MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGWIRAAFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF

February 19, 2018

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira, akifungua mafunzo ya siku tano ya  kufanya tathmini ya Mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini mjini Moshi Februari 19, 2018.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira, amewataka madaktari na watoa huduma za afya, wanaohuduria Mafunzo ya siku tano, (5), ya kufanya tathmini ya Mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi, kuzingatia miiko ya kazi zao wanapotekeleza jukumu hilo.

Mhe. Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo Februari 19, 2018, wakati akifungua mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) na kuwaleta pamoja madaktari zaidi ya 200 wa Kanda ya Kaskazini na kufanyika Mjini Moshi.
Alisema, lengo la Mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo Madaktari ili hatimaye watoe huduma kwa weledi na kwa urahisi kwa wafanyakazi wanaopatwa na madhara wawapo kazini katika maeneo mbalimbali nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba alisema, katika kipindi kifupi toka kuanzishwa kwa Mfuko kumekuwa na mafanikio kadhaa yaliyopelekea kutimiza malengo yaliyowekwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa wataalamu katika masuala ya tathmini ya ulemavu unaotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
Mafunzo haya ya siku tano, (5), yaliyoandaliwa na Mfuko ni sehemu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madaktari wenye ujuzi katika kufanya tathmini ya ulemavu utokanao na ajali na magonjwa yanayosababishwa na kazi.
“Lengo ni kuwa na madaktari wa kutosha kwenye hospitali zetu wenye uwezo wa kufanya tathmini sahihi na kwa wakati pindi mfanyakazi anapoumia au kuugua kutokana na kazi,” alisema Bw. Mshomba.
Alisema, Jukumu la utoaji mafunzo kwa madaktari nchini si dogo na linahitaji uwezo mkubwa wa kifedha. Hivyo, Mfuko utaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali wakiwemo Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika kutoa mafunzo kwa madaktari nchini kuhusu masuala ya tathmini za ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi
Bw. Mshomba pia alisema, Mfuko huu ni mkombozi mkubwa kwa Wafanyakazi, Waajiri na Taifa kwa ujumla, kutokana na ukweli kwamba matukio ya ajali, magonjwa ama vifo yanapotokea sehemu za kazi, licha ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa lakini pia huzorotesha shughuli za uzalishaji katika nyanja mbalimbali za uchumi.
“Hivyo, uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi na utekelezaji wa majukumu yake unalinda nguvu kazi ya Taifa na  kuchochea shughuli za uzalishaji na kuwa chachu katika kukuza uchumi wa viwanda na kuwa nchi ya kipato cha kati kufikia mwaka 2025.” Alisema.
Alizishukuru Taasisi za Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Ocean Raod, Taaisi ya Mifupa (MOI), MUHAS NA OSHA, kwa kuwaruhusu wataalamu wao kushirikiana na WCF katika kutoa mafunzo haya kwa Madaktari.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba ya ukaribisho kwenye mafunzo hayo.
Bw. Mshomba akitoa hotuba yake
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba za ufunguzi kabla ya kuanza kupata elimu juu ya tathmini kwa mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi
 Wawezeshaji (watoa mada), stari wa mbele wakisikiliza hotuba za ufunguzi.
 Mkuu wa Mkoa Mhe. mama Anna Mghwira (katikati), Mkuu wa wilaya ya Moshi, Mhe. Kipi Warioba, (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (wakwanza kulia), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Peter Anselim, wakiwa meza kuu mwanzoni mwa mafunzo hayo.
 Kiongozi wa timu ya wataalamu, Dkt. Peter Mhina, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 Mkuu wa kitengo cha Sheria, WCF, Bw.Abraham Siyovelwa, akipitia machapisho ya kisheria kabla ya kutoa mada.
 Bw.Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu sharia mbalimbali zinazosimamia Mfuko katika uendeshaji wake.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Laura George, (kulia), akiteta jambo na Dkt. Pascal kutoka kitengo cha Tiba na Tathmini.
Dkt. Abdulsalaam, akifafanua masuala mbalimbali kuhusu vigezo vinavyotumika katika kufanya tathmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Peter Anselim, akitoa mada kuhusu uendeshaji wa Mfuko.
Mshiriki akitumia laptop kunakili kilichokua kikizungumzwa.
Bw. Mshomba, (kushoto) na Dkt.Hussein, (katikati), wakimsikilzia Bw.Anslem.
Mhe. Mamam Anna Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akipokewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha wakati akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Lutheran Uhuru mjini Moshi, tayari kufungua mafunzo hayo.
Mhe. Mamam Anna Mghwira, akipeana mikono na Dkt. Abdulsalaam, mara baaya ya kufungua mafunzo hayo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kipi Warioba.
Bw. Mshomba akiwa na Dkt. Abdulsalaam wakati wakimpa taarifa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Mama Anna Mghwira, ofisini kwake kuhusu magfunzo hayo ya madaktari.
Bw. Mshomba akiwa na Dkt. Abdulsalaam wakati wakimpa taarifa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Mama Anna Mghwira, ofisini kwake kuhusu magfunzo hayo ya madaktari.
Bw. Mshomba akiongozana na Dkt. Abdulsalaam wakati wakitoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mjini Moshi.
Piacha ya kwanza ya pamoja na mgeni rasmi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Picha ya kwanza ya pamoja na mgeni rasmi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Khalfan Said Chief Photographer/Owner K-VIS MEDIA P.Box 77807 Mobile; +255 646-453/+255-653-813-033 Office; Mivinjeni Opp.Tanesco, Kilwa RD Blog:http//khalfansaid.blogspot.com Dar es Salaam, Tanzania

