MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MZEE KINGUNGE

February 05, 2018
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili, Alhaji Alli Hassan Mwinyi akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho.
 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili, Alhaji Alli Hassan Mwinyi akitoa heshima zake mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho.
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya msiba  wa Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kutoa heshima za mwisho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa mwanasiasa mkongwe na kiongozi wa muda mrefu marehemu Kingunge Ngombale Mwiru kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  
 Mama Maria Nyerere akiwasili katika viwanja vya Karimjee
 Baadhi ya viongozi wa kiserikali na chama wakiwa  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuagwa kwa mwili wa Kingunge Ngombale Mwiru
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Maria Nyerere wakati wa kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya Karimjee. 
Mwili wa Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru  ukiwasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa leo
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na baadhi ya viongozi wa kiserikali na chama wakiwa  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuagwa kwa mwili wa Kingunge Ngombale Mwiru
 Baadhi ya wanafamilia wa Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru wakiwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuagwa kwa mwili wa Kingunge Ngombale Mwiru
 Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru likiwa kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole mtoto wa kiume wa marehemu Kingunge anayefahamika kwa jina la Kinjekitile mara baada ya kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya Karimjee.

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MAZIKO YA MWANASIASA MKONGWE MAREHEMU MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

February 05, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mara baada ya kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye Kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuweka udogo kwenye kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Wajukuu wa marehemu pamoja na wafiwa wengine wakiwa katika hali ya majonzi makaburini hapo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waombolezaji mara baada ya maziko ya marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


WAZIRI KIGWANGALLAH AWASHUKIA VIONGOZI WANAOTAKA KUFUTWA KWA MAENEO YA HIFADHI

February 05, 2018
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa kwanza )  pamoja na  Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa tatu ) wakiruka viunzi  wakati walipotembelea  jana ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi katika  eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ambao umeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa   kufutwa  ili kujenga  mji mpya wa kitalii katika mkoa huo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu ambao alikutana nao kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo katika kikao cha  tatu cha kamati hiyo kilichofanyika jana mkoani Iringa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa pili kulia) Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) wakiwa wameambatana na   Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (katikati) wakipatiwa maelezo na Mkuu wa Idara ya mipango miji wa Halmashauri ya Iringa,  Wilberd Mtongani ( wa tatu kushoto) wakati walipotembelea eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi  ya kuhaulisha eneo hilo. Wengine ni Watalaamu ni wataalamu kutoka ofisi ya Mkoa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa tatu kulia)  Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) wakiwa na Mwenyekiti wa  Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu, Prof. Shabani Chamshama (wa kwanza kushoto)  wakipatiwa maelezo na Afisa  mipango miji wa Halmashauri ya Iringa,  Wicliph Benda ( wa tatu kushoto) wakati walipotembelea eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi  ya kuhaulisha eneo hilo. Wengine ni Watalaamu ni wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

 Naibu Waziri wa Wizara  Japhet Hasunga ( wa kwanza ) akiwa ameambtana na wataalam kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa wakiruka viunzi  wakati alipotembelea  jana ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi katika  eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ambao umeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa   kufutwa  ili kujenga  mji mpya wa kitalii katika mkoa huo
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa pili kushoto) akiwa pamoja na  Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga ( wa tatu kushoto) wakioneshwa ramani ya     eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo na  Mkuu wa Idara ya mipango miji wa Halmashauri ya Iringa  Wilberd Mtongani ( wa kwanza kulia) wakati walipotembelea eneo  hilo kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi  ya kuhaulisha ili kujenga mji mpya wa kitalii mkoani Iringa

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa kwanza kulia ) akiwa pamoja na  Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dkt. Ezekiel Mwakalukwa  ( katika ) wakati walipotembelea jana   eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi wa eneo hilo ambalo limeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa  kuhaulishwa ili kujenga  mji mpya wa kitalii katika mkoa huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza  wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu ambapo Waziri Kigwangallah anakutana nao kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo katika kikao cha tatu kilichofanyika jana mkoani Iringa.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu wakimsikiliza Waziri Kigwangallah katika kikao cha tatu kilichofanyika jana mkoani Iringa.
 Mwenyekiti wa  Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu, Prof. Shabani Chamshama akitoa neno la shukrani kwa viongozi  kwa niaba ya Wajumbe wa kamati hiyo katika kikao cha tatu kilichofanyika jana mkoani Iringa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangallah,( wa kwanza kulia ) akiwa ameambatana na wataalam wakati alipotembelea jana   eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo  ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi wa eneo hilo ambalo limeombwa na uongozi wa mkoa wa Iringa  kuhaulishwa ili kujenga  mji mpya wa kitalii katika mkoa huo.
 Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza ( wa pili kushoto) akiwa ameambatana na baadhi ya waandishi wa habari pamoja na wataalamu kutoka mkoani wakitembea kuangalia mipaka ya eneo la msitu wa hifadhi wa Kihesa Kilolo ambao umeombwa na uongozi wa mkoa huo   kufutwa ili kujenga  mji mpya wa kitalii katika eneo hilo.

