MPINA ABARIKI NARCO KUVUNJA MKATABA WA MWEKEZAJI MZEMBE KATIKA RANCHI YA KAGOMA

December 05, 2017
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina  akiwa na viongozi wa Mkoa wa Kagera wa Serikali mara baada ya kuwasili jana kukagua shughuli za mifugo katika Ranchi za Mifugo zilizopo mkoani hapo jana.
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina(mwenye Kofia )akitoa maelezo  ya kwa mkuu wa Wilaya ya Richard Lugango kuboresha ulinzi katika Ranchi ya Kagoma baada ya kumuamuru mwekezaji  katika Ranchi hiyo kuondoka mara moja baada ya kushindwa kutekeleza mkataba baina yake ya Serikali hapo jana.  

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina  akipima urefu wa bwawa la maji ya kunyweshea mifugo katika Ranchi ya Kagoma mkoani Bukoba ambapo aliamuru mwekezaji  Agri Vision Global Ltd katika  Ranchi ya Kagoma  mkoani Kagera kuondoka mara moja baada ya mwekezaji huyo kushindwa kutekeleza mkataba huo katika kipindi cha miaka mitano hapo jana.



Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina  akikagua eneo la ranchi ya Kagoma kuangalia  hali halisi ya uwekezaji wa shamba la mifugo hapo jana.


Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina  ameridhia  maamuzi ya Kampuni ya Ranchi za NARCO kuvunja mkataba baina ya mwekezaji Agri Vision Global Ltd katika  Ranchi ya Kagoma  mkoani Kagera na kuamuru aondoke mara moja baada ya mwekezaji huyo kushindwa kutekeleza mkataba huo katika kipindi cha miaka mitano.

Waziri Mpina ametoa maelekezo  hayo jana  alipotembelea Ranchi ya Kagoma kuangalia shughuli mbalimbali  katika Ranchi hiyo ambapo ametoa siku saba kwa mwekezaji huyo kuondoka katika eneo hilo na badala yake Serikali kupitia NARCO kuendelea kusimamia shughuli za mifugo katika Ranchi hiyo.

“Ninakuagiza  Mkuu wa Wilaya  kuanzia sasa  hakikisha unaimarisha ulinzi katika ranchi hii katika kipindi cha kukabidhi Ranchi baina ya Serikali na Mwekezaji  ili kusitokee hujuma zozote” alisisitiza Mpina

Alitaja baadhi ya mambo ambayo hayakutekelezwa na mwekezaji huyo kuwa ni pamoja na  kujenga  machinjio ya nyama,  kujenga kiwanda, kutoa gawio la shilingi bilioni tatu kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano, kutoa shilingi 2672 kwa hekta moja kama tozo la ardhi na kushindwa kuendeleza miundombinu ya NARCO waliyoikuta wakati  wanaingia mikataba hiyo miaka mitano iliyopita.

Waziri Mpina  amemuagiza Meneja Mkuu wa NARCO, Profesa  Philemoni Wambura  kuhakikisha kwamba ndani ya siku saba anampeleka Meneja katika Ranchi hiyo kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za ranchi hiyo na kuhakikisha kuwa inafanya kazi zake kisasa.

Aidha Mpina ametoa siku saba  kwa   Uongozi wa NARCO kuhakikisha kuwa imefanya tathmini  ya hasara zilizosababishwa na mwekezaji huyo ili taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi yake  ili aweze kuilipa Serikali ikiwa ni pamoja na shilingi bilioni kumi na tano kama  gawio la miaka mitano iliyokaa ambalo amesema halijawahi kulipwa hata shilingi moja.

“Sasa tumeamua kuchukua hatua na tutaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wawekezaji wasiowaaminifu wanaotaka kuihujumu serikali katika sekta hizi za mifugo na Uvuvi” alihoji Mpina

Alionya wawekezaji kuacha tabia ya kuidanganya serikali kwamba wanauwezo wa kuwekeza katika vitalu  ili wapewe lakini wanabadili matumizi baada ya kupewa. 

Aliongeza kwamba  Serikali imegundua  baadhi ya wawekezaji wanaopewa vitalu wanawakodisha wafugaji kutoka nchi jirani  na kujipatia faida wakati  Serikali haipati chochote.

Awali, akipewa ripoti ya maendeleo ya mifugo na uvuvi na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Deodatus Kinawiro mbaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba alisema kutokana na operesheni za uvuvi haramu zinazoendelea wilaya ya ngara imekamata tani 6 za samaki zilizokuwa zikipelekwa katika nchi ya burundi .

 

UNESCO LAUNCHES A CAMPAIGN WITH THE MAASAI IN NGORONGORO TO REDUCE FEMALE GENITAL MUTILATION

UNESCO LAUNCHES A CAMPAIGN WITH THE MAASAI IN NGORONGORO TO REDUCE FEMALE GENITAL MUTILATION

December 05, 2017
UNESCO, in close collaboration with the Ngorongoro District Council and the Council of Masaai traditional leaders, will conduct a large campaign to intensify efforts to address Female Genital Mutilation (FGM)in Ngorongoro, particularly during the FGM high season of December 2017 when girls go home from school and parents take the opportunity to circumcise them. The session is a continuation of a similar campaign held in June 2017 where trained campaigners managed to rescue four girls who were in the verge of being mutilated in Ngorongoro district. The December campaign will consist of three clusters: 1.A School-Based Campaign, targeting students, teachers, and school-parent committees in 28 schools (4 secondary); 2.A Community-Based campaign, targeting mostly parents and caretakers in 29 selected villages in Loliondo division through parent/caretakers village/sub-village sensitization meetings. 3.A Public Campaign through the Loliondo FCommunity Radiwhere a series of programmes will be broadcasted engaging community leaders, law enforcers, medical officials, religious leaders, former ngaribas (circumcisers) and young people. Expected to reach around 70,000 people, the campaign will kick-off with a 2-day orientation workshop in Wasso on 5 and 6December 2017. The workshop will bring together 65 campaigners and facilitators composed by district and ward officials, Maasai spiritual leaders and Maasai leaders to guide them on how best to deliver key messages to the targeted populationas well as organize for sheltering girls in need. In the Maasai community, the practice of female genital mutilation is deeply rooted in cultural practices and customary beliefs, part of the ritual passing from childhood to adulthood. According to district health statistics, in 2015, 90% (1,375) of the1693 Maasai women who gave birth at health facilities were circumcised. The Tanzania Demographic and Health Survey 2015/16 indicates that Arusha ranks third nationally on the regions where FGMis practised, with a41% prevalence, right after Manyara and Dodoma. Since 2015, UNESCO has been collaborating with government and traditional leadersin Ngorongoro district to strengthen the capacities of community-based structures to address sexual and reproductive health related issues including FGM & early marriage, facing girls and young women, as well as promoting girls education with a particular focus on school retention. Using the socio-cultural approach, UNESCO’s initiatives has gained community support and achieved notable impact including change of mind-set of some traditional leaders and more than 30 Ngaribas who are now strong advocates against the practice.