March 07, 2014

DC Muhingo alipozuru Chumba cha habari cha New Habari 2006 Ltd

Mkuu wa Wilaya Handeni, mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu, kulia akipitia gazeti la Michezo la Bingwa, akiwa sambamba na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda katikati, pamoja na mke wake Fatuma Waziri kushoto. 

New Habari ni wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai na The African, wakiwa na maskani yao Sinza Kijiweni, jijini Dar es Salaam. DC Muhingo alitumia muda huo alipotembelea chumba cha habari hicho na kujadili mambo mbalimbali na Kibanda. 

DC Muhingo ni kama vile ametembelea nyumbani kwake kutokana na taaluma yake ya habari, huku akiwahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo ambapo nafasi hiyo ipo chini ya Kibanda kwa sasa. Picha na Jumanne Juma.


March 07, 2014

Timu ya Machava FC yapewa msaada wa jezi

Meneja masoko wa kampuni ya Megatrade (T) Ltd,Goodluck Kway akikabidhi hundi ya sh Milioni 3 kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama ikiwa ni sehemu ya msaada kwa timu ya soka ya Machava fc inayoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro.shoto kwake ni Meneja mauzo wa Kampuni ya Megatrade(T)Ltd kanda ya kaskazini Edimund Lutaraka.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Megatrade (T) Ltd, Goodluck Kway akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama jezi zenye thamani ya kiasi cha sh Milioni 3 ikiwa ni sehemu ya msaada kwa timu ya soka ya Machava fc inayoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro,kushoto kwake ni Meneja mauzo wa Kampuni ya Megatrade(T)Ltd kanda ya kaskazini Edimund Lutaraka.

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AOMBOLEZA KIFO CHA MTOTO WA WAZIRI SOPHIA SIMBA DAR

March 07, 2014
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole.
 Marehemu Lefoord Simba, enzi za uhai wake.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwake  Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, leo kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni.
March 07, 2014

MECHI YA YANGA SASA KUCHEZEWA UWANJA HUU HAPA UJUE JINA NA WAPI LIVE HAPA!!

ALEX STADIUM
Baada ya ukimya na utata, sasa imetangazwa kuwa mechi kati ya mabingwa Afrika, Al Ahly na wale wa Tanzania Bara, Yanga itapigwa kwenye Uwanja wa Max mjini Alexandria.

Mji huo uko kwenye pwani ya bahari ya Mediterranean, kilomita zaidi ya 200 kutoka katika jiji hili la Cairo, mwendo wa zaidi ya masaa mawili.
March 07, 2014

BREAKIN NEWZZZ:- NA HII NDIO NDEGE MPYA YA AIRTANZANIA ILIPOTUA JANA BONGO KWA MARA YA KWANZA LIVE!!

  Ndege 5Y-WWA aina ya CRJ200 iliyowasili usiku wa jana
  Ndege 5Y-WWA aina ya CRJ200 Baada ya Kutua Jana usiku
March 07, 2014
March 07, 2014
March 07, 2014

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AZUNGUMZA NA WANAHABARI MJINI IRINGA LEO KUHUSU UCHAGUZI WA JIMBO LA KALENGA

 Msajili
Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini,Bwa.Sistyl Nyahoza akifafanua jambo
mbele ya Waandishi wa Habari  (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye
Ukumbi wa Ruaha International,mkoani Iringa kuhusiana na masuala
mbalimbali yanayohusu uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la kalenga,
ikiwa ni pamoja na Sheria ya gharama za Uchaguzi kwa wagombea na vyama
husika vinavyoshiri katika Uchaguzi huo utakaofanyika machi 16 mwaka
huu.
Pichani
wa tatu kulia ni Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini,Bwa.Sistyl
Nyahoza akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo asubuhi kwenye
Ukumbi wa Ruaha International,mkoani Iringa kuhusiana na masuala
mbalimbali yanayohusu uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la kalenga,
ikiwa ni pamoja na Sheria ya gharama za Uchaguzi kwa wagombea na vyama
husika vinavyoshiri katika Uchaguzi huo utakaofanyika machi 16 mwaka
huu.Shoto ni Bwa.Mihayo Kadete,Erald Martin na kulia ni Isaya Makoko
ambao wote ni Maofisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
March 07, 2014

MWENYEKITI WA CHADEMA WANGAMA AJISALIMISHA CCM, ASEMA WENGI WAKO NYUMA YAKE

Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa Bw. Godfrey Mgimwa akishiriki kucheza ngoma pamoja na Mwenyekiti wa (CCM) mkoa wa Iringa Bi. Jesca Msambatavangu wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika kijiji cha Wangama kata ya Luhota mahali ambapo pi ndiyo alipozaliwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia (CHADEMA) Bi Grace Tendega, Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema katika kijiji hicho Bw.John Mgata amejisalimisha na kurejea CCM ambapo amesema wanachama wengine zaidi ya 50 wamekata shauri na wameamua kumfuata na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KALENGA) 2Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa Bw. Godfrey Mgimwa akimpongeza Bw. Mwenyekiti wa CHADEMA katika kijiji cha Wangama Bw, John Mgata mara baada ya kurejea CCM katika mkutano huo uliofanyika kijijini hapo leo.
March 07, 2014

