ZAIDI YA WAJASIRIAMALI 300 KUSHIRIKI MAONESHO YA NGUVU KAZI/ JUA KALI NCHINI BURUNDI
WAJUMBE WA BODI YA JKCI WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina ambaye pia ni Mratibu wa huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Mkoa wa Rukwa akiongoza kikao cha tano cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge.
Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge akiwaonesha mfano wa jengo litakalojengwa katika Hospitali ya JKCI Dar Group wajumbe wa bodi hiyo wakati wa kikao cha tano cha Bodi kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akichangia mada wakati wa kikao cha tano cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni mjumbe wa Bodi hiyo CPA.Godfrey Kilenga ambaye pia ni Mtendaji Mkuu kutoka ofisi ya TAB Consult Audit Firm Partner.
Baadhi ya Viongozi wa Menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge wakati akitoa taarifa ya utendaji wa kazi zilizofanywa na taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba katika mwaka wa fedha wa 2023/24 wakati wa kikao cha tano cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
- Advertisement -
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Harun Matagane kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akichangia mada wakati wa kikao cha tano cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge akitoa taarifa ya utendaji wa kazi zilizofanywa na taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba katika mwaka wa fedha wa 2023/24 wakati wa kikao cha tano cha Bodi hiyo kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Benki Ya NMB Yasaidia Waathirika Wa Mafuriko Hanang
Waathirika wa mafuriko Wilayani Hanang, Mkoani Manyara, waliopoteza ndugu zao, makazi, pamoja na mali, wamepatiwa misaada ya kibinadamu na Benki ya NMB.
Misaada hiyo inajumuisha magodoro, vyakula na vifaa vingine, ikiwa lengo ni kutoa msaada muhimu baada ya janga hilo.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus, akikabidhi misaada hiyo, amesema benki hiyo inaungana na familia za wahanga na kutoa misaada ya kibinadamu. Msaada huo unalenga kutoa faraja na msaada wa msingi ili kusaidia katika kurejesha hali ya kawaida kwa wahanga wa mafuriko.
Mbunge wa Viti Maalumu, Asia Halamga, ameipongeza benki hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii, hasa kwa wahanga wa mafuriko katika kipindi hiki.Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus (aliyevaa fulana nyeupe), akikabidhi misaada kwa waathirika wa mafuriko Hanang. Anamkabidhi Mbunge wa Vijana wa Hanang, Asia Halamga, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa.
MWENYEKITI WA BODI YA NSSF AFANYA ZIARA YA KIKAZI MAKAO MAKUU YA NSSF
Na MWANDISHI WETU
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Mwamini Malemi, amefanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam, na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na Menejimenti pamoja na wafanyakazi wa Mfuko.
Katika ziara hiyo ya kikazi iliyofanyika tarehe 5 Desemba 2023, Bi. Malemi alikutana na kuzungumza na wajumbe wa Menejimenti ya NSSF, ambapo pamoja na mambo mengine alipokea taarifa ya utendaji kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mkuu, Bw. Masha Mshomba.
Taarifa ya NSSF iliyowasilishwa na Bw. Mshomba ilionesha utendaji mzima wa Mfuko, ikigusia uandikishaji wanachama, uchangiaji, uwekezaji pamoja na ulipaji mafao. Aidha Bw. Mshomba alizungumzia kuhusu uboreshaji huduma kwa wanachama, uboreshaji mifumo na namna wafanyakazi wanavyoshirikiana katika kuhakikisha majukumu ya Mfuko yanakamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza na Menejimenti ya NSSF, Bi. Mwamini alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kushika nafasi hiyo, ambapo aliahidi kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kufikia malengo na matarajio ya Mfuko.
Awali, Bw. Mshomba alimueleza Mwenyekiti huyo matarajio ya Mfuko ikiwemo kuendelea kuboresha huduma kwa wanachama kupitia njia mbalimbali ikiwemo ya matumizi ya TEHAMA kwani hicho ndio kipaumbele muhimu cha NSSF.
Bw. Mshomba alisema matarajio ya Mfuko ni kuona mwanachama baada ya kustaafu na kuwasilisha taarifa zake zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Sheria analipwa stahiki zake ndani ya muda mfupi.
MAJERUHI WA MAFURIKO YA HANANG WOTE WAMETIBIWA MANYARA BILA YA RUFAA.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa uboreshaji wa huduma za afya nchini na kufanya majeruhi wote wa mafuriko ya Hanang kupata huduma Mkoani Manyara bila kupewa rufaa.
“Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuhudumia vyema majeruhi wa mafuriko na kutibiwa bure bila gharama yeyote” amesema Dkt. Tulia.
Aidha ameipongeza Wizara ya Afya na wataalamu wote kwa kazi nzuri waliofanya katika kuwahudumia majeruhi hao na kuwataka wataalam kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi.