WATALI 54 KUTOKA CHINA WASHIRIKI TAMASHA LA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

December 28, 2023

 Pamela Mollel ,Arusha


Watalii zaidi 54 kutoka nchini China wamewasili Mkoani Arusha kwaajili ya kushiriki Tamasha la kupanda Mlima Kilimanjaro

Akizungumza katika hafla ya kuwapokea watalii hao,Mkuu wa Mkoa wa Arusha John V.K Mongella alisema ujio huo umetokana na mahusiano mazuri kati ya Tanzania na China

Alisema kuwa msimu wa mwisho wa mwaka ni msimu mzuri zaidi kwa kupanda mlima Kilimanjaro hali itakayowafanya wafurahi zaidi lakini pia kutangaza Tanzania kupitia mlima huo

Pia Mh.Mongella aliwatunuku vyeti vya pongezi kwa uamuzi mzuri wa kuja kupanda mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu zaidi Duniani

"Nawapongeza sanaaa kwa ujio wenu naamini mtafurahia sanaaa tamasha la kupanda mlima Kilimanjaro lakini pia niwapongeze kampuni ya kitalii ya Gosheni Safari kwa kuandaa tamasha hili"alisema Mongella

Ikumbukwe kuwa ujio wa watalii hao ni matokeo ya Filamu ya Royal Tour iliyoongozwa na Rais MaMa Samia Suluhu Hassan




 

 

BARAZA LA UUGUZI NA UKUNGA TANZANIA KUENDESHA MTIHANI KWA WATAHINIWA 4165

December 28, 2023

 Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania linatarajia kuendesha zoezi la Mtihani kwa watahiniwa 4165, ambao wamekidhi vigezo vya kufanya Mtihani huu, wakiwemo waombaji 3917 ambao wanafanya mtihani kwa mara ya kwanza na 248 wanaorudia. Kati yao, Wanaume ni 1647 na wanawake ni 2518.


Hayo yamesemwa na Kaimu Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Happy Masenga, leo Disemba 28, 2023, wakati akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa ofisi za Baraza hilo Jijini Dodoma.

Aidha, Mtihani huu utafanyika katika vituo vilivyotambuliwa na kukubaliwa na Baraza katika Mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, na Tabora siku ya Ijumaa 29/12/2023, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.

Lengo la Mtihani huu ni kupima umahiri wa watahiniwa ili kupata wataalamu wa Afya wenye sifa za kusajiliwa na kupewa leseni ya kutoa huduma kama Muuguzi au Mkunga kwa mujibu wa kifungu cha 15 (1) (a-b) cha Sheria ya Uuguzi na Ukunga.

Mtihani wa usajili na leseni umekuwa ukifanyika tangu kuanzishwa kwa Baraza mwaka 1953 kwa mujibu wa kifungu 6 (a) cha Sheria, ambapo hapo awali mtihani huu uliendeshwa kwa ushirikiano kati ya Baraza na Wizara ya Afya.

Baraza la Uuguzi na Ukunga Nchini lina jumla ya wauguzi na wakunga wenye leseni wapatao 49,994, ambao wanatoa huduma kwenye Hospitali za Rufaa, Mikoa, Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati. 

Idadi hii inajumuisha wauguzi na wakunga walioajiliwa Serikalini pamoja na sekta binafsi kwa ngazi ya Astashahada, Stashahada, Shahada, Uzamili na Uzamivu.




RAIS DKT. MWINYI AZUNGUMZA NA BALOZI WA TA NZANIA NCHI UGANDA

December 28, 2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Mhe.Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 28-12-20213..(Picha na Ikulu)  
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Mhe.Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulia akielekea Kituo chake cha kazi, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 28-12-2023.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Mhe.Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo 28-12-2023  kwa mazungumzo na kujitambulia akielekea Kituo chake cha kazi,  na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said,mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) 

PUMA ENERGY TANZANIA YATOA VIFAA VYA UJENZI KUSAIDIA WAATHIRIKA MAFURIKO YA MATOPE KATESHI

December 28, 2023


Na Mwandishi Wetu, Hanang



KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania imekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi zikiwemo nondo 1000, mabati 800 na saruji mifuko 600 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Kateshi wilayani Hanang mkoani Manyara.

