MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO AKIMSINDIKIZA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI

March 31, 2023
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa na Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris wakati akiwaaga wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kumuaga baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili nchini, leo tarehe 31 Machi 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakimuaga Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris na Mumewe Douglas Emhoff katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 31 Machi 2023 mara baada ya kuhitimisha ziara nchini Tanzania. (Picha Ofisi ya Makamu wa Rais)

HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO KUANZISHA KLINIKI ZA KIBINGWA ZA JIONI

March 31, 2023



HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo inatarajia kuanzisha huduma za Kliniki za Kibingwa wakati wa muda wa ziada wa jioni itakayoanza Aprili 11 mwaka huu katika hospitali hiyo.

Akizungumza leo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhan (Pichani) amesema huduma hizo zitaaza saa tisa na nusu jioni mpaka muda ambao wagonjwa watamalizika ambao watapata fursa ya kuonana na madaktari bingwa waliopo kwenye hospitali hiyo.

Dkt Juma alisema kwamba katika kliniki hiyo huduma mbalimbali za kibingwa ikiwemo magonjwa ya ndani,magonjwa ya ya upasuaji,magonjwa ya wakina mama,magonjwa ya watoto,magonjwa wa koo,pua pamoja na sikio .

Aidha alisema kwamba huduma hizo zitatolewa kwa wagonjwa wote wenye bima bila kujalia aina gani ya bima lakini pia wale wagonjwa wanaofanya malipo ya keshi yatapokelewa.

Hata hivyo alisema huduma hiyo itatolewa siku Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa tisa na nusu mpaka pale watakapomalizika.

Dkt Juma aliwahimiza wananchi wa mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kliniki hizo ili kuweza kukutana na madaktari bingwa wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga

Hata alisema uwepo wa kliniki hiyo utasaidia kutoa fursa kwa wagonjwa kuweza kukutana na madaktari bingwa ambao wataweza kuwasaidia hivyo watumie nafasi hiyo kuweza kuonana na madaktari hao bingwa waliopo kwenye hospitali hiyo.



Mwisho.





TASAC YATUMIA MAONESHO YA BIASHARA,UWEKEZAJI NA FURSA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

March 31, 2023


SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa elimu kwa wananchi kuhusu namna linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria wakati wa maonesho ya Biashara, Uwekezaji na Fursa yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mashujaa kuanzia tarehe 19 hadi 31 Machi, 2023 Mkoani Mtwara.

Akizungumza na vyombo ya habari wakati wa maonesho hayo Kaimu Afisa Mfawidhi wa Mkoa wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania Mkoa wa Mtwara,Joseph Myaka amesema kuwa katika kutekeleza majukumu yao shirika hilo limejikita katika kutoa elimu kwa wananchi kufahamu shirika hilo linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Amesema kuwa licha ya majukumu makubwa waliyonayo waliamua kushiriki maonesho hayo ili kuwapa elimu wananchi kuhusu fursa za biashara zilizopo katika Sekta ya Usafiri kwa njia ya Maji sambamba na elimu kuhusu Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa mazingira majini jukumu linalotekelezwa na Shirika hilo.

“TASAC tunashiriki maonesho haya ya Biashara Uwekezaji na Fursa mkoani Mtwara ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yanayotekezwa Kisheria. kama mdhibiti wa shughuli za usafiri kwa njia ya maji tunasimamia huduma zinazotolewa na Bandari, tunadhibiti na kusimamia ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira na kuratibu shughuli za uokoaji na utafutaji pale panapotokea dhoruba majini”

“Pia tunatoa elimu kwa wananchi wa Mtwara na wadau wa usafiri kwa njia ya maji katika jukumu letu la Udhibiti wa Safari kwa njia ya Maji na udhibiti Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira majini, wanaweza kufanya shughuli zao kwa usalama na kupata maendeleo na kuongeza pato la Taifa.” Ameeleza Joseph.

Kwa mujibu wa Sheria, TASAC ina wajibu wa kusimamia kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhimiza usimizi na shughuli za uwakala wa meli wenye ufanisi, kuhimiza shughuli za bandari na huduma za meli zenye ufanisi, kuhakikisha kunakuwepo usalama na ulinzi wa shehena, kuhimiza na kutunza mazingira, usalama na ulinzi wa bahari, maziwa na mito.

Maonesho hayo ya Biashara, Uwekezaji na Fursa ni maonesho ya Kwanza kufanyika Mkoani Mtwara yakiwa na lengo la kuwaleta pamoja wadau mbalimbali katika Sekta hiyo ili kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kujifunza biashara na uwekezaji wa kisasa pamoja na fursa zilizopo katika sekta hiyo na Mkoa wa Mtwara kwa ujumla.