BONANZA LA KWAYA ZA VIJANA KUTOKA SHARIKA MBALIMBALI ZA KANISA LA MORAVIAN JIJINI DAR LAFANA KATIKA VIWANJA VYA NIT

May 22, 2017
Kikosi cha kwaya ya Usharika wa Mabibo (waliovaa jezi za Dark Blue) na kwaya ya Usharika wa Kinondoni (waliovaa jezi nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi kuanza
Mpira ukiwa unaendelea ambapo kwaya ya Kinondoni waliibuka kuwa washindi
Baadhi ya wanakwaya pamoja na watumishi wa Sharika mbalimbali za Moravian jijini Dar wakiwa wanatazama Mpira
Mchezo wa Netball ukiendelea ambapo walikuwa wanacheza kwaya ya Usharika wa Mabibo na Uhuru ambapo kwaya ya Mabibo waliibuka washindi.
Kwaya ya Amani kutoka Usharika wa Mabibo wakifurahia ushindi baada ya kuibuka Videdea kwenye mchezo wa netball
Mpambano mwengine uliokuwa wakukata na shoka kati ya Kwaya ya Usharika wa Uhuru na Mabibo ambapo Mabibo waliibuka washindi
Hapa ni mashindano ya kukimbia kwa wanawake
Mashindano ya kukimbia kwa wanaume hapa watu walichomoka balaa
Hapa ilikuwa ni mashindano ya kukimbia na majunia ambapo ngoma ilikuwa nzito kweli lakini walioweza waliibuka kidedea
Hapa ilikuwa sasa kufukuza kuku ambapo baada ya purukushani akapatikana mshindi ambaye ndiye anaonekana hapo akifurahi.
Mshindi wa Kukimbiza Kuku Bw. Lewis kutoka Usharika wa Kinondoni akiwa amekabidhiwa zawadi yake ya Kuku.
Mshindi wa kukimbia na Majunia Bi. Emmy kutoka Usharika wa Uhuru akikabidhiwa nishani yake na katibu wa kwaya ya vijana kutoka usharika wa Mabibo.
Huyu dogo anaitwa Afsa ndiye aliibuka mshindi wa riadha kwa upande wa wanawake
Mshindi kwa kukimbiza upepo kwa upande wa wanaume Adam ajichukua zawadi yake
Washindi wa Mpira wa Miguu kutoka Usharika wa Kinondoni wakikabidhiwa kombe lao
Kwaya ya vijana kutoka Usharika wa Mabibo wakikabidhiwa kombe lao baada ya kuibuka washindi katika mchezo wa Netball

Picha zote na Fredy Njeje

MAOFISA UGANI WATAKIWA KUWA NA MASHAMBA YA MFANO

May 22, 2017
 Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus (kulia), akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa hilo. 
TIMUN YAAGIZWA KUANGALIA MUSTAKABALI WA DUNIA

