MH. ZELOTE STEPHEN AFANYA ZAIRA YA SIKU TATU MWAMBAO WA ZIWA TANGANYIKA

MH. ZELOTE STEPHEN AFANYA ZAIRA YA SIKU TATU MWAMBAO WA ZIWA TANGANYIKA

May 30, 2017
ZELO
Katika kuhakikisha Mkoa wa Rukwa Upo salama kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yatakayoweza kujitokeza, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amefanya ziara ya siku tatu katika mwambao wa ziwa Tanyangika kwenye Kata ya Kirando, Kabwe na Kasanga vijiji ambavyo vipo jirani na nchi  ya DRC ili kujionea namna Halmashauri ya Nkasi na Kalambo zilivyojipanga kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hautii mguu katika Mkoa na nchi kwa ujumla.
Ziara hiyo aliianza siku ya Ijumaa tarehe 26 hadi 28. 05. 2017 mara baada ya kumaliza kumalizika kwa mafunzo ya siku tatu yaliyohusu utumaji wa taarifa za magonjwa kwa kieletroniki (e-idsr) yenye kusisitiza tahadhari ya ugonjwa wa ebola uliopo katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yaliyotolewa kwa wahudumu wa afya wa Serikali na Sekta binafsi kwa Halmashauri mbili za Manispaa ya Sumbawanga na Sumbawanga vijijini.
Mafunzo ya awamu ya pili yanatarajiwa kumalizika tarehe 31. 05. 2017 kwa Halmashauri za Kalambo na Nkasi ikiwa ni muendelezo wa awamu ya kwanza kwa Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini na Manispaa ya Sumbawanga yaliyoisha tarehe 26. Mwezi wa tano.
Ili kujiridhisha na maandalizi ya Halmashauri zinazopakana na nchi za jirani yaani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na Zambia Mkuu wa Mkoa alipita katika bandari maarufu za pwani ya ziwa Tanganyika na kuongea na vyombo vya usalama ikiwemo uhamiaji, Sumatra, TRA, jeshi la polisi, jeshi la wananchi, maafisa forodha pamoja na maafisa afya kutoka Wilayani.
Pia Mh. Zelote aliongea na viongozi wa serikali za vijiji na kata wakiwemo madiwani, watendaji wa kata na vijiji, wenyeviti wa vijiji na vitongoji, maafisa ugani wa kata na vijiji, maafisa afya wa kata na vijiji na kufanya mikutano ya hadhara ili kuwapa wananchi ujumbe aliokwenda nao katika kuhakikisha ugonjwa huo haunusi katika mkoa wa Rukwa na nchi ya Tanzania.
Pamoja nae Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu, Mratibu wa Chanjo Mkoa Gwakisa Pamoja na Afisa kutoka Wizara ya Afya wa usimamizi na ufuatiliaji Solomon Mushi, Mkuu wa Wilaya, makatibu tawala wa wilaya pamoja na kamati za ulinzi na usalama za Wilaya.
Katika kila Wilaya aliyopita Mh. Zelote alihakikisha anapewa taarifa za maandalizi ya Wilaya na kisha kwenda kwenye mipaka ili kujionea kwa macho yake maandalizi hayo na pia kuongea na wananchi wanoishi karibu na mipaka hiyo.
Wakati akiwa kwenye ziara hiyo Mh. Zelote alikuwa akisisitiza utayari pamoja na kujihadhari kwa viongozi wa serikali za vijiji na kata na pia kwa vyombo vya usalama vya maeneo hayo ya mipakani.
Katika suala la utayari Mh. Zelote Alisema kuwa wananchi wanapaswa kuelimishwa juu ya athari ya ugonjwa huo na namna ya kujikinga nao ikiwa ni pamoja na kuelezwa dalili za ugonjwa na njia za maambukizi ya ugonjwa huo na kuwasisitiza wananchi kwenda zahanati pindi wanapojiskia kuumwa na sio kukimbilia kwenye maduka ya dawa na kuagiza vidonge bila ya kujua ugonjwa anaoutibu.
Pia katika kusisitiza hilo Mh. Zelote aliwasihi wananchi kutokimbilia kwa waganga wa kienyeji pindi wanapoumwa na badala yake wakimbilie kwa wataalamu wa afya kwenye zahanati ama vituo vya afya. Na kuwaonya kuwa kupitia hizi taarifa za ugonjwa wa ebola kunaweza kukajitokeza matapeli ambao watajitangaza kuutibu ugonjwa huo jambo ambalo si kweli, hivyo aliweka msisitizo kuwa ugonjwa wa Ebola hauna Tiba.
“Mtu yeyote atakayejiskia vibaya basi haraka akimbilie kwenye zahanati ama kituo cha afya na sio kwa mganga wa kienyeji, na mjiepushe mbali  sana na matapeli wanaotibu watu vichochoroni ama wanaosema dawa ya Ebola ipo,…. Hakuna,” Mh. Zelote alieleza.
Pamoja na hayo Mh. Zelote alionya kuwa katika kusimamia jambo hilo hatakuwa na utani, dhihaka ama masihara kwayeyote atakaekiuka taratibu zilizowekwa ili kujihadhari na ugonjwa huo kuingia katika mkoa wa Rukwa.
