WAHITIMU WA CHUO CHA PASIANSI NI HAZINA ADHIMU KWA MALIASILI NA UTALII NCHINI.
Na Sixmund J. Begashe
Sekta binafsi wanaojishughulisha na uhifadhi wa wanyamapori au biashara zinazoendana na uhifadhi wa wanyampori zimetakiwa kutoa nafasi za ajira kwa vijana waliohitimu katika Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi ili kuongeza tija katika shughuli za Uhifadhi na Utalii kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wanachi maendeleo kupitia Maliasili na Utalii.
Wito huo umetolewa kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula Jijini Mwanza, kwenye mahafali ya 59 ya Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi.
Mhe. Kitandula amesema wahitimu wa mafunzo ya Uaskari wa Wanyamapori na Himasheria, Uongozaji na Usalama wa Watalii na mafunzo ya muda mfupi kwa askari wa vijiji kutoka maeneo mbalimbali ni azina muhimu kwa Uhifadhi na Utalii hivyo ni vyema ikatumika vizuri kwa maslai mapana ya Taifa.
Aidha Mhe. Kitandula anetumia fursa hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wafadhili wa Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) kwa kulipia ada za masomo na mahitaji mengine iliyofanikisha kuhitimu mafunzo kwa baadhi ya wanachuo hao.
Akitoa Taarifa ya mafunzo hayo Mkuu wa Chuo hicho Bw. Jeremiah Msigwa amefafanua kuwa kati ya wanachuo 374 waliodahiliwa,Wanachuo 354 wamepewa vyeti vya kuhitimu mafunzo kulingana na viwango (grade) mbalimbali vya ufaulu wakiwemo wanachuo 222 wa kozi ya BTCWLE, 70 wa kozi ya TCWLE; 34 wa kozi ya BTCTGTS na 04 wa kozi ya TCTGTS.
SERIKALI YAAGIZA SHERIA YA USAJILI JUMUIYA KUZINGATIWA
CHATANDA AZINDUA MSAADA WA KISHERIA INAYORATIBIWA NA KAMATI YA HAKI NA SHERIA YA UWT
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda, akizindua kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna_DODOMA
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda ,amezindua kampeni ya msaada wa Kisheria inayoratibiwa na Kamati ya Haki na Sheria ya UWT yenye lengo la kuwasaidia wanawake na makundi maalum kupata haki ya msaada wa Kisheria nchini.
Bi.Chatanda akizungumza mara baada ya kuzindua kamati hiyo iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.
Amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuunga mkono jitihada za awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid Chini ya Wizara ya Katiba na Sheria inayofanya vizuri kwa sasa.
“Kampeni hii ya utoaji wa msaada wa kisheria itakuwa inafanya kazi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi yenye lengo la kutoa huduma za msaada wa kisheria na kuhakikisha upatikanaji wa haki sawa kwa wote kwa kuzingatia zaidi wanawake ,wasichana,watu wanaoishi na ulemavu na makundi mengine hatarishi,”amesema Bi.Chatanda
Amesema kuwa UWT pamoja na wadau wengine wanalenga kuhakikisha kwamba elimu ya kisheria na msaada wa kisheria inafika kwa watu wote hasa wanawake na makundi maalum.
“UWT inalenga kuchangia jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wote kuhusiana na matatizo ya ardhi,matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake urithi,Ndoa,kesi za madai na jinai.”amesema
Aidha ametoa maagizo kwa makatibu wa mikoa na wilaya kama watendaji kutoa ushirikiano wa kutosha pindi zoezi hilo la utoaji msaada wa kisheria litakapoaza kila jumamosi ya mwisho wa mwezi na kuhakikisha ripoti ya uendeshaji wa zoezi hilo.
Pia ametoa rai kwa wananchi hasa wanawake nchini kutumia fursa hiyo ya utoaji wa msaada wa kisheria ambayo imekwenda kuanza leo hapa Dodoma na baadae kwenye mikoa yote nchini kwa siku zijazo.ambapo kwenye viwanja vya Chinangali itakwenda kufanyika leo na kesho Septemba 8,2024.
kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Naibu Waziri TAMISEMI, Zainab Katimba amesema imeanzishwa kampeni ya msaada wa kisheria itakayoanza kwenye mikoa 10 na kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kwenye ofisi za UWT kutakuwa na watoa msaada kisheria.
Mhe.Katimba amesema kuwa Wanawake, watoto na watu wenye mahitaji maalum ndio walengwa kwenye kampeni hiyo na wameandaa program maalum kufikia watoto shuleni ili kupata elimu ya kujilinda na ukatili.
” Tunaandaa kanzi data ya mawakili ambao wako ndani ya UWT Ili kuwa na timu kubwa ya watu watakao toa msaada kisheria kwa wananchi katika Mikoa waliyopo,”amesema Mhe.Katimba
Aidha amefafanua kuwa Rais Dk.Samia aliona wananchi wanahitaji msaada ndio maana alianzisha kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia ambayo imekuwa na matokeo chanya
Katika hatua nyingine amesema kupitia kampeni hiyo wametengeneza programu ya kuwafikia watoto na kuwajengea uelewa namna ya kuepuka vitendo vya ukatili.
“Kutakuwa na programu maalumu ambayo itaaenda kuwafikia watoto na kutoa uelewa namna wanavyoweza kuepuka na vitendo vya ukatili,”amesema
Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga ,amesema kuwa uzinduzi wa Kampeni hiyo imekuja wakati mwafaka kukiwa na matukio mengi yasiyofaa katika jamii.
