DC SAME ATANGAZA KIAMA MAJANGILI AWAFANANISHA NA WAUJUMU UCHUMI

April 11, 2023

MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lengo likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani
MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni  kushoto akizungumza na Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi wakati alipofika kwenye hifadhi hiyo kuitembelea ikiwa ni  kuhamasisha utalii wa ndani
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye Hifadhi hiyo na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu 



Afisa Utalii wa Hifadhi wa Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi  kulia akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni wakati wa ziara yake kwenye hifadhi hiyo
Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni katika akiwa ni Meneja wa Benki ya CRDB wilaya ya Same kulia  
Watalii wakifurahia utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Tembo akiwa na mtoto wake katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi


Twiga akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi





Na Oscar Assenga aliyekuwa KILIMANJARO

MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni ametangaza vita mpya baada ya kuwatahadharisha majangaili ambao wanafikiria kupitia ujangili wanaweza wakanufaika kuachana na biashara hizo kutokana na kwamba wao wamejipanga kuhakikisha wanawashughulikia vilivyo.

Vita hiyo aliitangaza mwishoni mwa wiki wakati alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ikiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani ambapo alisema watahakikisha wanashughuliwa ili kuhakikisha hawagusi hifadhi ikiwemo kuwataka wajiandae kutafuta kazi nyengine .

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kama walifikiria hiyo ndio ajira yao wajiandae kutafuta kazi nyengine kwa sababu yenye ni mhifadhi na anafahamu umuhimu wa hifadhi na ndio Mwenyekiti wa Kamati ya usalama wa wilaya hiyo.

“Hifadhi nyingi zimekuwa zikikabiliwa na vitendo vya ujangili hivyo sisi kama Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya tumejipanga kuhakikisha tunashirikiana na hifadhi kutokomeza ujangili mikakati hiyo ni pamoja na tunapokuwa kwenye mikutano yao ya vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo miongoi mwa mambo tunaowaeleza ni umuhimu wa hifadhi na athari za kuwa na ujangili”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya wanapokuwa kwenye ziara katika vijiji hivyo wanawaelimisha wananchi umuhimu wa hifadhi na kuwaonya waache kufanya biashara za ujangili kwa sababu wanapoendelea kuifanya serikali kupitia vyombo vyake itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria.

“Kwa sababu wanakuwa kama wahujumu uchumi kutokana na kwamba hifadhi hizo zinafanya uchumi wa nchi unaweza kuimarisha hivyo kunapokuwa na majangili wanaoua wanyama ambao watalii wanakuja kuangalia hiyo ni hujuma hivyo serikali ya wilaya tumejipanga vizuri kushirikiana na hifadhi kuhakikisha havijitokezi”Alisema Mkuu huyo wa wilaya

Alisema kwamba Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ndio Hifadhi muhimu kwa Kanda ya kaskasini na kuna wanyama wengi wanaopatikana kwenye hifadhi nyengine nchini lakini ukifika eneo hilo una uhakika kuweza kumuona mnyama Faru kiurahisi sana na imesaidia wilaya ya sama kuwa na watalii wengi wanaokwenda kumuona mnyama huyo.

Hata hivyo alisema kwamba wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu amefanya mambo makubwa sana kupitia Royal Tour imewasaidia sana hifadhi kutokana na kwamba baada ya ziara hiyo wataalii wanaoingia kwa mwaka kwenye hifadhi hiyo kwa sasa ni zaidi ya 7000 hiyo ni faida kubwa walioipata kupitia ubunifu huo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba Rais Dkt Samia Suluhu kupitia Fedha za Tozo na Fedha za Covid ameweza kuimarisha miundombinu ya hifadhi nchini ambapo miongoni mwa hifadhi ambazo zimenufaika ni mkomazi ambapo kuna majengo ya utawala na barabara nzuri ambao zinahamasisha watalii hivyo Rais amekuwa mfano nzuri wa uhifadhi nchini.

