MAHUJAJI WA TANZANIA WAANZA KUWASILI SAUDI ARABIA

August 22, 2017

Na Mwandishi Maalum, Riyadh, Saudi Arabia
Mahujaji kutoka Tanzania wameanza kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza nguzo ya tano ya dini ya kiislamu ya kuhiji Makkah inayofanywa na watu mbalimbali duniani, wakiwamo Waislamu kutoka Tanzania.
Baadhi ya mahujaji wakionekana Uwanja wa Ndege baada ya kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya swala ya Hija.
Mahujaji kutoka Tanzania wakiwa wamewasili nchini Saudi Arabia.
Baadhi ya Waislamu wanaoendelea kuwasili nchini hapa wakionekana pichani.

Ibada ya Hijja mwaka huu inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti hadi mwanzoni mwa mwezi Septemba, huku jumla ya mahujaji 977 kutoka Tanzania wameshawasili katika miji ya Madina na Jeddah. Mahujaji hao waliwasili katika viwanja vya ndege vya Madina na Jeddah na kupokelewa na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania.

Tanzania kwa mwaka huu inataraijiwa kupeleka mahujaji wapatao 2,700. Indonesia ndiyo nchi inayoongoza kwa kupeleka mahujaji wengi mwaka huu inatarajiwa kuwa na mahujaji wapatao 168,000. Mwaka huu Saudi Arabia inatarajiwa kupokea mahujaji zaidi ya 2,000,000 kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni.

DKT. KALEMANI AITAKA TANESCO KUUNGANISHA NGUVU KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME YA KURASINI NA KIMBIJI

August 22, 2017



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani,(pichani anayeongea), amelitaka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanakamilisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusamabaza umeme kinachotarajiwa kujengwa huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kalemani ametoa maelekezo hayo leo Agosti 22, 2017, wakati alipofanya ziara kukagua miradi ya umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini, Kigamboni na eneo panapotarajiwa kujengwa kituo kingine cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Hakikisheni mradi wa uejenzi wa kituo hiki cha Kimbiji unakamilika ifikapo Machi 30, mwakani,(2018), na kuwaondolea adha ya upatikanaji wa umeme wananchi wa Kigamboni, chukueni mafundi waliokamilisha kazi ya kujenga kituo cha umeme kule Mtwara waje hapa, muwaache wale wanaojenga transition (njia ya kusafirisha umeme) wajenge, lakini wale mafundi wengine waleteni hapa ili mradi huu ukamilike.” Alifafanua.
Akiwa kwenye kituo cha kupoza na kusamabza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, Dkt. Kalemani aliipongeza TANESCO kwa juhudi kubwa walizofanya kwa hatua ujenzi waliyofikia ambapo sasa wameanza kufunga mashine kubwa. Kituo cha Kurasini ndicho kinachotegemewa sana na watu wa Mbagala, Kurasini na Kigamboni.
Ongezeko la haraka la wakazi kwenye maeneo ya Mbagala, na Kigamboni kumepelekea uhitaji mkubwa wa umeme ambapo umeme unaopatikana kwa sasa umekuwa haukidhi mahitaji ya wakazi wa maeneo hayo.
“Naomba niwaambie, mradi huu umechelewa sana, hivyo basi ongezeni kasi ili ifikapo Agosti 30, mwaka huu, mradi ukamilike nataka watu wa Mbagala, watu wa Kurasini, na watu wa Kigamboni wanaondokana na kero hii ya umeme, na mimi nitawaambia washeshimiwa wabunge wa Kigamboni Mheshimiwa Ndungulile (Dkt. Faustin Ndungulile) na Mheshimiwa Mangungu (Murtaza Magungu) Mbunge wa Mbagala kuhusu habari hii ili wawaambie wananchi wa maeneo haya wawe wavumilivu kwani mradi huu sasa utakamilika.” Alisema.
Dkt. Kalemani pia aliwaagiza viongozi wa TANESCO, kuhakikisha wanakusanya nguvu kwa maana ya vifaa kutoka ofisi zote za TANESCO mkoa wa Dar es Salaam, ili kuhakikisha wananchi wote wa Kigamboni wanaofikia 350 waliolipia ada za kuunganishiwa umeme wawe wamepelekewe umeme ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Agosti.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, aliwaambia waandishi wa habari kuwa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu waziri yatafanyiwa kazi kwa haraka ili kuhakikisha kero hiyo inaondoka.
Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam

 Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam
 Dkt. Kalemani (katikati), akitoa maagizo kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi huo wa Kurasini.

Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (watatu kushoto), akimpatia maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha umeme cha Kigamboni, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto)

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), akiwa na  Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James, (kushoto), akiongea na waandishi wa habari.


MWAKILISHI WA JIMBO LA TUNGUU ZANZIBAR MH SIMAI ASHIRIKI UJENZI WA MADARASA

August 22, 2017
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa na Wananchi wa jimbo lake katika kisiwa cha uzi ngambwa wakishangilia wakati wa ujenzi wa Taifa wa kujenga madarasa saba ya Skuli ya Msingi  katika Kijiji cha Ngambwa kutowa elimu kwa watoto wa kijiji hicho kupata elimu ya msingi karibu na makaazi yao. Madarasa hayo yanajengwa kwa nguvu za Mwakilishi na Mbunge kwa Wananchi wa Jimbo lao.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akizungumza na wananchi wa Kisiwa cha Uzi Ngambwa wakati wa ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi inayojengwa na Mbunge na Mwakilishi na nguvu Wananchi wa kijiji hicho. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwahutubia wananchi wa kisiwa cha Uzi Ngambwa jimbo lake wakati wa ujenzi wa Taifa wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa. 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhani Abdallah akizungumza na wananchi wa kisiwa cha Uzi Ngambw wakati wa ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Ngambwa. inayojengwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo la Tunguu na Nguvu za Wananchi wa Kijiji hicho.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akishiriki katika ujenzi wa skuli ya msingi uzi ngambwa. 
Wananchi wa Ngambwa wakiwa katika ujenzi wa Skuli yao ya Msingi.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akishiriki katika ujenzi huo wa Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi.
Mwananchi wakishiriki katika ujenzi huo wa skuli ya msingi katika kisiwa cha Uzi kijiji cha Ngambwa.
Wananchi wa kijiji cha Ngambwa wakifuatilia hafla hiyo ya ujenzi wa Skuli yao mpya ya msinga katika kijiji chao. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohamed Said akiwa na bero likiwa na mchanga akishiriki katika ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa katika kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
Jengo la madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa likiendelea na ujenzi wake.
Wananchi wa kijiji cha Ngambwa Uzi wakishiriki katika ujenzi wa madarasa katika kijiji hicho.
Wananchi wa kijiji cha Ngambwa kisiwa cha Uzi wakiwa katika ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa inayojengwa kwa nguvu na Mbunge na Mwakilishi kwa kushirikiana na Wananchi wa Kijiji hicho.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu ZanzibarMhe. Simai Mohamed Said akizungumza na Mwananchi wa jimbo lake mkaazi wa Ngabwa Uzi Bi. Mwanaacha Khatib mkulima wa mwani wakati wa hafla ya ujenzi taifa wa skuli ya msingi ngambwa kisiwani humo.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com
Zanzines.com.
othmanmaulid@gmail.com.