HATUA KALI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE KWA VIWANDA NA MIGODI INAYOFANYA SHUGHULI ZAKE ZA UZALISHAJI KWA KUHARIBU MAZINGIRA-MAKAMU WA RAIS.

June 04, 2017
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shda la maua kwenye Mnara wa kumbukumbu ya ajali ya ndege ya kivita iliyotokea mwaka 1978 kwenye Msitu wa Muhunda ,wilayani Butiama mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Mama Maria Nyerere nyumbani kwa Mama Maria Butiama leo mara baada ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira Duniani.#Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti kwenye Msitu wa asili ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kitaifa imeadhimishwa Butiama. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwagia maji mti alioupanda kwenye Msitu wa asili ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kitaifa meadhimishwa Butiama. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi kijijini Butiama mkoani Mara wakati wa kilele cha siku ya mazingira Duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kiatu cha kusaidia walemavu wakati alipotembelea banda la Kituo cha Walemavu cha Ziwa Victoria (Lake Victoria Disability Centre) kinachoshughulika na kutengeneza viungo bandia kwa watu wenye ulemavu kabla ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kilele chake kimefanyika kwenye viwanja vya Mwenge,Butiama
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia namna samaki anaweza kufugwa vizuri bila kuharibu mazingira na kuleta manufaa kabla ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kilele chake kimefanyika kwenye viwanja vya Mwenge,Butiama

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa viwanda na migodi ambayo inafanya shughuli zake za uzalishaji kwa kuharibu mazingira ikiwemo utitirishaji wa kemikali kwa wananchi kwani kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa wananchi na viumbe hai wengine.

Makamu Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo tarehe 4-Jun-2017 kijijini Butiama mkoani Mara wakati anahutubia wananchi katika kilele cha siku ya mazingira Duniani.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema uharibifu wa mazingira ukiachiwa uendee nchini ni hatari kwa usalama wa maisha na viumbe hivyo ni muhimu kwa viongozi katika ngazi zote kuchukua hatua zitakazosaidia kukabiliana na vitendo hivyo kote nchini.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa umefika wakati kwa viongozi kwa ushirikiano na jamii kuhakikisha wanaweka mikakati ya kuokoa mifumo ya ikolojia, uhifadhi wa bioanuai, kudhibiti uchomaji miti kiholela ili kurejesha uoto wa asili ambao umeharibiwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika maeneo mengi nchini.

“Kutozingatia hifadhi ya mazingira kunaweza kusababisha kuparaganyika kwa mfumo huo na kufanya maisha yetu na ya vizazi vijavyo kuwa mashakani”. Amesisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema katika kuadhimisha siku ya mazingira Dunia viongozi wanapaswa kuchukua hatua za kuelimisha wananchi na kuwahamasisha ili kila mtu ashiriki katika juhudi za kuwa na uchumi unaozingatia hifadhi ya mazingira.

Kuhusu wananchi kutembelea hifadhi za taifa nchini, Makamu wa Rais aipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuruhusu wananchi kutembelea hifadhi za taifa bila kiingilio na kusema mpango huo ni mzuri na unatakiwa kufanyika kila mwaka.

Amesema kuwa mkakati huo unalenga kuhamasisha wananchi ili kuwa mahusiano rafiki na mazingira kwa kuzingatia ukweli kwamba jinsi wananchi wanapoona ndipo wanapoamini na kuelewa umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.

Ameeleza kuwa katika kuadhimisha siku hiyo inapasa jamii kutafakari mchango wa kila sekta na kila mwananchi katika uhifadhi wa mazingira kwenye maeneo wanayoishi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira January Makamba amesema Serikali imeamua kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani kijijini Butiama kama hatua ya kuenzi mchango mkubwa uliofanya na baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere katika uhifadhi wa mazingira.

Amesema baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere alifanya kwa vitendo katika kuhifadhi mazingira ambapo alianzisha msitu wake katika eneo la Butiama hivyo wananchi wote ni lazima waige mfano huo katika kulinda na kutunza mazingira.

Kwa upande wa familia na mwalimu Nyerere wameishukuru Serikali kwa kupeleka maadhimisho hayo kijijini Butiama ikiwa ni sehemu ya kuenzi na kutambua mchango wa baba wa taifa katika uhifadhi wa mazingira nchini.

Kabla ya Kuhutubia katika Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan alipanda miti katika msitu wa Mwalimu Nyerere na kuweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya ajali ya Ndege ya Kivita ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) uliopo katika
msitu wa Muhunda katika kijiji cha Butiama mkoani MARA.

