kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutekeleza miradi ya Maendeleo”
Akizungumza kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.
Mwisho.

NAIBU WAZIRI MPINA ATEMBELEA TAASISI ZA MUUNGANO KWA UPANDE WA ZANZIBAR

August 10, 2016
 Alieyesimama katikati ni Naibu Gavana wa Bank Kuu tawi la Zanzibar Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa Bank hiyo kwa upande wa Zanzibar kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, menejimenti ya Bank Hiyo na Ujumbe wa Naibu Waziri, haupo pichani, Ulipotembelea taasisi hiyo ya muungano, aliyekaa kushoto ni  Bw. N. K. mboje Mkurugenzi wa Tawi hilo kwa upande wa Zanzibar.
 Anayeongea kwa vitendo ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa menejimenti ya Bank Kuu tawi la Zanzibar mara baada ya kutembelea taasisi hiyo ya muungano mjini Unguja.
 Bi Safia Hashim, Mtengenezaji na Muuzaji wa mapambo na sabuni zitokanazo na zao la mwani, mdau anayefadhiliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia COSTECH taasisi ya muungano iliyopo chini ya wizara ya Elimu na Sayansi ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania tawi la Zanzibar, akimuelezea Naibu Waziri Mpina faida na matumizi ya zao la mwani na kuonyesha bidhaa zake katika maonyesho yaliyoandaliwa na taasisi hiyo mjini Unguja wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Mpina.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na baadhi watumishi wa tume ya sayansi tawi la Zanzibar. COSTECH alipotembelea taasisi hiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar. (Picha zote na Habari na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.)

                                                  EVELYN MKOKOI
                                                     AFISA HABARI
                                           OFISI YA MAKAMU WA RAIS
                                            HABARI KUTOKA ZANZIBAR
Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameendelea na ziara yake Mjini Ugunja na kutembelea taasisi za Muungano ikiwa ni pamoja na Bank kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar na Tume ya Sayansi na Teknolojia iliyopo chini ya Wizara ya Elimu na Sayansi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya uwasilishwaji wa taarifa fupi ya utekelezaji wa Bank kuu tawi la Zanzibar, na Naibu Gavana wa Bank hiyo Dkt. Natu Mwamba,  Bw. Mansour  Abdalla  Meneja wa fedha na utawala wa Bank hiyo tawi la Zanzibar alieleza kuwa dhana ya ajira kwa watumishi wa Bank hiyo kwa ni ya upendeleo na kujuana haina ukweli wowote kutokana na sababu kuwa taratibu ajira za Bank hiyo zimewekwa pamoja katika makao makuu ya Bank hiyo jijini Dar es Salaam na huwa nafasi za kazi hutangazwa katika magazeti na wananchi wenye vigezo kupata kazi.
“wananchi wajenge tabia ya kusoma magazeti hasa kwa wale wanaotafuta ajira katika bank hii kwani kazi za hapa huwa zinatangazwa huko na bank inatoa ajira bila upendeleo na kwa upande wa Zanzibar asilimia 48% ya watumishi ni wazanzibari na asilimia inayobakia ni ya upande wa pili wa Muunano.”  Alisisitiza Bw. Mansour.
Akitolea ufafanunuzi suala la mgawo wa asilimia 4.5% ya mapato ya Bank hiyo kwa Zanzibar kama sehemu ya Muungano, Mkurugenzi wa Fedha wa Bank hiyo Tawi la Zanzibar bw. Jamhuri Ngelime alisema kuwa hana Jibu la moja kwa moja kuhusu mgao huo ila serikali hizi mbili za muungano zilikubaliana kuwa asilimia 45% ya faida ya Mapato yote ya Bank hiyo nchini igawiwe kwa Zanzibar, na hivyo sheria ndiyo inavyosema.
Kwa Upande wake Naibu Waziri Mpina, aliitaka Bank hiyo kufanya bidii ili kuhakikisha inafikia malengo ambayo serikali imejiwekea, na kuishauri bank hiyo kuongeza huduma zake za ki bank hasa kwa upande wa Pemba na kuweka masharti nafuu kwa wafanya biashara wenye ma bank, ili kuweza kutoa huduma hiyo na kuondoa gape ya kifedha iliyopo kati ya Unguja na Pemba.
Wakati Huo Huo,
Naibu Waziri Mpina aliitembelea Tume ya Sayansi na Teknolojia tawi la Zanzibar COSTECH na katika majadiliano na watumishi wa tume hiyo Naibu Wazri Mpina alisema kuwa tafiti za kisayansi ni muhimu sana kwa nchi yoyote duniani kuendelea, nchi haiwezi kuingia kwenye Biashara ya Gas na oil bila wana sayansi kufanya tafiti zao.
Na kupongeza mchango wa taasisi hiyo katika jamii, ikiwa ni pamoja na kufadhili wanachuo wanasansi mbali mbali nchini.
Ziara ya Naibu Waziri Mpina Mjini Unguja ilihusisha kutembelea taasisi za Muungano, Kumuwakilisha Mhe. Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika siku ya Kizimkazi alipozaliwa Makamu wa Rais, Pamoja na Kutembelea Ofisi zake zilizopo Tunguu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI MAENEO MBALIMBALI AKIWA NJIANI KUELEKEA MWANZA MJINI

