WALIOKULA FEDHA ZA USHIRIKA WATAZILIPA-MAJALIWA

WALIOKULA FEDHA ZA USHIRIKA WATAZILIPA-MAJALIWA

July 10, 2017
lod1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaeleza   wananchi wa Kijiji cha Kiangala  jinsi serekali ya awamu ya tano inavyo shughulikia kero za za wananchi Nchini Wananchi hao   walijitokeza July 10, 2017  ili waweze kumueleza kero  zinazo wasumbua  Waziri  yupo Wilayani Liwale Mkoa wa lindi Kwaziara ya Kikazi ya siku Nne 
………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitahusika na ulipaji wa deni la fedha za Ushirika na badala yake kila aliyekula fedha hizo atazilipa mwenyewe.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 10, 2017), wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Liwale katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa wilaya.
Waziri Mkuu ambaye yuko katika na ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, amesema Serikali haiwezi kukubali Ushirika ukafa nchini kwa ajili ya watu wachache wasiokuwa waaminifu.
Amesema watu wote waliopewa dhamana ya kuongoza Vyama vya Ushirika na kuamua kujinufaisha kwa kula fedha za vyama watazilipa.
Waziri Mkuu amewaagiza Viongozi wa Mkoa wa Lindi kufanya ukaguzi katika Vyama vyote vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) ili kubaini ni wakulima wangapi wanadai.
Amesema baada ya kufanya uchunguzi na kubaini idadi ya wakulima wanaodai na kiasi cha fedha wawachukulie hatua wahusika wote kwa mujibu wa sheria.
Awali, Waziri Mkuu alizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale katika Ukumbi wa Tengeneza, ambapo amewataka Watumishi wa Umma Nchini kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Amesema Watumishi wanawajibu wa kuwahudumia Wananchi bila ya kutengeneza mazingira ya kuomba rushwa na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Amesema Watumishi wa Umma wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya kiutumishi jambo litakaloondoa malalamiko kutoka kwa Wananchi.
“Lazima Wananchi waone na wanufaike na kazi inayofanywa na Serikali yao, hivyo ni wajibu wa Watumishi kuwatumikia Wananchi popote walipo na si kukaa maofisini.”
Pia amewataka Watumishi hao kupanga mipango itakayoleta tija kwa Wananchi na si vinginevyo.

WAZIRI MKUU AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAFANIKIO

July 10, 2017
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waiyo hudhuria katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waiyo hudhuria katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na mama Zakia Megji wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea shada la maua wakati akikaribishwa kwenye maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni kwenye maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, (kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani na (kulia) ni muwakilishi wa AKDN Resident Amin Kurji, wakati alipomwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Muwakilishi wa AKD resident Amin Kurji katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli,(katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Aga Khan Suleiman Shabbudin Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta jambo na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani, katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea maandano ya maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee, Waziri Mkuu amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika sherehe hiyo, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

……………………………………………………………..

*Asema nchi ina utulivu wa kisiasa na uchumi unaokuwa kwa kasi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji watakaokuja nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa kisiasa na uchumi wenye kukua kwa kasi.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 09, 2017) alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan alipochaguliwa kuwa Imamu Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.

Ameupongeza mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Nawahakikishia kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na baraka kwa sababu nchi imetulia kisiasa na uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini fursa bado zipo.”

Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya Madhehebu ya Shia Ismailia Tanzania, Bw. Amin Lakhani ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa na kwamba ameahidi kuendelea kushirikiana nayo katika kuboresha sekta mbalimbali nchini.

Amesema mtandao wa maendeleo wa Aga Khan unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za afya, elimu, kilimo na kunaendesha miradi katika mabara ya Afrika na Asia kwa kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili kujikwamua kiuchumi.

