MASAUNI AHITIMISHA ZIARA YAKE MIKOA YA KUSINI KWA KUTEMBELEA GEREZA LA KILIMO NA MIFUGO LAMAJANI, WILAYANI MASASI, MKOA WA MTWARA

MASAUNI AHITIMISHA ZIARA YAKE MIKOA YA KUSINI KWA KUTEMBELEA GEREZA LA KILIMO NA MIFUGO LAMAJANI, WILAYANI MASASI, MKOA WA MTWARA

March 26, 2017
sau1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Seleman Mzee, wakati alipokuwa anawasili wilayani humo, Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
sau2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiongozwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa (kulia), kuingia Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasikwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
sau3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anamfafanulia jambo mara baada ya kutoka ndani ya Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi kwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
sau4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anatoa maelezo kuhusu Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi. Gereza hilo lina wafungwa zaidi ya 60 ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. Kikao hicho kilifanyika ofisi ya Mkuu wa Gereza hilona kuhudhuriwa na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo vilivyo chini ya wizara yake pamoja na viongozi wa wilaya hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
sau5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiiangalia moja ya nyumba za askari magereza zilizopo jirani na Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara. Katikati ni Mkuu wa Magereza Mkoa huo (RPO), Ismail Mlawa. Kushoto ni Ahmed Bakari, Kaimu Mkuu wa Gereza hilo. Masauni alimaliza ziara yake ya mikoa ya kusini kwa kutembelea Gereza hilo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
RC NDIKILO AGEUKA MBOGO KWA VYAMA USHIRIKA VYA MSINGI VYA KOROSHO(AMCOS)

RC NDIKILO AGEUKA MBOGO KWA VYAMA USHIRIKA VYA MSINGI VYA KOROSHO(AMCOS)

March 26, 2017
images
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo,ametoa wiki mbili kwa vyama vya ushirika vya msingi vya korosho,vya Rifiji, Kibiti na Mkuranga,kwenda kujieleza kwa wakuu wa wilaya zao kuhusu upotevu wa mamilioni ya fedha.
Aidha amewaasa kuacha tabia ya wizi kwa wanunuzi na kuhujumu zao hilo la biashara.
Mhandisi Ndikilo pia amekemea tabia ya wanunuzi wanaochelewa kulipia korosho na kuziacha kwenye maghala kwa muda mrefu.
Akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi wilayani Rufiji, Kibiti na Mkuranga, alitaka vitendo hivyo visijirudie katika msimu ujao.
Mkuu huyo wa mkoa, alieleza kwamba, Bungu B Amcos wamemuuzia mnunuzi tani 320 ambapo alikuta 298 huku  tani 22 zikiwa hazipo zenye gharama ya sh. Mil 72.9.
“Bungu Amcos mnunuzi alikuta tani 11 hazipo zenye thamani ya mil. 33.
“Bungu Mahege mil. 12 zimetiwa mfukoni, Mjawa Amcos tani 4 zimepigwa zilizogharimu mil. 11″alisema mhandisi Ndikilo.
Mhandisi Ndikilo, alielezea kuwa, hawezi kukubali kuona vyama vya ushirika vinashiriki kuupa mkoa fedheha.
Alifafanua kuwa, vyama vilivyojihusisha kutapeli wanunuzi vitoe sababu za msingi kwa wakuu wa wilaya kueleza ubadhilifu huo na wakibainika kufanya wizi vyombo vya sheria vifanyekazi yake.
Akizungumzia mfumo wa stakabadhi ghalani aliomba utumike vizuri kwani bila kufanya hivyo utateteleka.
Mhandisi Ndikilo alisema ni lazima haki itendeke ili wakulima wanufaike badala ya kuwabana kwa kuwapa masharti magumu hali itakayosababisha kuondoa imani na mfumo huo ambao ndio unawanufaisha kwa sasa.
Hata hivyo alisema wanunuzi wa korosho wanapaswa kutimiza wajibu wao wa kulipa wakulima katika muda stahiki .
“Safari hiii atakaebainika kufanya ujanja ujanja tutamfunga, na hapo ndipo mtajua kama mna RC mkali ,msile jasho la wanyonge ,”alisisitiza.
Mbali ya hilo, mhandisi Ndikilo, alihimiza kilimo cha mazao yanayohimili ukame ikiwemo muhogo, kunde ili
kujiepesha na baa la njaa.
Katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji, Shangwe Twamala alisema, wataalamu kutoka bodi ya korosho ndio wana hakiki ubora wa korosho katika vyama vyote vya msingi vilivyokusanya korosho kwa kushirikiana na CORECU na kisha kuandaa muongozo kwa wanunuzi.
Alisema muongozo wa mauzo namba 1 wa mwaka 2015,kifungu namba 4.4 wa bodi ya korosho Tanzania  kinasema mnunuzi ataruhusiwa kuhakiki ubora wa korosho zilizopo kwenye ghala baada ya kufanya utaratibu wa kulipa korosho .
Twamala alieleza, baada ya malipo mnunuzi ataruhusiwa kuhakiki baada ya kufanya utaratibu huo atapewa idhini ya kwenda na mwendesha ghala ama bodi ya korosho kwa maandishi .
Kwa upande wao viongozi wa Amcos hizo, akiwemo mwenyekiti wa Kibiti Amcos Saidi Lipenda, alisema matajiri, wanunuzi waangaliwe wasitake kuvuruga mkoa.
Nae kiongozi wa Bungu B Amcos, Sada Omary,alisema korosho zikiwa mbichi kwenye maghala zikija kukauka tani zinapungua.
Alieleza wanunuzi waache kung’ang’aniza kupima.
DK MWAKYEMBE AWAAMBIA WADAU WA MICHEZO CHA KUFANYA ILI MAMBO YAENDA VIZURI

DK MWAKYEMBE AWAAMBIA WADAU WA MICHEZO CHA KUFANYA ILI MAMBO YAENDA VIZURI

March 26, 2017
mwakyembe
Waziri mpya wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewataka wanamichezo kumpa ushirikiano katika kuendeleza gurudumu la maendeleo.
Dk Mwakyembe ambaye amechukua nafasi ya Nape Nnauye amesema anaweza kufanya vizuri kama watashirikiana pamoja na wadau wa michezo.
“Tukishirikiana kila jambo litaenda vizuri, serikali inataka mabadiliko, inataka mafanikio na hii ni kwa faida ya wanamichezo. Tushirikiane,” alisema.
Jana, Dk Mwakyembe alikaa kikao cha kwanza cha Kamati ya Serengeti Boys na baadaye akaenda Uwanja wa Taifa kuiunga mkono Taifa Stars iliyokuwa inacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Botswana na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, yote yakifungwa na nahodha Mbwana Samatta.

MAKABURI 22 YA WATU WENYE UALBINO YAFUKULIWA TANZANIA...TAS YAMUOMBA JPM KUFANYA KAMA DAWA ZA KULEVYA NA VIROBA

March 26, 2017

Inaelezwa kuwa tangu kuibuka kwa mauaji ya watu wenye ualbino mwaka 2007 takribani makaburi 22 nchini Tanzania yamefukuliwa na watu wasiojulikana. 

Chama hicho kimeiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi kama ilivyoonesha nguvu za kutosha katika vita ya dawa za kulevya na pombe aina ya viroba. 

Akizungumza juzi kwenye kikao cha viongozi wa chama watu wenye ualbino kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa ambayo ni Mara,Mwanza na Shinyanga na wanachama wengine Afisa mahusiano na habari TAS taifa Josephat Torner vitendo vya kufua makaburi ya watu wenye ualbino yanatishia amani yao 

Torner alisema wanaiomba serikali kuelekeza nguvu katika masuala ya mauaji na ufukuaji wa makaburi ili kuwafanya watu wenye ualbino waishi kwa amani ndani ya nchi yao. “Katika suala la mauaji ya watu wenye ualbino ambao wamekuwa wakiishi kwa hofu tunaomba serikali hata kuwataja kwa majina wanunuzi hao kama ilivyotokea kwenye masuala ya vita ya dawa zakulevya na uuzaji bombe aina ya viroba”,alisema Torner. 

Aidha alisema wanalaani kitendo cha kufukuliwa kwa kaburi la Nelson Msogole (50) aliyekuwa akiishi mji wa Songwe baada ya kufariki tarehe 28/3/2011 na kaburi lake kuonekana kufukuliwa tarehe 20/3/2017na watu wasiojulikana. “Matukio haya yanaendeshwa kwa usiri hivyo tunahoji kwanini imeshindikana ikiwa kwenye dawa za kulevya wameweza kutaja na kumepiga hatua?”,alihoji Torner. 

