CHADEMA KUFUNGUA KESI KUOMBA MAHAKAMA KUU KUAMURU JESHI LA POLISI KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAFUASI WAKE WANAOSHIKILIWA KATIKA VITUO MBALIMBALI

September 09, 2016
 Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam leo mchana, wakati akitoa madai ya kushikiliwa kwa wafuasi wa chama hicho zaidi ya 70 wasiofahamika na wengine 10 katika vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya Umoja wa Kupinga Udikiteta (Ukuta), bila ya kufikishwa mahakamani. Kushoto ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.
 Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam leo mchana, wakati akitoa madai ya kushikiliwa kwa wafuasi wa chama hicho zaidi ya 70 wasiofahamika na wengine 10 katika vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya Umoja wa Kupinga Udikiteta (Ukuta). Kulia ni Mwenyekiti Baraza la Umoja wa Vijana Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi na kushoto ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kinakusudia kufungua maombi katika Mahakama Kuu ya kuiomba mahakama hiyo kuiamuru Polisi kuwafikisha mahakamani watu wanaoshikiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo inatokana na chama hicho kudai kuwa kuna watu 10 ambao wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) na Kituo cha Oysterbay vya Dar es Salaam kwa zaidi ya wiki mbili bila kupewa dhamana ya polisi au kufikishwa mahakamani.

Kauli hiyo ya Chadema imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu yake yaliyo mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo mchana.

Akifafanua kuhusu Habeas Corpus alisema, ni mamlaka iliyonayo Mahakama Kuu ya kuamuru mamlaka yoyote ya kiserikali inayomshikilia mtu kumpeleka mtu huyo mahakamani.

Lissu alisema, vijana hao walikamatwa katika mikoa mbalimbali kwa makosa aliyodai kuwa ni kujihusisha na haraka za kinachoitwa Umoja wa Kupambana na Udikteta (UKUTA) pamoja na masuala mengine ya kisiasa.

“Kama ikifika Jumanne hawajapelekwa mahakamani au hawajapewa dhamana ya polisi, tutakwenda Mahakama Kuu kufungua maombi ya habeas corpus, imuite IGP au DCI au Ma-RPC au wakuu wa vituo wanakoshikiliwa hao waeleze kwa kwanini wanawashikilia hao watu kwa zaidi ya wiki mbili,” alisema Lissu

Lissu alisema tayari wameshaanza maandalizi ya hati hizo ambazo zitapelekwa Mahakama Kuu ili iweze kuwaita kati ya Mkuu wa Polisi (IGP), Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Makamanda wa Polisi wa Mikoa au Wakuu wa Vituo vya Polisi wanakoshikiliwa watu hao.

Alifafanua kuwa alionana na watu hao ambao wamedai mbali na kushikiliwa lakini pia wamepigwa na kuteswa huku wakidai kuwa wamekuwa wakichukuliwa usiku na kupelekwa katika eneo lililopo Mikocheni ambako wanateshwa na kurudishwa polisi.


Alisema jeshi la polisi linakiuka sheria na haki za binadamu kwa kuwashikilia watu hao kwa muda mrefu bila kuwapa dhamana au kuwafikisha mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashitaka.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 DK. SHEIN AKUTANA NA WATENDAJI WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS KATIBA,SHERIA,UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA

DK. SHEIN AKUTANA NA WATENDAJI WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS KATIBA,SHERIA,UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA

September 09, 2016
zna1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mkutano Mpango wa Utekelezaji  wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi  CCM  mwaka 2015-2020 katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 09/09/2016.
zna2
Mshauri wa Rais Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa (kushoto) pamoja na Viongozi mbali mbali wa Wizara ya  Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika mkutano Mpango wa Utekelezaji  wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi  CCM  mwaka 2015-2020,chini ya Mwenyekiti  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 09/09/2016.
zna3
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe,Said Hassan Said (kulia) akiwa na Viongozi wengine wa Wizara ya  Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora   katika mkutano Mpango wa Utekelezaji  wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi  CCM  mwaka 2015-2020,chini ya Mwenyekiti  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 09/09/2016.
LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA SIKU TATU MFULULIZO

LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA SIKU TATU MFULULIZO

September 09, 2016
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo mitano ya Mzunguko wa Nne.
Miongoni mwa michezo hiyo, itakuwa ni ile ya upinzani wa jadi kati ya JKT Ruvu itakayokaribishwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Mwadui itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Mbali ya michezo hiyo, pia Young Africans itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, wakati Azam FC ambayo itakuwa mgeni tena kwenye Uwanja wa Sokoine ikicheza na Mbeya City na kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Ndanda itaikaribisha Kagera Sugar ya Kagera.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili Septemba 11, 2016 kwa Simba kuikaribisha Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, lakini uliokuwa uzikutanishe timu za African Lyon na Mbao hapo kesho umesogezwa mbele hadi Jumatatu Septemba 12, 2016. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Uhuru baada ya African Lyon kubadili uwanja kutoka Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
NAPE KUZURU TFF JUMAMOSI, KUTETA NA MALINZI

NAPE KUZURU TFF JUMAMOSI, KUTETA NA MALINZI

September 09, 2016
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (MB) kesho Jumamosi Septemba 10, anatarajiwa kutembelea Ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.

Akiwa TFF kuanzia saa 4.30 asubuhi, Waziri Nape atazungumza na Mwenyeji wake Rais wa Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji pamoja na Sekretarieti kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari ambao TFF imeawaalika katika ziara hiyo.
Katika ratiba hiyo, Nape ataonyeshwa maendeleo ya michezo hususani mashindano yanayodhaminiwa na Kampuni ya Airtel na kuratibiwa na TFF ambako kwa mikoa mbalimbali iliyofanya vema, kesho timu za wanawake na wanaume zitacheza hatua ya nusu fainali kabla ya fainali za Jumapili ambazo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

BAYERN UGENINI KUVAANA NA SCHALKE 04 IJUMAA HII

September 09, 2016





Na Dotto Mwaibale

BAADA ya kufungua pazia la ligi ya Ujerumani Bundesliga kwa ushindi wa magoli 6-0 dhidi 
ya Werder Bremen, Bayern Munich watakuwa ugenini Ijumaa hii kuvaana na Schalke 04 mchezo utakaoonekana moja kwa moja kupitia visimbuzi vya StarTimes

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika dimba la Allianz Arena, Bayern walianza kwa kishindo mbio za kuunyakua tena ubingwa wa ligi hiyo kwa mchezo waliokuwa wakicheza kwa kujiamini kabisa. 

Mshambuliaji hatari wa Bayern, Roberto Lewandoski, alifunga magoli matatu na kushika usukani wa ufungaji wa magoli huku akifukuziwa kwa karibu na muafrika Pierre Emerick Aubameyang ambaye naye alitupia magoli mawili wakati timu yake ya Borrusia Dortmund ilipoilaza 2-1 Mainz 05.

Akizungumza Dar es Salaam leo kuhusu msimu mpya wa ligi hiyo ambayo inaonekana kupitia visimbuzi vya StarTimes pekee, Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif amebainisha kuwa hii ni fursa nyingine tena kwa wateja wao na watanzania wote kwa ujumla kufurahia mechi zote moja kwa kupitia chaneli mahususi za michezo kama vile SPORT FOCUS, SPORT ARENA, WORLD 
FOOTBALL, SPORT PREMIUM na SPORT LIFE kwa gharama nafuu kabisa ambazo kila mtu anaweza kumudu.

“Ningependa kuchukua fursa hii kuwafahamisha wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa msimu wa ligi kuu ya Ujerumani msimu wa mwaka 2016/2017 maarufu kama Bundesliga umerudi tena. 