Awali, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema aliipongeza taasisi hiyo kwa mpango wake wa upanuzi wa hospitali na kuongeza vituo 35 vya afya kutoka 15 walivyonavyo.
RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AKABIDHI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA MIKOA YA SIMIYU, KAGERA NA GEITA

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AKABIDHI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA MIKOA YA SIMIYU, KAGERA NA GEITA

July 10, 2017
jak1
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za Umiliki wa nyumba 50 za Watumishi wa Afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita.
jak2 jak3
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita kabla ya kukabidhi Hati za umiliki wa nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa hiyo mitatu.
jak4 jak5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kukabidhi nyumba 50 kwa wizara ya Afya.
jak7 jak8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kukabidhi nyumba hizo 50 zitakazotumika katika Sekta ya Afya katika mikoa ya Kagera, Simiyu na Geita.
jak9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakati Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini,  Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akihutubia wananchi wa Chato mkoani Geita.
jak10 jak11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kumaliza ziara yake Chato mkoani Geita ambapo alikabidhi nyumba 50 zitakazotumika katika sekta ya afya katika mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera.

KIWANDA MALI YA MCHINA KUFUNGWA KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

July 10, 2017

Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb.) akiongea na baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mivinjeni Buguruni Sukita leo Alipowatembelea kufuatia kero ya utiririshwaji wa maji yanayosadikiwa kuwa na  kemikali kutoka katika baadhi ya viwanda maji yanayotumiwa na wakazi wa maeneo hayo kwa kumwagilia bustani za mboga mbonga. Kutoka kulia kwake ni Naibu Meya wa  wa Manispaa ya Ilala Bw. Omary Kumbilamoto, Afisa Mazingira Ilala Bw. Adon Mapunda na Diwani wa kata ya Buguruni Bw. Adam Fugane.


Bwana Jafari Chimgege mratibu wa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la usimamizi na Hifadhi ya mazingira NEMC kanda ya mashariki akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mpina kuhusu Kiwanda cha ANBANGS kinachomilikiwa na raia wa China kivyokaidi kutoa faini ya shilingi milioni 25, iliyotozwa mwaka jana mwezi November kutokana na uchafuzi wa mazingira.



Naibu Waziri Mpina Akiongea na Wanahabari katika Bonde Buguruni Sukita jijini Dar es Salaam alipofanya Ziara leo.


Katika picha mboga za majani aina ya giligilani iliyopandwa katika eneo la mivinjeni Buguruni inayosadikiwa kumwagiwa maji yenye kemikali yatokayo viwandani.



Katika picha kijana ambaye jina lake halikupatikana akimwagilia maji yanayosadikiwa kuwa na kemikali mbogamboga aina ya majani ya Maboga zinazochipua katika eneo la mtaa wa mivinjeni buguruni sukila, leo. (Habari na Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limepewa siku saba kukagua na kujiridhisha na uzalishaji, management na utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake kwa Kiwanda cha ANBANGS kinachotengeneza mifuko aina ya viroba vinavyotumika kama vifungashio vya saruji, sukari na aina nyingine ya nafaka, na kukifunga kwa kile kinachodaiwa kukaidi maagizo ya serikali ya awamu ya tano ya kutokulipa faini kwa uchafuzi wa mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alitoa agizo hilo Leo alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Buguruni baada ya kupata malalamiko yaliyoibuliwa na wakazi wa mtaa wa sukita mivinjeni kupitia kituo cha ITV ambapo  Naibu waziri Mpina alitembelea eneo hilo na kujionena namna ambavyo kiwanda hicho kinavyoendelea kutiririsha maji machafu.
Akiwasilisha taarifa ya ukaguzi wa kiwanda hicho Bw. Jafari Chimgege ambae ni Mratibu wa mazingira kutoka NEMC kanda ya Mashariki alimueleza Naibu waziri Mpina, kuwa “Kama unakumbuka Mhe. Waziri Tulikuja hapa mwaka jana Novemver na tukafanya ziara na ukaguzi hapa na kila tukija hapa hawa wachina wanashindwa kuonyesha ushirikiano na kusema kuwa wao hawajui lugha ya Kiswahili, tuliona makosa mengi na tuliwatoza faini ya shilingi milioni 25, na ilitakiwa walipe ndani ya wiki mbili, lakini Mhe. Hiyo Faini haikulipwa. Na bado wanaendelea na uchafuzi wa mazingira pamoja na kukaidi agizo za serikali.” Alisisistiza Chimgege.
Pamoja na maelezo hayo ya Bw. Chimgege Naibu Waziri alielekeza Baraza hilo kupitia documents zote muhimu zinazohusu, kiwanda hicho ambacho awali hakikuwa na cheti ya tathmini ya athari ya mazingira wala vibali ya aina yoyote ya kutirirsha maji yaliyotibiwa na kuuganishwa na mfumo wa mji taka wa DAWASCO hali ambayo ilimpelekea Mpina pamoja na hilo kuagiza wamiliki wa kiwanda hicho kufikishwa mahakamani
Katika Ziara zake za  ukaguzi wa Mazingira na viwanda jijini Da es Salaam, Mpina amehadi kuingia hatua ya kushirikiana na mamlaka husika kuchukua sampuli za maji yanayopita katika bonde la mto msimbazi katika eneo la viwanda vya karibu na mtaa wa sukita mivinjeni ili kuyafanyia vipimo na kijirisha kama yana madhara kwa viumbe hai na mazingira hususani mboga mboga zinazomwagiliwa maji katika maeneo.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI JUNI,2017 WAPUNGUA KWA ASIMILIA 5.4