         (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangallah amesema kuwa hatajibu maombi yoyote yaliyowasilishwa ofisini kwake kutoka kwa  Wakuu wa mikoa, Halmashauri pamoja na  Wakuu wa wilaya  ya kufuta  maeneo ya Hifadhi ili maeneo hayo  yaweze kutumika Kwa ajili ya  matumizi mengine.

Amesema kuwa maeneo hayo yalitengwa kisheria na yana umuhimu mkubwa kiuchumi na kijamii hivyo lazima yaendelee kuhifadhiwa kwa ajili ya faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Amesema katika kipindi  cha Uwaziri wake hatajibu ombi lolote lile linalohusu kubadili matumizi ya maeneo hayo kwa vile kuwa na misitu sehemu za mijini ni sehemu ya maendeleo.

Aliyasema hayo jana   mjini Iringa wakati alipokuwa akizungumza kwa mara ya kwanza na kamati ya kitaifa ya ushauri wa misitu iliyokutana kwa ajili ya kufanya kikao chake cha tatu tangu ilipoundwa mwaka jana ikiwa pamoja na kutembelea msitu wa Hifadhi wa kihesa Kilolo uliiombwa na uongozi wa mkoa kufutwa ili upate kutumika kwa kuweka miundo mbinu mipya ya mji wa kitalii.

Katika kikao hicho ambacho Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alishiriki, Waziri Kigwangallah  alimuomba Mkuu  huyo awafikishe ujumbe  Wakuu wa mikoa wengine  ambao walituma na wanaotarajia kutuma maombi ya namna hiyo kuwa yeye  hatakaa ayajibu hadi pale  tu yule  aliyemteua ampe maelekezo na si vinginevyo"

Amesema kuwa  Halmashauri nyingi nchini kila zikiona maeneo ya Hifadhi zimekuwa zikifikiria kubadili matumizi ya maeneo hayo ili yatumike kwa shughuli zingine za maendeleo kama vile kupima viwanja  ili kuwauzia wananchi kwa lengo la kukusanya mapato.

"Ofisin kwangu kuna maombi mengi mno ambayo hata sielewi nianze na lipi na niache lipi, nasema sitajibu ombi lolote lile" alisisitiza Waziri Kigwangallah.

Aidha,  Waziri Kigwangallah   mara baada ya kuzungumza na kamati hiyo alitembelea eneo la hifadhi ya msitu huo huku akiwa ameongoza na kamati hiyo  pamoja na Uongozi wa Mkoa wa huo .

Katika kutembelea eneo hilo, Waziri Kigwagwallah aliwashukia viongozi wa Halmashauri  kwa kuanzisha dampo   katika  eneo hilo  huku kamati ikijionea magari matatu ya taka yakiendelea kumwaga uchafu kwenye eneo hilo jambo ambalo ni kinyume na sheria za uhifadhi.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Japhet Hasunga  aliwashukia watendaji wa mkoa huo  wakati  walipokuwa wakipishana kutoa maelezo kuhusiana na mipaka na matumizi ya eneo hilo endapo Wizara itaridhia ombi lao la  kubadili matumizi ya eneo hilo.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza  alimuhakikishia Waziri kuwa eneo hilo endapo watapewa litatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.

Waziri Kigwangallah mara baada ya kutembelea eneo hilo wakati akitoa majumuisho yake, Alisema kuwa kufuatia ziara hiyo anasubili ushauri utakaotolewa na kamati ya kitaifa ya msitu ndipo atakapokuwa na  jibu kuhusiana na ombi  la kubadilia matumizi la eneo hilo .

