ESRF YARATIBU ZIARA YA WATAALAM WA UCHUMI KUTEMBELEA SHUGHULI ZA WAJASIRIAMALI WA SIDO

May 02, 2018


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii. (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) na Profesa Kaushik Basu (katikati), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni inayojishughulisha na uuzaji wa asali , Fredy Swai , wakati wa ziara ya kutembelea Shirika la Uendelezaji Viwanda Vidogo (SIDO), ili kuona jinsi wajasiriamali wanavyoendesha shughuli zao. Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Abubakari Akida)

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, akimuelekeza jambo Profesa Joseph Stiglitz wakati wa ziara ya kutembelea Shirika la Uendelezaji Viwanda Vidogo (SIDO), ili kuona jinsi wajasiriamali wanavyoendesha shughuli zao. Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni inayotengeneza bidhaa ya mafuta ya kupaka kwa kutumia malighafi ya mimea, Obed Musiba (kulia), akitoa maelezo juu ya bidhaa zake kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (aliyeshika losheni) na Profesa Joseph Stiglitz, wakati wa ziara ya kutembelea Shirika la Uendelezaji Viwanda Vidogo (SIDO), ili kuona jinsi wajasiriamali wanavyoendesha shughuli zao. Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati), akiwaongoza wageni kutembelea eneo la Shirika la Uendelezaji Viwanda Vidogo(SIDO), ili kuweza kukagua shughuli za wajasiriamali wanaojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.Kulia ni Profesa Kaushik Basu na Kushoto ni Profesa Sabina Alkire, ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Abubakari Akida)

Geofrey Adroph BLOGGER P.O.BOX 24793, Mob: +255 755 274953 /+255 713 363965, Email: pamojapure@gmail.com. Blog: http://www.pamoja.co.tz/ DAR ES SALAAM, TANZANIA

GGM na TACAIDS kuzinduwa Kilimanjaro Challenge 2018

May 02, 2018
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko (kushoto)  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa zoezi la upandaji wa Mlima Kilimanjaro  (Kilimanjaro Challenge 2018), litakalo kwenda sambamba na kuendesha harambee kuchangisha fedha  kwa mwaka 2018 kwa ajili ya kusaidia mapambano ya kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI nchini. Kulia ni Makamu wa Rais miradi endelevu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo.



Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
Makamu wa Rais miradi endelevu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa zoezi la upandaji wa Mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2018), litakalo kwenda sambamba na kuendesha harambee kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya kusaidia mapambano ya kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko.

Watendaji wa MGODI wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) wakijadili jambo mara baada ya kumaliza mkuatano wa waandishi wa habari mapema leo.
Watendaji wa MGODI wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkuatano wa waandishi wa habari mapema leo