Aidha pia alisema wanapokuwa na hifadhi inayofikika kirahisi wanapata watalii wengi ambazo wanasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu

Hata hivyo aliwahimiza watanzania kutembelea hifadhi za hapa nchini ili kuweza kujionea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo kuwataka pia wananchi wa wilaya ya Same watumie wikiendi zao kuweza kufika mkomazi kuweza kuona vivutio vilivyopo na hivyo kusaidia serikali kuingiza mapato ambayo yatasaidia maendeleo kwenye wilaya yao.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Utalii wa Hifadhi wa Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kutokana na kupelekea fedha za Uviko ambapo waliweza kuzitumia kujenga lango maalumu ambalo ni la kuingilia wageni wanaofika kutembelea hifadhi hiyo na kuweza kupata huduma nzuri za utalii.

Alisema kwamba kupitia fedha hizo wameweza kujenga barabara nzuri yenye utefiu wa zaidia ya kilomita 140 na pia kutengeneza viwanja vya ndege na hiyo imetoa fursa kwa wageni ambao hawana muda wa kutembea kwenye magari kwa muda mrefu wakati wa safari zao kutoka maeneo mbalimbali kwenda kuitembelea hifadhi hiyo

Happiness alisema kwa kujengwa uwanja huo kumesaidia wageni kusafiri kutumia ndege kufika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi moja kwa moja kutoka kwenye viwanja vyengine

WAUGUZI HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO WAFUNDISHWA NAMNA YA KUPIMA USIKIVU WA WATOTO WANAPOZALIWA

April 11, 2023

Muuguzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Prisca Massawe kushoto akimpima usikivu mtoto aliyezaliwa katika hospital hiyo wakati wa mafunzo  ya kuwafundisha namna ya kupima usikivu kwa watoto wachanga wanapozaliwa juzi  kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Hamisi Shaban Mtitho kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Muuguzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Prisca Massawe kushoto akimpima usikivu mtoto aliyezaliwa katika hospital hiyo wakati wa mafunzo  ya kuwafundisha namna ya kupima usikivu kwa watoto wachanga wanapozaliwa juzi  kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Hamisi Shaban Mtitho kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili



 WAUGUZI katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo wamefundishwa namna ya kupima usikivu wa watoto wadogo wanapozaliwa ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa ufanisi na tija kubwa kwa wananchi wanaowahudumia

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mwishoni mwa wiki ,Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt Edwin Liyombo alisema kwamba wameamua  kuwafundisha wauguzi program ya kupima usikivu kwa watoto wanaozaliwa ili kuweza kuwasaidia watoto wanaokuwa na shida hiyo pindi wanapozaliwa.

Alisema kwa sababu imeonekana kuna watoto wengi wanajulikana wana matatizo ya usikivu na wanashindwa kuongeza pindi wanapokuwa na umri wa kuanza kwenda shule ikiwemo wanaozaliwa hawawezi kuongea hivyo mpango huo unasaidia kugundua mtoto pale anazaliwa  mpaka mwezi mmoja.

Aidha alisema kwa sababu kuna mashine maalumu ya kuwapima kama wana matatizo na wakibainika mapema inawasaidia kuweza kuona namna ya kulipatia ufumbuzi.

“Tunawafundisha wauguzi jinsi ya kufanya uchunguzi na baadae itakwenda nchi nzima kwani hawa wanaowafundisha baadae watakuwa walimu na kufundisha wengine lakini tutawaleta mashine ndogo itakayotumika kupima watoto wanapozaliwa”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba wanaomba watu wajitokeze wakati wa mpango huo wa kupima usikivu huku akieleza kwamba katika zoezi lao wamepima watoto 20 wengi hawana matatizo kadri watakavyopima wengi watajua hali ipo vuzri na hivyo kuisaidia wizara kupanga bajeti ili kuona namna ya kuwasaidia.

Katika hatua nyengine Dkt Edwin alisema kwamba takwimu zinaonyesha kwamba kati wa watu 100 watu 7 wana tatizo la usikivu na watoto wadogo na ndio sababu Hospitali ya Taifa ya Muhimimbiili walianzisha program ya kuweka kipandikizi kwa ajili ya kusikia ambayo tokea mwaka 2017 mpaka sasa watoto 57 wamekwisha kufanyiwa.

Alieleza kwamba watoto wengi wanakuwa na matatizo wakati wanazaliwa au wakiwa na umri mdogo wameona wakiwagundua mapema inasaidia kufuatilia kuona ni sababu zipi zinapelekea kuwepo kwa hali hiyo kwa watoto ili kuweza kuzuia lisiweze kujitokeza.