August 10, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanahabari baada ya kuhutubia maeneo mbalimbali akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanahabari baada ya kuhutubia maeneo mbalimbali akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akitoa taarifa fupi kwaRais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla kumualika kuongea na wakazi wa Sengerema akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
 Dkt. Charles John Tizeba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Buchosa na  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi akisalimia wananchi mjini Sengerema kabla Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hajaongea
  Mbunge wa Sengerema Mhe. William Ngeleja akiwashukuru wananchi wa jimbo lake kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jimboni mwake  akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
 Wakazi wa Sengerema wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipozungumza nao  akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Sengerema akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi na wasafiri mbalimbali wa eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa akimsaidia mwanahabari wa ITV kuripoti ziara ya Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na wakazi na wasafiri mbalimbali wa eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Misungwe Mhe. Charles Kitwanga baada ya kuzungumza na wakazi na wasafiri eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwalimu Mstaafu Mama Zena Seif (61) ambaye alimfundisha darasa la tatu wakati akisoma shule ya msingi ya Chato. Hii ni baada ya kuzungumza na wakazi na wasafiri mbalimbali wa eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini. 

 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na wabunge na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Mwanza akiwa katika pantoni MV Misungwi wakati akivuka kuelekea Mwanza mjini.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na wabunge na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Mwanza akitoka kwenye  pantoni MV Misungwi wakati akivuka kuelekea Mwanza mjini.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  wananchi eneo la  Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi.
  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia wananchi eneo la  Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi.

  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia mtoto na mama yake baada ya kuongea na wananchi eneo la  Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi mbalimbali wa Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi. 
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mbunge wa Misungwe Mhe. Charles Kitwanga akimtajia badhi ya changamoto jimboni kwake mbele ya  wakazi  wa Usagara katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya Mstaafu wa Biharamulo akiongea na kumkaribisha  mbele ya  wakazi  wa Usagara katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Mkuu wa Wilaya Mstaafu wa Biharamulo  eneo la Usagara katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wakazi mbalimbali wa Usagara
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi mbalimbali wa Usagara
 Wakazi wa Usagara wakimuaga Rais
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono kuwaaga wakazi mbalimbali wa Usagara
 Sehemu nyingi alikuta wananchi wametanda barabarani wakimtaka awasalimu na kuongea nao
 Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula akiongea na wananchi waliokuwa wametanda barabarani kutaka kumsikia Rais
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Buhongwa nje kidogo ya jiji la Mwanza
  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mamia ya wananchi wa Mwanza waliofurika barabarani kumsubiri
 Palikuwa hapatoshi
 Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anawaambia wananchi kwamba yeye ni Rais wa kila mtu nchini na atawatumikia wote bila kuwabagua
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli huku wakimtaka aendelee kuongea nao
  
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Kila mtu alikuwa na shauku yakumuona na kumsikia Rais
 Wengi walitumia simu zao za mkononi kunasa kila alichokisema
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Wananchi wameziba njia ili kumtaka Rais asiwapite bila kuongea nao
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuongea na wananchi wa Mwanza 
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahakikishia wananchi wa Mwanza kwamba atawatumikia wote bila kujali dini zao, makabila yao wala  itikadi zao za kisiasa
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Msafara unapokaribia katikati ya jiji la Mwanza unakutana na umati mkubwa wa wananchi
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anajikuta hana jinsi bali kuzungumza nao 
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katikati ya jiji la Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuzungumza na wananchi katikati ya jiji la Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katikati ya jiji la Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuzungumza na wananchi baada ya kuwasili katikati ya jiji la Mwanza. PICHA ZOTE NA IKULU