Na Mwandishi Wetu

MGODI wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) inatarajia kuzindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2018), litakalo kwenda sambamba na kuendesha harambee kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini. Akizungumzia tukio hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko alisema shughuli hiyo itafanyika Mei 4, 2018 katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Dar es Salaam. Dk. Maboko alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambapo atafanya zozezi la ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka 2017 baada ya wadau mbalimbali kupanda na kuendesha baiskeli kwa kuzunguzuka Mlima Kilimanjaro. Aidha aliishukuru na kuipongeza kampuni ya GGM kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa kuchangisha fedha kupitia Kilimanjaro Challenge against HIV & AIDS, fedha ambazo alisisitiza zimekuwa na mchango mkubwa katika mapambano kudhibiti ugonjwa huo maeneo mbalimbali. Akifafanua zaidi, Dk. Maboko alisema Kilimanjaro Challenge against HIV & AIDS, ni mfuko unachangia juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutoa elimu kwa jamii kuhusu maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU). Aliongeza kuwa, Kilimanjaro Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo. Mfuko huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU//UKIMWI sambamba na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani na nje kuupanda mlima Kilimanjaro. Takwimu zilizotolewa na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), zimeonesha kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 % mwaka 2011/ 2012 hadi asilimia 4.7% mwaka 2016/17. “Mwaka wa 2016, inakadiriwa kuwa watu milioni 1.5 nchini wanaoishi na VVU na UKIMWI hadi sasa watu 225 wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa siku. Ugonjwa huu umewaathiri zaidi vijana na watoto yatima zaidi. Tunahitaji kubadilisha hali hii. Lengo la kukusanya fedha ni kuweza kusaidia serikali ya Tanzania katika jitihada zake kufikia sifuri tatu. Sifuri katika maambukizi mapya, sifuri ya unyanyapaa, sifuri katika vifo vitokanavyo na UKIMWI." " TACAIDS kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na wadau wengine kwa kupitia mpango huu wa Kili Challenge tunapenda kutoa mchango na ushirikiano wetu kwa Taifa ili kutunisha mfuko utakaowezesha kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huu. Tuna matumaini ya kujenga timu imara yenye hamasa ya kupambana na janga hili. Tunatoa wito kwa makampuni na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, wajitokeze ili tusaidiaane kutunisha mfuko wa Kili Challenge na mwishowe kufikia malengo yetu ya kuhakikisha tunakuwa na kizazi kisicho na maambukizi ya VVU/ UKIMWI,” alisema Dkt. Leonard Maboko. Naye Makamu wa Rais miradi endelevu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo akizungumza alisema, watoto watakaoshiriki katika zoezi la Kilimanjaro Challenge mwaka huu ni wa kiume na wa kike wenye umri kuanzia miaka 13. Watoto hao yatima kutokana na tatizo la VVU/ UKIMWI wamesaidiwa na Kituo cha kulea watoto yatima cha Moyo wa Huruma Orphanage Center kilichopo Geita. Bw. Shayo alibainisha kuwa, changamoto kubwa inayotokana na janga la UKIMWI ni pamoja na maelfu ya watoto yatima wanaohitaji misaada baada ya wazazi wao kufariki, wajane wasiokuwa na kipato, pamoja na wazee wanaolazimika kuwalea wajukuu walioachwa na watoto wao ambao walifariki kutokana kwa ugonjwa huo. “Aidha, pia kuna tatizo linaloikabili jamii sasa ambapo baadhi yao wanawatenga na kukataa kuishi na watu wenye maambukizi ya VVU/ UKIMWI, kutokana na tatizo hilo Mgodi wa Dhahabu wa Geita, umeamua kuwekeza katika mradi huu kwa kuuwezesha kuwa mradi wa kitaifa na si wa GGM,” alisema Makamu wa rais miradi endelevu wa kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo. “Huu ni mwaka wa 17 sasa tangu Kili Challenge ianze. Pia zaidi ya watu 750 kutoka pande mbalimbali za dunia wameshiriki. Taasisi zaidi ya 40 zimefaidika kutokana na utunishaji wa mfuko huu kwa sababu taasisi ambazo hazina fedha za kuendesha kampeni na shughuli mbalimbali za mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI zimekuwa zikifaidika na mfuko huu. Pamoja na mambo mengine, watoto waliopoteza wazazi wao sasa wanaweza kutabasamu tena kutokana na uangalizi pamoja na upendo wanaoupata kutokana na mfuko huu. “Tunapenda pia kutambua ushirikiano wa kampuni na taasisi mbalimbali kama vile ACACIA, AKO, Mantrac, NSSF, PUMA, TOYOTA, Prime Fuels, Coastal Aviation, Airtel, Capital Drilling, PPF, Serena Hotel, Geita Power Limited, SGS na wadau wengine tunaoshirikiana nao. Tunawashuruku kutokana na ushirikiano wenu katika mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI hivyo, tunaweza kufurahia mafanikio haya kwa kuwa na mradi endelevu,” aliongeza Simon Shayo. Balozi wa Kili Challenge ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini Tanzania, Bw. Mrisho Mpoto ameileleza jamii ya Tanzania kuacha kuwa tegemezi kwa sababu ina uwezo wa kujisimamia kwa kutumia vyombo vya habari, na watu wenye ushawishi mkubwa na kwa pamoja UKIMWI unaepukiki. Tanzania inaweza kufikia malengo ya kuwa huru dhidi ya maambukizi ya UKIMWI kufikia mwaka 2030 kama tukishirikiana kwa pamoja katika vita hii. Aliongeza kuwa, ili kushiriki Kili Challenge, muhusika anaweza kuchangia mfuko huu kwa kujifadhili au kumfadhili mwingine kupanda au kuendesha baskeli kuzunguka mlima Kilimanjaro. Kuwa sehemu ya mafanikio. Kwa mawasiliano zaidi au kutoa mchango wasiliana nasi kupitia email: GGMkilichallenge@anglogoldashant.com, au tovuti www.geitakilichallenge.com. Geita Gold Mine na TACAIDS tunatumia mwamvuli huu wa Kilimanjaro Challenge katika kuelimisha jamii kuhusu janga hili la VVU/Ukimwi na tunatarajia siku moja Tanzania itatangaza kuisha kwa maambukizi ya VVU/ UKIMWI. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.geitakilichallenge.com