TIMUN YAAGIZWA KUANGALIA MUSTAKABALI WA DUNIA

May 22, 2017
Vijana kutoka mataifa mbalimbali waliokusanyika katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN), mjini Arusha wametakiwa kuchambua masuala yaliyopo mbele yao kwa makini ili kutoa jawabu kwa matatizo ya dunia yanayohitaji ushiriki wao. Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa serikali katika mkutano huo Ngusekela Karen Nyerere, Ofisa anayeshughulikia dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Aliwataka vijana wanaoshiriki TIMUN kuhakikisha wanaangalia kwa makini mambo yanayogusa nchi zao na kuyatafutia ufumbuzi kwa kuwa ndio njia pekee ya kutekeleza malengo endelevu ya dunia ambayo yanahitaji ushirikiano wa ndani na wa kimataifa. TIMUN ambayo kirefu chake ni Tanzania International Model United Nations hufanyika kila mwaka na ujumbe mbalimbali na mwaka huu ujumbe wa TIMUN ni: “kuwawezesha vijana katika diplomasia na uongozi” Picha juu na chini ni Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaofanyika kwenye Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) mjini Arusha.[/caption] TIMUN huandaliwa na Shirikisho la vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) taasisi ya vijana isiyotengeneza faida inayotangaza shughuli za Umoja wa Mataifa na kushirikisha vijana katika utekelezaji wa shughuli hizo. Aidha aliwashukuru waandazi wa mkutano huo kubwa unaofanana na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (General Assembly) wenye lengo la kukutanisha vijana kujadili mustakabali wa malengo ya dunia. Alisema vijana wana nafasi muhimu katika utekelezaji wa malengo hayo ya maendeleo endelevu jukumu ambalo dunia imejipa kwa miaka 15 hadi mwaka 2030. Pamoja na kuwashukuru Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST) kwa kukubali kuwa mwenyeji wa kambi hiyo, hali iliyoonesha kwamba wanajali vijana, mwakilishi huyo wa serikali alisema kwamba Tanzania ipo tayari kusukuma mbele ajenda ya ushirikishaji vijana katika maendeleo endelevu kwa kuwa inaamini juu ya hilo. “Wakati serikali inafanyakazi kwa karibu na taasisi nyingine kuhakikisha kwamba malengo ya maendeleo yanatekelezeka, baraza la vijana ambalo litakutana litakuwa na kazi kubwa ya kutengeneza sauti ya pamoja namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo” Alisema kwamba malengo ya dunia ambayo yapo 17 yanagusa kila sehemu ya maisha na hivyo ni vyema kama vijana watatoka na majibu ya maswali yanaoumiza vichwa kuhusu malengo hayo hasa mazingira na dunia endelevu. Aliwataka vijana kutumia nafasi yao vyema katika jukwaa hilo kwani maisha ya watu bilioni 7 duniani wanategemea namna ambavyo wanajengwa na vijana, wenye mchango muhimu wa kulinda mazingira na kuhakikisha maendeleo endelevu. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017), unaofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) mjini Arusha[/caption] Awali Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kwamba zaidi ya vijana elfu 20 nchini Tanzania wamefunzwa malengo endelevu ya dunia, toka ulipofanyika uzinduzi Juni, 2016. Akizungumza katika hafla ya kambi ya mwaka huu ya Tanzania International Model United Nations (TIMUN), inayofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha (NM-AIST), Bw. Rodriguez alielezea kufurahishwa na idadi hiyo ya vijana waliohamasishwa na kusema kwamba malengo ya maendeleo endelevu 2030 yanahitaji kila mmoja kushiriki. Aidha alielezea umuhimu wa ushiriki wa vijana katika masuala ya maendeleo kutokana na uwingi wao hapa nchini. Asilimia 67 ya watu nchini ni vijana. Mkutano ukiendelea katika ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) jijini Arusha.[/caption] Bw. Rodriguez alishukuru machampioni kwa kuwezesha vijana wenzao kutambua malengo endelevu ya dunia na kuwataka kuendelea kufanya vizuri zaidi katika kuwashawishi vijana wenzao kuelewa na kushiriki katika malengo hayo. “Nataka kuwatafadhalisha kwamba huu ni mwanzo tu, kuna mengi ya kufanya. Kama Umoja wa Mataifa, tunawataka wote mshiriki, si tu katika kuelimisha kuhusu malengo haya ya dunia, lakini pia katika kuangalia mwenendo wa maendeleo hayo katika jamii na namna yanavyotekelezwa. Tukio kama hili la TIMUN linasaidia kuongeza uwezo wa kufikia malengo ya dunia,” alisema Bw. Rodriguez. Vijana 50 wa kwanza machampioni walifunzwa mwaka jana katika TIMUN 2016. Kwa sasa kuna vijana machampioni 500 nchini Tanzania ambao wamepeleka ujumbe kwa vijana wenzao 20,000. Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN 2017), Tajiel Urioh akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaoendelea jijini Arusha.[/caption] Ujumbe ambao umekuwa ukisambazwa na machampioni kwa wenzao umeelezwa kulenga kuchochea hamasa ya kuelewa malengo kwa ajili ya maendeleo. “Kama watu hawatajua malengo ya maendeleo endelevu, hawataweza kufanya malengo hayo kuwa ya kweli,” aliusema ujumbe huo Gloria Nassary, ambaye ni mmoja kati ya vijana 50 waliopewa mafunzo ya kwanza ya kuwa machampioni wa malengo ya dunia. Naye Tajiel Urioh ambaye ni Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN 2017), pamoja na kusisitiza amani kama sehemu muhimu ya kusukuma mbele utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu aliwahimiza vijana kutokata tamaa katika kuhimiza utekelezaji wa malengo hayo. Ofisa wa Mawasiliano NUNV anayeshughulikia tovuti na mitandao ya kijamii katika ofisi ya Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Edgar Kiliba akiendesha kipindi cha maswali na majibu wakati wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN 2017) unaoendelea jijini Arusha kwenye ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) jijini Arusha.[/caption] Alisema bila amani kuanzia katika ngazi ya familia, uwezekano wa kutekeleza malengo hayo unakuwa mgumu kwa kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya amani na utekelezaji wake. Alisema amani ni kionjo muhimu cha maendeleo kinapokosekana hata jukumu la vijana kulinda mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu halitawezekana. Alisisitiza kulinda mazingira kwa ajili ya maendeleo na kufikiwa kwa malengo ya Umoja ya Mataifa ambayo ni malengo ya dunia katika kuimarisha ustawi wa jamii na kuinua uchumi . Urioh katika mazungumzo yake alisema suala la uchafuzi wa mazingira ni suala gumu na mtambuka na kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na kuvurugwa kwa tabaka la ozoni halihusu Ulaya pekee, ambao wanachafua bali kila mmoja duniani; akiongeza kuwa mwishoni mwa siku wanaoathirika ni zaidi nchi zinazondelea akitolea mfano nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara. Championi wa Malengo ya dunia (Global Goals) nchini, Rio Paul akitoa maoni katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Baraza Kivuli la Vijana la Umoja wa Mataifa (TIMUN-2017) unaoendelea jijini Arusha.[/caption] Alisema suala la kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi si kutulia bali kuwajibika kutekeleza wajibu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba hakuna uharibifu wa mazingira unaofanyika katika taifa la Tanzania. Alisema vijana wanaweza kufanya zaidi ya yale ambayo kwa sasa wameyafanya katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu kwa kuhakikisha kwamba wana elimu ya kutosha kuhusu malengo hayo na kushirikiana kuyatekeleza kwa kuangalia changamoto mbalimbali ambazo wanazipatia majibu. Alisema lengo la malengo hayo ni kusaidia jamii vivyo hivyo vijana nao wanatakiwa kujitoa mhanga kuhakikisha kwamba jamii inaendelea kustawi na kuendelea kwa manufaa ya kizazi kijacho. Mmoja wa washiriki kutoka nchini Uingereza akiuliza swali kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Aliwataka vijana kutafuta majawabu ya mambo yanayoikabili dunia kwa namna ya busara na kitaalamu zaidi huku wakizingatia diplomasia. Septemba 2015, wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa walikubaliana juu ya malengo mapya ya dunia, malengo ya maendeleo endelevu. Malengo hayo yanatarajiwa kufanyiwa kazi katika kipindi cha miaka 15 ijayo na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii, uchumi na mazingira kwa namna ya kuwa endelevu.