July 10, 2017
 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigwabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leokuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa Mwezi Juni. Kulia  ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira, Ruth Minja.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Juni  umepungua hadi kufikia asilimia 5.4 ikilinganishwa na asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Mei 2017.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa na wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana kuhusu mfumuko huo wa bei.

Kwasigabo alisema kasi hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2017 imepungua zaidi ikilinganishwa na kasi iliyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2017.

"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.10 mwezi Juni,2017 kutoka 103.47 mwezi Juni 2016" alisema Kwesigabo.

Alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Juni 2017 umepungua hadi hadi asilimia 9.6 kutoka asilimia 11.6 ilivyokuwa mwezi Mei,2017

Alisema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Juni 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 9.8 kutoka asilimia 11.8 mwezi Mei 2017.

Aliongeza kuwa badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa zisizo za vyakula umeongezeka hadi asilimia 3.11 mwezi Juni 2017 kutoka asilimia 3.1 mwezi Juni, 2017 kutoka asilimia 3.0 mwezi Mei 2017.

Amil Shivji aelezea filamu ya T-Junction iliyofungua pazia tamasha la ZIFF 2017

Amil Shivji aelezea filamu ya T-Junction iliyofungua pazia tamasha la ZIFF 2017

July 10, 2017
Amil Shivji aelezea filamu ya T-Junction iliyofungua pazia tamasha la ZIFF 2017 Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji ambaye yupo visiwani hapa Zanzibar na ‘crew’ yake ameelezea kwa kina filamu yake mpya na ya pili katika filamu makala ijulikanayo kama ‘T-JUNCTION’ ambayo usiku wa Jumamosi wa Julai 8,2017 imepata kuwa filamu ya kipekee huku ikishuhudiwa na Rais Mstaafu wa awami ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa tamasha la filamu la Kimataifa la nchi za Jahazi (ZIFF) ambalo mwaka huu linaadhimisha miaka 20, tokea kuanzishwa kwake. Akizungumza na wanahabari pamoja na wadau wa filamu katika mkutano maalum wa ZIFF, Amil Shivji amebainisha kuwa, T-JUNCTION ni filamu ya pili ya Kijiweni Productions, na amejisikia furaha na thamani kubwa yeye na ‘Crew’ yake kwa mara ya kwanza kuweza kuzinduliwa kidunia kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya tamasha la ZIFF mwaka huu kwani ni fursa ya kipekee katika njia ya mafanikio ya filamu hiyo. Amil Shivji amefafanua kuwa, T-Junction inawatambulisha mabinti wawili katika tasnia la filamu akiwemo; Hawa Ally (Fatima) na Magdalena Christopher (Maria) huku pia ikishirikisha sura mpya, Mariam Rashid (Mama Fatima), Sabrina Kumba (Mama Maria) akiwemo pia David Msia (Chine) katika jamii wa waigizaji. “Mbali na sura hizi mpya katika filamu hii. Pia tumeweza kuchanganya na waigizaji mashuhuri kama Cojack Chilo akiicheza kama Iddi, mkaka mkimya na mwenye imani. Mzome Mohamed (Mangi) na Tin White akicheza kama Shabani mkaka mchangamfu na mcheshi.” Alieleza Amil Shivji. Shivji ameendelea kufafanua kuwa, Kuhusu Filamu hiyo ya T-Junction ni kisa kinachowahusu mabinti wawili na jamii zao. Jamii moja ikiishi kiholela huku faraja yao ni kujua wana umoja na furaha. Jamii yao inazingatia sana mifumo, kanuni na taratibu za utu. Fatima, kigoli mwenye asili ya kihindi na kiafrika amefiwa na baba yake kutokana na pombe. Anashindwa