MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA TIBA YA MIFUPA , AJALI NA UPASUAJI WA UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU (MOI) DOKT. OTHUMANI KILOLOMA AFUNGUA MKUTANO WA TATU WA MADAK. WA MIFUPA DAR ES SALAAM

May 27, 2015


  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (kulia) akifungua Mkutano wa tatu  wa Madaktari Bingwa wa Mifupa uliyofanyika katika Taasisi hiyo Dar es Salaa 
Daktari Bingwa wa Mifupa wa Taasisi hiyo Dk. Edmund Ndalama (kulia)  akizungumza na Makt. Bingwa tota Nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania na Marekani ambapo lengo ni kubadilishana ujuzi kwa Nadharia na Vitendo na unatarajia kumaliza  29-Mei 2015 
 Dokt. Zehrabanu Zulfikar akizungumza na Madkt. wakati wa Mkutano huo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (kulia) akisalimiana na Dkt. Bingwa na Rais  wa Fracture Care International  Dkt Lewis Zirkle, ambaye ametoa msaada kwa Hospitali 10 za Tanzania ikiwemo na Taasisi ya Mifupa, ambapo kila chuma kimoja ni Dola 600/= na Moi hadi sasa imesaibiwa Vyuma 4000
 Madkt. wakifatilia kwa makini
 Wakifatilia jambo kwa Umakini mkubwa
 Dkt. Bingwa na Rais  toka Maerkani na Muasisi wa Fracture Care International, Dkt Lewis Zirkle (kulia) akiwa na Dkt. Bingwa wa Taasisi ya Mifupa Moi Dk. Rabi Ndeserua
 Dk. Edmund Ndalama (mbele) akiwa na madkt. Bingwa wa Mifupa wakifatilia jambo wakati wa Mkutano huo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (kushoto) akifatiliajambo wakati wa mkutano huo wa madkt. wa Mifupa  kwenye Mkutano huo wakati alipokuwa akizungumza  Dkt. Bingwa na Rais wa  Fracture Care International toka Marekani na Muasisi  Dkt Lewis Zirkle,
 Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) wakishirikiana na madaktari bingwa
 Makt. wakiwa katika picha ya pamoja Baada ya kufanya Upasuaji wa Mifupa kwa mgonjwa

 Dkt. wa Mifupa Moi Dkt. Billy Haonga akielekeza jambo kwa madkt. Bingwa wenzake toka Nchi mbalimbali    kabla ya kumfanyia mgonjwa mwingine
 Wauguzi wa Taasisi ya Mifupa Moi wakimwangalia mgonjwa kwa ukaribu baada ya kufanyiwa Upasuaji katika Taasisi hiyo
 Dkt. Bingwa na Rais wa  Fracture Care International toka Marekani na Muasisi  Dkt Lewis Zirkle (kulia), akijadiliana na Madkta wenzake kabla ya Kumfanyia mgojwa huyo
 Dkt. Bingwa na Rais wa  Fracture Care International toka Marekani na Muasisi  Dkt Lewis Zirkle (wa pili kushoyo), akijadiliana na Madkta wenzake kabla ya Kumfanyia mgojwa huyo wakipitia Fail lake

 Madaktari Bingwa wa Mifupa wakijisajili kabla ya kuanza Mkutano wao wa Tatu (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa UJIJIRAHAA BLOG
KIKAO CHA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI CHAANZA LEO MKOANI MOROGORO

KIKAO CHA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI CHAANZA LEO MKOANI MOROGORO

May 27, 2015

ns1
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa hotuba ya ufunguzi leo Mei 26, 2015 kwenye Kikao cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini kinachofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
ns2
Wajumbe wa Kikao ambao ni  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchiniwa kifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Joel Bukuku.
ns4
Mshauri Mwelekezi katika Maboresho ndani ya Jeshi la Magereza Nchini, Dkt. Haji Semboja kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha Mada ya Maboresho ndani ya Jeshi la Magereza kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini.
ns5
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja(kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil kwenye kikao  cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini kinachofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
ns7
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(shati jeupe) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini waliosimama nyuma(wa sita kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja(wa tano kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(wa tatu kulia) ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka azindua Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) jijini Arusha

May 27, 2015

 Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka akizungumza wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) jijini Arusha leo,kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa NHIF,Michael Mhando na kulia ni Makamu Mwenyekiti  aliyechaguliwa wa Baraza la Wafanyakazi,Deudedit Rutazaa.
 Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini(NHIF),Michael Mhando akitoa hotuba yake leo wakati wa mkutano wa uchaguzi na uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa mfuko huo.
 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Taifa,Deusdedit Rutazaa akizungumza baada ya kuchaguliwa na kuhaidi kutoa utumishi uliotukuka.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF)wakiimba wimbo wa Mshikamano kuhamasisha umoja na  maslahi bora kazini.
 Wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo.
 Wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo.
 Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya NHIF.
Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Mameneja wa mfuko wa  NHIF.
MAAFISA WA SOKA WAKAMATWA ZURICH

MAAFISA WA SOKA WAKAMATWA ZURICH

May 27, 2015

Maafisa sita wa shirikisho la soka duniani Fifa wamekamatwa katika hoteli moja mjini Zurich,Switzerland. kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Watuhuhumiwa hao ambao wanasemekana kuwa ni pamoja na makamu wa rais wa Fifa,wanashikiliwa wakisubiri kusafirishwa kwenda Marekani.
Shutma hizo zinahusisha rushwa ya takriban kiasi cha dola za Marekani milioni 100 kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20
Wanachama wa Fifa wanakutana mjini Zurich kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka siku ya ijumaa, ambapo rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter anawania muhula wa tano.
Mwana mfalme Ali Bin Al-Hussein wa Jordan,ambaye ndiye mpinzani pekee wa Blatter amesema tukio hilo ni "baya kwa maendeleo ya soka".