Vifaa hivyo vya ujenzi vyenye jumla ya thamani ya Sh.milioni 70 vimekabidhiwa leo Desemba 28,2023 wa Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja ameishukuru Kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa kutoa vifaa vya ujenzi ambavyo kwa sasa ndivyo vinahitahika zaidi.

“Kwa niaba ya Serikali anachukua nafasi hiyo kuupongeza uongozi wa Puma Energy Tanzania kwa kufika Kateshi kutoa misaada wa vifaa vya ujenzi.Tumepokea mifuko ya saruji 600, bati pisi 800 na nondo 1000.

“Vifaa hivi vya ujenzi vitasaidia eneo la ujenzi kwani tunakusudia kuanza ujenzi hivi karibuni kujenga nyumba za waathirika wale ambao wamepoteza makazi na mchango huu una thamani ya Sh.milioni 75,”amesema Mayanja.

Ameongeza kuwa msaada huo wa nondo, bati na saruji unakwenda kuongeza nguvu katika jitihada za Serikali za Awamu ya Sita chini ya ya Dk.Samia Suluhu Hassan ambayo imeamua kujenga nyumba kwa waathirika baada ya kutokea mafuriko Desemba 3, 2023

Aidha amesema msaada huo umekuja wakati muafaka kwani wamekuwa wakipokeza zaidi msaada wa mahitaji ya chakula na dawa lakini kwa sasa wako kwenye hatua za mwisho kuanza ujenzi wa nyumba za waathirika kwa kutambua baada ya mafuriko kuna baadhi ya makazi yameharibiwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Bi Fatma Mohemed Abdallah, Meneja Uhusiano wa Puma Energy Tanzania Limited Godluck Shirima amesema bodi ya wakurugenzi chini ya Mwenyekiti wake Dk.Selemani Majige, Menejimenti ya Kampuni chini ya uongozi wa Bi Fatma Mohamed Abdallah, wafanyakazi na wadau wote wameguswa na kuhuzunishwa na mafuriko yalio wakuta wananchi wa Katesh.

“Hivyo viongozi wetu wakatuelekeza kuleta msaada huu wa vifaa vya ujenzi ili kuunga mkono juhudi na jitihada za Serikali kuwajengea makazi waathirika waliopoteza makazi yao kwenye mafuriko.

“Puma Energy pia ni muathirika wa mafuriko haya, ambapo kituo chao cha Kateshi kiliharibiwa na mafuriko, kwa hiyo kama waathirika na mkazi wa Kateshi, kampuni iliona ni vyema kutoa mchango wake kwa jamii ya Katesh,”amesema Shirima.


Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja (wa pili kulia )akipokea mfuko wa saruji ukiwa ni sehemu ya mifuko 600 ya saruji kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambaye ni Meneja Uhusiano Godluck Shirima( wa tatu kushoto) Meneja Masoko Lilian Kanora(wa kwanza kulia) na Meneja Rasilimali Watu Bw. Joseph Jaruma ( wa pili kushoto).Wa kwanza kulia ni Ofisa Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Methew Giramisi .

Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja (wa tatu kushoto) akipokea bati kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambaye ni Meneja Uhusiano Godluck Shirima( wa pili kulia).Wanaoshuhudia Meneja Masoko Lilian Kanora(wa pili kushoto) na Meneja Rasilimali Watu Bw. Joseph Jaruma ( wa kwanza kulia).Wa kwanza kushoto ni Ofisa Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Methew Giramisi .













RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UZAMIVU YA USIMAMIZI WA UTALII NA MASOKO CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA).

