OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAENDESHA MAFUNZO KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI TANZANIA BARA WA MWAKA 2017/18

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAENDESHA MAFUNZO KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI TANZANIA BARA WA MWAKA 2017/18

June 06, 2017
unnamed
Mkufunzi anayesimamia mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 (2017/18 HBS) Sergiy Redyakin akimwelekeza mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) namna ya kujaza dodoso litakalotumika katika utafiti huo unaotarajia kufanyika nchini kuanzia mwezi Agosti, 2017.
1
Baadhi ya Watakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayotolewa na mkufunzi anayesimamia mafunzo hayo Sergiy Redyakin (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 yaliyofanyika hivi karibuni katika makao makuu ya NBS Dar es Salaam.
2
 Baadhi ya watakwimu kutoka NBS wakijifunza namna ya kujaza madodoso kwa njia ya kieletroniki wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 unaotarajia kufanyika nchini kuanzia mwezi Agosti, 2017.
3
 Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Hellen Mtove (wa kwanza kulia) akimhoji mmoja wa wanakaya wakati wa majaribio ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 unaotarajia kufanyika nchini kuanzia mwezi Agosti, 2017.
(PICHA NA EMMANUEL GHULA)
RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA ANNA MGHWIRA KUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA ANNA MGHWIRA KUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO

June 06, 2017
unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia tukio hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akisaini Hati ya Kiapo cha Udilifu kwa Viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akizungumza mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira, Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na viongozi wengine Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira huku Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi pamoja na wakuuu wa Wilaya za Ubungo na Ilala wakipiga makofi
1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira Ikulu jijini Dar es Salaam.
2
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akielekea kwenye gari tayari kabisa kwa kuondoka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
3
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira akiwa amekaa kabla ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

MWILI WAMWANAMUZIKI HALILA TONGOLANGA WAAGWA MAZISHI LEO KIJIJINI MCHICHILA TANDAHIMBA

June 06, 2017

Halila Tongolanga amefariki jana usiku katika hospitali ya Muhimbili. Alikuwa mwanamuziki wa siku nyingi na alifahamika kwanza  kwa wengi baada ya kuanza kusikika kibao chake cha lugha ya Kimakonde cha Kila munu ave na kwao, chenye tafsiri ya ‘Kila mtu ana kwao’ ambacho alikirekodi akiwa bendi ya jeshi ya CTU Monduli, iliyojulikana kama  Les Mwenge. 