HATUA ZA KUFUATA BAADA YA KUACHWA NA NDEGE

May 22, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

Ni jambo la kawaida kuachwa na usafiri kama vile basi, boti, treni au ndege licha ya kufanya maandalizi ya kutosha. Baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia mtu mpaka kuachwa na usafiri ni kama vile foleni barabarani, ajali au usafiri kupata matatizo na kukosea muda wa kuwasili.

Hali ya kuachwa na usafiri ni ngumu sana kama haijawahi kukutokea kabla na hauna mbinu mbadala ya kukuwezesha kusafiri kama ulivyokukusudia. Zipo hatua kadhaa za kufuata pindi uchelewapo ndege ambazo Jumia Travel ingependa uzifahamu na kuzizingatia pindi utakapokumbwa na changamoto kama hii.

Wasiliana na shirika la ndege unalosafiri mara moja. Kitu cha kwanza kabisa baada ya kugundua kwamba utachelewa au umechelewa ndege ambayo ulitakiwa kusafiri nayo ni kuwasiliana na shirika husika. Mara nyingi mawasiliano huwemo kwenye tiketi au tovuti ya shirika. Kwa kufanya hivyo utajua ni msaada gani wanaweza kukupatia kulingana na hali uliyopo.

Kuwa makini na sheria na masharti ya tiketi uliyokata. Kila shirika la ndege linakuwa na taratibu za uendeshaji wa safari zake. Zipo ambazo zinawasafirisha na ndege nyingine wateja wao waliochelewa, zingine siku inayofuata kama hamna kwa siku hiyo na zingine kutoza malipo ya ziada kwa kuchelewa ndege. Kwa hiyo kabla ya kukata tiketi ulizia taarifa hizo au soma kwenye tiketi yako kama zipo. 