TANESCO YANG'ARA SHEREHE ZA MEI MOSI 2018 IRINGA

May 02, 2018

Rais Dk John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti Mfanyakazi Bora wa Shirika la Umeme nchini Tanesco, ambaye ni Fundi Mchundo Endure Kiswaga kutoka kituo cha kufua Umeme Pangani Tanga.

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ni miongoni mwa maelfu ya wafanyakazi waliojitokeza kwa wingi Mjini Iringa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani MEI MOSI ambapo kitaifa iliadhimishwa mkoani humo na kuongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli.

Mwanadada mfanyakazi wa Tanesco akionesha utalaam wake wa kuunga waya za umeme katika nguzo kubwa wakati gari lao la maonesho likipita mbele ya mgeri rasmi katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
Magari ya Tanesco yakiwa katika maandamano hayo ya Mei Mosi mjini Iringa.

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ni miongoni mwa maelfu ya wafanyakazi waliojitokeza kwa wingi Mjini Iringa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani MEI MOSI ambapo kitaifa iliadhimishwa mkoani humo na kuongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli.

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ni miongoni mwa maelfu ya wafanyakazi waliojitokeza kwa wingi Mjini Iringa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani MEI MOSI ambapo kitaifa iliadhimishwa mkoani humo na kuongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli.

WABUNGE WAPONGEZA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI

May 02, 2018

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (aliyesimama) akifafanua hoja za wabunge kwenye semina ya Sekta ya Uvuvi kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Katikati Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa na kushoto Katibu Mkuu Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba.(Picha na John Mapepele)


Mbunge wa Kiteto, Mheshimiwa Emmanueli Papian akichangia hoja kwenye semina ya Sekta ya Uvuvi kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.(Picha na John Mapepele)

bunge wa Kyerwa mkoani Kagera, Innocent Bilakwate akichangia hoja kwenye semina ya Sekta ya Uvuvi kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.(Picha na John Mapepele)

Na John Mapepele, Dodoma

BUNGE limejitosa kuunga mkono vita dhidi ya uvuvi haramu iliyotangazwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kutaka viongozi wa ngazi zote wanaoshiriki au kufadhili uvuvi haramu watajwe kwa majina ili Taifa liweze kuwafahamu.

Hali hiyo itasaidia kumaliza kabisa tatizo la uvuvi haramu lililosababisha nchi ishindwe kunufaika na rasilimali hizo muhimu za uvuvi licha ya kuwa na eneo kubwa la maziwa,mito na bahari lenye jumla ya kilomita za mraba 346,337 sawa na asilimia 36.7 ya eneo lote la Tanzania ni maji.