December 28, 2023

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine akiwa kwenye maandamano ya Kitaaluma wakati walipokuwa wakiingia kwenye Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu kwa ajili ya kushiriki Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambapo Chuo hicho kimemtunuku Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi kupitia Sekta ya Utalii tarehe 28 Desemba, 2023.


 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Aman Abeid Karume katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu walipohudhuria Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) tarehe 28 Desemba, 2023.

WAZIRI WA UCHUMI WA BULUU NA UVUVI AZUNGUMZA NA WAANDISHI ZANZIBAR.

WAZIRI WA UCHUMI WA BULUU NA UVUVI AZUNGUMZA NA WAANDISHI ZANZIBAR.

December 28, 2023





Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleimana masoud Makame akijibu maswali alioulizwa na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio na Changamoto za Wizara yake kuelekea Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar,Hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.



Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleimana masoud Makame akisisitiza jambo wakati akijibu maswali alioulizwa na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio na Changamoto za Wizara yake kuelekea Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar,Hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.

Mwandishi wa Habari Mwandamizi Salum Vuai akiuliza maswali katika Mkutano na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleimana masoud Makame alipokua akizungumzia kuhusiana na Mafanikio na Changamoto za Wizara yake kuelekea Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar,Hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Na Takdir Ali – Habari Maelezo.

Waziri wa Uchumi wa buluu na Uvuvi Suleiman Massoud Makame amesema miradi ya maendeleo imeongozeka katika wizara hiyo kutoka miradi 10 ya maendeleo mwaka 2020 hadi kufikia 17 mwaka 2023.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa akilezea makakati na mafanikio ya Wizara hiyo, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema miradi hiyo imejumuisha sekta mbalimbali ikiwemo Uvuvi, Mwani, Ufugaji, Viwanda vya kusarifu madagaa na mwani, masoko na madiko, uhifadhi wa Bahari na utafiti.

Ameeleza kuwa mafanikio hayo ya kimaendeleo yanaifffiisha Serikali katika shabaha za kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2050, na Mpango wa Maendeleo ya Zanzibar (ZADEP).

Aidha amesema Serikali inaendelea kuwawezesha wajasiriamali kwa kuwapatia elimu, ubunifu na zana za kujiongezea ajira katika maeneo yao.

Amefahamisha kuwa Serikali imeweka mkakati wa kuwawezesha wakulima wa mwani na wafugaji wa mazao ya baharini 23,000 ambao zaidi ya asilimia 90 ni wanawake wa vijijini.

Mbali na hayo amesema, Usafirishaji wa mwani nje ya Nchi umeongezeka kutoka Tani 11,382 zenye thamani ya Tzs Bilioni 11.70 mwaka 2020 hadi kufikia Tani 12,563 zenye thamani ya Tzs Bilioni 12.581 kwa mwaka 2023.

Sambamba na hayo amesema maendeleo ya kiuchumi na kijamii ni lazima yazingatie uhifadhi wa maliasili hivyo amewaomba Wananchi kuunga Mkono juhudi za Serikali katika kuleteleza mikakati iliojipangia.

Mbali na hayo amesema Serikali imetilia mkazo utafiti na sayansi ya bahari ili kupata taarifa sahihi zinazoimarisha utekelezaji wa sera za Uchumi wa Buluu.

MZUMBE YAPOKEA RASIMU YA MICHORO YA UJENZI WA MIUNDOMBINU KUPITIA MRADI WA HEET.

MZUMBE YAPOKEA RASIMU YA MICHORO YA UJENZI WA MIUNDOMBINU KUPITIA MRADI WA HEET.

December 28, 2023

 


Uongozi wa chuo kikuu Mzumbe umeitaka kampuni ya Y & P Architect yenye mkataba wa Huduma ya Ushauri elekezi, usanifi na usimamizi wa ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho kuongeza kasi katika utekelezaji wa shughuli hiyo kuwezesha kuendelea kwa hatua nyingine ikiwemo kumpata Mkandarasi wa ujenzi mapema mwakani.