Kama kawaida yetu mechi zote tutazionyesha moja kwa moja kupitia chaneli tano kwa msimu wote ambapo tayari pazia lilishafunguliwa Agosti 26 na kushudia mabingwa watetezi Bayern Munich ikiibuka na ushindi mnono wa magoli 6 bila ya majibu dhidi ya Werder Bremen.” Alisema, Hanif

“Ninaamini huu utakuwa ni msimu mwingine tena wa kufurahia na kupata msisimko wa ligi hii ambayo inazidi kujizolea umaarufu mkubwa barani Afrika ambapo tunawakilishwa vema na mchezaji kutoka Gabon, Pierre Emerick Aubameyang. 

Na StarTimes kama ndio wenye haki miliki pekee ya kuionyesha ligi hiyo tutahakikisha 
kila mtanzania anapata fursa ya kuitazama na kufurahia. Mchezaji huyo ameingia kwenye historia ya soka la Ujerumani kwa kuwa muafrika wa kwanza kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi ya Bundesliga kwa msimu wa 2015/16 na kuingia kwenye kikosi cha ligi hiyo cha mwaka. 

Hili ni jambo la kujivunia kwetu sisi waafrika kwamba soka letu linathaminiwa na vipaji 
vyetu kuonekana. Na ninaamini siku za usoni tutawaona watanzania wakipenya na 
kufikia viwango hivyo.” Aliongezea, Hanif

Mbali na mechi kati ya Schalke 04 na Bayern Munich itakayoonekana kupitia chaneli ya World Football siku ya Ijumaa saa 3:30 usiku, pia siku za Jumamosi na Jumapili kutakuwa na michezo mingine itakayopigwa katika viwanja tofauti.

Siku ya Jumamosi kutakuwa na mechi zifuatazo: Bayer Leverkusen na Hamburger SV (saa 10:30 jioni, World Football), Darmstad na Eintracht Frankfurt (saa 10:30 jioni, Sports Premium), Freiburg na Borussia Moenchengladbach  (saa 10:30 jioni, Sports Arena), Ingolstadt na Hertha Berlin (saa 10:30 jioni, Sports Life), Wolfsburg na FC Cologne (saa 10:30 jioni, Sports Premium) na RasenBallsport Leipzig na Borussia Dortmund (saa 1:30 usiku, Sports Premium).

Na siku ya Jumapili wikiendi itaisha kwa mechi zifuatazo: Werder Bremen na Augsburg (saa 10:30 jioni, World Football) na Mainz 05 na Hoffenheim (saa 12:30 jioni, Sports Life).  “StarTimes siku zote inajitahidi kuhakikisha inawapatia wateja wake maudhui bora ya michezo hususani mpira wa miguu. Mbali na Bundesliga pia liga ya Italia nayo inaonekana moja kwa moja na pekee kupitia 
visimbuzi vyetu na mwishoni mwa wiki hii kutakuwa na michezo mbalimbali ikiendelea 
ambapo vilabu vikubwa kama vile Juventus, SSC Napoili, AC Milan, Inter Milan, AS Roma na Fiorentina vitakuwa vikimenyana. 

Ningependa niwakumbushe kuwa mechi zote hizi zinaonekana kwa ubora wa hali ya juu kabisa na kwa gharama nafuu kabisa za vifurushi vya mwezi kwa kuanzia malipo ya shilingi 12,000 tu.” Alisema, Hanif


SHULE TANO ZA MSINGI MKOANI KIGOMA ZAPATA MSAADA WA MADAWATI 185 TOKA TIGO

September 09, 2016

Meneja wa kanda ya ziwa wa kampuni ya simu ya mkononi ya tigo Kamara Kalembo (kulia) akikabidhi kwa Mkuu wa wilaya Kigoma Samson Anga (kushoto) sehemu ya madawati 185 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa shule tano za msingi mkoani Kigoma.