Alisema Tangu kuanze kuibuka mauaji ya watu wenye ualbino mwaka 2007 makaburi 22 nchini yamekwisha fukuliwa katika mikoa ya Mbeya ,Tabora,Mwanza,Mara ,Kagera,Rukwa, na Shinyanga. 

Aliiomba serikali ya awamu ya tano iweke mikakati ya uelewa kwenye jamii kwani huenda hawana uelewa na watuhumiwa wakibainika waadhibiwe kwa mujibu wa sheria. “Hiki ni kipimo cha serikali ya awamu ya tano kwa sauti ya wanyonge kwani kuna baadhi ya watu wanaishi kwenye nchi yao kwa hofu na unyonge na kuondolewa utu wao hivyo tuna imani serikali itaweka nguvu kubwa kuliko kipindi cha nyuma”,aliongeza Torner. 

Naye Mwenyekiti wa chama hicho kutoka mkoani Mwanza Alfredy Kapole alisema mkoa wa Mwanza unaongoza kwa mauaji ya vifo vya albino zaidi ya 17 vimetokea tangu mwaka 2007 hivyo aliiomba serikali kuweka ulinzi mkubwa kwa watu hao kwani wanakiuka katiba ya nchi kwani kila mtu anastahili kuishi. 

Mwenyekiti wa chama hicho kutoka mkoani Mara Joseph Sinda alisema kitendo cha kufukua kinawafanya waishi kwa hofu kubwa na kuitaka serikali ijaribu kuchunguza chanzo chake ni nini na kuthibiti kama kwenye madawa ya kulevya na pombe aina ya viroba walivyofanya ili waweze kuishi kwa amani. 

Mwanaharakati kutoka mkoani wa Shinyanga Eunice Zabroni aliiomba serikali wawaimarishie ulinzi na elimu itolewe kwani wanaishi kwa hofu kwa kukosekana ulinzi imara kuanzia ngazi ya vitongoji,vijiji kata na wilaya hadi mkoa. 
Chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) kimelaani vikali vitendo vya ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino vinavyoendelea kujitokeza nchini hali inayowafanya waishi kwa hofu kubwa katika nchi yao. 
Katikati ni Afisa mahusiano na habari wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS )Josephat Torner akizungumza wakati wa kikao cha viongozi na wanachama wa chama hicho ambapo walilaani vitendo vya ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino.Kulia ni Mwenyekiti TAS mkoa wa Mara Joseph Sinda,kushoto ni mwenyekiti TAS mkoa wa MwanzaAlfred Kapole -Picha zote na Suzy Butondo-Malunde1 blog
Afisa mahusiano na habari wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS )Josephat Torner ambapo alisema chama hicho kinaiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli kuongeza kasi katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ualbino 
Baadhi ya wanachama wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania wakiwa katika kikao hicho. Picha na Suzy Butondo-Malunde1 blog

ZIWA JIPE NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU HATARINI KUTOWEKA

March 26, 2017
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Mtendaji wa Kijiji cha Butu, Kata ya Jipe Wilayani Mwanga Bw. Nassor Abdul wakati Waziri Makamba alipotembelea Ziwa Jipe ambalo limeathiriwa kwa kiasi kikubwa na magugu maji ambayo yanasababisha kupungua kwa shughuli za uvuvi ambazo ndio chanzo kikubwa cha mapato kwa wakazi wa eneo hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Aron Mbogho.
Mifano kwa vitendo: Pichani Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa amembeba mtoto Meshack Ombeni  katika Kijiji cha Butu pembezoni mwa Ziwa Jipe. Waziri Makamba amewaasa wananchi hao kulinda Ziwa hilo ili liweze kunifaisha vizazi vijavyo na kuwatahadharisha kuwa uharibifu wa mazingira utahatarisha uhai wa ziwa hilo.
Upungufu mkubwa maji katika bwawa la nyumba ya Mungu. Inasemekana kupungua kwa kina cha maji kunatokana na ukame wa muda mrefu na uharibifu mkubwa  wa mazingira kutokana na shughuli za binadamu katika vyanzo vya maji vinavyopeleka maji katika bwawa hilo ukiwemo Mto Kikuletwa.