DKT KIGWANGALLA AITEMBELEA FAMILIA YA AKWILINA ,ATOA UBANI WA POLE

February 19, 2018
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo ametembelea nyumbani kwa familia ya Akwilina na kutoa ubani wa pole kwa msiba huo.
"Nimefika hapa kama Raia mwema tu ambaye nimeguswa na msiba huu na nimetafakari kwani na mimi kipindi fulani nilipitia chuo hasa kutoka familia zetu hizi masikini kwa hiyo inapotokea ukio kama ili unaona ni pigo kwa familia, pigo kwa jamii, pigo kwa wanafunzi wenzake na pigo kwa Taifa kwa ujumla wake" alieleza Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na vyombo vya Habari msibani hapo.
Dkt.Kigwanalla ambaye alifika msibani hapo majira ya saa saba mchana, aliweza kuungana pamoja na ndugu na jamaa wa wafiwa ambapo pia alipata chakula cha mchana pamoja na waombolezaji wengine sambamba na kutoa ubani wake kama mwananchi mwingine.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli ambaye yupo hapo kwa ajili ya kusimamia shughuli  kwa upande wa Serikali, amebainisha kuwa wataendelea kuratibu baadhi ya mambo yanayoendelea hapo kwani msiba huo kwa namna moja Serikali imeguswa nao.
Mbali na Mkuu wa Wilaya hiyo, Wengine waliofika hapo ni pamoja na Mkurugenzi wa Ubungo, John Kayombo ambapo kwa pamoja na watendaji wengine wa Kiserikali wameweza kusaidiana na familia ya marehemu katika shughuli mbalimbali zinazoendelea msibani hapo.
Aidha, jana viongozi wengine waandamizi wa Serikali akiwemo Waziri Elimu, Mh. Ndalichako, Naibu Waziri wa Ulinzi Masauni na IGP  Siro waliweza kutembelea kutoa pole katika familia hiyo.
Akwilina kabla ya kifo chake alikuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuia maandamano ya chama cha siasa cha CHADEMA. 
Marehemu Akwilina enzi za uhai wake
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa familia ya Akwilina alipotembelea hapo kutoa pole
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akipata taarifa kutoka kwa ndugu Akwilina amabye alikuwa ni mlezi wa binti huyo.
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo
Waombolezaji wakipata chakula cha mchana msibani hapo
Viongozi wa Serikali wakipata chakula msibani hapo
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya ndugu na jamaa walijitokeza katika msiba huo, Mbezi Luis, Jijini Dar e Salaam
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio hilo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akizungumza na wanahabari wakati wa tukio hilo
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio hilo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akizungumza na wanahabari wakati wa tukio hilo.









--

Andrew Chale

Blogger Personality | Journalist | Activist | CEO & Online Editor BONGONEWS | Comedian |Volunteer Red Cross | Sauti za Busara & ZIFF Festivals 2007 to present.