Usihamaki/usiwe na hofu. Wewe sio wa kwanza kuachwa na ndege hali hiyo ishawakuta watu wengi hivyo vuta pumzi na tuliza akili yako ili ujue nini cha kufanya. Usipohamaki utaweza kupata suluhu ya tatizo haraka sana kama vile kuulizia cha kufanya, kuahirisha au kutafuta uwanja wa ndege ulio karibu ili usafiri na kuwahi shughuli zako kama ulivyopanga. Kwani kama kuchelewa umekwisha chelewa hakuna cha kufanya kutokana na hali hiyo.
Ulizia kwa wafanyakazi wa kampuni husika ya ndege machaguo uliyonayo. Kama umeshindwa kupata mawasiliano au haujui taratibu za shirika la ndege ulilokatia tiketi ya kusafiri basi ni vema ukauliza. Mashirika mengi yanakuwa na ofisi kwenye viwanja vya ndege au kama hawana basi ulizia wafanyakazi wa pale naamini wao wana uzoefu mkubwa wanaoweza kukupatia.

Lipia gharama za ziada baada ya kukosa ndege kama ulishafika tayari. Kama unaona kwamba utachelewa shughuli zako huko uendako basi huna budi kuongeza pesa kidogo ili uweze kusafiri na ndege inayofuata. Hii itakuwa nafuu zaidi kuliko kukata tiketi upya au kuahirisha safari. Kwa hiyo ni vema pia kuwa na fedha au chanzo za ziada pindi unapokuwa unasafiri kwani chochote kinaweza kutokea.

Tazama kama kuna ndege zingine zinazoelekea mahali uendapo. Kwa kawaida kwenye viwanja vya ndege vingi kunakuwa na ubao unaoonyesha ndege za mashirika tofauti zinazokwenda sehemu mbalimbali kwa siku hiyo. Hivyo inaweza kuwa fursa kwako kwa kufanya maamuzi ya kukata tiketi ili kuwahi shughuli zako.

Tumia muda huo kufanya mambo mengine. Kuchelewa safari haimaanisha kwamba ndiyo mwisho wa maisha. Kwa mfano upo Arusha na umechelewa ndege ya kukurudisha Dar es Salaam kwa siku hiyo, unaweza kuamua kutembelea vivutio kadhaa vilivyopo karibu na eneo hilo kama vile hifadhi ya Serengeti au Ngorongoro au hata Mlima Kilimanjaro. 
Ifahamishe hoteli utakayofikia mapema. Mara nyingine huwa tunafikia kwenye hoteli kwa mahali tunapoelekea labda uwe unarudi nyumbani. Kwa hiyo nina uhakika utakuwa umelipia hoteli wakuhifadhie chumba au kuomba usafiri wa kuja kukuchukua uwanja wa ndege. Ifahamishe hoteli utakayofikia mapema kwamba utachelewa au utafika siku inayuofuata ili kuondoa usumbufu kwao na kulipishwa gharama za ziada.

Jifunze kutokana na makosa yako. Kufanya makosa ni sehemu ya kujifunza mambo mengi maisha yetu. Hivyo basi hakikisha kwamba baada ya kuchelewa safari hii utakuwa makini zaidi wakati mwingine. Kama ulichelewa kwa sababu ya usafiri basi hakikisha unatoka mapema zaidi, kama ni ulikosea kuangalia muda basi muombe mtu wa karibu yako akukumbushe. 
Sababu ni nyingi ni zingine haziwezei kuzuilika kwa upande wa abiria na hata kwa shirika la ndege. Kuna wakati mwingine unaweza kuchelewa ndege kutokana na sababu za kiufundi za shirika lenyewe. Mara nyingi kwa sababu kama hizo abiria huwa wanafidiwa na mashirika ya ndege. Lakini kama ni sababu zako binafsi, Jumia Travel inakuasa kwamba uwe makini kwani utaishia kupoteza muda, kuvuruga mipango yako na kuingia gharama za ziada usizozitarajia.

DC UBUNGO MHE KISARE MAKORI AAGIZA KUJENGWA DARAJA LA MBEZI MSUMI

May 22, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisikiliza malalamiko ya wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam wakielezea adha wanayokumbana nayo kutokana na uharibifu wa Daraja
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori  sambamba na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally wakikagua daraja lililovunjika eneo la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam.
Muonekano wa Daraja la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam likiwa limeharibika
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam
 
Na Nasri Bakari, Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Leo Jumamosi, Mei 20, 2017 ameagiza kujengwa kwa daraja  jipya kutokana na kuharibika kwa daraja la awali katika eneo la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam.

Agizo hilo amelitoa mapema hii leo wakati akizungumza Na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa Hadhara uliowajumuisha pia Mtendaji wa Kata,  wajumbe wa mitaa na wataalamu mbalimbali kutoka Manispaa ya Ubungo.

Tanzania: Marriott International to debut The Ritz-Carlton in the Zanzibar Archipelago

May 22, 2017
Mr. Saleh Said, Directors of Pennyroyal Gibraltar Limited and Mr Alex Kyriakidis, President and Managing Director, Middle East and Africa, Marriott International, along with other executives from both companies.
.