“Mimi nafahamu kwamba watu wanaoishi humu kwenye mipaka wameoa ama kuolewa katika nchi za jirani, na kwamba watanzania utamaduni wetu ni ukarimu kwa wageni lakini katika hili tupunguze ukarimu mpaka jambo hili liishe, na yeyote atakayegundulika anamhifadhi mgeni kinyume na taratibu, huyo ni mhalifu,” Mkuu w Mkoa alisema.
Katika kuonesha athari kubwa inayoweza kupatikana endapo uginjwa huo utapenya katika nchi yetu Mh. Zelote alieleza kuwa gharama za kumshughulikia mgonjwa mmoja ni kubwa sana na kuongeza kuwa endapo ugonjwa huo unathibitishwa kwenye nchi Fulani basi tatizo hilo si la nchi hiyo tu ni la dunia nzima.
“Nguo inayotumika kumshughulikia mtu mmoja inauzwa milioni 10 na kwa wenzetu huko afrika ya magharibi Ivory Coast ambako walikumbana nao watu 11,000 walifariki, wakiwemo madaktari ambao walikuwa wakiwauguza wagonjwa, mtu mmoja tu akiupata basi kijiji kizima kinafungwa hakuna mtu kuingia katika kijiji hicho wala kutoka,” Mh. Zelote alisisitiza.
Lakini pia aliwatoa hofu wananchi na kuwaambia kuwa mpaka sasa Tanzania hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ebola.
Nae Daktari wa Mkoa Dkt. Kasululu alisema kuwa tangu ugonjwa huo kutolewa taarifa na Wizara ya Afya tarehe 12. 05. 2017 watu watatu wlikuwa wamefariki na wengine 12 walikuwa wako chini ya uangalizi lakini hadi kufuikia tarehe 25. 05. 2017 idadi ya wagonjwa iliongezeka hadi kufikia wagonjwa 45 na kuongeza kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka kadiri siku zinavyokwenda mbele.
“Idadi ya wagonjwa imekuwa ikiongezeak kila kukicha hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunajiandaa na kujihadhari kweli, maana wagonjwa hawa wapo kwenye misitu ambapo usafiri wa kawaida haufiki isipokuwa Helkopta na pikipiki, hivyo wagonjwa wanaweza kuwa wengi na bado hawajajulikana,” Dkt Kasululu alisisiza.
Nae Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Dk. Makundi Maige alielezea mikakakti ya Halmashauri ya Nkasi namna ilivyojipaga kuhakikisha wanakaa mbali na ugonjwa hatari wa Ebola.
“ Wilaya imeainisha kata tatu za Kirando, Kabwe na Wampembe ambazo zimetengwa kwaajili ya kupokea wageni kutoka nchi za jirani, tukifahamu kuwa katika mwambao wa Ziwa Tanganyia kuna Kata 10 ambazo ugonjwa huu unaweza kuingia kwa urahisi, ambazo ni Kabwe, Kirando, Wampembe, Itete, Kipili, Mkinga, Korongwe, Ninde, Kizumbi na Kala,” Dk. Makundi aliainisha.
Katika kubainisha upokezi wa wageni hao Dk. Makundi alisema kuwa kituo cha Wampembe kitapokea wageni wanoelekea kijiji cha Kilambo hadi Msamba, Kituo cha Kirando kitapokea wageni wanaoelekea kijiji cha Ninde hadi Kazovu na kituo cha Kabwe kitapokea wageni wanaoelekea kijiji cha Utinta hadi Kalila.
Na kuongeza kuwa wageni wote kutoka nchi za jirani watalazimika kupitia katika vituo hivyo na sio kuingia kiholela kama ilivyozoeleka na kabla ya kuendelea na safari zao watakuwa wakichunguzwa afya zao.
Kwa kuzingatia namna ugonjwa huo unavyoenea Wilaya imetenga eneo maalum kwaajili ya matibabu ili kuepuka kuchanganya wagonjwa watakaobainika kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola.
Pamoja na hayo Wilaya imejipaga kuzizungukia kata zote 10 na kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wa maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha viongozi wa dini, wazee maarufu, vijana, waalimu na wanafunzi juu ya ugonjwa huo hatari.
Nao upande wa Wilaya ya Kalambo  walieleza mipango yao juu ya udhubiti wa ugonjwa huu, ambapo mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Alcado mwamba aliweza uainisha tahadhari mbalimbali ambazo Wilaya imezichukua kuhakikisha wanaudhibiti ugonjwa huo kutokuingia katika Wilaya hiyo.
Miongoni mwa tahadhari walizochukua ikiwa ni kuwasambazia wananchi vipeperushi vyenye kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola lakini pia kuihamasisha jamii kutoa taarifa haraka kwa uongozi wa serikali pindi tu wakibaini kuna mgeni aliyeingia kinyume na taratibu zilizowekwa.

NCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUWEKEZA KATIKA KILIMO

May 30, 2017
 Meneja wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB), Daniel Otunge, akizungumza wakati akitoa mada kwenye semina ya siku tatu iliyowakutanisha wanahabari na watafiti wa kilimo kutoka nchi tano za Afrika Uganda, Kenya, Burknafaso, Ethiopia na Tanzania ambayo ilikuwa mwenyeji wa semina hiyo iliyoanza juzi jijini Mwanza.

TWIGA CEMENT KUENDELEA KUWA VINARA WA UZALISHAJI SARUJI LICHA YA KUIBUKA KWA MAKAMPUNI MENGINE NCHINI

May 30, 2017
                   Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kampuni ya Saruji nchini ya Tanzania Portland Cement inayozalisha Twiga Cement, imesema kuwa itaendelea kuwa kinara kwa mauzo ya Saruji hapa nchini, licha ya kuwepo wa viwanda vingi katika miaka ya hivi karibuni.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Alfonso Velez, alipokuwa akitoa ripoti ya mauzo ya kampuni hiyo na changamoto inazokabiliana nazo katika mkutano wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

“licha ya makampuni mengine kuja na mpango wa ujanja wa kushusha gharama za saruji bado Twiga Cement imeendelea kuwa ndio saruji bora kwenye soko licha ya changamoto ya kupambana na bei ya soko”

Amesema wao wameshuhudia wakiona washindani wao wakihangaika juu ya upataji wa mali ghafi ambazo zitaweza kuwasaidia kuendelea kufanya bishara kwa bei ya chini lakini TPCC bado haijatetereka.

Amesema kuwa mshindani wake bado ana wakati mgumu kwani yuko mbali na soko na inamchukua muda mrefu kusafirisha mzigo mpaka sokoni hivyo wakati wowote atapandisha bei ya saruji na Twiga itabaki pale pale, kwani ameweza kufanya hivyo katika nchi zingine alizowekeza ambapo amepandisha bei kuwa juu hili kufidia gharama za uzalishaji.
Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya TPCC , Osward Urasa akizungumza katika mkutano huo juu ya wanahisa kutoa taharifa zitakazosidia kujenga kampuni kuzidi kuwa imara.
Mwenyekiti wa kampuni ya Tanzania Portland Cement, Alfonso Rodriguez akizungumza katika mkutano huo wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika leo katika hotel ya Ramada
Mkaguzi wa Mahesabu wa kampuni hiyo kutoka kampuni ya Ernist nd Young , Elibariki Fanuel akieleza juuya mehesabu ya mwaka ya kampuni hiyo
Mkurugenzi wa Twiga Cement Alfonso Velez akizungumza juuya mafanikio ya kampuni hiyo mara baada ya kuwepo wa ushindani wa makampuni mengine nchini
Sehemu ya Wanahisa katika mkutano huo wakiwa wanasikiliza kwa makini

MAGHEMBE APONGEZA OPERESHENI YA KUONDOA MIFUGO HIFADHINI MKOANI KAGERA

May 30, 2017
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akisalimiana na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera katika ziara yake mkoani humo kuzungumzia operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria na mahakama. Anayeongoza utambulisho huo (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba kuhusu operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro. 