KAMPENI YA KUPAMBANA NA HOMA YA INI YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk. Meshack Shimwela, akielezea madhara ya ugonjwa wa Homa ya Ini.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick amezindua rasmi kampeni ya kupambana na Ugonjwa wa Homa ya Ini katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Kampuni ya Global Pulishers Ltd wakishirikiana na Wizara ya Afya, SD Africa, Sanofi, Megra Clinic, Damu Salama na Tamsa.
Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka wadau mbalimbali kuonyesha ushirikiano katika kupambana na ugonjwa huo hatari kuliko HIV huku akiwaasa wananchi kuacha vitendo vinavyoweza kuleta maambukizi ya ugonjwa huo unaombukizwa kwa njia sawa na za HIV.
(PICHA ZOTE NA GPL)
Shigongo akiwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kupambana dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Ini.
March 07, 2014

HOSPITALI YA KCMC NA CRDB WAZINDUA HUDUMA YA KULIPIA GHARAMA ZA MATIBABU KWA NJIA YA KADI

Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheli dayosisi ya kaskazini Dk Martini Shao akiwa na mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB pamoja na kaimu mkurugenzi wa hosptali ya KCMC .Prof Raimosi Ollomi wakati akizindua tawi dogo la Benki ya CRDB.
Mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB,Dk Charles Kimei akimuelekeza jambo Askofu Dk Martin Shao kabla ya uzinduzi wa huduma ya malipo ya gharama za matibabu kwa njia ya Kadi.
March 07, 2014


*MATUKIO KUTOKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA LEO
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira akiwaeleza jambo wajumbe wenzie Bi. Anna Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Richard Ndassa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sumve, kabla ya kuingia katika Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi John Magufuli akimweleza jambo Mjumbe mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo Bw. John Mnyika Mapema leo Mjini Dodoma.
March 07, 2014

SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA USAWA WA KIJINSIA NCHINI

Na Jovina Bujulu ,MAELEZO DODOMA
Serikali itaendelea kuchukuwa hatua za utekelezaji katika maeneo ya kijamii ili kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh. Dkt. Pindi Chana hivi karibuni Mjini Dodoma.
Akizataja hatua hizo hizo Dkt. Pindi alisema kuwa serikali imemekuwa ikiwajengea wanawake uwezo wa kisheria ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha na jamii kwa ujumla.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF LEO

March 07, 2014

WANG’AMUZI VIPAJI MABORESHO STARS WAJICHIMBIA LUSHOTO
Wang’amuzi vipaji 28 wanakutana Lushoto mkoani Tanga kwa siku saba katika mpango maalumu wa maboresho ya Taifa Stars ambapo watatoka na orodha ya mwisho ya wachezaji waliopatikana katika mechi za maboresho hayo zilizochezwa nchi nzima.

Katika kikao hicho, wang’amuzi hao watapitia majina ya wachezaji walioteuliwa ikiwemo kuwaangalia tena kwenye video kwa vile mechi zote zilirekodiwa. Wachezaji watakaoteuliwa katika mpango huo baadaye wataingia kambini mkoani Mbeya.

Wang’amuzi vipaji ambao wanaoondoka Machi 9 mwaka huu kwenda Lushoto ni Abdul Mingange, Boniface Pawasa, Charles Mkwassa, Dan Korosso, Dk. Mshindo Msolla, Edward Hiza, Elly Mzozo, Hafidh Badru, Hamimu Mawazo, John Simkoko, Jonas Tiboroha, Juma Mgunda na Juma Mwambusi.

Kanali mstaafu Idd Kipingu, Kenny Mwaisabula, Madaraka Bendera, Madaraka Selemani, Mbarouk Nyenga, Mohamed Ally, Mussa Kissoky, Nicholas Mihayo, Peter Mhina, Salum Mayanga, Salvatory Edward, Sebastian Nkoma, Sekilojo Chambua, Selemani Jabir na Shabani Ramadhan.

MAFUNZO YA GRASS ROOT KWA WANAFUNZI WA SHULE MSINGI WILAYA YA TANGA LEO

March 07, 2014
Mkufunzi mwalimu Raymound Gweba kutoka shirikisho la soka nchini TFF akisisitiza kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi wilayani Tanga walishiriki kwenye mafunzo ya grass root yaliyofanyika kwenye shule ya msingi Masiwani jijini Tanga jana,



Mkufunzi mwalimu Raymound Gweba kutoka shirikisho la soka nchini TFF akisisitiza kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi wilayani Tanga walishiriki kwenye mafunzo ya grass root yaliyofanyika kwenye shule ya msingi Masiwani jijini Tanga jana,