Wakichangia mjadala katika semina kwa wabunge kuhusu vita dhidi ya uvuvi haramu iliandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kufanyika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni jijini Dodoma baadhi ya wabunge hao waliitaka Serikali kuchukua hatua kali zaidi kwa watu wote wanaojihusisha na kufadhili uvuvi haramu ili nchi iweze kunufaika na rasilimali hiyo muhimu.

Mbunge wa Kyerwa mkoani Kagera, Innocent Bilakwate alisema mambo mengi katika Taifa letu kwa miaka mingi yamekuwa hayaendi kwa sababu ya viongozi waliopewa dhamana kushindwa kuchukua hatua

“Naomba Serikali iendelee kuchukua hatua kali zaidi za kupambana na uvuvi haramu na niombe waheshimiwa wabunge tushirikiane katika vita hii mambo mengi yameharibika kwa ajili ya sisi wanasiasa hivyo ni wakati wa kumuunga mkono Mhe Waziri na Mhe Rais katika kulinda rasilimali zetu za uvuvi”alisema Bilakwate.

Naye Mbunge wa Kiteto, Emmanueli Papian alisema anaamini suala la uvuvi haramu litafika mwisho na heshima ya Tanzania itarudi kutokana na maamuzi magumu yanayochukuliwa na Serikali huku akiitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutaja hadharani orodha ya viongozi wote wanaoshiriki na kufadhili uvuvi haramu ili Taifa liweze kuwafahamu kwa majina watu wanaohujumu rasilimali na kisha hatua stahiki zichukuliwe bila kujali nafasi za vyeo vyao .

Pia Mbunge huyo pia aliitaja nchi ya Uganda kama kielelezo cha mapambano dhidi ya uvuvi haramu kutokana na juhudi kubwa wanazofanya Serikali ya nchi hiyo na kuiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwachukua baadhi ya wabunge na waandishi wa habari kwenda nchini Uganda kuona namna wanavyoshughulikia uvuvi haramu.

“Kule Uganda wameweka Sheria kali ambazo zimetokomeza kabisa uvuvi haramu, naamini hili suala hili la uvuvi haramu litafika mwisho katika nchi yetu na heshima inarudi kutokana na maamuzi magumu yanayochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano ni vema tukubaliane hapa Waziri taja hadharani viongozi wanaofadhili uvuvi haramu”alisisitiza

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa, alimhakikishia Waziri Mpina kuwa Bunge linaunga mkono vita dhidi ya uvuvi haramu na kutaka orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kujihusisha au kufadhili uvuvi haramu itajwe ili Bunge liweze kuwafahamu na hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

Awali akizungumza katika semina hiyo Waziri Mpina alisema inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 70 na 90 za nyavu zilizokuwa Ziwa Victoria zilikuwa haramu pamoja na matumizi makubwa ya sumu aina ya Theodani na Thonex, aidha katika operesheni inayoendelea maarufu kwa jina la ‘Operesheni Sangara 2018 ‘ jumla ya nyavu haramu zenye urefu wa mita milioni 34 zimekamatwa na kuteketezwa kwa moto, nyavu hizo zimekamatiwa katika maeneo mbalimbali ya ziwani,mipakani,madukani,kwenye maghala na viwandani.

“Kama zana hizi haramu zingeendelea kubaki majini shughuli za uvuvi katika ziwa Victoria zingekoma”alisema.

Alisema jumla ya kilo 310,569 za samaki zilizokuwa zimevuliwa kwa njia haramu na kinyume cha sheria zimekamatwa na kutaifishwa na Serikali kati ya samaki hao jumla ya kilo 132, 325 za samaki wachanga na wazazi zimegawiwa kwenye hospitali, shule, magereza na wananchi na pia kilo 178,244 za kayabo na kilo 4,967 za mabondo zimeuzwa kwa njia ya mnada na fedha kuingia kwenye mfuko wa Serikali.

Akielezea kuhusu ukwepaji mkubwa wa kodi za Serikali, Waziri Mpina alisema kwa kipindi kirefu Serikali imekuwa ikipata kiasi kidogo cha mapato kutokana na biashara ya mazao ya uvuvi ambapo inakadiriwa kuwa chini ya asilimia 25 ya kiasi cha mapato inayostahili.