VIDEO:TEMBO 110 WAVAMIA MASHAMBA, WAUA MWANAKIJIJI MMOJA TUNDURU

June 04, 2017

Tembo 110 wamevamia mashamba ya wananchi na kufanya uharibifu wa mazao katika kata za Mbati,Kalulu,Namwinyu na Jakika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kuua mk azi mmoja wa Mbwembwele aliyejulikana kwa jina moja la Kalengo mwenye umri wa miaka 70, Taarifa zaidi hii hapa video yake.
TBL Group yatekeleza kauli mbiu ya ‘Hifadhi mazingira, Muhimu kwa Tanzania ya Viwanda’kwa vitendo

TBL Group yatekeleza kauli mbiu ya ‘Hifadhi mazingira, Muhimu kwa Tanzania ya Viwanda’kwa vitendo

June 04, 2017
MAZE1
Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group muda mfupi baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti katika shamba la Baba Wa Taifa kijijini Butiama katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
MAZE2
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakishiriki kupanda miti katika shamba la Baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere katika Kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani
KA1
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mbeya wakifanya usafi katika kata ya Ilomba eneo la Stendi ya Mabasi Jijini Mbeya katika  kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
KA2
KA4
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mbeya katika picha ya pamoja baada ya kushiriki kazi za usafi katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
………………………………………………………
Wafanyakazi washiriki kuadhimisha Siku ya Mazingira

 Katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani 2017 Kampuni ya TBL Group iliyopo chini ya kampuni ya kimataifa ya vinywaji ya ABInBev imetekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya siku ya mazingira duniani nchini ya “Hifadhi mazingira, Muhimu kwa Tanzania ya Viwanda, ambapo wafanyakazi wake wameshiriki katika shughuli mbalimbali za maadhimisho.

Wafanyakazi kutoka viwanda vya TBL Group vilivyopo katika mikoa ya  Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Moshi wameshiriki katika shughuli za usafi wa mazingira na upandaji wa miti ambapo baadhi yao wameshiriki katika maadhimisho ya kitaifa kijijini Butiama na kushiriki kampeni ya kupanda miti  iliyoongozwa na Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa mgeni wa heshima.

Akiongea kuhusu mkakati wa kampuni kuhusiana na suala ya mazingira, Afisa wa Masuala Endelevu wa TBL Group, Irene Mutiganzi,alisema mazingira ni suala ambalo kampuni inalipa kipaumbele kikubwa kwa kuwa katika moja ya malengo ya kampuni mama ya TBL Group ya ABiNBEV inayojulikana kama ‘Kujenga Mazingira ya Kuishi katika Dunia iliyo safi’ suala la utunzaji mazingira linatekelezwa kwa vitendo katika maeneo yote  ya biashara za kampuni.

Alisema kwa kufuata mwongozo huu kampuni imejiwekea malengo ya kufanikisha kuhusiana na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya matumizi mazuri ya maji katika mchakato wa uzalishaji, kutumia nishati mbadala zisizochafua hewa, kushiriki kampeni za kupanda miti na utunzaji wa vyanzo vya maji,kutumia vifungashio rafiki kwa mazingira.

 Kuhusiana na matumizi ya maji kwa umakini amesema TBL imepunguza matumizi ya maji katika mchakato wa uzalishaji wa bia  kutoka hectolita 6 za maji zilizokua zinatumika katika miaka ya karibuni hadi hectolita 3.6 kwa kila lita moja ya bia inayozalishwa kwa sasa na inaendeleza mkakati wa kupunguza matumizi zaidi ambapo pia imekuwa ikifanya utakatishaji wa maji taka  na kuharibu taka ngumu na nyepesi kwa kutumia teknolojia za kisasa ambazo ni rafiki kwa mazingira.

Mutiganzi alibainisha kuwa kampuni tayari imeanza kutekeleza hatua za kufanya uzalishaji kwa kutumia nishati mbadala zisizokuwa na athari kwa uchaguzi wa hewa ambapo katika kiwanda cha TBL Mwanza kinafanya uzalishaji kwa kutumia mashine zinazozalisha nishati zinazotokana na pumba za mpunga na katika kiwanda cha TBL Mbeya zimefungwa paneli za umeme wa jua ambayo inawezesha kupatikana umeme wa jua unaotumika katika baadhi ya shughuli za mchakato wa uzalishaji.