Kwa kifupi ni kuwa baada ya hapo aliitwa kujiunga na bendi iliyokuwa mali ya Dr Alex Khalid, iliyokuwa ikiitwa Makondeko Six. Wakati huo Dr Khalid alikuwa na sehemu kubwa ya burudani iliyokuwa pia na ukumbi na ilikuwa inaitwa Makondeko ikawa na bendi ya watu sita hivyo bendi hiyo ikaitwa Makondeko Six. Bendi hii awali ilikuwa ikipiga muziki kwa kufuata nyayo za bendi ya Tatu Nane, lakini Dr Khalid baada ya kuona bendi haina umaarufu kutokana na aina ya muziki iliyokuwa ikipiga, ndipo alipomuita Halila Tongolanga nae akaja na baadhi ya wanamuziki wakajiunga na kuanzisha kundi lililoendelea kutumia jina la Makondeko Six japo wanamuziki walikuwa wengi zaidi ya sita. Na ndipo katika kundi hili lilikuwa na wanamuziki wengine kama Innocent Nganyagwa, Anna mwaole wakaweza kurekodi tena wimbo wa Kila Munu Ave na kwao na kundi kupata umaarufu mkubwa mpaka baada ya kusambaratika kwa Makondeko baada ya kifo cha Dr Alex Khalid, lakini Tongolanga aliendelea kutumia jina la Makondeko.
Baadhi ya wanamuziki waliowahi kufanya kazi na Tongolanga katika kundi la makondeko Six, wakiwa wanasubiri kusafirisha mwili wa mpendwa wao.Toka kushoto, Innocent Nganyagwa, Meneja wa bendi, mpiga solo, Waninga
                       Tongolanga amefanya kazi nyingi za muziki ikiwemo kuwa mmoja wa kundi lililoundwa na wanamuziki wengine mahiri kama Moshi William, Muhidin Mwalim, Huluka Uvuruge, Kandaya na wengine lililojulikana kama Bana mwambe, ambapo waliweza kutoka nyimbo nyingi nzuri sana wakati biashara ya kuuza album ilipokuwa ina faida. Tongolanga ameagwa na wapenzi wa muziki ndugu na marafiki, lakini kulikuwa na uhaba mkubwa wa wanamuziki wenzie katika kundi lililokuja kumuaga mwanamuziki huyu. Waliojitokeza hasa ni wanamuziki wale tu ambao waliwahi kupiga nae katika kundi la Makondeko na Bana Mwambe na wanamuziki wengine wachache wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki John Kitime, Katibu Mkuu wa Chamudara Hassan Msumari. Serikali iliwakilishwa na Katibu Mtendaji wa BASATA.  Katika jambo moja kubwa lililotokea wakati wa kuaga mwili ni kujitokeza kwa balozi wa Msumbiiji Bi Monica Patricio Clemente aliyefika Muhimbili kuaga mwili wa Tongolanga akiwa amesindikizwa na maafisa wengine, na pia Balozi huo alitoa rambirambi zake kama Balozi na alitoa rambirambi kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji. Hili lilikumbusha usemi wa wahenga ‘Nabii hathaminiwi kwao.’ Taarifa zilizopatikana pale ni kuwa Tongolanga alikuwa mtu maarufu sana nchini Msumbiji, na aliyekuwa ni msanii muhimu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nchini humo.
Balozi wa Msumbiji Bi Monica Patricio Clemente akiaga sanduku lililokuwa na mwili wa Halila Tongolanga
Nilipokutana nae kwa mara ya mwisho akiwa kitandani Tongolanda kwa sauti ya uchovu alinambia alikuwa na mengi ya kunambia, wakati tunasubiri taratib kukamilika za kuanza kusafirisha mwili, Innocent Nganyagwa ambaye alikuwa mmoja ya wanamuziki waliotengeneza kundi la Makondeko Six alinambia Tongolanga alikuwa amepanga kufanya onyesho la ‘Usiku wa Makondeko’ na alikuwa na mipango mingine mikubwa ya kufanya kupitia kipaji chake. Pengine ndiyo hayo aliyotaka kunambia Mungu pekee anajua. 
Shukrani za pekee zimfikie Mbunge wa Tandahimba Mheshimiwa Katani Ahmed Katani, kwani kwa juhudi zake Tongolanga alisafirishwa akiwa hai kutoka Ndanda hadi Dar es Salaam kwa matibabu, na pia ndie aliyeusafirisha mwili wa mwanamuziki huyu kwenda Mchichila kwa ajili ya mazishi.
Toka kushoto Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Nyangamale, Balozi wa Msumbiji nchini, Katibu Mtendaji wa BASATA, Mbunge wa Tandahimba Mhe Katani Katani, afisa wa Ubalozi wa Msumbiji
Tongolanga anategemewa kuzikwa kijijini kwao Mchichila kesho Junanne 6 Juni 2017.
Mungu Amlaze Pema Halila Tongolanga 
Mpiga Kinanda Geophrey Kumburu, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, Katibu Mkuu wa CHAMUDATA Hassan Msumari
John Kitime, wanamuziki wa Makondeko Six, Mngereza, KumburuAdd caption

Sanduku alilolazwa Halila Tongolanga likitayarishwa kuingizwa kwenye gari la kusafirisha kuelekea Mcjichila




Sanduku likiingizwa kwenye gari

Imetayarishwa na John Kitime wa www.tanzaniarhumba.blogspot.com