“Baada ya kuanza kwa operesheni mapato yatokanayo na uvuvi yaliongezeka kwa asilimia 300, katika ukanda wa Ziwa Victoria ambapo katika soko la Kirumba Mwanza kwa miezi mitatu kabla ya operesheni makusanyo yalikuwa sh. milioni 104 na baada ya kuanza operesheni makusanyo yamefikia sh. milioni 335, hii ni mara tatu ya makusanyo ya awali”alisema Mpina.

Akizungumzia utoroshaji wa mazao ya uvuvi, Waziri Mpina alisema katika mpaka wa Tanzania na Zambia ulioko Tunduma mwaka 2016/2017 jumla ya kilo 5,398,900 za dagaa zilipitishwa kwa magendo kwenda nchi za Zambia na Malawi , kwa upande wa mpaka wa Tanzania na Kenya uliopo Sirari jumla ya kilo 876,500 za dagaa zilisafirishwa kwa njia za magendo na kuvushwa kwenda nchi ya Kenya. Aidha kwa mipaka hiyo pekee Serikali imepoteza jumla ya sh. bilioni 1.14 kwa kipindi hicho.

Aliongeza kuwa wakati mwingine mauzo ya Sangara nje ya nchi, Tanzania na Kenya yamekuwa ya kilingana licha ya kuwa Tanzania inamiliki asilimia 51 ya Ziwa Victoria huku Kenya ikiwa na asilimia 6 tu.
Kwa upande wake mtoa mada kuhusu Operesheni MATT, Inspekta wa Polisi, Juma Muhada alisema uvuvi haramu wa kutumia mabomu umepungua kwa asilimia 88 ambapo kabla ya Serikali kuanza kuchukua hatua hizi mabomu yalikuwa yakipigwa kila sehemu katika ukanda wa pwani ambapo wavuvi wengi walijeruhiwa na wengine kupoteza maisha.

Alisema hali hiyo ilichangia kutishia usalama ambapo pia ilisababisha baadhi ya watalii kuogopa kuja nchini mwetu ambapo inakadiriwa mlipuko wa bomu moja huathiri mzunguko wa mita 15 hadi 20 na kuua samaki na viumbe vingine vyote mayai na mazalia yake.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kusimamizi wa Bahari Kuu(DSFA) Dkt. Omary Ali Amir akitoa mada kuhusu Operesheni Jodari alisema kwa kipindi kirefu Serikali imekuwa ikipata mapato kidogo sana kutokana na uvuvi wa ukanda wa bahari kuu(EEZ).Meli za kigeni zinazokuja kuvua nchni mauzo yao ni wastani wa shilingi bilioni 450 kwa mwaka lakini wastani wa mapato ya Serikali kwa mwaka ni bilioni 3.2 tu.

Alisema katika Operesheni inayoendelea meli 21 kati ya 24 zilizokaguliwa zilikutwa na makosa, ambapo meli 20 zilipigwa jumla ya faini ya shilingi bilioni 20 kutokana na makosa mbalimbali wakati meli moja ya Buah naga One imefikishwa katika Mahakama ya Mtwara na kesi inaendelea.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Emmanuel Bulayi akiwasilisha Mada ya Operesheni Sangara 2018 kweye ukanda wa Ziwa Victoria alisema vita dhidi ya uvuvi haramu na biashara haramu ya mazao ya uvuvi haina suluhu ambapo alisema hivi sasa kumeibuka biashara ya mabondo ambayo imechochea kasi ya uvuvi na biashara haramu ya mazao ya uvuvi, bei ya kilo moja ya bondo inauzwa kati ya shilingi 70,000 hadi shilingi 900,000.Thamani ya bondo ni kubwa kuliko samaki mwenyewe.

Alisema jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 7 zimekusanywa kutokana na mauzo ya samaki, kayabo na mabondo pamoja na faini katika Operesheni hiyo.