UWANJA WA MCHEZO WA GOFU WAZINDULI ZANZIBARI

UWANJA WA MCHEZO WA GOFU WAZINDULI ZANZIBARI

February 09, 2015

1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini akisalimiana na wageni waliohudhuria  katika ufunguzi wa Kiwanja kipya cha Mchezo wa Gofu jana uzinduzi alioufanya kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa kaskazini Unguja.
Picha na Ikulu
2
Mwenyekiti wa Kampuni ya Sea Cliff Resort and Spa Zamzibar Bw.Subhash Patel (kushoto) akibadilishana mawazo na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini baada ya kufungua kiwanja kipya cha Mchezo wa Gofu jana alipomuwakilisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa kaskazini Unguja.
4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini akitoa hutuba ya ufunguzi wa kiwanja kipya cha Mchezo wa Gofu kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Sea Cliff  iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa Kaskazini Unguja.
5
Msimamizi na Mtengenezaji wa  ujenzi wa kiwanja kipya cha mchezo wa Gofu Bw.Peter Matkovich kutoka Afrika Kusini alipokuwa akitoa shukurani zake wakati wa sherehe za ufunguzi wa kiwanja hicho  jana katika Hoteli ya Sea Cliff  iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa Kaskazini Unguja,
6
Baadhi ya wageni mbali mbali kutoka Ndani na nje ya Zanzibar wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa kiwanja kipya cha mchezo wa Gofu kilichofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Kiombamvua Wilaya ya Kaskazini B. Mkoa wa kaskazini Unguja,

SERIKALI YAIPONGEA BENKI YA ACCESS KUFUNGUA TAWI LAKE JIJINI MBEYA

February 09, 2015

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Access wakati alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo jijini Mbeya mwishoni wa wiki iliyopita. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Dk. Norman Sigallah King na kutoka kushoto ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa Access Bank, Jonas Muganyizi Bisheko, Meneja wa Mkoa wa Benki ya Access Mbeya, Emmanuel Venance na Mwakilishi wa Benki ya Access kutoka Makao makuu jijini Dar es salaam, Sebastian Gaissert. 
(PICHA ZOTE NA CATHBERT ANGELO KAJUNA WA KAJUNASON BLOG-MBEYA).
Mwakilishi wa Benki ya Access kutoka Makao makuu jijini Dar es salaam, Sebastian Gaissert, akitoa hotuba yake katika sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani Mbeya.

Meneja wa Mkoa wa Benki ya Access Mbeya, Emmanuel Venance akizungumza machache wakati wa sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani Mbeya.

Wafanyakazi na wageni walioalikwa waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro akikata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Benki ya Access tawi la Mbeya. Pembeni kulia ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa Access Bank, Jonas Muganyizi Bisheko na Mwakilishi wa Benki ya Access kutoka Makao makuu jijini Dar es salaam, Sebastian Gaissert.
Akiweka na jiwe la Msingi...

Meneja wa Tawi la Benki ya Access- Mbeya, Makange Kilimali akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro mara baada ya kuingia ndani ya Benki hiyo.

Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wakifungua akaunti katika Benki ya Access baada ya kuzinduliwa rasmi.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro akionyesha kitambulisho chake mara baada ya kufungua akaunti katika benki hiyo.
Viongozi wakiwa katika picha na Mkuu wa Mkoa, Mh. Abbas Kandoro (wa pili toka kulia) pembeni yake ni Mkuu wa Wiyala ya Mbeya, Mhe. Mhe. Dk. Norman Sigallah King na Ofisa Masoko Mwandamizi wa Access Bank, Jonas Muganyizi Bisheko. Wengine toka kushoto ni Meneja wa Tawi la Benki ya Access- Mbeya, Makange Kilimali, Meneja wa Mkoa wa Benki ya Access Mbeya, Emmanuel Venance na Mwakilishi wa Benki ya Access kutoka Makao makuu jijini Dar es salaam, Sebastian Gaissert.
Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya.
---

*WANANCHI WAMETAKIWA KUITUMIA KUPATA MIKOPO.