Mkuu wa wilaya Kigoma Samson Anga akikabidhi madawati 50 kwa Mwalim Mkuu wa shule ya msingi Karuta Manispaa ya Kigoma Ujiji Therezia Edward ikiwa ni sehemu ya madawati 185 yaliyotolewa na kampuni simu ya mkononi ya tigo  kwa shule tano za msingi mkoani Kigoma


Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Karuta Athuman Juma (katikati) akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya simu ya mkononi ya tigo ambayo ilitoa madawati 50 kwa shule hiyo ili kukabili upungufu wa madawati unaoikabili shule hiyo.

Mkuu wa wilaya Kigoma Samson Anga (wa pili kulia) akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Karuta Manispaa ya Kigoma Ujiji baada ya kupokea madawati 185 kutoka kwa kampuni ya simu ya mkononi ya tigo yaliyotolewa kwa shule tano za msingi mkoani Kigoma.

MRADI WA KUONGEZA UJUZI NA IDADI YA WAKUNGA MAENEO YA VIJIJINI NCHINI WATAMBULISHWA MKOANI MWANZA

September 09, 2016
Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Projestus Rubanzibwa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, kwenye kikao cha Utambulisho wa Mradi wa kuongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi, kilichofanyika hii leo Jijini Mwanza.

Amesisitiza kwamba Wakuu wa Vyuo vya vya Ukunga nchini wanao wajibu wa kuhakikisha kwamba wanatoa mafunzo bora kwa wahitimu wa vyuo hivyo ili watakapohitimu masomo yao waweze kusaidia kutoa huduma bora afya.

Mradi wa kuongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini, unatekelezwa na Shirika la Jhpiego kwa kushirikiana na Taasisi ya Wakunga nchini Canada, Shirika la Amref, Serikari ya Canada, Taasisi ya Wakunga Tanzania na Wizara ya Afya nchini, lengo likiwa ni kuboresha huduma za afya kwa akina mama na mtoto ili kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi maeneo ya Vijijini nchini.
Na BMG
Kaimu Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, Dr.Silas Wambura, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, ambapo amesema mkoa wa Mwanza unakabiriwa na upungufu mkubwa wa idadi wa wakunga pamoja na vifaa tiba hali ambayo inasababisha kuwepo kwa vifo vya akina mama na watoto.
Dr.Dustan Bishanga ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Mama na Mtoto Shirika la Jhpiego, amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha unaongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga maeneo ya Vijijini hapa nchini ambapo wahitimu wa masomo ya Sayansi katika maeneo hayo watakuwa wakipewa ufadhiri wa masomo kwa makubaliano ya kurudi kwenye maeneo yao ili kutoa huduma za afya. Mradi huo unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2021.
Kikao cha Utambulisho wa Mradi wa kuongeza ujuzi na idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi kilichofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Dr.Dustan Bishanga ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Mama na Mtoto Shirika la Jhpiego, akizungumza na wanahabari kwenye kikao hicho.
Martha Rimoy ambaye ni Mratibu wa Taifa wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), amesema bado maeneo mengi nchini yanakabiloiwa na upungufu wa Wakunga kutokana na idadi ya Wakunga wanaohitimu vyuoni kutoendana na idadi ya ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya huku wengine pia wakishindwa kwenda kufanya kazi maeneo ya Vijijini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mazingira duni.
Gustav Moyo ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, amesema hali ya upungufu wa Wakunga nchini hususani maeneo ya Vijijini si nzuri hivyo Serikali inatumia jitihada mbalimbali ikiwemo kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi ili kutatua changamoto hiyo. 

Amesema asilimia kubwa ya mikoa ya Kanda ya Ziwa inakabiliwa na upungufu huo na kwamba Serikali itakuwa ikitolea kipaumbele kwenye mikoa hiyo pindi inapotoa ajira kwa Wakunga.
Kikao hicho kimewajumuisha wadau mbalimbali wa afya wakiwemo Wakunga, Waganga Wakuu wa Wilaya na Maafisa Elimu ambao watakuwa na wajibu wa kuwahamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi ili kuongeza idadi ya Wakunga.
Wadau wa afya kutoka Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Tabora, Kigoma na Mara wameshiriki kwenye kikao hicho.