“Kampeni hii imekuja wakati mwafaka kutokana na mambo ambayo yamekuwa yakijitokeza na tunaamini itakuwa muarobaini wa matukio,”amesem
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda,akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Sheria ya UWT, Zainab Katimba ,akielezea malengo ya kampeni hiyo wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Bi.Pili Mbaga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septe.ba 7,2024 jijini Dodoma.
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Mhe.Subira Mgalu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septe.ba 7,2024 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda, akizindua kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Marry Chatanda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua kamati ya Haki na Sheria ya UWT,iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria leo Septemba 7,2024 jijini Dodoma.
WMA, TAKUKURU WATEKELEZA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA
Na Veronica Simba, WMA Dodoma
Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Dodoma imetoa elimu ya vipimo kwa Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), hivyo kutimiza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan yanayozitaka Mamlaka na Taasisi za Umma kupanga na kutekeleza kwa pamoja majukumu mbalimbali ya Serikali.
Akifungua Semina hiyo ya siku moja iliyofanyika jijini Dodoma, Septemba 6, 2024, Katibu Tawala wa Mkoa, Kaspar Mmuya amepongeza ushirikiano wa Taasisi hizo mbili unaolenga kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais na kuwahudumia wananchi ipasavyo.
“Nimefurahishwa na ushirikiano wa Taasisi hizi mbili wenye lengo la kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu dhana ya kufikiri kwa pamoja na kutenda kwa pamoja kama Serikali.”
Aidha, Katibu Tawala Mmuya amewataka washiriki kutumia semina hiyo kupambanua endapo kuna mapungufu yoyote katika Sheria ya Vipimo inayosimamiwa na WMA na kutafuta suluhisho la pamoja ili kuboresha utekelezaji wake.
Vilevile, amewataka WMA kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa wafanyabiashara na walaji ili pande zote mbili zipate kilicho stahiki. Pia, ameongeza kwamba katika utoaji elimu, wakulima waeleweshwe kuachana na utamaduni wa kutumia madalali bali wauze mazao yao katika maghala.
“Mheshimiwa Rais ametoa maelekezo kwamba mazao yauzwe kwenye maghala na huko kwenye maghala kuwe na mizani ambazo zimekaguliwa na kuhakikiwa na Wakala wa Vipimo ili kumlinda mlaji na mfanyabiashara,” ameeleza Mmuya.
Mmuya ametoa wito kwa wafanyabiashara, walaji wa bidhaa na huduma mbalimbali kuzingatia matumizi ya vipimo sahihi na kuwakumbusha kwamba sheria ya vipimo imewapa WMA mamlaka ya kutoza faini kwa yeyote atakayekiuka mwongozo wa sheria hiyo.
Amewataka WMA na TAKUKURU kuwa mfano kwa sheria wanazozisimamia na kuchukuliana hatua baina yao endapo kutabainika ukiukwaji wa sheria.
“TAKUKURU, mtumishi yeyote wa WMA akitenda ndivyo sivyo kwa kujihusisha na rushwa basi achukuliwe hatua, vivyo hivyo kwa WMA, mkibaini mtumishi wa TAKUKURU anajihusisha na uvunjifu wa sheria ya vipimo katika shughuli zake kama mtanzania wa kawaida ikiwemo kilimo, biashara na nyinginezo, msisite kumchukulia hatua,” amesisitiza.
Kwa upande wake, Meneja wa WMA Mkoa wa Dodoma, Karim Zuberi amesema lengo la kutoa semina hiyo kwa watumishi wa TAKUKURU ambao ni watumiaji wa vipimo, ni kuwapatia uelewa ili wajue haki zao wanaponunua bidhaa au kupata huduma mbalimbali.
“Kupitia semina hii watapata uelewa ni kwa namna gani kipimo kinatakiwa kuwa kabla, wakati na baada ya kununua bidhaa au kupata huduma,” amesema Zuberi.
Vilevile, amesema malengo mengine ni kutekeleza moja ya majukumu ya WMA ambalo ni utoaji elimu ya vipimo kwa jamii kupitia makundi mbalimbali kama wafanyabiashara, viongozi, wanasiasa, watumishi wa umma na mengineyo ambapo TAKUKURU ni kundi mojawapo.
Amesema, lengo jingine ni kupata maoni ya TAKUKURU kuhusu namna bora ya kutekeleza sheria ya vipimo endapo watabaini mapungufu wakati wa uwasilishwaji mada katika semina husika.
Naye Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Victor Swela ameishukuru WMA kuona umuhimu wa kuandaa semina hiyo ili kuwajengea uelewa wa masuala ya kivipimo hivyo kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kiufanisi katika sekta hiyo.
“Tutashirikiana na wenzetu wa WMA kuwaelimisha wananchi na kusimamia kuhakikisha kila upande unazingatia matumizi ya vipimo sahihi kwa manufaa ya pande zote yaani wafanyabiashara na walaji.”
Sehemu ya watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa semina kuhusu matumizi ya vipimo sahihi iliyoandaliwa na Wakala wa Vipimo (WMA), Mkoa wa Dodoma kwa watumishi wa TAKUKURU, Septemba 06, 2024 jijini Dodoma.
PIANO SUNDAYS ARE GOLDEN WITH JOHNNIE WALKER: DJ KAYGEE TAKES THE STAGE AT 1245
RAIS DK. MWINYI KUSHIRIKI SHEREHE ZA MIAKA 50 YA SIKU YA USHINDI MSUMBIJI
RAIS SAMIA AWAHIMIZA DIASPORA KUWEKEZA NCHINI
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AAPISHWA KUWA KAMISHNA WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA, AAHIDI USHIRIKIANO