MKUU WA WILAYA YA UBUNGO ATOA MAAGIZO MANNE KUTEKELEZWA, IKIWEMO KUJENGWA KWA MADARASA NANE SHULE YA MSINGI UBUNGO PLAZA

May 22, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza katika Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kufika Shule ya Msingi Ubungo Plaza kwa ajili ya Mkutano uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akikagua Mipaka ya eneo la Shule ya Msingi Ubungo Plaza kabla ya Mkutano  uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017
Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa Utumishi Mkuu Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally akijibu baadhi ya maswali ya wananchi wakati wa Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017 
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo Na Ofisa Mtendaji wa Kata Ya Ubungo Ndg Isihaka Waziri wakisikiliza Maelezo kuhusu Shule ya Msingi Ubungo Plaza kabla ya Mkuu wa Wilaya kuzuru shuleni hapo kwa ajili ya Mkutano
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati wa Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati wa Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 19, 2017 ameagiza kujengwa madarasa nane mapya katika shule ya Msingi Ubungo Plaza Jijini Dar es salaam kutokana Na uchakavu wa Majengo ya madarasa yaliyopo sasa.

Ametoa agizo hilo katika mkutano wake na uongozi wa shule hiyo ukiwajumuisha mtendaji na wajumbe wa mitaa,walimu na wananchi  ambao waliohudhuriwa katika viwanja vya  shule ya Msingi Ubungo Plaza.

Mhe Makori amesema kuwa ili kuboresha elimu katika Wilaya ya Ubungo ni wazi kuwa ni lazima kuwe Na miundombinu rafiki kwa wanafunzi wanapokuwa darasani kwa ajili ya masomo kwani ubovu wa Majengo ya shule,ubovu na uhaba wa vyoo ni miongoni mwa mambo yanayopelekea wanafunzi kufeli kutokana na kutokuwa Na miundombinu rafiki.

Alisema kuwa Kodi zinazokusanywa Na serikali kwa wananchi ni kwa ajili ya kuwaimarishia miundombinu kuboresha afya, na Elimu hivyo serikali ni lazima ishughulikie na Kusimamia shughuli zote ikiwemo Ujenzi wa madarasa kwa manufaa ya wanafunzi Na wananchi kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ametoa maagizo hayo Wakati akijibu Risala iliyosomwa Na Mkuu wa Shule ya Msingi Ubungo Plaza Bi Theresa Masaba ambayo ilibainisha changamoto nyingi ikiwemo Ukosefu wa Vyoo Bora, Ukosefu wa Uzio, Uchakavu wa Majengo ya shule, Upungufu wa Majengo (Ofisi ya Walimu, Darasa la awali Jiko, Maktaba), Maji taka kuelekezwa kwenye eneo la shule, Eneo la shule kufanyika kama sehemu ya kuvutia bangi Wakati wa jioni na siku za Wikendi sambamba na Upungufu wa samani za shule.

Mhe Mkuu wa wilaya ameagiza pia kuvunjwa kwa Vyoo vilivyopo Na kujengwa Vyoo vingine vipya sambamba na kujengwa kwa  uzio wa shule ili kuepuka kadhia ya watu wanaotumia kama Eneo la kuvutia bangi Na vitendo vingine viovu visivyo kubalika katika jamii.

Aidha amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya kuhakikisha anawakamata watu wote wanajihusisha Na uvutaji bangi katika Eneo la shule kwani Jambo hilo halikubaliki si tu Na shule hiyo Bali Na serikali kwa ujumla.

Sambamba Na hayo pia Mkuu wa wilaya ameagiza kuvunjwa kwa ukuta wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) ambapo Uzio wake umejengwa ndani ya Eneo la shule.
Alisema kuwa Kanisa hilo tayari lilishapewa Notisi ya siku Saba tangu Mei 8 mwaka huu kwa ajili ya kuvunja ukuta huo lakini hawakufanya hivyo.

Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya Walimu Na wanafunzi wa shule, Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya Msingi Ubungo Plaza Ndg Ramadhani Maughuu amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kutembelea shule hiyo Na kutatua changamoto hizo zilizokuwa zinaikabili shule hiyo kwa muda mrefu.

Maughuu ametoa pongezo zake pia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kwa ufanisi Na uchapa Kazi wake sambamba Na pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa weledi Na ufanisi wa kuwahudumia watanzania Na kauli mbiu ya HapaKaziTu.