Telephone: +255767076376
Golden Jubilee Towers, Ohio Street, 6th Floor
Po Box  Dar es Salaam,Tanzania

DIAMOND PLATNUMZ AITWA NA NYOTA YAJAA GOME

February 19, 2018


Na Richard Mwaikenda, Goms

MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Bakari Omari Bwere 'Nyota ya Yajaa' amesema anatamani akutane na msanii nguli Abdul Naseeb 'Diamond Platnumz' ampige tafu ili asonge mbele kimuziki kama alivyo yeye.

Nyota ya Yajaa ambaye yuko mbioni kuibua kibao chake kipya cha Nisharizia , amesema anafanya mipango ya kumuona Diamond ili amsaidie kumvusha katika hatua aliyopo kwenda kwenye mafanikio.

Msanii huyo ambaye makazi yake yako Gongo la Mboto (Goms) ana ndoto ya siku za mbeleni kuwa mmoja wasanii maarufu Tanzania na nje ya nchi, kama alivyo Diamond.

Hivi sasa yupo mbioni kuachia video ya wimbo wa Nimerizia aliofanya pamoja na PNC wenye vionjo vya mapenzi baada ya kuachia audio siku ya Valentine Day.

Nyota Yajaa ambaye yupo chini ya usimamizi wa NYOTA ENTERTAINMENT, ambayo ipo chini ya umiliki wa nyota yajaa mwenyewe,

Ameahidi makubwa kupitia video hiyo inayokuja akiamini italeta ushindani mkubwa kwenye soko la muziki nchini Tanzania, Pia amezungumzia ujio wa wimbo wake mpya utakayofuata baada ya Nisharizia.

Nyota yupo mbioni kufanya Kolabo wasanii wakubwa wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Tanzania, Nyota alidai nimapema sana kuzungumzia kolabo hiyo na Mkali huyo wa miondoko ya Bongo fleva nchini Tanzania. 

kikubwa alisema mashabiki wakae mkao wa kula kwani hata waangusha.

Mbali na muziki NYOTA ENTERTAINMENT pia inasimamia kazi za maigizo za nyota yajaa na wasanii wengine chipukizi waliopo ndani  ya Lebo hiyo.

Nyota yajaa amefanikiwa kuachia filamu kama NIPE RISITI,MAPENZI MAJINI,KUTEKWA KWA ROMA,KABAKA KUKU, JINSIA GANI, N.K.

Akishirikiana na wasanii wakongwe kama Mzee Majanga, Ringo, Dula Matenda,N.k.

Kutazama Kazi za NYOTA ENTERTAINMENT BONYEZA HAPA https://www.youtube.com/channel/UCWFfp-FHOkG5rUaFWSotRbg

TAKUKURU TANGA YAPOKEA TAARIFA 204 ZA VITENDO YA RUSHWA

February 19, 2018
 Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Christopher Mariba wakati akitoa taarifa za utendaji wao kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2017.

 Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua matukio
 Sehemu ya wanahabari mkoani Tanga wakifuatilia matukio katika mkutano huo
 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Tanga (Takukuru) imepokea taarifa 204 za vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi wakizilalamikia idara mbalimbali za serikali na sekta binafsi.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Christopher Mariba wakati akitoa taarifa za utendaji wao kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2017.

Alisema taarifa hizo ni ongezeko la taarifa 30 sawa na asilimia 17 ukilinganisha  na kipindi cha miezi sita iliyopita ambapo taarifa zilizo pokelewa ni 174.

Aidha alisema katika taarifa hizo 52 zilihusu serikali za mitaa, ardhi/ mabaraza ya ardhi 33,vyama vya siasa 28,Polisi 23,Elimu 18,Mahakama 16,Afya 15,Kilimo 8,Tasaf 5,Bandari (TPA) 1,Maji 1,Ushirika 1,Uhamiaji 1,Tanesco 1 na Misitu 1.

Mkuu huyo alisema kati ya taarifa hizo 204 zilizopokelewa taarifa 92 zinaendelea kuchunguzwa wakati nyengine 66 uchunguzi wake ulikamilika na majalada kufungwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi.

Aliongeza kuwa taarifa 46 zilihamishwa kwenye idara nyengine kwa sababu zilikuwa zikihusiana na makosa chini ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Hata hivyo alisema katika uendeshaji wa mashitaka takukuru mkoa wa Tanga imefanya uendeshaji wa kesi 18 mahakamani ambapo kati ya kesi hizo 9 zilifunguliwa kipindi cha Julai 2017 hadi Desemba 2017 na kesi 9 ni za kabla ya Julai 2017.