Na Mwandishi Wetu, Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka wakazi wa jiji la Mbeya kuacha kasumba ya kuhifadhi fedha nje ya mfumo wa kibenki kwa kuwa unadidimiza ukuaji wa kiuchumi.
Kandoro aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tawi la Benki ya Access katika hafla iliyofanyika kwenye viunga vya tawi hilo Mafiati jijini Mbeya.
Alisema katika utafiti uliofanyika mwaka 2013 ulibaini kuwa ni asilimia 7 tu ya wakazi wa Mkoa wa Mbeya ambao hutumia mifumo ya kibenki kuhifadhi fedha zao huku asilimia 93 wakihifadhi majumbani mwao.
Alisema tabia ya kuhifadhi fedha majumbani haisadii katika kuongeza mzunguko wa fedha bali huchangia kudidimiza uchumi wa Mkoa kutokana na fedha hizo kutoingia kwenye mzunguko wa soko.
Aliongeza kuwa kitendo cha kuhifadhi fedha majumbani pia huchangia kuwavutia majambazi ambao huweza kuvamia na kuiba hivyo njia pekee ya kuhifadhi fedha ni kwa njia ya benki.
Aidha Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa watumishi wa benki kufanya kazi kwa uadilifu na kuwa waaminifu kwa wateja wao kwa kuepuka kuiba fedha kwenye akaunti zao pamoja na kuvujisha siri za ndani za akaunti ya Mteja.
“ Ni toe wito kwa watumishi epukeni kuvujisha siri za akaunti za wateja wenu, wizi kwa njia za mtandao hivyo jengeni imani kwa wananchi kwa kufanya kazi kwa uadilifu” alisema Kandoro.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Benki hiyo kutoka Makao makuu Dar es salaam, Sebastian Gaissert, Benki hiyo imevutiwa kufungua tawi mkoani Mbeya kutokana na kuwa miongoni mwa Mikoa yenye shughuli nyingi za kiuchumi na inayokua kwa kasi kimaendeleo.
Alisema sababu nyingine ya kufungua tawi Mkoa wa Mbeya ni kutokana na kuiunganisha Tanzania na nchi jirani hivyo kuchochea shughuli za kibiashara pamoja na kuwa tegemeo kwa kilimo cha mazao ya chakula na biashara.
Aliongeza kuwa sababu ya pekee ni kuimarika kwa ulinzi na usalama hivyo kuipelekea benki hiyo kuvutiwa na hali hiyo na kuona ni sehemu salama kwa ajili ya uwekezaji mkubwa.
Alisema tangu kufunguliwa kwa Tawi hilo Mkoani Mbeya Januari Mwaka huu zaidi ya mikopo 600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 imetolewa kwa wateja wao pamoja na kufanikiwa kufungua akaunti mpya zaidi ya 1500.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI IKULU

February 09, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadaye katika mazungumzo na uongozi wa juu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es salaam uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo February 9, 2015. Ujumbe huo umeongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania Dkt Alex Malasusa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba la taifa (NHC) na Mwenyekiti wa Harambee ya chuo hicho ambacho kinamilikiwa na kanisa la KKKT. PICHA NA IKULU


Kilichoamriwa na Halmashauri ya Manispaa ILALA kuhusu jengo la ghorofa 15 na watu wanaoishi JANGWANI DAR

Kilichoamriwa na Halmashauri ya Manispaa ILALA kuhusu jengo la ghorofa 15 na watu wanaoishi JANGWANI DAR

February 09, 2015

Kettenbagger_CAT_325C_LN
Kuanguka kwa majengo marefu katikati ya Jiji la Dar es Salaam na sehemu nyingine Tanzania ni moja ya vituambavyovimetajwa kuhatarisha maisha ya watu, kitu ambacho kimesababishwa kuibuka maswali mengi kwamba wenye mamlaka wanakuwa wapi wakati ujenzi wa aina hii ukiwa unafanyika?
Kamati ya Ardhi na Mipango Miji ya Manispaa ya Ilala imefanya maamuzi ya kuvunjwa kwa jingo al ghorofa 15 lililojengwa katikati ya Jiji baada ya kubainika kuwa lilijengwa chini ya kiwango.
Mhandisi wa Manispaa hiyo Bwigane Jafary amesema amri ya Mahakama pia imeagiza kuvunjwa nyumba zote zilizoko mabondeni bila kulipwa fidia baada ya wananchi kushindwa kesi.
“Uvunjaji wa majengo marefu si wasa na uvunjaji wa majengo ya kawaida… jingo lile limebanwa na majengo mengine.. njia pekee ambayo tunatakiwa tuitumie pale ni kutumia excavator yenye mikono mirefu…”—Bwigane Jafary.
Kwa wakazi wale wa jangwani ambao walikuwa wamefungua kesi Mahakamani kuipinga Halmashauri ile kesi imekwenda ba hatimaye wale wakazi wameshindwa…” aliongea Bwigane Jafary kuhusu ishu ya wakazi wa Jangwani, Dar.

Serikali yajipanga kutumia nguzo za zege kusambaza umeme

February 09, 2015

Wataalam wa Sekta ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), wakiongozwa na Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kushoto), wakiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa Kampuni ya Sunshine Group Ltd (Kulia). Mazungumzo yalifanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam na yalihusu uanzishwaji wa Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya kusambaza umeme nchini.
Ujumbe kutoka Kampuni ya Sunshine Group Ltd, ukiwa katika mazungumzo na wataalam wa Sekta ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme nchini – Tanesco (hawapo pichani). Kampuni hiyo iliwasilisha mapendekezo (proposal) ya kuanzisha Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya matumizi ya hapa nchini.

Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga (Kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sunshine Group Ltd, Bw. Sun Tao aliyekuwa akitoa ufafanuzi wa jambo fulani, mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina ya Wataalam wa Wizara na wawakilishi wa Kampuni hiyo kuhusu uwezekano wa kuanzisha Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya kusambaza umeme nchini.

Na Veronica Simba

Serikali inaendeleza jitihada za kuachana na matumizi ya nguzo za umeme za miti na badala yake kutumia nguzo za zege ikiwa ni hatua mojawapo ya kuboresha huduma ya usambazaji na upatikanaji wa umeme nchini.

Hayo yalibainika mwishoni mwa wiki katika kikao baina ya uongozi wa Kampuni ya Sunshine Group Ltd na wataalam wa sekta ya umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme nchini (Tanesco).

Katika kikao hicho, Kampuni ya Sunshine iliwasilisha mapendekezo (proposal) ya kuanzisha kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya matumizi ya hapa nchini.

Akieleza msimamo wa Serikali kuhusu mapendekezo hayo, Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga alisema Serikali ina dhamira ya kutumia nguzo za umeme zilizotengenezwa kwa zege na kuachana na za miti zinazotumika sasa kutokana na manufaa yake.

Mhandisi Luoga aliyataja manufaa ya kutumia nguzo za zege kuwa ni pamoja na uimara wa nguzo husika. “Huwezi kulinganisha uimara wa nguzo za zege na hizi za miti tunazotumia hivi sasa. Nguzo za zege ni madhubuti na imara zaidi,” alisema.

Akifafanua zaidi, Mhandisi Luoga alisema, kutokana na uimara wa nguzo za zege, uhai wake ni wa muda mrefu kulinganisha na nguzo za miti.

“Uhai wa nguzo za zege ni kati ya miaka 70 hadi 100, wakati uhai wa nguzo za miti ni miaka 50,” alisema Luoga na kusisitiza kuwa sifa hiyo ya uhai mrefu wa nguzo za zege inazalisha manufaa mengine kwa Serikali na wananchi kwa ujumla endapo nguzo hizo zitatumika.

Akielezea manufaa yanayotokana na uhai mrefu wa nguzo za zege, Mhandisi Luoga alisema Serikali itatumia fedha kidogo kutokana na nguzo za zege kudumu kwa muda mrefu, tofauti na nguzo za miti ambazo uhai wake ni mdogo.

Aidha, faida nyingine za kutumia nguzo za zege, zilizotajwa na wataalam katika kikao hicho ni pamoja na kuwa rafiki wa mazingira ambapo huepusha ukataji wa miti.

Nyingine ni uwezo wake wa kutopitisha maji na kutoshika moto kwa urahisi (water and fire proof). Akihitimisha mazungumzo husika, Kamishna Luoga alisema Serikali itaendelea kufanya mazungumzo na Kampuni hiyo pamoja na wawekezaji wengine wenye nia ya kutengeneza nguzo za umeme za zege ili kufikia makubaliano yatakayowezesha pande zote mbili kunufaika.

“Mkakati wetu ni kwa Tanesco kutengeneza nguzo za zege kwa matumizi ya ndani ya nchi lakini ni vema tukapata wawekezaji wengine watakaosaidia kutengeneza nguzo hizo kwani mahitaji ni makubwa sana,” alisema.

WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO WA KUKUZA STADI ZA KKK

February 09, 2015

*Ataka AZISE zishirikishwe kikamilifu
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua Mpango wa Kitaifa wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) unaolenga kukuza viwango vya uelewa kwa watoto wa darasa la kwanza na la pili kwa nchi nzima.
Mpango huo wa miaka mitatu ulioanza kutekelezwa 2014/2015 hadi 2016/2017 umelengwa kuwahusisha watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 13 walio kwenye mfumo rasmi wa elimu na usio rasmi (MEMKWA).
Akizungumza na wadau wa elimu, walimu na wanafunzi walioshiriki uzinduzi huo jana jioni (Jumamosi, Februari 7, 2015) Waziri Mkuu Pinda alisema mpango huo ni mkubwa na umeandaliwa mahsusi kujibu changamoto zilizojitokeza miaka ya nyuma.

Aliwataka watekelezaji wakuu wa mpango ambao ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kuhakikisha kuwa wanazishirikisha asasi zisizo za Kiserikali ambazo zinajihusisha na masuala ya elimu.

“Kuna mashirika mengi yasiyo za kiserikali ambayo ni chachu ya kuhimiza elimu nchini... jaribuni kuwashirikisha sababu wao ni wadau wazuri sana wa suala hili. Pangeni utaratibu wa kukaa na hawa wadau na kuwapa mrejesho wa mpango huu mzima,” alisema Waziri Mkuu.

Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwataka wahusika wakuu wa mpango waangalie mgawanyo wa mikoa iliyoingizwa kwenye mpango huo kwa kuzingatia kanda ili kuleta matokeo ya mtawanyiko badala ya hali ilivyo sasa. “Nimeangalia jinsi mlivyogawa mikoa yenu, inanipa taabu kidogo... kuna mikoa inahitaji msukumo wa pekee, mikoa ya wadugaji, mikoa iliyoko pwani ya bahari na maziwa, yote inahitaji msukumo wa tofauti,” alisema.

Katika taarifa yao, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilisema mpango huo wa KKK au LANES (Literacy and Numeracy Support Programme)  unafadhiliwa na Ushirika wa Kimataifa wa Maendeleo ya Elimu (Global Partnership for Education – GPE) na wahisani wengine.

Wahisani hao ni pamoja na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) kupitia mradi wa EQUIP-T unaotekelezwa katika mikoa saba ya Kigoma, Shinyanga, Mara, Simiyu, Lindi, Dodoma na Tabora; Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu kwa Mtoto (UNICEF) wanaofadhili utelekezaji wa Mpango wa LANES katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe; na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) kupitia Mradi wa TZ-21 unaotekelezwa katika mkoa wa Mtwara.

Mapema, akisoma taarifa ya mpango huo mbele ya Waziri Mkuu, Kamishna wa Elimu nchini, Prof. Eustella Bhalalusesa alisema mpango huo umelenga kuongeza ufanisi katika stadi za KKK, kurahisisha kazi ya walimu wanaofundisha watoto wa darasa la kwanza na la pili pamoja na kuongeza ushiriki wa jamii katika kuboresha elimu na hasa ujifunzaji wa stadi za KKK.

Alisema mpango huo utachangiwa sh. bilioni 150 ambazo zitaingizwa moja kwa moja kwenye mfuko wa elimu kupitia Wizara ya Fedha.

Alisema maandalizi yote ya utekelezaji wa mpango huu yamekamilika ikiwa ni pamoja na mtaala wa darasa la kwanza na darasa la pili, muhtasari wa KKK kwa darasa la I & II, pamoja na Mwongozo wa Mwalimu wa kufundisha kusoma kuandika na kuhesabu.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMAPILI, FEBRUARI 8, 2015.

HIVI NDIVYO WAFANYABIASHARA WA SOKONI NGAMIANI WANAVYONYONYOA KUKU

February 09, 2015
 Wafanyabiashara wa kuku soko kuu la Ngamiani Tanga, wakinyonyoa kuku wa mteja baada ya kununua ukiwa ni utaratibu wa wachuuzi sokoni hapo endapo mteja atapendezwa na kulipa ujira wa shilingi elfu moja kwa kuku mmoja. Kuku mmoja alikuwa akiuzwa kati ya shilingi 8,000 hadi 10,000 kulingana na ukubwa wake.