Pia, Waziri Kigwangallah aliiagiza ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kuwa maeneo ya milima kwa vile sio moja ya  maeneo ya hifadhi  yaongezwe katika eneo la hilo  lengo  likiwa ni kuzuia uharibifu wa uoto wa asili unaoendelea katika maeneo hayo.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati hiyo wakati akitoa neno la shukrani alimhakikishia Waziri kuwa watamshauri jambo lolote lile  linalohusu misitu bila kujali litamfurahisha au litamuudhi, kitakachoangaliwa hapo ni maslahi mapana ya taifa.


Katika hatua nyingine ,Waziri Kigwangallah  ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu nchini  (TFS) kuanza kuweka nguvu nyingi katika kuhifadhi misitu baadala ya kuvuna na kufanya biashara ya mazao ya misitu.

Alisema licha ya kuwa TFS imekuwa ikifanya vizuri katika baadhi ya maeneo  lakini katika suala la kuhifadhi misitu imekuwa kama vile  sio kazi yake    " yenyewe kazi yake imekuwa  ni kuvuna kilichopandwa, kuuza na kukusanya mapato yatokanayo na mazao ya misitu" alisema. 

Wakati huo huo, Waziri Kigwangallah amesema Wizara inakusudia kuchukua misitu yote iliyo chini ya vijiji na Halmashauri kwa vile zimeshindwa kuisimamia ipasavyo na hivyo kupelekea sehemu kubwa ya nchi kugeuka kuwa jangwa.

Mbali na hilo amewaonya wananchi wanaowazuia watendaji  kuweka vigingi katika mipaka ya hifadhi, huku wengine wamekuwa wakivingoa na wengine kuhamisha vigingi hivyo kutoka eneo moja hadi jingine kuwa  waache tabia hiyo moja la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. .