NA HAMZA TEMBA - WMU
---------------------------------------------------------

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Kagera unaongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu kwa kufanikisha operesheni ya kuondoa mifugo katika maeneo ya hifadhi mkoani humo huku akitoa tahadhari kwa watumishi wa hifadhi hizo kupoteza ajira zao endapo wataruhusu mifugo hiyo kurudi tena katika hifadhi hizo.

Ametoa pongezi na tahadhari hiyo jana mjini Bukoba wakati akizungumza na uongozi wa mkoa huo na kusema kuwa, kazi hiyo ni ya kupongezwa sana kwakua imeleta matumaini ya uhifadhi mkoani Kagera na taifa kwa ujumla.

“Napenda niwashukuru kipekee kabisa kwa jinsi ambavyo mlifanya ile operesheni ya kuondoa mifugo kwenye hifadhi zetu, tulifanya kwa ueledi uliotukuka, hata kama umesikia watu wanalalamika lakini hakuna aliyesema kuku wangu waliuawa, walipigwa risasi, tulinyang’anywa mifugo, kazi hii ilifanywa vizuri na kwa ueledi mkubwa sana”, alisema Prof. Maghembe.

Aliongeza, “Hatutaruhusu tena mifugo hiyo irudi huko ndani ya hifadhi, hili ni jambo kubwa ambalo ni wajibu wa wahifadhi wote kuhakikisha  kwamba hakuna mifugo itakayokuwa inaingia humo ndani, Kuanzia sasa kama tutakuta mtu ameingia kwenye hifadhi yako wakati tunamuondoa tunamuondoa yeye na wewe na familia yako yote ili mbegu yako mbaya isibaki katika uhifadhi wa wanyamapori”.

Alisema ili kuimarisha ulinzi katika hifadhi hizo, utaratibu wa kutumia ndege maalum za doria na “drones” (ndege zisizo na rubani) utawekwa ili kuwabaini wahalifu watakaokuwa wamekaidia agizo hilo ili wachukuliwe hatua za kisheria.  

“Tutakua tunarusha ndege mara moja kila baada ya wiki tatu au wiki mbili kuhakikisha kwamba hakuna mtu anaingia na mifugo humo ndani, lakini pili tutafanya doria na ndege zile ambazo hazina marobani kuhakikisha kwamba tunaangalia kinachotokea humo ndani wakati wote.

“Najua wanaweza kubadilisha “system” (utaratibu) ikawa ya usiku na hawa askari hawa tutawapa mafunzo maalum chini ya jeshi la wananchi wa Tanzania, kuanzia miezi sita mpaka tisa, wajifunze namna ya kuhangaika na hawa ambao wanaingia kwenye hifadhi zetu”, alisema. 

Akizungumzia operesheni hiyo, alisema ulitolewa muda maalum kwa watu kutoa mifugo yao kwa hiari katika mapori ya akiba na hifadhi za misitu mkoani humo ambapo wale wote waliotii hakuna mashtaka yeyote yalifunguliwa dhidi yao ispokuwa wale waliokaidi walifikishwa mahakamani na mifugo yao ikataifishwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori kifungu namba 111 sehemu ya kwanza ambayo inaruhusu kutaifisha mali itakayokutwa hifadhini.

Alisema kuwa kumekuwepo na malalamiko mbalimbali juu ya utaratibu wa upigaji mnada mifugo iliyotaifishwa ikiwemo minada hiyo kufanyika ndani ya maeneo ya hifadhi, wenye mifugo kutoruhusiwa kuingia na wakati mwingine kuwepo kwa malalamiko ya idadi tofauti ya mifugo iliyotaifishwa na inayopelekwa mnadani.

Ili kuondoa malalamiko hayo alielekeza kuwa baada ya amri ya mahakama kutoka ni lazima mamlaka ya Wilaya husika ijulishwe na zoezi hilo lifanyike katika maeneo ya wazi ili kila mwananchi anayehitaji aweze kushiriki mnada husika.

