Tanzania na Poland kukuza sekta ya kilimo nchini.

Tanzania na Poland kukuza sekta ya kilimo nchini.

October 01, 2015

0.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira akiongea na ujumbe wa wataalam wa kilimo kutoka nchini Poland ulioongozwa na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijini wa Poland Bi. Zofia Szalczyk hivi karibuni jijini Dar es salaam wakati wa mkutano uliohusu makubaliano yanalenga kuinua sekta ya kilimo na kurahisisha upatikanaji wa matrekta hapa nchini. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu Kayandabila.
0..
Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijini wa Poland Bi. Zofia Szalczyk (wa kwanza kulia) akiwa na zawadi aliyopokea kutoka kwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira hivi karibuni jijini Dar es salaam mara baada ya mkutano kati ya mkutano wan chi hizo mbili uliohusu makubaliano yanalenga kuinua sekta ya kilimo na kurahisisha upatikanaji wa matrekta hapa nchini.
0,
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa ujumbe wa wataalam wa kilimo kutoka nchini Poland ulioongozwa na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijini wa Poland Bi. Zofia Szalczyk hivi karibuni jijini Dar es salaam.
…………………………………………………
Na Eleuteri Mangi MAELEZO
Serikali ya Tanzania na Poland zimeingia makubaliano ya ushirikiano yatakayosaidia kukuza sekta ya kilimo kwa kuwawezesha wakulima kupata zana bora za kilimo kupitia Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus kutoka nchini Poland itakayoanza kufanya kazi zake nchini Tanzania mwanzoni mwa mwaka 2016.
Akizungumza mara baada ya kufanyika kwa mkutano wa makubaliano hayo kati ya Serikali ya Tanzania na ujumbe wa wataalam wa kilimo kutoka nchini Poland ulioongozwa na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijini wa Poland Bi. Zofia Szalczyk jana jijini Dar es salaam, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira alisema kuwa makubaliano hayo yanalenga kuinua sekta ya kilimo na kurahisisha upatikanaji wa matrekta hapa nchini.
Alisema Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus kutoka Poland imepewa jukumu la kuleta vipuri vya matrekta na kuviunganisha hapa hapa nchini ikishirikiana na Shirika la Uchumi na Maendeleo la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT).
“Tumeingia mkataba na Seikali ya Poland ili kuinua na kuimarisha sekta ya kilimo nchini kupitia uundwaji wa matrekta hapa nchini, kazi hii itasaidia kupunguza kilimo cha jembe la mkono ambacho kinafikia asilimia 62 na asilimia 38 iliyobaki inajumuisha kilimo cha jembe la kukokotwa na wanyamakazi “plau” pamoja na matrekta” Alisema.
Aliongeza kuwa Serikali itawajengea uwezo SUMA JKT ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuondoa hali iliyopo ya uagizaji wa matrekta yaliyounganishwa ambayo hutumia gharama kubwa na kusababisha wakulima wengi hushindwa kumudu gharama ya kuyanunua.
“Wakulima wataunganishwa na Benki ya kilimo nchini kwa kupewa mikopo mbalimbali ya kununua vifaa vya kutendea kazi ikiwemo mbegu pamoja na mbolea ili kukifanya kilimo kiwe cha kisasa zaidi” alisema Wasira.
Wasira alisema kuwa Maghala yaliyopo nchini yanauwezo wa kuhifadhi chakula tani 240,000 baada ya kukamilika ujenzi wa maghala mapya kutakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 446,000 za chakula kwa mwaka ambapo zitatumika Dola za Kimarekani milioni 110 katika ujenzi wa maghala hayo.
Aidha, Wasira aliongeza kuwa ili kuwa na mafanikio katika sekta ya kilimo nchini, Serikali itapeleka wataalamu wa matrekta kila mkoa.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijini wa Poland Bi Zofia Szalczyk alisema kuwa hatua iliyofikiwa na Serikali ya Tanzania ni ya muhimu katika katika kuongeza tija katika uzalishaji kupitia sekta ya kilimo.
Alisema Poland imefanikiwa katika sekta ya kilimo kwa sababu inashirikiana na taasisi za kifedha za kimataifa ambapo ameisifu Tanzania kuchukua uamuzi huo ambao utaiwezesha kuwa na kilimo chenye tija.
Adha, ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na Waziri wa Fedha nchini na kuahidi kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.
MCHAKAMCHAKA WA MWIGULU NCHEMBA WATUA SIMANJIRO,KONDOA NA KITETO,CCM YAENDELEA KUUNGWA MKONO KWA KISHINDO