 
Rais wa Fifa ambaye anawania muhula wa tano ndani ya shirikisho hilo, Sepp Baltter
Gazeti la New York Times limesema askari kanzu walichukua funguo za chumba cha hoteli kutoka eneo la mapokezi ya hoteli ya Baur au Lac hotel ambayo maafisa hao walikuwa wakiishi na kuingia vyumbani mwao.Gazeti hilo limesema Operesheni hiyo ilifanyika kwa utulivu.
Jeffrey Webb, Mkuu wa shirikisho la Amerika ya Kaskazini na Kati na Visiwa vya Caribbean ametajwa kuwa mmoja kati ya maafisa waliokamatwa.
Maafisa wengine wa Fifa walishuhudiwa na BBC wakisindikizwa na Polisi kutoka kwenye hoteli hiyo ni:
Mkuu wa Shirikisho la soka la Costa Rica, Erduado Li, ambaye alikuwa akitarajia kuwepo kwenye mkutano wa kamati ya Fifa siku ya ijumaa.Wengine ni rais wa shirikisho la Uruguay Eugenio Figueredo,rais wa shirikisho la soka Amerika kusini Conmebol na wa Brazil,Jose Maria Marin,mwanakamati ndani ya Fifa,Polisi walionekana wamebeba mikoba yake kwenye mifuko ya Plastiki.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwa vipi Blatter amekuwa Kiongozi wa Fifa kwa muda mrefu, pamoja na kuwepo kwa ripoti nyingi za vitendo vya rushwa lakini ameendelea kushikilia wadhifa huo.
Wizara ya sheria ya Uswiss imesema katika tamko lake siku ya jumatano kuwa maafisa wa serikali ya Marekani waliwashuku maafisa hao kupokea rushwa ya dola milioni 100, tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa ajili ya michuano ya Amerika ya kati.
Serikali ya Uswiss imesema itaidhinisha haraka kusafirishwa kwao.
Mwanzoni mwa mwezi huu, Blatter alisema anafahamu baadhi ya wafanyakazi wenzake wa zamani walikuwa wakichunguzwa lakini amekanusha kuwa uchunguzi huo ulimhusu pia.
CHANZO.BBC

LIGI KUU YA ZANZIBAR YAENDELEA KUSHIKA KAKSI,MTENDE RANGERS YAKUBALI KICHAPO CHA BAO 1-0 DHIDI YA ZIMAMOTO

May 27, 2015


 Mshambuliaji wa timu ya Mtende akijaribu kumpita beki wa timu ya Zimamoto wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar timu ya Zimamoto imeshinda 1--0


 Mchezaji wa timu ya Mtende Khatib Said (kushoto) na wa Zimamoto Hassan Said wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya Zimamoto imeshinda 1--0
 Mshambuliaji wa timu ya Mtende Ibrahim Hamad, akiwapita mabeki wa timu ya Zimamoto, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya Zimamoto imeshinda 
1--0 
  Wachezaji wa timu ya Zimamoto Ramadhan Abdalla na wa mtende Khamis Said wakiwania mpira
Beki wa timu ya Zimamoto Ramadhan Abdalla na mshambuliaji wa timu ya MtendeRangers Jumanne Seif wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Timu ya Zimamoto imeshinda 1--0.

Kituo cha Sheria Zanzibar (ZLSC) na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAMAZA) Watowa Mafunzo ya Haki za Binadamu na Sheria za Waandishi wa Habari Zanzibar.

May 27, 2015



Mwandhishi wa Habari Muandamizi Zanzibar Bi Maryam Hamdan akifungua Mafunzo ya Haki za Binaadamu na Sheria za SWaadishi wa Habari Zanzibar, mafunzo hayo yamewashirikisha waandishi Waandishi wa Habari mbalimbali Zanzibar, yalioandaliwa na Kituo cha Sheria Zanzibar ZLSC kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAMAZA) yaliofanyika katika ukumbi wa kituo hicho migombani Zanzibar.kushoto Katibu Mtendaji wa Tume ya UtangazajiZanzibar Ndg Chande Omar na kulia Mwenyekiti wa WAMAZA Bi Salma Said
Washiriki wa Semina ya Waandishi wa Habari Zanzibar wakimsikiliza Bi Maryam Hamdan akitowa nasaha zake na Kuwataka waandishi kutumia Kalamu zao Vizuri wakati wa kuriopoti habari kwa wananchi.