“Minada hii ifanywe kwa maelekezo ya mamlaka, hukumu ikitoka mkuu wa wilaya ajulishwe, na kwamba mifugo kadhaa itapigwa mnada, na yeye ataamua mnada ufanyike wapi na lini, na iwe sehemu ambayo kila mtu anaweza kufika, minada hiyo iwe ya wazi na matangazo yatolewe ili malalamiko yasiwepo ndio maana maelekezo yametoka minada isitishwe kwa muda wa siku saba mambo haya yawekwe sawa”, alisema Maghembe.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu alishukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka Wizara ya Maliasili katika kipindi chote cha utekelezaji wa operesheni hiyo ambayo amaeielezea kuwa na mafanikio makubwa ikiwemo wanyamapori kuanza kurudi kwenye maeneo yao katika Mapori ya Akiba ya Biharamulo Burigi na Kimisi.

“Niishukuru wizara yako mmetupa ushirikiano mzuri, kule tumesafisha tumehakikisha hakuna mifugo, hakuna kilimo, vitendo mbalimbali vya kibinadamu vilivyokuwa vikifanywa kule vya kilimo, ukataji miti hovyo, kuchoma mikaa, kulima mashamba mbalimbali ya mahindi, bangi, mirungi sasa hayapo tena, Nashukuru kwa muda huu mfupi wanyama wengi wamesharudi, wengi tuu, hadi Simba wamesharudi kwenye maeneo yao” alisema Kijuu.

Operesheni ya kuondoa mifugo na wananchi waliovamia Hifadhi ya Misitu ya Biharamulo, Nyantaka na Ruiga na Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi na Kimisi mkoani Kagera ilianza tarehe 30 Machi, 2017 ambapo jumla ya mifugo 5,939 ilikamatwa (Ng’ombe 5754, Mbuzi 140 na kondoo 45) na watuhumiwa 185 walikamatwa na kufikishwa mahakamani.  
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba kuhusu operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro (kulia), Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Diwani Athuman (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba. 
Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili (katikati waliokaa) na kamati ya ulinzi na usala ya Mkoa wa Kagera muda mfupi baada ya kikao cha kujadili operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria.

MFUKO WA PPF WAENDELEA KUKABIDHI VIFAA TIBA

May 30, 2017
Mfuko wa Pensheni wa PPF umeendelea kukabidhi vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya nchini kulingana na sera yake ya uchangiaji na udhamini. 
 
Katika wilaya ya Kisarawe, Mfuko wa PPF umekabidhi vifaa tiba hivyo kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jaffo kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambavyo ni vitanda 2 vya kujifungulia wakinamama, vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida, mashuka 56 na vifaa vinavyotumika kujifungulia wakinamama. Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Jaffo alisema Mfuko wa PPF walichofanya ni jambo kubwa kwa vile hospitali za wilaya ya Kisarawe zilikuwa zikikabiliwa na changamoto katika sekta ya afya. 
 
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, alisema Mfuko umetoa vifaa tiba hivyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kurudisha kwenye jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya PPF. Alisema Kisarawe ni wilaya ya nne kupata vifaa hivyo na kwamba wataendelea kutoa kwenye hospitali nyingine 12 nchini. 
 
Lulu alisema Mfuko wa PPF, umetoa vifaa tiba vyenye jumla thamani ya Sh. 99,983,700/-. Shughuli hiyo ya kukabidhi vifaa tiba kutoka Mfuko wa PPF ilienda sambasamba na taarifa ya kukabidhi vifaa tiba kutoka kwa Mfamasia Mfawadhi wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI),Regina Joseph kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jafo, alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli ametoa vitanda 20 vya kulalia, vitanda sita vya kujifunguli. Vifaa kama hivyo vinasambazwa katika hospitali nyingine nchi nzima.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akiongea na wafanyakazi na wananchi waliojitokeza katika halfa ya kupokea vifaa tiba ikiwemo vitanda 2 vya kujifungulia wakinamama, vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida, mashuka 56 na vifaa vinavyotumika kujifungulia wakinamama kutoka kwa Mfuko wa PPF katika kutekeleza sera yake ya uchangiaji na udhamini. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG-KISARAWE. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Nedesa akielezea machache juu ya changamoto zilizokuwa zikiikabili wilaya yake katika upande wa afya. Pembeni yake ni Naibu wa Waziri (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Hamis Dikupatile. Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Lulu Mengele akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika jana katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.