Alieleza pia katika kipindi hicho usikilizwaji wa kesi moja huko wilayani Lushoto kwa mshtakiwa aliyejulikana kwa jina la Ally Mgovi ambaye alikuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Funta ambapo alifikishwa mahakamani kwa makosa ya ubadhirifu wa pembejeo za ruzuku zilizotolewa na serikali kwa ajili ya wakulima.

Alisema mshtakiwa huyo alipatikana na hatia alihukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Tsh Milioni 1.9 ambapo alishindwa kulipa faini hivyo alipelekwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitatu.

Akizungumzia fedha ambazo zimeokolewa na kazi za uchunguzi na udhibiti ambapo katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2017 kumekuwa na ongezeko la fedha walizookoa na kuzirejesha serikalini kutoka milioni 6,450,000 kwa miezi sita ya mwanzo hadi Milioni 52,508,260.

Alieleza fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya malipo ya wanafunzi hewa ndani ya mpango wa elimu bila malipo katika shule za sekondari,mishahara hewa na gharama kwa ajili ya semina hewa
February 19, 2018


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Tanga (Takukuru) imepokea taarifa 204 za vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi wakizilalamikia idara mbalimbali za serikali na sekta binafsi.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Christopher Mariba wakati akitoa taarifa za utendaji wao kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2017.
Alisema taarifa hizo ni ongezeko la taarifa 30 sawa na asilimia 17 ukilinganisha  na kipindi cha miezi sita iliyopita ambapo taarifa zilizo pokelewa ni 174.
Aidha alisema katika taarifa hizo 52 zilihusu serikali za mitaa, ardhi/ mabaraza ya ardhi 33,vyama vya siasa 28,Polisi 23,Elimu 18,Mahakama 16,Afya 15,Kilimo 8,Tasaf 5,Bandari (TPA) 1,Maji 1,Ushirika 1,Uhamiaji 1,Tanesco 1 na Misitu 1.
Mkuu huyo alisema kati ya taarifa hizo 204 zilizopokelewa taarifa 92 zinaendelea kuchunguzwa wakati nyengine 66 uchunguzi wake ulikamilika na majalada kufungwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi.
Aliongeza kuwa taarifa 46 zilihamishwa kwenye idara nyengine kwa sababu zilikuwa zikihusiana na makosa chini ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Hata hivyo alisema katika uendeshaji wa mashitaka takukuru mkoa wa Tanga imefanya uendeshaji wa kesi 18 mahakamani ambapo kati ya kesi hizo 9 zilifunguliwa kipindi cha Julai 2017 hadi Desemba 2017 na kesi 9 ni za kabla ya Julai 2017.
Alieleza pia katika kipindi hicho usikilizwaji wa kesi moja huko wilayani Lushoto kwa mshtakiwa aliyejulikana kwa jina la Ally Mgovi ambaye alikuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Funta ambapo alifikishwa mahakamani kwa makosa ya ubadhirifu wa pembejeo za ruzuku zilizotolewa na serikali kwa ajili ya wakulima.
Alisema mshtakiwa huyo alipatikana na hatia alihukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Tsh Milioni 1.9 ambapo alishindwa kulipa faini hivyo alipelekwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitatu.
Akizungumzia fedha ambazo zimeokolewa na kazi za uchunguzi na udhibiti ambapo katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2017 kumekuwa na ongezeko la fedha walizookoa na kuzirejesha serikalini kutoka milioni 6,450,000 kwa miezi sita ya mwanzo hadi Milioni 52,508,260.
Alieleza fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya malipo ya wanafunzi hewa ndani ya mpango wa elimu bila malipo katika shule za sekondari,mishahara hewa na gharama kwa ajili ya semina hewa.

NAIBU WAZIRI DK. NDUGULILE AZINDUA BARAZA LA WATOTO MKOA WA SHINYANGA,AKABIDHI OFISI,KOMPYUTA

February 19, 2018
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile leo Jumatatu Februari 19,2018 amezindua Baraza la Watoto Mkoa wa Shinyanga na kukabidhi rasmi ofisi na kompyuta kwa ajili ya baraza hilo. 