Akizungumza wakati wa kikao baina ya menejimenti ya Chuo hicho Kikuu Mzumbe na Kampuni hiyo ya Y & P Architect kupokea na kupitisha rasimu ya michoro ya ujenzi wa miundombinu ya majengo unaotekelezwa na serikali kupitia mradi wa HEET Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. William Mwegoha amesema pamoja na kuzingatia ubora mradi huo unapaswa kukamilika kwa wakati.

“Hii ni kazi muhimu katika chuo chetu kwa sababu itakapo kamilika itatuongezea huduma kwenye chuo chetu ambayo mwisho wa siku ni mkakati wa kuongeza masuala ya Udahiri , mifumo ya TEHAMA, masuala ya kuendeleza bunifu na matumizi ya Mtandao kuwezesha mafunzo ya masafa” . Alisema Prof. William Mwegoha makamu mkuu wa chuo kikuu Mzumbe

Katika kikao hicho kampuni ya Y & P Architect imewasilisha rasimu ya michoro ya majengo matatu ya.Academic Complex, TEHAMA na Uvumbuzi pamoja na jengo la Mgahawa (Cafteria) yanayotarajiwa kujengwa eneo la Maekani Kampasi kuu Morogoro.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Y & P Architect, Yasin Mringo, ameishukuru Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe kwa ushirikiano uliosaidia kuwa na ufanisi hadi hatua iliyofikiwa ambapo pamoja na kupokea mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya maboresho ameahidi kuongeza kasi kwenye utekelezaji wa shughuli zilizobaki kuhakikisha kazi zilizobaki zinakamilika mapema hata kabla ya muda wa mkataba.

“Tumekwisha kamilisha hatua ya kwanza tunashukuru mungu leo kwa kushirikiana na Uongozi wa chuo kikuu Mzumbe baada ya sikukuu hizi za mwisho wa mwaka kupita nimategemeo yetu kwamba katika kipindi cha miezi miwili na nusu ya kufanya kazi tutakamilisha mategemeo yetu ili kufikia mwezi wa Nne au watano mkandarasi kwa ajili ya ujenzi awe amepatikana”. Alisema Msanifu Majengo Yasin Mringo.

Mkataba wa huduma ya Ushauri Elekezi, Usanifu na usimamizi wa ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho uliosainiwa Oktoba 9,2023 baina ya Chuo kikuu Mzumbe na kampuni ya Y & P Architect, sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa HEET kuboresha miundombinu ujenzi wa majengo eneo la chuo kikuu Mzumbe, pia kuanza mchakato wa ujenzi wa Kampasi mpya ya Chuo hicho katika mkoa wa Tanga.

RAIS MWINYI ARIDHIA UWANJA WA AMAAN KUITWA “NEW AMAAN SPORTS COMPLEX”

RAIS MWINYI ARIDHIA UWANJA WA AMAAN KUITWA “NEW AMAAN SPORTS COMPLEX”

December 28, 2023




Na, Brown Jonas – WUSM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameridhia ushauri wa kuubadili jina uwanja wa Amaan na kuitwa “New Amaan Sports Complex” wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya Uwanja huo uliofanyika Desemba 27, 20203 kisiwani humo

Rais Mwinyi ameridhia ushauri huo uliotolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alipokua akitoa salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuufanya uwanja huu kuwa wa kisasa na wenye viwango vya Kimataifa, mimi naomba niubadilishe jina uitwe New Amaan Stadium” alisema Dkt. Ndumbaro.
- Advertisement -

Hafla ya Uzinduzi wa Uwanja huo ilipambwa na Burudani mbalimbali ikiwemo Muziki na mechi ya mpira wa miguu ya kirafiki baina ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania Bara “Kilimanjaro Stars” na Timu ya Mpira wa Miguu ya Zanzibar “Zanzibar Heros ambazo zilitoka sare ya bila kufungana.