UNESCO YAZINDUA RIPOTI YA UFUATILIAJI WA ELIMU DUNIANI (GEM) 2016

September 09, 2016
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akielezea siku ya kisomo duniani na dhumuni la UNESCO kuanzisha siku hiyo.
 Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta akizungumzia juhudi za serikali za kuhakikisha kila mtanzania anajua kusoma.
  Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, Basilina Levira akitoa taarifa jinsi hali ilivyo kwa watu wazima ambao wanajua kusoma na wasiojua kusoma.
Afisa Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo akielezea mradi wa XPRIZE ambao unasimamiwa na UNESCO ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao watoto katika maeneo mbalimbali nchi
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akitoa maelezo kuhusu Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM).
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akimkabidhi mgeni rasmi, Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta, Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM)
  Mgeni rasmi, Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta akionyesha Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM) baada ya kuipokea kutoka kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez
 Wageni waalikwa katika maadhimisho ya siku ya kisomo duniani wakionyesha Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM) wakiongozwa na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez (wa kwanza kushoto).
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akimkabidhi mgeni rasmi, Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta, sanduku la Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM).
 Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya kisomo, Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta akigawa Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM) kwa baadhi ya wafanyakazi wa wizara yake.


Na Mwandishi wetu
Katika kutambua umuhimu wa kusoma na kuandika Tanzania na mataifa mengine duniani zimeungana kwa pamoja kuadhimisha siku ya Kisomo Duniani ambayo huadhimishwa kila Septemba, 8 ya kila mwaka ambapo pamoja na maadhimisho hayo pia iliambatana na Uzinduzi wa Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani (GEM).

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez alisema kuwa dhumuni la UNESCO kuweka siku hii ya Septemba 8 kila mwaka kuwa siku ya kisomo kimataifa ili kuziunganisha jamii zote za kimataifa duniani kuweka na kuendeleza nguvu na juhudi kwa watu kujua kusoma na kuandika ili kuleta maendeleo katika jamii mbalimbali.

“Kauli mbiu hii inatufungulia milango ya uelewa juu ya malengo na mafanikio ya miongo mitano iliyopita ambayo yaliwekwa ya kutaka kila mtu anajua kusoma,” alisema Bi. Rodrieguez na kuongeza.

“Tunataka kujua ni changamoto gani zinazoikabili sekta ya elimu katika kusoma na kuandika na tunataka kufahamu namna ya kukabiliana na changamoto hizo ili kufikia malengo ambayo UNESCO iliyakusudia kufikiwa ya kila mmoja awe anajua kusoma.”

Kwa upande wa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta ambaye alimuwakilisha Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo alisema serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imejizatiti kuondoa tabaka la wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa vijana na watu wazima kwa kujenga uwiano sawa wa utoaji wa elimu kwa watu wote.

“Wizara imejipanga vizuri, na lengo kubwa la wizara ni kuhakikisha tunakuwa na mtanzania aliye elimika na aliye na stadi, maarifa na uwezo wa kutumia elimu aliyoipata,” alifafanua Bureta.

Vile vile Bw. Bureta amesema kwa sasa wizara ipo kwenye mpango wa kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) ambao unaanzia chini kwa wanafunzi wa awali mpaka shule za msingi.

Katika mpango huo walimu wamekuwa wakipata mafunzo mbalimbali ya namna ya kumuwezesha mwanafunzi kujua Kusoma Kuandika na Kuhesabu katika ngazi ya elimu ya awali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, Basilina Levira amesema kwamba kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, asilimia 78 ya vijana na watu wazima ndio waliokuwa wakijua kusoma na kuandika.

Akaongeza kuwa mwaka 2015 idadi hiyo ya wanaojua kusoma na kuandika ilishuka na kufikia asilimia 77 ambapo ilipelekea wizara hiyo kutoka na mikakati inayokusudia kuondoa kabisa tabaka la watu wasiojua kusoma na kuandika nchini.