MHE BITEKO AAGIZA NDANI YA WIKI MBILI KUFUNGULIWA MGODI WA NYAKAVANGALA MKOANI IRINGA

February 19, 2018
Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018.
Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisikiliza maelezo mbalimbali kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ,mara baada ya kuwasili katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018.
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari Mkoani Iringa wakinasa kumbukumbu muhimu kwa ajili ya kuhabarisha wananchi juu ya ziara ya Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko mkoani humoLeo 19 Februari 2018.
Umati mkubwa wa wachimbaji wadogo katika mgodi wa mgodi wa Nyakavangala uliopo katika Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa wakisikiliza hatma ya mgodi huo kutoka kwa Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika Leo 19 Februari 2018.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko aakikagua mashimo mbalimbali kabla ya kuzungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018. 

Na Mathias Canal, Iringa

Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameagiza kufunguliwa ndani ya wiki mbili mgodi wa Nyakavangala uliopo katika Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa ili kuwarahisishia huduma wachimbaji wadogo za kujiingizia kipato chao.

Mhe Biteko ameyasema hayo Leo 19 Februari 2018 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara Mara baada ya kuwasili mgodini hapo kukagua hatua za kiusalama zilizofikiwa tangu kufungwa kwa mgodi huo 12 Februari 2018 kufuatia matukio matatu ya ajali ambayo yalipelekea vifo vya wachimbaji wanne.

Mhe Biteko akiwa ameambatana na Mkuu Wa Mkoa Wa Iringa Mhe Amina Masenza, Kamati za ulinzi na usalama Wilaya na Mkoa wa Iringa, Mkuu Wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela na wataalamu Wa Madini kutoka Wizara ya Madini ameagiza kuchukuliwa hatua za haraka za kujiridhisha uhakika Wa usalama Wa wachimbaji kuanzia Leo 19 Februari 2018 hadi kufikia 5 Februari 2018 mgodi uwe umeanza uchimbaji.

Alisema kuwa kufunguliwa kwa mgodi huo kutaongeza kipato cha wachimbaji hao huku akisisitiza wachimbaji hao pindi mgodi utakapofunguliwa kuzingatia taratibu za usalama mgodini na kulipa kodi stahiki za serikali.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kuwanufaisha wananchi kupitia rasilimali zao ikiwemo Madini ambapo Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi kwa uchimbaji Madini ilihali wananchi hawanufaiki ipasavyo na rasilimali hiyo.

Mhe Rais Magufuli ametuagiza kuwalea na kuwasimamia wachimbaji wadogo nchini ili kutoka kwenye uchimbaji mdogo na kuwa wachimbaji wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa ili uchumi wa nchi ushikwe na watanzania wenyewe.

Alisema kuwa wachimbaji hao wanapaswa kushirikiana na serikali kuwafichua waovu wanaoiibia serikali rasilimali Madini kwa kuyatorosha kwenda sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi pasina kulipa kodi.

"Jichungeni na kujilinda wenyewe ili kila kinachopatikana serikali ijue imepata kiasi gani na wachimbaji wameingiza kiasi gani na kisemwe hadharani, ndugu zangu Rais anahangaika kuona kila eneo ambalo lina wachimbaji wadogo wana rasimishwa na hatimaye wananufaika na madini yao, lakini bado kuna watu wanatorosha madini" Aliongea kwa msisitizo Mhe Biteko na kuongeza kuwa

"Na Mimi nataka niwaambieni wale wote wanaofikiri katika serikali hii inayoongozwa na Rais Magufuli wanaweza kupenya na dhahabu watafute jambo jingine la kufanya maana jambo hilo limepitwa na wakati"

Alisisitiza kuwa wamiliki wa leseni kote nchini wanapaswa kutunza kumbukumbu za biashara nzima ya madini ikiwemo mapato na matumizi kwa muda usiopungua miaka mitano kinyume na hapo kwa mujibu wa sheria watatozwa faini ama kifungo jela

Kwa upande wake Mhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza alisema kuwa wachimbaji hao wanapaswa kutofanya kazi kwa mazoea huku akisisitiza wachimbaji hao kuwa na ushirikiano na kupendana.

Sambamba na hayo pia aliwasihi kuwa makini na kutofanya ngono zembe kwani matokeo yake ni kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI jambo litakalopelekea kupoteza nguvu kazi katika familia na Taifa kwa ujumla.