 Mutiganzi alisema TBL Group inaliangalia suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji sio kwa kiwango cha maslahi ya viwanda vyake kupata malighafi tu bali kwa jamii nzima ambapo kampuni inafanyia biashara  kwa kuwa sera ya kujenga ‘Dunia Maridhawa’ (Better World) inashahabiana  Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa  (SDGs)  na suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji ni moja ya suala ambalo limepewa umuhimu mkubwa.

“Kupitia sera ya kampuni ya ‘Kujenga Dunia Maridhawa’ tumeweza kutekeleza kwa vitendo kanuni za utunzaji wa mazingira, Kuhamasisha jamii unywaji wa kistaarabu na kuunga mkono jitihada za serikali kusaidia kufanikisha changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii hususani katika sekta ya afya,usalama barabarani na elimu na siku zote kampuni na wafanyakazi wote tutaendelea kufanikisha  uwekezaji wenye kuleta manufaa kwa jamii nzima”.Alisema Mutiganzi.

Sera ya kujenga Dunia Maridhawa ya ABInBev ambayo inatekelezwa katika maeneo yake yote ya biashara imejikita katika ufanikishaji wa malengo makuu matatu ambayo ni ‘Dunia inayokua ‘ inayolenga kukuza shughuli mbalimbali na kuwapatia watu fursa ya kujiendeleza kimaisha,’Kujenga Dunia iliyo safi inayolenga kulinda mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo na ‘Kujenga Dunia ya watu wenye Afya ambayo inahimiza  utumiaji wa vinywaji kistaarabu bila kuleta athari kwa jamii.

WASTAAFU PSPF MWAKA 2017/18 “KULAMBA” SHILINGI TRILIONI 1.3 ZA MAFAO

June 04, 2017
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, aliongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji Bi. Neema Muro na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Bw. Gabriel Silayo, baada ya kufungwa kwa semina kwa wastaafu watarajiwa wa wilaya zote za mkoa wa Mwanza iliyofanyika ukumbi wa chuo cha watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, huko Capri-point jijini Mwanza.
Katika hotuba yake aliyotoa Kati wa ufunguzi rasmi wa semina hiyo, Bw. Mayingu alisema, PSPF inatarajia kulipa wastaafu kiasi cha shilingi Trilioni 1.3 kwa mwaka huu tu wa 2017/18.
 
”Kwa mwaka 2017/18 pekee, Mfuko unatarajia kuwalipa wastaafu 9,552 jumla ya mafao yanayofikia shilinginTrilioni 1.3.Kisai hiki cha Mafao ni kikubwa, hivyo kupitia semina hii Wastaafu watarajiwa wa PSPF wamejifunza namna ya kupanga
maisha yao baada ya kustaafu ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji wa mafao yao ili mafao haya yaweze kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi na kuongeza fursa za ajira.” Alisema Bw. Mayingu katika hotuba yake.
 
 Miongozi mwa mambo waliojifunza wastaafu hao wanaokadiriwa kufika 450, ni pamoja na uanzoshwaji wa viwanda vidogo vidogo, namna bora ya utunzaji fedha kwenye taasisi za fedha, (mabenki), lakini pia mbinumbalimbali za ujasiriamali. 
 
Bw. Kuhusu mafunzo yaliyotolewa na SIDO, Bw. Mayingu alisema Mfuko ulikutana na Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo (SIDO) na kujadiliana namna ambavyo taasisi hizi mbili zinaweza kushirikiana na kuwafanya wastaafu wa PSPF wapate ujuzi wa kuwekeza na kuweza kutengeneza ajira kwa vijana. 
 
“Lengo likiwa SIDO iwajengee uwezo kitaalamu na kuwapatia vifaa ili wastaafu wa PSPF waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo na shughuli nyingine za uzalishaji.” Alisema Bw. Mayingu. 
 
