WAZIRI MWAKYEMBE, MASAUNI WAFANYA ZIARA MKOANI GEITA, WAZUNGUMZA NA UONGOZI GGM, WATEMBELEA GEREZA CHATO

July 14, 2016
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya mkoani Geita (GGM) pamoja na Viongozi wa Serikali wa mkoa huo, kuhusiana na masuala mbalimbali ya utatuaji wa migogoro iliyopo kati ya GGM na wananchi wanaoishi jirani na mgodi huo. Waziri Mwakyembe aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, katika ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga (katikati), na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto) mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi zilizofanywa na viongozi hao wa Wizara. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Geita (GGM), Terry MulPeter akizungumza katika kikao kati ya uongozi wa kampuni yake na viongozi wa serikali uliokuwa unaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hawapo pichani). Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo katika kikao cha viongozi wa serikali pamoja na viongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Geita (GGM) cha kujadiliana masuala mbalimbali ya utatuzi wa migogoro kati ya kampuni hiyo na wananchi wanaoishi jirani na kampuni hiyo. Kikao hicho ambacho kiliongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (wanne kulia) ambacho kilifanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga. Wa pili kulia ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kushoto kwa Dk Mwakyembe), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati ya Dk Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa) pamoja na viongozi wengine wakitoka kulikagua Bweni la Mahabusu la Gereza Chato linalojengwa mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo ndani ya Bweni la Mahabusu la Gereza Chato linalojengwa mkoani Geita. Wapili kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa kiongozi wa msafara huo. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu, Edward Kaluvya.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari mjini Chato, mkoani Geita mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yao na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto). Katika ziara yao licha ya kufanya majukumu mengi ila walifanikiwa kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini mkoani Geita (GGM) na pia walilikagua Gereza Chato linalojengwa mkoani humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI MBARAWA ATEMBELEA VIWANJA VYA NDEGE JULIUS NYERERE

July 14, 2016

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Maafisa Uhamiaji katika Kiwanja cha Ndege Cha Kimataifa Cha Julius Nyerere(Terminal II), alipotembelea kuangalia utendaji kazi na vifaa vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa malekezo wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi George Sambali (Katikati), alipotembelea Mamlaka hiyo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa malekezo wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi George Sambali (Katikati), alipotembelea Mamlaka hiyo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa malekezo wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi George Sambali (Katikati), alipotembelea Mamlaka hiyo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na Mawakala wanaofanya kazi  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),alipotembelea kuona utendaji kazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Swissport, Gaudence Temu, wakati alipotembelea Ofisi hiyo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) hawapo pichani, wakati alipoongea nao jijini Dar es Salaam. 
                                                   (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo)
WAZIRI MBARAWA AIAGIZA TAA KUONGEZA MAPATO.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuongeza kiwango cha ukusanyaji mapato kutoka Bilioni 74 hadi kufikia bilioni 105 katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo mara baada ya kukagua majengo matatu na ofisi mbalimbali zilizopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA).
Amesisistiza wafanyakazi wa Uwanja huo kuhakikisha kiasi cha ukusanyaji wa mapato hayo kinaongezeka siku hadi siku ili kukuza uchumi wa taifa na kuchochea fursa za kimaendeleo.

“Ni lazima muongeze kasi ya kufanya kazi ili mapato yaongezeke kwa kuwa uwezo mnao na nimeona kwenye viwanja vyenu kuna sehemu nyingi za biashara, hivyo mna kila sababu ya kukusanya kiasi hicho cha fedha”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, katika ziara hiyo Waziri Prof. Mbarawa alibaini ucheleweshwaji wa vibali kwa abiria wanaoingia katika Uwanja wa Ndege wa  JNIA ambapo abiria huchukua zaidi ya saa moja kupata vibali.

“Nimesikitishwa na kitendo cha ucheleweshwaji wa vibali kutoka Idara ya Uhamiaji na huduma za kibenki zinazotolewa… hali hii haileti picha nzuri kwa wageni wetu. Abiria kuwekwa zaidi ya saa moja akisubiri kupata huduma, sitaki kuona hali hiyo ikiendelea”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Sambamba na hilo amezitaka taasisi zote zinazofanya kazi katika viwanja vya ndege kushirikiana kwa ukaribu ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na kuongeza mapato kwa taifa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Eng. George Sambali amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa mapungufu yaliyobainishwa yatafanyiwa kazi ili kuongeza ufanisi na huduma bora kwa abiria.
“Kwa kushirikiana na taasisi zote ambazo zinafanya kazi katika Kiwanja hiki tutahakikisha tunatoa huduma nzuri na kuongeza ufanisi katika utendaji ili kufikia malengo”, amesema Eng. Sambali.

Waziri Prof. Mbarawa amefanya ziara ya siku moja katika Kiwanja cha JNIA ili kuona utendaji kazi na maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria ambapo jengo hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2017 na litakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya abiria milioni sita kwa mwaka.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano .

MAJI MAREFU AMWAGA MADAWATI JIMBONI MWAKE.

July 14, 2016
 Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Robet Gabriel kushoto akipokea madawati 200 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu jana ambapo madawati hayo yalitolewa kupitia fedha za mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa madawati kwa shule za msingi wilayani Korogwe
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngony'ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu kulia kushoto ni Diwani wa Kata ya Kerenge wilayani Korogwe wakiwa wamebeba moja kati ya madawati 200 ambayo yalikabidhiwa leo na mbunge huyo kupitia Fedha za mfuko wa Jimbo kwa ajili ya shule za msingi wilayani Korogwe jana,Picha na
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM),Steven Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kutoa madawati
  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM),Steven Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu wa kwanza kushoto akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Robert Gabriel ofisini kwake kabla ya kumkabidhi madawati 200 leo
wanafunzi wa shule za msingi wilayani Korogwe wakiwa wamekaa kwenye madawati 200 yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Proffesa Maji Marefu kupitia Mfuko wa Jimbo.



Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Proffesa Maji Marefu kupitia Mfuko wa Jimbo katikati akiwa amekaa kwenye madawati 200 aliyoyakabidhi leo kwa shule za msingi wilayani humo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Robert Gabriel kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe,Abeid Mohamed