MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAHIMIZA WAKAZI WA TANGA KUJIUNGA NA MFUMO WA WOTE SCHEME

May 30, 2016
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PFF mara baada ya kufungua maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Tanga yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwakidila jijini
 Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile akiwa kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesho hayo

Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile wa pili kulia akitoa elimu kwa mkazi wa Tanga namyanatolewa na mfuko huo.

na ya mafao WAKAZI wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kutumia fursa ya kujiunga na Mfumo wa wote scheme unaotolewa na Mfuko wa Pensheni PPF ili kuwawezesha kukithi mahitaji kwa sababu unalengo kuu la kutambua mchango wa ushiriki kwenye sekta isiyo rasmi katika kuinua uchumi.

 Hayo yalisemwa jana na Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile wakati alipozungumza na gazeti hili katika maonyesho ya nne ya biashara ya kimataifa ya Tanga yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwakidila jijini hapa ambapo alisema mfumo huo utasaidia kufikia wananchi wengi.

 Alisema kuwa fao hilo likuwa likitoa fursa mbalimbali kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta iliyo rasmi na isiyorasmi ili kuwawezesha kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa mustakabali wa maendeleo yao. 

“Niwaambieni kila mtu au kikundi chenye mlengo wa kiuchumi kilichopo kwenye sekta isiyorasmi kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, mama lishe, waendesha pikipiki, wajasiriamali wadogo wadogo kwa lengo la kuhakikisha wananufaika kupitia mfumo huo “Alisema. 

Aliongeza kuwa pia mfumo huo unawagusa wasanii, wana michezo, wachimbaji madini wadogo wadogo wanaweza kujiunga na mfumo huo kwa lengo la kupata manufaa yanayotokana na mfuko huo. 

Sambamba na hilo pia alisisitiza uwepo wa mafao yanayotolewa na mfuko huo kuwa ni ule wa Afya, Fao la Uzeeni, Mkopo wa elimu ambao unalengo la wanachama kukopa na kujiendeleza kielimu na PPF na mkopo ambao unakuwezesha kutimiza ndoto yako.

WANANCHI WA KATA YA MABATINI JIJINI MWANZA WATAKIWA KUUNDA ZAIDI VIKUNDI VYA KIJAMII.

May 30, 2016

Diwani wa Kata ya Mabatini, Deus Mbehe, akizungumza katika uzinduzi wa Kikundi cha Ushirikiano People's cha Mabatini.

DAWASCO YAKANUSHA GARI YA DAWASCO KUJERUHI WATATU

May 30, 2016
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imekanusha taarifa iliyoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari juu ya gari linalodaiwa kuwa la DAWASCO lenye namba za usajili T 369 BUZ ambalo liliparamia kituo cha mabasi cha Mbuyuni kilichopo maeneo ya Namanga Oysterbay na kujeruhi watu watatu.
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Meneja uhusiano wa Dawasco, Bi. Everlasting Lyaro amesema kuwa gari hilo sio mali ya Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam, bali ni moja ya gari linalomilikiwa na watu binafsi   ambao wanasaidiana na Dawasco katika kusambaza huduma ya maji maeneo ambayo huduma hiyo bado haijafika kwa kutumia magari makubwa ya kusambaza Maji (maboza) ambayo yamesajiliwa na kuwekwa nembo ya Dawasco.
“Gari hili sio mali ya Dawasco, bali limesajiliwa na Dawasco na kuwekewa viambatanisho vyote muhimu  ili kusambaza huduma ya Maji maeneo ambayo mtandao wa Maji haujafika haujafika” alisema Lyaro.
Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, Dawasco ilianza zoezi maalum la kusajili visima pamoja na magari yote makubwa ya kusambaza huduma ya Maji jijini Dar es salaam, ambapo tayari magari makubwa takribani 256 ya kusambaza huduma ya Maji jijini Dar es Salaam yamekwisha sajiliwa.
Dawasco inapenda kuvikumbusha vyombo vya habari kuzingatia taratibu za kazi kwa  kuandika taarifa zenye uhakika na ukweli ili kuepuka upotoshaji wa habari kwa wananchi.
Everlasting Lyaro
Kaimu Meneja uhusiano- Dawasco
022-2194800 au 08001164
Dawasco Makao Makuu
30/05/2016
Vijana nchini washauriwa kujiunga na mashirika ya kujitolea ili wajiongezee ujuzi na maarifa

Vijana nchini washauriwa kujiunga na mashirika ya kujitolea ili wajiongezee ujuzi na maarifa

May 30, 2016

Vijana nchini Tanzania wameshauriwa kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea ili kujiongezea ujuzi, uwezo, maarifa na kuleta mabadiliko katika jamii zao,hayo yalielezwa na Meneja wa Maendeleo ya Vijana wa shirika la Raleigh Tanzania, Genos Martin wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.

