Msafara wa Mhe. Mwakilishi Mpya wa Jimbo la Kiembesamaki ukiingia
katika viwanja Baraza la Wawakilishi kumshindikiza kwa ajili ya
kuapishwa leo asubuhi.
Gari iliomchukuwa Mhe. Mahmoud Thabit Kombo likingia katika viwanja vya
Baraza leo asubuhi kwa ajili kuhudhuria kuapishwa na kushiriki katika
Kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea kujadili Ripoti za Kamati
za Baraza Zinazowakilishwa na Wenywviti wa Kamati hizo.
Mhe. Mwakilishi Mteule akiwasili katika viwanja vya Baraza la
Wawakilishi Chukwani tayari kwa kuapishwa Rasmin kuwa Mwakilishi wa
Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar,akishindikizwa na Mwakilishi wa Jimbola
Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira na katikati Mwakilishi wa Bububu Mhe
Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) wakimshindikiza katika ukumbi wa Mkutano
kwa ajili kuapishwa
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Yahya Khamis Hamad,
akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit
Kombo alipowasili katika Ofisi ya Katibu wa Baraza kwa ajili
kujitambulisha na kuhudhuria kuapishwa kwake kuingia katika Baraza la
Wawakilishi baada ya kushinda kiti hicho katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo
la Kiembesamaki uliofanyika wiki iliopita.
Mhe. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho
akiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuaza kwa
taratibu za shughuli za Kikao na kumapisha Mwakilishi Mpya wa Jimbo la
Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo. wakati wa Kikao cha
asubuhi leo.
Mhe. Spika Pandu Ameir Kificho akisoma Dua kabla ya kuaza kwa Kikao cha Baraza cha Asubuhi leo.