Alisema wameamua kufanya hivyo kwa kzuingatia ukweli kuwa, katika kufuatilia wastaafu wa Mfuko wamegundua kuwa baadhi yao hujiingiza katika biashara mbalimbali ambazo hawakujiandaa vema na matokeo yake kupoteza mafao yao.
 Washiriki wakijadiliana
 Mkurugenzi wa Masoko wa wa Mfuko wa uwekezaji wa pamoja UTT-AMIS, Daudi Mbaga, akitoa mada ya namna wanachama wa taasisi hiyo wanavyoweza kufaidika kwa kuwekeza kwenye Mfuko huo.
 Mshiriki akizungumza kwenye semina hiyo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku mbili
 Mmoja wa wastaafu wa PSPF, ambaye kwa sasa ni mteja wa benki ya NMB, akitoa ushuhuda jinsi alivyofaidika baada ya kuitumia benki hiyo pale alipostaafu ambapo sasa anaedesha miradi mbalimbali kufuatia mikopo anayompewa na benki hiyo na kumfanya aishi maisha ya amani.
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), Mkurugezni wa Uendeshaji, Bi.Neema Muro, (katikati) na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabriel Silayo, wakifurahia michango ya mawazo kutoka kwa washiriki wa semina.
 Meneja wa Mfunzo kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo SIDO, Bi. Beata Minga, (kulia), akiongoza kikao wakati wa kufungwa kwa semina ya siku mbili ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa
 Mshiriki akichangia mawazo yake kwenye semina hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (katkati), akiwa na viongozi wengine wa Mfuko kutoka kushoto ni Meneja Mipango na Utafiti, Bw.Luseshelo Njeje, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bi. Neema Muro, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabriel Sulayo, na Meneja wa Pensehini za Wastaafu, Bw.Mohammed Salim.
Bw. Mayingu, (kushoto), akijadiliana jambo na Bwana Dominic Haule, Mkurugenzi IMADS, (wakwanza kulia), wengine wanaosikiliza kutoka kushoto ni Bi. Neema Muro, Bw. Gabriel Silayo, Bw.Bw.Luseshelo Njeje na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, baada ya kufungwa kwa semina hiyo
 Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambaye awali aliifungua rasmis semina hiyo, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, (watatu kulia waliokaa), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw.John Mongella, (watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (wapili kulia), na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, viongozi wengine na wafanyakazi wa PSPF
 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, (kushoto) na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro wakiwasili ukumbini
 Naibu waziri wa fedha na mipango, Dkt. Asshatu Kijaji, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Bw. Nyakimuro Muhoji (katikati) na Mkurugenzi Mkuu, Bw. dam Mayingu wakiwasili ukumbini.

TPDC MSHINDI WA TUZO YA BANDA BORA SEKTA YA NISHATI NA MAZINGIRA

June 04, 2017

Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe kushoto akimkabidhi  Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale tuzo ya mshindi wa banda bora la sekta ya nishati na mazingira katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara wakati alipokwenda kuyafunga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella.
 Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe kushoto akifurahia jambo na  Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale mara baada ya kumkabidhi tuzo ya mshindi wa banda bora la sekta ya nishati na mazingira katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara wakati alipokwenda kuyafunga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella.

 Watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiongozwa na Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale kulia na katikati ni Mwanasheria wa TPDC Kelvin Gadi wakiwa na tuzo yao walioipata
 Watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiongozwa na Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale kulia na katikati ni Mwanasheria wa TPDC Kelvin Gadi wakiwa na tuzo yao waliyoipata
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kulia ni Mwanasheria wa Shirika hilo Kelvin Gadi
 Mwanasheria wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Kelvin Gadi kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto mara baada ya kulitembelea banda lao
 Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe wa pili kutoka kulia mwenye miwani akiteta jambo na watumishi wa shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mara baada ya kulitembelea
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe wa pili kutoka kulia mwenye miwani akiwa kwenye picha ya pamoja  na watumishi wa shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mara baada ya kulitembelea

CUF YA MAALIM SEIF YAZINDUA OFISI MAGOMENI JIJINI DAR ES SALAAM

June 04, 2017
Suleiman Msuya

IKIWA ni takribani miezi 10 sasa kwa Chama cha Wananchi (CUF), upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad kuvamiwa katika Ofisi Kuu za Bugurunina kundi la Profesa Ibrahim Lipumba chama hicho kimezindua ofisi mpya za chama hicho katika eneo la Mtaa wa Idrisa, Kata ya Mzimuni, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Aidha, Seif amesisitiza kuwa hatarajii kukutana na  Profesa Lipumba kwa kile alichodai kuwa hatambuliki katika chama na hana  sifa hizo kwa sasa.

Akizindua ofisi hiyo ambayo lengo kubwa ni kwa ajili ya wabunge 40 wa CUF, Seif alisema  uamuzi wa wabunge hao kumpatia ofisi ya kufanyia kazi hapo ni cha kiungwana na kinahitajika kuungwa mkono na wanachama wote.