Aidha, Basilina amesema kuwa Serikali ilipitisha sheria ya vyumba vya madarasa ya shule zote nchini kutumika kufundishia vijana na watu wazima ambao hawajui kusoma na kuandika muda wa jioni baada ya wanafunzi wa kawaida wanapomaliza masomo yao.

Amefafanua kwa kusema kuwa, wizara imeandaa programu ambayo iko kwenye mfumo wa Televisheni na picha za video (DVD) yenye masomo 65 ya kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu, ambapo kwa kutumia programu hiyo mwanafunzi anaweza kujua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa muda wa miezi 4 mpaka 6.
Mafunzo hayo kwa njia ya Televisheni na Picha za Video tayari yameanza kutumika kwa wilaya za Ilemela, Dodoma Manispaa, Songea Manispaa, Bagamoyo, Mkuranga, Temeke, Ilala na Kinondoni, ambapo asilimia 65 ya vijana na watu wazima wasiojua kusoma na kuandika wamejitokeza kujiunga na Elimu hiyo huku idadi kubwa ikiwa ni ya wanawake.

Siku ya Kisomo Duniani huadhimishwa Duniani kote kila ifikapo Septemba, 8 ya kila ya mwaka, ambapo mwaka huu 2016 maadhimisho hayo yametimiza miaka 50 tangu yalipoanza kuadhimishwa mwaka 1966.

Kauli mbiu ya siku ya kisomo duniani kwa mwaka huu ni ‘Tunasoma yaliyopita, Tunaandika yajayo, Elimu endelevu’ ambayo kwa lugha ya kiingereza ni ‘Reading the future, Writing the past’.
-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.

RC SHIGELLA ATEMBELEA BANDARI YA TANGA

September 09, 2016
 Kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa kwanza kulia aliyekaa kwenye boti wakati alipofanya ziara ya kuitembelea bandari hiyo
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa kwanza kulia akitazama maeneo ya bahari akiwa kwenye boti wakati alipoitembelea kuona namna ya utendaji wao  katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari wa Tanga Henry Arika
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika wa pili kutoka kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kulia wakati alipofanya ziara ya kuitembelea Bandari hiyo kuona namna inayofanya kazi kwa ufanisi,
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akishuka kwenye boti la Bandarini akisaidiwa kushuka wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella aliyoitembelea bandari hiyo kuona namna inavyofanya kazi zake

Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akipanda ngazi kuelekea kwenye meli ya mizigo iliyotia nanga Bandari ya Tanga wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella ambaye aliitembelea Bandari hiyo anayefuatia ni Mkuu huyo wa mkoa

Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akipanda ngazi kuelekea kwenye meli iliyotinga nanga baharini wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella juzi kuona namna inavyofanya kazi zake

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akipanda ngazi kuelekea kwenye meli ya mizigo iliyotia nanga bandari ya Tanga wakati wa ziara yake ya kuitembelea Bandari hiyo

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akipanda ngazi kuelekea kwenye meli hiyo akifuatiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga,Faidha Salim wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella

 Kaimu Meneja wa Bandari wa Tanga Henry Arika akipanda ngazi kuelekea kwenye meli ya mizigo iliyotia nanga kwenye bandari ya Tanga wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kuitembelea Bandari hiyo kuona shughuli zake anayefuatia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katikati akiteta jambo na PRO wa Mamlaka ya Bandari ya Tanga,Moni Jarufu wakati wa ziara yake

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa kwanza kushoto akionyeshwa kitu na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,(Ras) Mhandisi Zena Saidi wakati wa ziara yake ya kuitembelea Bandari hiyo jana
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi wakiteta jambo wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa kuitembelea Bandari hiyo kuona namna inayofanya kazi zake kulia ni PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu

Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiwa ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika kushoto wa kwaza kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa wakifurahia jambo wakati wakiwa kwenye ziara ya kuitembelea Bandari ya Tanga