WAANDISHI WA HABARI ZA KILIMO TANZANIA (TAJF) WAKUTANA MALAIKA BEACH RESORT JIJINI MWANZA KUPANGA MIKAKATI

May 30, 2017
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo Tanzania (TAJF), Gerald Kitabu (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wanachama wa TAJF wakati wa kikao kilichofanyika Ufukwe wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza jana kujadili masuala mbalimbali ya chama hicho.
MBIO ZA MWENGE WA UHURU ZAZINDUA MNARA WA ASKARI JIJINI DAR ES SALAAM

MBIO ZA MWENGE WA UHURU ZAZINDUA MNARA WA ASKARI JIJINI DAR ES SALAAM

May 30, 2017
ask1
Muonekano wa Mnara wa Askari uliopo kati ya barabara  ya Azikiwe na Samora mara baada ya kuzinduliwa mapema hii leo na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa 2017,Amour Hamad Amour.
ask2
Mwenge wa Uhuru ukiwasili katika bustani ya Mnara wa Askari uliopo kati ya barabara  ya Azikiwe na Samora kwa ajili ya ya uzinduzi wa bustani hiyo uliofanywa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa 2017,Amour Hamad Amour.
ask3
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa 2017,Amour Hamad Amour (katikati) akipata maelezo toka kwa msimamizi wa bustanai ya mnara wa Askari uliopo kati ya barabara  ya Azikiwe na Samora mara baada ya kuizindua bustani hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam,
ask4
Baadhi ya wananchi wakishuhudia tendo la uzinduzi wa bustanai ya mnara wa Askari uliopo kati ya barabara  ya Azikiwe na Samora mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
ask5
Baadhi ya wananchi wakishuhudia tendo la uzinduzi wa bustani ya mnara wa Askari uliopo kati ya barabara  ya Azikiwe na Samora mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
ask6

MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA JIJINI TANGA

May 30, 2017
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko huo kwa wakazi wa Jiji la Tanga kwenye banda lao lililopo katika eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara ya kimataifa
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akiptia kwenye banda la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) wakati alipofungua maonyesho ya kimataifa ya  biashara ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akisalimiana na mmoja wa watumishi Tanapa wakati wakati alipotembelea banda lao kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akiendelea na shughuli ya kukagua mabanda ya Maonyesho
Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao
 Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao
 Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao

 Maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakitoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Tanga katika Banda lao lililopo kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunapofanyika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tano kutoka kushoto ni Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo katikati ni Sabrina Komba ambaye ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu na kulia ni Afisa matekelezo Macrina Clemens
 kulia ni Sabrina Komba ambaye ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kulia ni Afisa matekelezo Macrina Clemens wakimsikiliza kwa umakini mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alifika kwenye banda lao kupata ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na mfuko huo
 Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemens kulia akisitiza jambo kwa mkazi wa Jiji la Tanga kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali muhimu ikiwemo za matibabu kushoto ni Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga,Ally Mwakababu katikati ni  Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kulia kwake ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu Sabrina Komba

 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akiwa na maafisa wengine wa mfuko huo wakiwa tayari kutoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Tanga kuhusu namna wanavyoweza kunufaika kupitia mfuko huo
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alitembelea banda lao
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao kuhusu faida za wakazi wa Jiji la Tanga kujiunga na mfuko huo lakini pia namna walivyojiandaa na ujio wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga

MWENGE WA UHURU KUWASILI WILAYA YA UBUNGO KESHO 31 MEI 2017

May 30, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Kibamba Chama-Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza na Waandishi wa habari

Mwenge wa Uhuru Mwaka 2017 utawasili kesho Tarehe 31 Mei 2017 katika Wilaya ya Ubungo kuanzia saa moja kamili asubuhi na kuzuru katika Miradi mitano ya Maendeleo.   
     
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amesema kuwa katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Mradi mmoja wa kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la msingi.

Alisema kuwa Miradi mingine itakayozinduliwa ni Mradi wa Ujenzi wa Jengo la kutolea huduma za VVU katika Kituo cha afya Mbezi, Uzinduzi wa madarasa nane katika shule ya Msingi Malambamawili iliyopo Kata ya Msigani, Uzinduzi wa Kituo cha mabasi SIMU 2000 Kata ya Sinza na Uzinduzi wa Zahaanti ya Mburahati.

Mhe Makori alisema kuwa Miradi yote hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu Bilioni 2,854,647,991.89

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amewasihi wakazi wa Manispaa ya Ubungo kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru ambao utawasili katika eneo la SAISAI Kata ya Gobaukitokea Manispaa ya Kinondoni.

Pia amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Barafu, Shule ya Msingi Mburahati kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru.

Imetolewa Na:
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo