KIPA SIMBA SC AFARIKI DUNIA

December 26, 2013

Imewekwa Desemba 27 Saa 12:27 Usiku.

Na Princess Asia, Dar es Salaam 

KIPA wa zamani wa klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, James Kisaka amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Burhan, Dar es Salaam.

Mdogo wa marehemu, Benny Kisaka ameiambia blog hii asubuhi hii kwamba, James Kisaka amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kichwa, macho na miguu kwa muda mrefu.
Pumzika kwa amani James Kisaka, utakumbukwa daima

Benny amesema mwili wa marehemu kwa sasa bado upo hospitali na wanafamilia wanajikusanya kukutana kupanga utaratibu wa mazishi.
Kisaka mara ya mwisho alikuwa kocha wa makipa wa Simba SC na alifanya kazi hiyo hadi mwishoni mwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara msimu huu.
Baada ya hapo ndipo alipoanza kusumbuliwa na maradhi hadi hali yake ilivyokuwa mbaya kiasi cha kuaga dunia.  

KUFURU LA DR. JOSE CHAMELEONE JANA AT MWANZA LIVE HAPAKUTOSHAZZZZ!!

December 26, 2013


Hatari tupuuuuuu...!


RAIS KIKWETE ALIPOKUTANA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA NEW YORK

December 26, 2013

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani juzi (24/12/2013) .Viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya kimataifa hususan masuala ya amani na ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali Afrika na katika nchi nyingine duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Darfur nchini Sudan na Lebanon.
Rais Kikwete yupo jijini  New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake. Picha na Freddy Maro
 Wakikwa katika mazungumzo.
Wakiagana baada ya mazungumzo
TANGA WATAHADHARISHWA NA KUHUSU KIMBUNGA

TANGA WATAHADHARISHWA NA KUHUSU KIMBUNGA

December 26, 2013
DSCN7186 
Imewekwa Desemba 27 saa 12:16 USIKU.
Wakazi wa Jiji la Tanga wametahadharishwa kuwepo kwa mchafuko wa bahari, hali inayotokana na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hewa katika Bahari ya Hindi na Visiwa vya Comoro.
Kufuatia hatua hiyo, wananchi wote hususan wavuvi na waogeleaji baharini wanaagizwa kuchukua ahadhari kubwa ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

RC TANGA AWAONYA MADEREVA MWENDO KASI.

December 26, 2013
IMEWEKWA DESEMBA 26.
Na Oscar Assenga, Muheza.
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa amewataka madereva mkoani Tanga kuhakikisha wanajiepusha na ajali barabarani kwa kutoendesha mwendo kasi hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
 
Gallawa alitoa kauli hiyo juzi wilayani hapa wakati akizungumza wananchi wa mkoa wa Tanga mara baada ya makabidhiano ya zawadi za krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi ya wazee wasiojiweza misufini kata ya Ngomeni wilayani hapa.

CCM TANGA YAMPONGEZA JK

December 26, 2013
Na Mbaruku Yusuph,Tanga.
Imewekwa Desemba 26 saa 12:25 Mchana.
 
CHAMA cha Mapinduzi CCM,Mkoani Tanga kimempongeza Mh;Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuridhia maamuzi ya  bunge ya kuwataka Mawaziri wanne kujiuzulu nyadhifa zao.

Akizungumza na TANGA RAHA ofisini kwake Katibu wa CCM Mkoa Tanga,Gastav Muba  kuwa msimamo uliowekwa na Bunge kwa Mawaziri hao wanne wa kuwajibishwa ni sahihi kwa lengo la kulinda maslahi ya chama na  mwananchi kwa ujumla.