                     Na Lulu Mussa,Mwanga - Kilimanjaro

Imebainika kuwa Ziwa Jipe liko hatarini kutoweka endapo hatua za haraka hazitachukuliwa katika kulinusuru. Hayo yamesemwa leo na Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira Mh. January Makamba alipofanya ziara ya kukagua ziwa hilo ambalo sehemu kubwa imezungukwa na magugu maji.
Waziri Makamba amesema kuwa ziwa hilo ni rasilimali muhimu na hivyo ni lazima kuwe na mpango wa muda mfupi na ule wa muda mrefu. Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamiza wa Mazingira (NEMC) ameazimia kutangaza kupita Tangazo la Serikali kuwa eneo hilo ni eneo nyeti kimazingira."Tutatanga eneo hili kuwa eneo nyeti kimazingira na tutaweka masharti ya matumizi katika eneo hili" Alisisitiza Makamba
Azimio hilo la kutangaza kuwa eneo mahsusi ama nyeti kimazingira itasaidi katika kuandika maandiko mbalimbali ya miradi na kupata fedha kutoka kwa wadau na washirika wa maendeleo. Pia litawekwa chini ya uangalizi maalumu na kuweka masharti ya matumizi bora ya eneo hilo. " Tutaweka masharti makali na magumu zaidi ili watakao kiuka wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria" Aliongezea Waziri Makamba.
Aidha, Waziri Makamba amesisitiza kuwa ni vema kunusuru ziwa hilo sasa maana ndani ya miongo 2-3 huenda ziwa hilo likatoweka.  "Bila hifadhi ya mazingira hakuna maisha, na ukiyaharibu mazingira hakuna msamaha yatakuadhibu tu" Akiongea katika Mkutano wa hadhara kijijini Butu, Waziri Makamba amesema kuwa shughuli zozote za maendeleo iwe uvuvi, kilimo, utalii, mifugo kwa namna moja ama nyingine zinategema hifadhi endelevu ya mazingira.
Katika hatua za muda mrefu Waziri Makamba amewataka wasimamizi wa Bonde la Pangani, Wizaya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kukutana mara moja kuandaa mpango na mtazamo wa pamoja wa kunusuru Ziwa Jipe.
Akiwa njiani kuelekea Nyumba ya Mungu Waziri Makamba alipitia katika Kiwanda cha Kifaru Quarries Co. Ltd na kukuta kikiendelea na uzalishaji wa kokoto bila kuwa na cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeutaka uongozi wa Kiwanda hicho kusitisha uzalishaji mara moja na kutakiwa kulipa faini kwa kukiuka Sheria ya Mazingira kifungu namba 81 na 196.
Waziri Makamba pia amefanya ziara katika Bwawa la Nyumba ya Mungu na kufanya mkutano wa hadhara na wakazi wa kijiji cha Kakongo ambao kwa pamoja wamelalamikia zuio la kufanya shughuli za uvuvi katika bwawa hilo kutokana na kupungua kwa kina cha maji na samaki katika bwawa hilo.
Bw. Charles John Waziri Mkazi wa Kijiji cha Kagongo amesema kuwa kuna hujuma katika matumizi ya rasilimali maji ambapo imebainika kuwa wakulima wanaotumia kilimo cha umwagiliaji wamekua wakitumia maji kwa kiasi kikubwa na kusababisha upungufu katika bwawa.
Akijibu kero na malalamiko ya wananchi hao Waziri Makamba ameagizia kufanyika kwa doria na kuainisha pampu zote zinazovuta maji kutoka bwawani hapo "Naaagiza Mamlaka ya Wilaya ya Mwanga, Serikali ya Mtaa na Mamlaka ya Bonde Pangani kufanya doria na kuhakiki pampu zote kujua uhalali wake kama zimesajiliwa na kama zinavibali, zitakazobainika kutokuwa na vibali zote zitaifishwe" Alisisitiza Waziri Makamba.
Waziri Makamba yuko katika ziara maalumu ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira, changamoto na kuweka mikakati ya muda mfupi na muda mrefu wa kukabiliana nazo. Mpaka sasa Waziri Makamba ameshatembelea Mkoa wa Pwani, Tanga na Kilimanjaro.