Martin alisema kuwa ni vyema kwa vijana kujiunga na mashirika ya kitaifa na ya kimataifa ya kujitolea kwani kwa kufanya hivyo kutawapa vijana fursa ya kuongeza ujuzi na maarifa ambao utawasaidia katika sehemu mbalimbali.
Martin alisema, "Kufanya kazi kwa kujitolea ni kitu kigeni nchini kwetu tofauti na Mataifa ya nchi zilizoendelea, watu waliowahi jitolea wanapewa kipaumbele kwenye maombi ya kazi tofauti na nchini kwetu. Hii inafanya kujitolea kuwa jambo la muhimu sana kwenye mataifa ya wenzetu" 

"Vijana wengi wanalalamika kuwa nafasi nyingi za kazi zinawataka wawe na uzoefu wa miaka mitatu nakuendelea, hawajui ni vipi wanaweza kupata uzoefu lakini kama wakijiunga na haya mashirika ya kujitolea wanaweza pata huo uzoefu na kuwafanya wawe na nafasi nzuri pindi waombapo ajira" aliongezea Martin.

Aidha, Afisa Mawasiliano wa Raleigh Tanzania, Kennedy Mmari alieleza kuwa ni kawaida ya shirika hilo kutafuta vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao huungana na vijana wenzao kutoka mataifa ya mbali mbali ya Ulaya na Amerika.

Mmari aliongezea, "Raleigh tuna programu kwa vijana zinazohusu ujasiriamali, usafi, maji na utunzaji wa mazingira, kijana yeyote anaweza kujjiunga nasi na kufanya program zetu. Hatutoi malipo yoyote wala hawatulipi chochote isipokuwa tunagharamia mahitaji yao yote ya msingi pindi wakiwa kwenye programu"
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chibe iliyopo kata ya Old Shinyanga mkoani Shinyanga wakishuhudia ufunguzi wa kituo cha elimu ya awali kilichojengwa na na vijana wa kujitolea kwa msaada wa shirika la Raleigh Tanzania.
Kwa upande wa vijana waliofanya programu na shirika hilo  wameshukuru kwa nafasi waliyopewa kwani imewasaidia kupata ujuzi na ufahamu wa mambo tofauti ikiwemo jinsi ya kuandaa na kusiammia biashara.

Mmoja wa vijana ambao wamepata fursa hiyo, Sia Malamsha,  alisema kuwa anajiona wa tofauti baada ya kumaliza programu, hakuwahi fikiria kama kuna watu Tanznaia hawana huduma za maji safi na salama lakini kupitia programu za Raleigh nimeweza fika kwenye jamii hizo na kuwasaidia kutatua matatizo hayo.
"Nimekuwa sehemu ya mabadiliko makubwa katika nchi yangu, najivunia kuona nimefanya kitu kuikomboa jamii ya Watanzania" aliongezea Bi. Malamsha.

Vijana wa Shirika la kujitolea la Raleigh wakishiriki ujenzi wa choo katika moja ya miradi yao
Naye kijana Ashiru Said aliyefanya programu ya ujasiriamali amesema kua programu za Raleigh zimemsaidia kupata elimu ya kusimamia na kuendesha biashara.
"Nimeweza kupata elimu ya ujasiriamali, baada ya kurudi nyumbani jamii imefaidika na elimu niliyoipata kwani nimeweza waelimisha vijana wenzangu jinsi ya kuanzisha na kusimamia biashara zao wenyewe" alimalizia Said.

Raleigh Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali lenye ofisi zake mkoani Morogoro na kufanya programu za kujitolea kwa lengo  la kuisaidia jamii ya Tanzania sehemu mbalimbali.
photo Krantz Mwantepele Founder & CEO , KONCEPT Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Website;www.koncept.co.tz

DAWASCO YABAINI WIZI WA MAJI MSIMBAZI BONDENI.

May 30, 2016
Maelezo ya picha kushoto:  Fundi kutoka Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) akiondoa Mpira wa Maji uliokuwa umeunganishwa kwenye kisima kinyume na utaratibu ambapo walikuwa wakitumia huduma ya Maji bila kuwa na mita wala akaunti namba ambapo walinzi jengo hilo awali walidai maji wanayotumia ni ya kisima kwenye jengo lilipo eneo la Msimbazi Bondeni jijini Dar es Salaam.



Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji katika eneo la kata ya Ilala mchikichini mtaa wa Msimbazi Bondeni ambapo walinzi wa jengo hilo walikuwa wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume cha utaratibu nakujifanya kuwa wanatumia Maji ya Kisima.

Akizungumza kwenye eneo la tukio Afisa biashara msidaizi  wa Dawasco Ilala Sezi Mavika amesema kuwa jengo hilo haliishi mtu bali wapo walinzi tu na mwenye jengo hilo anajulikana kwa jina moja tu la Duncan na kueleza kuwa walinzi hao wamejiunganishia huduma ya Maji kwa muda mrefu na wanatumia kumwagilia maua pamoja nakufanyia shughuli za usafi kwenye jengo hilo.

“Tumekuta walinzi wameunganisha huduma ya Majisafi kwenye jengo hili linalomilikiwa na bwana Duncan ambapo wamejiunganishia kwa kupitisha kwenye kisima kisichofanya kazi nakudai kuwa Maji wanayotumia niya Kisima ndipo tulipo shirikisha ofisi ya serikali ya mtaa nakuweza kukagua nakuona kuwa wajiunganishia maji yetu na hawana mita wala akaunti namba na watumia kwa muda mrefu huduma ya maji ya Dawasco” alisema Sezi.

Kwa upande wa makamu mwenyekiti wa serikali ya mtaa ya Msimbazi Bondeni bi Cecilia Kasele ametoa rai kwa wananchi wote wa mtaa wao kujiepusha na tabia ya wizi wa Maji na kuwasihi wananchi kuwataja wezi wa Maji kwenye maeneo yao kwani hao ndio wanaofanya wakose huduma bora ya Maji.

“Napenda kuwasihi wananchi wote wa mtaa wangu kujiepusha na tabia ya wizi wa Maji na pia nawasihi wale wote wanaofahamu wezi wa Maji kujitokeza na kuwataja kwani hao wezi ndio wanasabisha Dawasco kutokuweza kutoa huduma bora kutokana nakuhujumiwa na watu wachache” alisema Kasele.

Dawasco inaendelea na operesheni yake ya kukamata wezi wa Maji kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na hivyo inawasihi wananchi wote waliojiunganisha huduma ya Maji kinyume na utaratibu wajitokeze nakusajiwa kihalali pia watumie fursa hii ya zoezi la kuunganishia wateja wapya kupata huduma ya Maji kihalali, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaokamatwa wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume na utaratibu.

DIWANI WA KATA YA MABATINI JIJINI MWANZA AZINDUA KIKUNDI CHA USHIRIKIANO PEOPLE'S

May 30, 2016
Diwani wa Kata ya Mabatini Jijini Mwanza, Deus Mbehe (Chadema) akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Kikundi cha Kusaidiana cha USHIRIKIANO PEOPLE'S kinachoundwa na Wanachama zaidi wa 100 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kata ya Mabatini.
Na BMG
Kikundi hicho kiliundwa baada ya kuibuka stofahamu ya wananchi kusaidiana katika masuala mbalimbali ikiwemo misiba, baada ya baadhi ya wanachama wa chadema kutengwa katika shughuli za misiba katika Kata ya Mabatini.

Uzinduzi wa Kikundi hicho ulifanyika katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Mabatini Stand huku ukiambatana na harambee kwa ajili ya kukiimarisha kikundi ambapo diwani wa Kata ya Mabatini ambae alimwakilisha diwani wa Kata ya Butimba, akichangia shilingi Laki Tano huku wageni wengine waalikwa wakifanikisha harambee hiyo kufikisha shilingi Milioni Moja, laki moja na elfu sabini.

Wanachama nao waliahidi kila mmoja kuchangia shilingi elfu kumi, pesa ambazo kwa ujumla zitasaidia kukabiliana na mapungufu yanayokikabili kikundi hicho. Mapungufu hayo ni pamoja na viti 120, sufuria nne, turubai mbili pamoja na sahani 200 lengo likiwa ni kujiimarisha katika mahitaji mbalimbali yanayohitajika katika shughuli mbalimbali.

Mwenyekiti wa Kikundi hicho chenye wanachama 103 hadi sasa, Salma Ibrahim, amewasihi wananchi wengine kujiunga na kikundi ili kuongeza nguvu ya kusaidiana katika masuala mbalimbali ikiwemo sherehe, misiba na kuinuana kiuchumi bila kujali itikadi zao za kisiasa.