kumuombolezea maana kwa kweli hawakuwa na ukaribu wowote. Hakupata kuwa karibu nae katika uhai wake, waliishi katika giza la utengano. T-Junction ni filamu inayohusu matabaka katika jamii ya Kitanzania. Ambapo jamii ya daraja la chini kabisa wanapambana na misukosuko vinavyowakabili ambapo miongoni mwa mambo hayo na mengine yenye visa vya kukufanya ubaki kinywa wazi na hata wakati mwingine kuangusha chozi ama kucheka kwa kufurahia kwa hali ya juu kwani kila muhusika ameweza kuitendea haki nafasi aliyopangiwa. Kijiweni Production: Amil Shivji anabainisha kuwa, kupitia kampuni yao hiyo, wameweza kuendelea kupata mafanikio makubwa ya kufanya vizuri kwa filamu zake mbili Shoeshine na Samaki Mchangani na filamu ya Aisha iliyokuwa na mafanikio makubwa.
Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa masuala ya filamu (hawapo pichani) mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Hata hivyo, Amil Shivji amewekwa wazi kuwa, kuwa filamu hiyo ya T-junction kutokana na kisa cha kweli kilichotokea eneo la Upanga. Eneo aliloishi tangu kipindi cha utoto wake. Ameendelea kuchunguza ukinzani wa matabaka dhidi ya ukuaji wa maeneo ya mjini kwa kasi. “Filamu hii imenichukua zaidi ya miaka 6, kuanzia kuifikilia na hata kuchukua maamuzi ya kuiandaa na hadi nikatimiza malengo yangu kwani ilikuwa ipo kichwani mwangu tokea utotoni mwangu na nimeweza kufanya kitu” ameeleza Amil Shivji. Shivji ameongeza kuwa, filamu hiyo iliweza kuwakusanya pamoja zaidi ya watu 30 wakiwa ni wenye ujuzi wa sanaa na watu wenye ujuzi tofauti kutoka tasnia ya filamu kwa takribani siku 20, kuanzia mwezi Februari mpaka mwezi Machi mwanzoni huku upigaji picha (shooting) ukifanyika kwenye maeneo tofauti ya Jiji la Dar es salaam. “T-Junction ni filamu ambayo kwa hakika inaonyesha vipaji vilivyopo katika tasnia ya filamu Tanzana. Tunajivunia kwamba baada ya maadhimisho ya kidunia katika tamasha la ZIFF, T-Junction itaonyeshwa kwa mara nyingine katika jijini la Dar se salaam (Tanzania Bara) hasa katika kumbi kubwa za sinema ikiwemo Century Cinemax- Mlimani City mwezi wa Agosti mwaka huu, tunawaomba watanzania na watu wote kuweza kujitokeza kwa wingi kuishuhudia filamu hii kwani imejaa mambo mengi na yenye mafunzo” alimalizia Amil Shivji. Kwa upande wao washiriki wageni katika filamu hiyo kwa nyakati tofauti wameelezea kuwa katika hali ya furaha kipindi chote kwani wamejiskia furaha kwa kutazamwa na watu wengi kupitia tamasha hilo ambapo wanaamini nyota zao zitaendelea kung’aa zaidi na zaidi kadri siku zinavyoenda na wanaamini hilo itafanya vizuri.
Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa masuala ya filamu mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.

Muigizaji mpya Hawa Ally alietumia jina la Fatuma akielezea namna alivyoweza kuucheza uhusika kwenye filamu ya T-junction. Kushoto ni Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.

Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji akiwatambulisha Hawa Ally (Fatima) na Magdalena Christopher (Maria) mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.

Amil Shivji akiwa pamoja na 'Crew' yake pamoja na mgeni rasmi Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati)

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa KIJIWENI PRODUCTION mara baada ya uzinduzi wa tamasha la ZIFF 2017.

Amil Shivji (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Baba yake Mzazi, Profesa Issa Shivji mara baada ya uzinduzi huo wa tamasha la 20 la ZIFF 2017. (PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE).