IGP SIMON SIRO AANZA KAZI, AZUNGUMZIA MKAKATI WA KUTOKOMEZA MAUAJI KIBITI

IGP SIMON SIRO AANZA KAZI, AZUNGUMZIA MKAKATI WA KUTOKOMEZA MAUAJI KIBITI

May 31, 2017
1
Mkuu wa jeshi la polisi Nchini (IGP),Simon sirro akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua mbalimbali za  kudhibiti masuala ya uhalifu likiwemo la mauaji yanayoendelea Kibiti leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MAMBO YA NDANI)
2
Mkuu wa jeshi la polisi Nchini (IGP),Simon sirro aksisitiza jambo wakati alipozungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua mbalimbali za kuweza kudhibiti masuala ya uhalifu likiwemo la mauaji yanayoendelea Kibiti leo jijini Dar es Salaam.
3 4
Sehemu ya waandishi wa habari pamoja na Makamanda wa Jeshi la Polisi wakimsikiliza IGP Mpya, Simon Sirro alipokuwa akizungumza na Wanahabari mapema leo jijini Dar es Salaam

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 38, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 31, 2017

May 31, 2017


 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akisoma dua ya kuliombea Bunge katika  kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Dk.Medard Kalemani akiwasilisha Randama za Makadirio na Matumizi ya Wizara yake  kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe.George Masaju akifuatilia jambo kutoka kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk.Suzan Kolimba  katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira,Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe akimskiliza Mbunge wa Mtama(CCM) Mhe.Nape Nnauye katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 38 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 31, 2017.

MILIONI 180 ZAKUSANYWA MWEZI MEI KUTOKANA NA MAKOSA YA BARABARANI TABORA.

May 31, 2017
Na Tiganya Vincent, RS- Tabora

31 Mei, 2017

Jumla ya shilingi milioni 180 zimekusanywa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora katika kipindi cha Mwezi huo kutokana na makosa mbalimbali yaliyofanywa na waindeshaji wa vyombo vya moto.

Takwimu hizo zilitolewa jana mjini Tabora na Kamanda wa Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake wakati akitoa ufafanuzi juu ya jitihada mbalimbali wanazozifanya katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu mkoani humo.

Alisema makusanyo hayo yametokana tozo kwa madreva wa magari, pikipiki na bajaji na waendesha baiskeli walivunjia Sheria za Usalama barabarani katika kipindi hicho.

Kamanda alitaja baadhi ya makosa ni madereva wa Bodaboda kutovaa kofia ngumu wao na abiria wao , madereva wa magari kuendesha bila kuwa na leseni, mwendokasi, kutozingatia alama za barabara na kupakia abiria zaidi ya uwezo wa chombo cha usafiri.

Kamanda Mtafungwa alitoa wito kwa watu wote wanaoendesha vyombo vya moto Mkoani Tabora kuepuka kuvunja Sheria za Usalama Barabarani ili waokoe fedha wanazozipata zitumike kusaidia familia zao katika  matumizi mengine ya maendeleo badala kulipa faini.

“Naomba waendeshaji wa vyombo vya moto kuzingatia Sheria za Usalama barabarani ili wasipigwe faini ambazo zinawafanya watoe fedha ambazo zingewesaidia wao na familia katika shughuli mbalimbali” alisema Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora.

Aidha , alitoa wito kwa vijana wote wanaoendesha Bodaboda na baiskeli maarufu kama daladala kujisajili katika vituo(vijiwe) na kukaa katika maeneo yao waliopagwa na viongozi wao ili kuwasaidie kuwafichua baadhi ya Wahalifu kujificha katika usafiri huo.

Kamanda Mtafungwa alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuwabaini baadhi ya wahalifu ambao wanapenda kujificha katika kazi hiyo kwa kutokubali kukaa eneo moja kwa hofu ya kubainika uovu wao.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia watu sita wakiwemo madereva wa bodaboda wawili kwa tuhuma za kuvunja nyumba usiku na kuiba na wengine kununua mali inayodhaniwa ni ya wizi.

Kamanda Mtafungwa alisema kati ya watuhumiwa hao wanne walikiri kuhusika na uvunjaji nyumba na kuiba mali na wengine wawili walikutwa na mali zinazodhaniwa kuwa za wizi.

