CHADEMA YAPANIA KUCHUKUA KATA ZOTE SITA KANDA YA KASKAZINI.

December 04, 2013


KATIBU WA CHADEMA KANDA YA KASKAZINI,AMANI GOLUGWA KATIKAI AKIMKABIDHI VIFAA VYA AWALI MWENYEKITI  WA CHADEMA KATA YA SUNGA JIMBO LA MLALO EDWARD NGEREZA ANAYESHUHUHIA NI KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TANGA,JONATHAN BAWEJE.



KATIBU WA CHADEMA KANDA YA KASKAZINI,AMANI GOLUGWA KATIKATI AKISISITIZA JAMBO KABLA YA KUKABIDHI VIFAA KWA MWENYEKITI WA CHADEMA KITONGOJI CHA LUANDE KATA YA KIOMONI  MWANAMTAMA BAKARI KUSHOTO NA KULIA NI KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TANGA,JONATHAN BAHWEJE.

WANACHAMA WA CHAMA HICHO MKOANI TANGA WAKIMSIKILIZA KATIBU WA KANDA YA KASKAZINI,AMANI GOLUGWA AMBAYE HAYUPO PICHANI LEO

KATIBU WA CHADEMA KANDA YA KASKAZINI,AMANI GOLUGWA AKISISITIZA JAMBO LEO.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)kimesema kuwa licha ya kuwepo msuguano wa ndani lakini kimetamba kuwa kitachukua kata zote sita zilizopo kanda ya kaskazini katika uchaguzi utakaofanyika hivi karibuni hapa nchini. 

Uchaguzi huo wa marudio unatokana na kata za Kiomoni,Mtae mkoani Tanga na Sombetini mkoani Arusha,Kiborolioni mkoani Kilimanjaro na Karachimbi Kiteto mkoani Manyara kutokuwa na madiwani wake kutokana na baadhi yao kujiuzulu na wengine kufariki dunia.


Tambo hizo zilitolewa na Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini,Amani Golugwa wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho mkoani hapa kwenye mafunzo ya Chadema ni msingi ambayo yalikuwa na lengo la kuwajengea uwezo pamoja na kukabidhi vifaa vya awali vya kampeni kwa kata zinazokabiliwa na uchaguzi huo ambazo ni Kiomoni na Mtae

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

December 04, 2013
Release No. 205
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba 4, 2013

RAIS TFF AUNDA KAMATI MBILI MAALUMU
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati mbili maalumu (ad hoc) kwa ajili ya kutathmini muundo wa ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha, na kutahmini muundo wa Bodi ya Ligi na kupendekeza namna ya kuuboresha ikiwemo kuunda kampuni.

Kamati ya Kutathmini Muundo wa Ligi inaongozwa na Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Dk. Mshindo Msolla wakati Katibu ni Ofisa Mashindano wa TFF, Idd Mshangama. Wajumbe ni Rahim Kangezi, Amri Said, Sunday Manara, Salim Bawazir na Lucas Kisasa.