MCHAKAMCHAKA WA MWIGULU NCHEMBA WATUA SIMANJIRO,KONDOA NA KITETO,CCM YAENDELEA KUUNGWA MKONO KWA KISHINDO

October 01, 2015


Mjumbe wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Ndg.Mwigulu Nchemba akiwasili Jimbo la Simanjiro na kupokelewa na Mbunge mtarajiwa wa Jimbo hilo Ndg.Ole Sendeka mapema hii leo.
Mwigulu Nchemba akimnadi Ole Sendeka kwa wananchi wake,Kubwa ni Ujasiri wa Ole Sendeka kwenye kutetea maslahi ya taifa,Ufuatiliaji wa Miradi ya maendeleo kama barabara zinazokwenda kujengwa kwa kiwango cha rami kuunganisha na mikoa inayopakana na Simanjiro.
Ole Sendeka akizungumza na Wananchi wake wa kata ya Engesbert kuhusu Ilani ya CCM na maendeleo ya Jimbo la SImanjiro.Kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Simanjiro linakwenda kujengwa barabara za Rami Zaidi ya Tatu za kutoka Arusha,Mererani na Dodoma na ile ya Babati kwenda Simanjiro.
Mbali na hilo,Uboreshaji wa Mfumo wa majini na Uchimbaji wa Visima ndio kipaumbele cha kwanza kwa Ole sendeka kwa Wananchi wa Simanjiro.
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Namalulu Jimbo la Simanjiro.
Twende na Magufuli popote alipo.
Wananchi wa kata ya Namalulu wakionesha Umoja wao kuichagua CCM kwa nafasi za Udiwani,Ubunge na Urais katika Uchaguzi wa October 25 Mwaka
huu.
Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa kata ya Namalulu.

Bi. Samia Suluhu Amnadi Dk Magufuli Majimbo ya Serengeti na Mwibara Musoma

October 01, 2015

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwahutubia baadhi ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwahutubia baadhi ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda.
Sehemu ya wananchi wakiwa katika mkutano wa mgombea mwenza wa CCM, Jimbo la Mwibara leo.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Mwibara, Alphaxard Kangi Lugola akiwahutubia wanaCCM na wananchi wapenzi wa chama hicho waliokuwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu leo Jimbo la Mwibara. 
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi na wanaCCM Mji wa Mugumu, Wilaya ya Serengeti leo. Ambapo katika hotuba yake amewahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa muda mfupi baada ya kuingia madarakani atatoa maelekezo kwa waziri wa kazi kuhakikisha makampuni yaliyowekeza Serengeti yanatoa ajira bila upendeleo huku wakizingatia kutoa kipaumbele kwa wanaSerengeti.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Kampeni ya Chama Cha Mapinduzi Taifa akizungumza kunadi sera za chama hicho katika mkutano uliofanyika Mjini Mugumu Wilaya ya Serengeti leo.  

wananchi na wanaCCM Mji wa Mugumu, Wilaya ya Serengeti wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara leo. 
Mmoja wa mwangalizi maalumu wa masuala ya Uchaguzi Mkuu akiendelea na kazi katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika Mugumu leo. 
Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Mwibara wakiwa wamemsimamisha njiani mgombea mwenza wa CCM, kusikiliza kilio chao njiani alipokuwa akielekea katika mkutano wa kampeni wa hadhara leo. Wananchi hao kilio chao ilikuwa ni kuiomba Serikali iharakishe mchakato wa kuipa hadhi ya wilaya Jimbo la Mwibara ili kusogezewa huduma anuai. 
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwahutubia baadhi ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda.
Sehemu ya umati katika mkutano wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwahutubia baadhi ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda.
Sehemu ya umati katika mkutano wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiwahutubia baadhi ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda.
Sehemu ya msafara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu pamoja na viongozi, wa CCM wakiwa meza kuu. 

*Imeandaliwa na www.thehabari.com -- ___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com
TFF, NHIF ZASAINI MKATABA

TFF, NHIF ZASAINI MKATABA

October 01, 2015
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na mfuko wa huduma ya afya (NHIF) kwa ajili ya kutoa huduma kwa wachezaji wa Ligi Kuu pamoja na viongozi wa benchi la ufundi.

Hafla ya kusaini mkataba huo imefanyika katika hoteli ya Protea Courtyard iliyopo Upanga jijini Dar es salaam ambapo katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF Rehani Athumani walisaini kwa niaba ya pande hizo mbili.
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uwekaji sahihi mkataba huo, Mwesigwa amesema anaishukuru NHIF kwa kudhamini kutoa huduma ya afya kwa wachezaji na mabenchi ya ufundi kwa vilabu vyote 16 vinavyoshiriki Ligi kuu ya Vodacom.
Aidha Mwesigwa ameviomba vilabu vya Ligi Kuu nchini kutoa ushirikiano na watoa huduma ya afya kwa wachezaji na viongozi kutoka NHIF pindi watakapokuwa wanafika kwenye vilabu vyao kwa ajili ya shughuli mbalimbali.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF,  Rehani Athumani akiongea kwa niaba ya mfuko huo amesema wako tayari kufanya kazi na kutoa huduma ya afya kwa ngazi zote ikiwemo kwa timu za madaraja ya chini pia.
TFF na NHIF zimeingia mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini wa huduma ya afya kwa wachezaji kwa ligi kuu na viongozi wa benchi la ufundi, mkataba ambao unaeza kuongezwa kila unapomalizika.
TFF kwa kupitia bodi ya ligi inavitaka vilabu vyote vya Ligi Kuu vitoe ushirikiano kwa wafanyakazi wa NHIF katika kurahisiha shughuli za usajili ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa na nyaraka sahihi zikiwemo picha za wahusika katika muda sahihi.
U15 YAICHAPA KOMBAINI TANGA 4-0