POLEPOLE AZINDUA MUONEKANO MPYA WA GAZETI LA UHURU LEO JIJINI DAR ES SALAAM

February 05, 2018
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Idara ya Itikadi na Uendezi Humphrey Polepole (wapili kushoto) akifurahia nakala ya gazeti la Uhuru baada ya kuzindua muonekano mpya wa gazeti hilo katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Uhuru Publications Limited UPL), mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Said Nguba aliyewahi kuwa Mhariri Mtendaji wa UPL, na Wengine kutoka watatu kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Rhoda Kangero, Mhariri Mtendaji wa zamani wa UPL Jose[h Kulangwa na Kaim Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali
MWANZO
 Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Rdhoda Kangero akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa UHURU FM Angel Akilimali (kulia) wakati akimsubiri Polepole kuwasili ofisi za UPL kuzindua muonekano mpya wa gazeti la Uhuru, leo
 Katibu wa NEC ya CCM Humphrey Polepole akisalimiana na baadhi ya maofisa wa UPL baada ya kuwasili. Kushoto ni Kaimu MJhariri Mterndaji wa UPL Rhoda Kangero na kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali.
 Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Rhoda Kangero akimpeleka Ndugu Polepole ofisini
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ofisini kwa Mhariri Mtendaji wa UPL. Kulia ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Rhoda Kangero
 Ndugu Polepole akizungumza jambo na Kangero
 Baadhi ya waliowahi kuwa Wahariri Watendaji wa UPL wakiwa katika Ofisini ya |Mhariri Mtendaji wa UPL. Kutoka kushoto ni Jacquelin Liana, Joseph Kulangwa na Saidi Nguba. Kushoto ni Kamimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza na Viongozin wa UPL na wageni waalikwa katika Ofisi ya Mhariri Mtendaji wa UPL
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akifungua mfuko wenye gazerti la Uhuru, kuzindua muonekano mpya wa gazeti hilo leo. Kulia ni kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Rhoda Kangero na Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa zamani saidi Nguba
Polepole akionyesha furaha yake baada ya kuzindua muonekano mpya wa gazeti hilo la Uhuru
Mhariri Mtendaji wa zamani Joseph Kulangwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali wakifurahia nakala ya Uhuru lenye muonekano mpya baada ya kuzinduliwa muonekano huo
 Polepole akilifurahia nakala ya Uhuru akiwa akiwa na viongozi kadhaa wa UPL na waalikwa baada ya kuzindua muonekano mpya wa gazeti hilo leo
  Polepole akilifurahia nakala ya Uhuru akiwa akiwa na viongozi kadhaa wa UPL na waalikwa baada ya kuzindua muonekano mpya wa gazeti hilo leo
 Polepole akilifurahia nakala ya Uhuru akiwa akiwa na viongozi kadhaa wa UPL na waalikwa baada ya kuzindua muonekano mpya wa gazeti hilo leo
 Baadhi ya wafanyakazi wa UPL wakiwa na nakala za gazeti la Uhuru lenye muonekano mpya. Wapili kushoto ni Mhariri wa habari wa Uhuru FM Pius Ntiga
 Polepole na wafanyakazi wa UPL na waalikwa wakiendelea kulitazama gazeti hilo la Uhuru lenye muonekano mpya.
 Polepole akimshukuru Kulangwa kwa kuhudhuria hafla hiyo. Kushoto ni Said Nguba
 Polepole na msafara mzima wakienda chumba cha habari kujadili muonekano mpya wa gazeti hilo
 Polepole na msafara mzima wakienda chumba cha habari kujadili muonekano mpya wa gazeti hilo
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Polepole akizungumza jambo na Kaimu Mhariri Mtendaji Ndugu Kangero wakati msafara ukienda katika chumba cha habari
 Kangero akiongoza msafara kuingia katika chumba cha habari cha UPL
Polepole,  Watumishi wa UPL na wageni waalikwa wakiwa wamesimama kufanya dua kabla ya kuanza kulijadili Uhuru 
 Kila mmoja akiwa makini kulisoma Uhuru wakati wa mjadala
  Kila mmoja akiwa makini kulisoma Uhuru wakati wa mjadala
  Kila mmoja akiwa makini kulisoma Uhuru wakati wa mjadala
 Mkutubi wa UPL Mussa Salmin akilipitia kwa makini gazeti la Uhuru
 Kaimu Naibu Mhariri Mtendaji wa UPL Rashid Zahor akilipia kwa makini gazeti la Uhuru. Kulia ni Kaimu Mhariri Mtendaji Roda Kangero
 Wahariri watendaji wa zamani wa UPL Said Nguba na Joseph Kulangwa wakipita gazeti hilo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM angel Akilimali
 Kaimu Mhariri Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM Angel Akilimali akilisoma kiwa makini gazeti la Uhuru  Mhariri wa habari wa Uhuru FM Pius Ntiga akisoma kwa makini gazeti la Uhuru lenye muonekano mpya. Kushoto ni Jacqueline Liana
 "Unaona hiyo?" Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Rhoda Kangero akimuonyesha moja ya habari picha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole alipokuwa akipitia nakala ya gazeti loa kwanza la Uhuru lililoanza kuchapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1961
 Polepole akilitazama kwa makini nakala hiyo ya kwanza ya gazeti hilo la Uhuru
 "Ohhh... very nice" akasema Polepole wakati akitazama nakala ya gazeti hilo la uhuru la mwaka 1961
 "Safi sana,," akasema tena Polepole
 Polepole akionyesha nakala ya gazeti la kwanza la Uhuru la mwaka 1961. Kulia ni Kangero
 Mtangazaji wa Uhuru FM Ndugu Amina  akisoma gazeti la Uhuru kwa makini
 Mjadala wa gazeti ukiendelea
 Mhariri Mwandamizi wa UPL Jane Mihanji (kushoto) akifuatilia kwa makini mjadala wa gazeti sehemu ya mengineyo. Kulia ni kaimu Mhariri wa Makala Selina Wilson
 Ndani ya chumba cha habari cha UPL wakati mjadala ukiendelea
 Mhariri Mtendaji wa zamani Said Nguba akisoma kwa makini nakala ya Uhuru lenye muonekano mpya
 Mfanyakazi wa Idara ya |Matangazo UPL akiuliza jambo kuhusu uboreshwaji wa upande huo kwenye gazeti la UPL
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Polepole akizungumza kukamilisha mengineyo ya mjadala wa gazeti hilo la uhuru
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Polepole akizungumza kukamilisha mengineyo ya mjadala wa gazeti hilo la uhuru
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Polepole akizungumza kukamilisha mengineyo ya mjadala wa gazeti hilo la uhuru
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Polepole akizungumza kukamilisha mengineyo ya mjadala wa gazeti hilo la uhuru
 Ndugu Poloepole akiagana na Ndugu Masota wakati akiondoka. Kushoto ni Ndugu Rhoda
 Wafanyakazi wa UPL wakiwa katika picha ya kumbukumbu baada ya uzinduzi huo wa muonekano mpya wa gazeti la Uhuru. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO -- Best regards ...