BODI YA KWANZA YA CHUO CHA TAALUMA YA UREKEBISHAJI TANZANIA YAZINDULIWA

May 31, 2017
 Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba ya ufunguzi wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam leo Mei 31, 2017.
 Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Dar es salaam leo Mei 31, 2017.
 Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza – SACP. Gideon Nkana akitoa historia fupi ya Chuo.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bodi hiyo wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Dkt. James Jesse akitoa neno la shukrani baada ya hotuba ya Mgeni rasmi.

MAKUMI WAFUNGULIWA KWENYE MKUTANO WA OYES 2017 JIJINI MWANZA

May 31, 2017
Makumi ya wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake waliohudhuria kwenye mkutano wa Injili wa OYES 2017 (Open Your Eyes and See) jana wamefunguliwa na kumpokea Kristo.

Kabla ya kuanza mkutano huo, Mchungaji Garry White (kushoto) kutoka Marekani alitoa semina kwa akina mama, vijana na wanandoa ambapo tamati ya mkutano huo unaofanyika viunga vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya, nyumba ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza ni jumapili June 04,2017.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Kulola, amewasihi watu wote kuhakikisha wanahudhuria mkutano huo uliojaa mahubiri na mafundisho ya neno la Mungu yakilenga kumfungua kila mmoja ili kuuona Ukuu na Utukufu wa Mungu.
#BMGHabari
Mchungaji Garry White kutoka Marekani akihudumu kwenye mkutano wa OYES 2017
Mchungaji Garry White kutoka Marekani akihudumu kwenye mkutano wa OYES 2017
Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola, akihudumu kwenye mkutano wa OYES 2017
Ibada ya kuabudu ikiendelea
Wakazi wa Jiji la Mwanza wakifuatilia mafundisho kwenye mkutano wa OYES 2017 Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza
Mkutano huu ulianza jumamosi Mei 27 na utafikia tamati jumapili June 04,2017. Muda ni kuanzia saa tisa na nusu mchana isipokuwa jumapili ambapo ibada zitaanza asubuhi.

TBS walia na wajasirimali kushindwa kusajili bidhaa zao

May 31, 2017
Wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa nchini wameshauriwa kutumia fursa ya bure ya ukaguzi wa bidhaa zao inayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania TBS.

Hayo yamesemwa na Afisa Masoko Mwandamizi kutoka katika shirika hilo,Gladnes Kaseka pichani kushoto juu wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya tano ya biashara ya Mkoa wa Tanga .

Alisema kuwa licha ya TBS kutoa fursa hiyo lakini bado wazalishaji wadogo na wakati wameshindwa kuitumia fursa hiyo kwa ukamilifu wake na kusababisha kuendelea kuwepo kwa bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora.

"Bado wazalishaji wetu wengi hawajaweza kuifikia fursa hiyo ambayo itaweza kuwasaidia kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora lakini wataweza kuingiza bidhaa zao kwa urahisi katika masoko ya ushindani tofauti na sasa" alisema Kaseka.

Aidha alisema kuwa bado wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanaziondosha katika soko bidhaa ambazo ni hafifu kwa kufanya ukaguzi wa Mara kwa Mara katika masoko na maeneo yote yanayohusika na shughuli za uuzaji wa bidhaa.

Nae Mfanyabiashara Aisha Kisoki alisema kuwa changamoto kubwa ni muingiliano wa bidhaa kutoka nje ambazo kwa hapa nchini zinauzwa kwa bei rahisi tofauti na wanazozizalisha.

Alisema kuwa iwapo TBS wataweza kudhibiti uingiaji usio rasmi wa bidhaa kutoka nje utasaidia sana wafanyabiashara wa ndani ya nchi kuona umuhimu wa kuweka nembo bidhaa zao.

OLE NASHA AHIMIZA MATUMIZI YA MBEGU BORA KWA WAKULIMA

May 31, 2017


Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,William Ole Nasha(kushoto)akitambulishwa wafanyakazi wa kampuni ya Monsanto Tanzania baada ya ofisi yao kufunguliwa hapa nchini eneo la Njiro mkoani Arusha,kushoto kwake ni  Mkurugenzi wa Monsanto Afrika,Dk Shukla Gyanendra.

Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,William Ole Nasha(kushoto)akikagua ghala la mbegu bora zenye uwezo wa kumpa mkulima mazao bora.

Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,William Ole Nasha akizungumza jambo baada ya kukagua ghala la mbegu bora za kampuni ya Monsanto zenye uwezo wa kumpa mkulima mazao bora

Meneja Kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsato Tanzania,Frank Wenga  akieleza mipango kamambe ya kuwafikishia mbegu bora wakulima kote nchini.

Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa ofisi ya Monsanto Tanzania.