U15 YAICHAPA KOMBAINI TANGA 4-0

October 01, 2015
Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 (U-15) leo imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za kujipima nguvu, baada ya kuichapa mabao 4-0 kombaini ya U-15 ya Tanga Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ushindi huo umetokana na mabao mawili ya Issa Abdi dakika ya 21 na 23, Frank George dakika ya tisa na Ibrahim Abdallah Ali dakika ya 80.
Pamoja na ushindi huo, lakini vijana wa U-15 ya Taifa walikutana na ushindani kutoka kwa wachezaji wenye vipaji wa U-15 ya Tanga.
Kivutio zaidi alikuwa ni kiungo Joseph Yakobo ambaye Tanga wanamuita ‘Sure Boy’ na mshambuliaji George Chande aliyeisumbua mno ngome ya timu ya taifa iliyoongozwa na Nahodha, Maulid Lembe.
Wachezaji wote waliokwenda majaribio Orlando Pirates ya Afrika Kusini mwezi uliopita, Asad Ali Juma, Issa Abdi Makamba, Kevin Deogratius Kahego, Amani Amede Maziku na Athumani Maulid Rajab walicheza leo.  
Huo unakuwa mchezo wa tano kushinda, kati ya mechi saba tangu kuundwa kwa timu hiyo Aprili mwaka huu, ikifunga jumla ya mabao 15 na kufungwa mawili tu.
Timu hiyo iliifunga 4-1 na 3-0 Mbeya, ikaifunga 4-0 na 1-0 Zanzibar na kutoa sare ya 0-0 na 1-1 na Morogoro kabla ya ushindi wa leo.
U15 inayoandaliwa kwa ajili ya mechi za kufuzu Fainali za vijana Afrika mwaka 2017 nchini Madagascar zitakazoanza Juni mwakani, imekuwa ikiweka kambi kila mwishoni mwa mwezi kwa ajili ya michezo ya kujipima nguvu chini ya kocha Sebastian Nkoma.
Kesho U15 Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo wake wa mwisho mjini hapa, itakapomenyana na U-17 ya mkoa Tanga hapa hapa Mkwakwani.
Wachezaji wa kikosi cha U15 ya Taifa wote ni wanafunzi wa sekondari mbalimbali nchini na ndiyo maana hukutanishwa mwishoni mwa mwezi tu kwa mazoezi ya pamoja.

KONGAMANO LA ELIMU YA JUU LAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA

October 01, 2015
Afisa Masoko wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) wa Tawi la Arusha, Regina Lema akitoa maelezo kwa mmoja ya wageni waliofika katika maonyesho yaliyoandaliwa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) yanayofanyika jijini Arusha sambamba na kongamano la saba la elimu ya juu lililoanza leo Oktoba 1 -2, 2015.
Baadhi ya wakuu wa vyuo na viongozi mbalimbali wa Taasisi zinazohusika na masuala ya elimu wakipata maelezo toka banda la GEL.
Mwanafunzi wa Chuo cha St. Joseph akitoa maelezo jinsi mfumo wa Mita za kipekee za kutoa umeme kufuatana na matumizi ya mteja ambapo hata kama wateja wapo kumi kila mmoja anaweza tumia kutokana na mahitaji yake.
Chuo Kikuu cha Muhimbili cha jijini Dar es Salaam kimeshiriki katika maonyesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) yanayofanyika jijini Arusha sambamba na kongamano la saba la elimu lililoanza leo Oktoba 1 -2, 2015.
Mmoja ya washiriki ambaye amebuni mtambo wa kuchuja maji akitoa maelezo machache.
Mmoja ya washiriki ambaye amebuni mtambo wa kuchuja maji, akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Profesa Awadh Mawenya, Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania aliyeambatana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya akiwaonyesha ubora wa chujio linalotumika kutoa maji safi na salama.
Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine nao wapo...
Mwakilishi wa Chuo cha CBE cha jijini Dar es Salaam, akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Profesa Awadh Mawenya, Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ambaye aliambatana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya akiwaonyesha jinsi wanavyozingatia ubora wa vipimo kwa kuweka alama katika mizani.
Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Agha Khan cha jijini Dar es Salaam, akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Profesa Awadh Mawenya, Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania. amyeambatana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya na viongozi wengine.
Mwakilishi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial, akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Profesa Awadh Mawenya, Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ambaye aliambatana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya.
Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Mandela cha jijini Arusha, akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Profesa Awadh Mawenya, Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania aliyeambatana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya.
Maprofesa wakiwa katika kongamano la saba la elimu ya juu 2015 lililoanza leo Oktoba 1 -2, 2015 jijini Arusha.
Washiriki wakiwa katika kongamano la saba la elimu ya juu 2015 lililoanza leo Oktoba 1 -2, 2015 jijini Arusha.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''