Alisema kwa muda wa miezi 10 sasa wamekuwa wakishindwa kufanya kazi hasa upande wa Tanzania Bara jambo ambalo limewaathiri sana hivyo kupatiwa ofisi kutamsaidia kutimiza majukumu yake vilivyo bila hofu yoyote.

Maalim Seif alisema kukosa ofisi kumewaathiri sana katika baadhi ya mambo hivyo anaamini kwa sasa akifikia Dar es Salaam anamahali pa kukutana na wakurugenzi wake.

“Nimekuwa ni kija hapa nakosa sehemu ya kukutana na wakurugenzi, viongozi mbalimbali wanachama ila hiki ambacho wabunge wamefanya ni cha kuungwa mkono sijawahi kufanya kazi na wabunge wanao kipenda chama kama kipindi hiki,” alisema.

Katibu huyo alisema atahakikisha kuwa anaanza kazi haraka iwezekanavyo kwa kukutana na wakurugenzi wake ili waweze kutekeleza majukumu ya chama.

“Hakuna shaka kuwa hu u unaoitwa mgogoro umeturudisha nyuma sana hivyo naamini wakati wa kufanyakazi umerejea na hawa wabaya wetu hawata ambulia kitu kwani CUF ni  chama imara hakitikisiki,” alisema.

Maalim Seif alisema jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukimaliza chama ni kubwa lakini hawataweza kufikia lengo hilo kutokana na misingi ya chama hicho.

Alisema kwa sasaa atafanya kazi katika ofisi hiyo ambayo amepewa na wabunge hadi hapo muafaka wa ofisi kuu Buguruni utakapopatikana huku akisisitiza kuwa haki haipotei ila inachelewa.

Katibu huyo alisema anaimani na   mahakama kuwa ita wapatia haki stahiki hivyo kuwataka wanachama kuendelea kuwa na subira.

Aidha, alisema kupitia mgogoro huo hadi sasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini inashikilia zaidi ya sh. bilioni 1.2 ambazo ni ruzuku ya chamahicho.

Maalim Seif alisema fedha hizo ni pamoja na zile ambazo ofisi ya msajili ilimpatia Lipumba hivyo waamini mgogoro ukiisha wata pata haki yao.

Kwa upande mwingine Katibu huyo alisema hana mpango wa kukutana naLipumba kuhusu mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho kwa kile alichodai kuwa si kiongozi wala mwanachama wa chama hicho.

Alisema CUF haimtambui Lipumba kwa sifa yoyote tofauti na kumfukuza uanachama hivyo yeye hawezi kukukutana na mtu  kamahuyo.

Maalim Seif alisema pamoja na kuwa hawamtambui Lipumba kama kiongozi au mwanachama ila akiomba msamaha wapo tayari kumsamehe.

Akizungumza baada ya kuzinduliwa ofisi hizo Mbunge wa Viti Maalum na Kiongozi wa Wabunge wa CUF bungeni, Riziki Ngwali alisema wamelazimika kufungua ofisi nyingine ili wapate mahali pa kukutana wakiwa nje ya Bunge.

Ngwali alisema kupitia ofisi hiyo wataweza kujadiliana mambo mbalimbali yanayo wahusu wabunge na wananchi na kuja na ufumbuzi.

Kwa upande wake Mbunge wa Temeke CUF, Abdallah Mtolea alisema katika ofisi hiyo wanatarajia kuajiri wataalam mbalimbali ambao watasaidia kufanya tafiti na kupitia tarifa mbalimbali za Bunge ili kuwarahisishia katika uchangiaji bungeni.


Alisema katika ofisi hizo wameingia mkataba wa kulipa sh. milioni 18 kwa mwaka ambazo zitatolewa na wabunge wenyewe kwa maslahi ya chama chao.

KAMPUNI YA BIMA YA BRITAM-TANZANIA YAZINDUA BIMA YA AFYA KUHUDUMIA MAKAMPUNI MAKUBWA

June 04, 2017

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam-Tanzania, Stephen Lokonyo akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wiki iliyopita, wakati wa uzinduzi wa bima ya afya hapa nchini. Katikati ni Mkuu wa Bima ya Afya ya kampuni hiyo, Christine Mungi na kulia ni Mkuu wa Fedha na Utawala, Irene Godson. (NA MPIGA PICHA WETU)


Na Dotto Mwaibale


KAMPUNI ya Bima ya Britam-Tanzania imezindua bima ya afya inayolenga kuhudumia makampuni makubwa, biashara ndogo na za kati (SMEs).

Bima hii inajumuisha gharama za matibabu ya wagonjwa waliolazwa, vipimo vya magonjwa mbalimbali pamoja na majeraha yaliyotokana na ajali kwa waajiriwa wasiopungua 10. Bima hii itagharimu kati ya shilingi milioni 5 mpaka milioni 200.

Akiongea katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo,Steven Lokonyo alisema bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi mpaka hosipitali, ushauri wa daktari, gharama za chumba maalumu cha uangalizi (ICU), mazoezi ya viungo, tiba ya mionzi, pamoja gharama za upasuaji.

Pia bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi kwa ndege au gari kwenda hosipitali kupata huduma za matibabu, gharama za uchunguzi za eksirei na uchunguzi wa  kimaabara.  

"Bidhaa hii tunayoileta kwenye soko inakuja kuleta mabadiliko katika sekta ya afya na itaenda mbali kusaidia biashara ndogo na za kati na makampuni makubwa hivyo kukuza ustawi pamoja na uzalishaji wa wafanyakazi wao" alisema Lokonyo.

Lokonyo alibainisha pia kwamba bima hiyo ina faida za nyongeza kama vile tiba ya ugonjwa sugu uliogunduliwa, magonjwa ambayo mtu anayo kabla ya kuanza kutumia bima,UKIMWI na magonjwa mengine kama kisukari, kansa, magonjwa ya figo, ukurutu, maumivu ya viungo, magonjwa ya ini na kadhalika.

Uzinduzi wa bima hiyo umefanyika kwa kuzingatia uhitaji wa soko pia ni mkakati wa kampuni kupanua biashara yake ya bima nchini kwa kuangalia makundi ya watu ambayo yalikuwa hayajafikiwa na huduma za bima.

"Bima hii imeanzinduliwa kwa kuangalia uhitaji wa biashara ndogo na za kati pamoja na makampuni. Kampuni yenye wafanyakazi 10 sasa inaweza kupata huduma ya bima ambayo kila mtu anajua afya ya wafanyakzi ni muhimu kwa biashara yoyoye" aliongeza Lokonyo.

Takwimu za hivi karibuni zimeonyesha kuwa matumizi ya bima nchini Tanzania ni chini ya asilimia moja ya pato la taifa ambacho ni kiwango cha chini ukilinganisha na nchi zilizoendelea na nchi nyingine nyingi za kiafrika. Katika jitihada zake za kufikia watanzania wengi zaidi, Britam inapanua matawi yake nchini ambapo kwa sasa wapo katika mikoa saba ya Dar-es-salaam, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Mtwara, na Arusha.

Kampuni ya bima ya Britam Tanzania amabayo ilijulikana kama kama 'Real Insurance' hapo mwanzo ni kampuni tanzu ya 'Britam Holdings' ambayo inatoa huduma mbalimbali za kifedha katika bima, usimamizi wa mali, na benki.

WAZIRI WA MALISILI NA UTALII AZINDUA MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NA VIWANDA MKOANI KILIMANJARO

June 04, 2017
Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya tatu ya kimataifa ya Utalii yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu Ushirika mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Devota Mdachi akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho makubwa Afrika Mashariki ya Utalii na Viwanda yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ushirika mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB,Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akisalimia wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.
Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Kili Fair inayoratibu maonesho hayo Dominic Shoo akisoma taarifa kuhsu maonesho hayo yanayofanyika wa mara ya tatu sasa .
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akitoa neno kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya Kili Fair yanayojumuisha zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi tisa.
Mkurugenzi wa Kili Fair ,Dominic Shoo akimuongoza mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo,Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe kutembelea sehemu maonesho katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimsadia Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii,TTB Bi Devota Mdachi kufika katika eneo la mfano wa Kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi (TTB) Jaji Mstaafu ,Thomas Mihayo,Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba na viongozi wengine wakiwa katika kilele cha Uhuru cha Mfano kilichopo katika maonesho yanayoendelea katika uwanja wa chuo kikuu cha ushirika mjini Moshi.
Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine mara baada ya kufungua maonesho ya Kili Fair.
Waziri Prof Maghembe akitizama ngoma ya kikundi cha jamii ya Maasai kikitoa burudani katika maonesho hayo.
Bidhaa mbalimbali na zikiwa katika mabanda ya maonesho ndani ya uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi ambako maonesho ya Kili Fair yanafanyika.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.