Mama Samia Suluhu Asimikwa Umalkia Wilayani Maswa, Wamwita ngole
Mgombea mwenza wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia)
akisimikwa kuwa Malkia wa Wasukuma Wilaya ya Maswa na akinamama wa
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT) alipowasili Jimbo la
Maswa Mashariki kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni kunadi ilani ya
Chama Cha Mapinduzi kwa wanaMaswa.
………………………………………………………………………………….
Na Thehabari.com
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan leo amepewa
heshima ya kusimikwa kuwa malkia wa Wasukuma Wilaya ya Maswa na kupewa
jina jipya la Ng’walu Majura.
Mama Samia Suluhu amepewa heshima
hiyo leo na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT)
alipowasili Jimbo la Maswa Magharibi kufanya mkutano wa hadhara wa
kampeni kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanaMaswa.
Mama Suluhu ambaye amepewa jina
jipya la heshima hiyo la Ng’walu Majura alivishwa mavazi maalum ya
kimila ya heshima ‘Ngole’ yaani malkia na kukabidhiwa mkuki maalum, ungo
na usinge pamoja na kupewa zawadi anuai za vyakula vya kimila kwa
kabila la Wasukuma eneo hilo.
Wakimpa heshima hiyo akinamama wa
UWT walisema Mama Samia Suluhu amepewa heshima hiyo kwa kuwa ni mwanamke
aliyekuja kuibua mambo mazuri kwa ushindi wa CCM na Tanzania kwa
wanawake. Akinamama hao waliahidi kumuunga mkono ili kuhakikisha
anashinda na kuwatoa kimasomaso Wanawakea wa Tanzania.
Kwa upande wake Mama Samia Suluhu
amewashukuru akinamama hao kwa heshima na zawadi mbalimbali walizompa na
kuwaahidi kupigania maslahi yao zaidi endapo chama chake kitafanikiwa
kuunda Serikali katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015.
Alisema licha ya kupigania maendeleo ya taifa zima yeye kama mwanamama
ana ajenda maalum za kuwapigania akinamama kuanzia huduma za kijamii
hadi uwezeshwaji kwao ili kuleta usawa na maendeleo kwa jamii hiyo.
Alisema amepokea kilio cha maji
Maswa na kwa kuwa wanawake ndio waathirika wakubwa wa ukosefu wa maji
atahakikisha Maji yanapatikana kupitia miradi anuai inayotekelezwa eneo
hilo na kwa kuanzia watachimba visima 10 maeneo mbalimbali ya Maswa ili
kuwapatia maji wakazi wa maeneo hayo.
Mapema majira ya asubuhi Mama
Samia Suluhu alifanya mkutano wa kampeni katika Jimbo la Meatu akiinadi
ilani ya CCM kwa wananchi, ambapo aliwaomba kuichagua CCM kwani imepanga
kufanya mengi kwa wanaMeatu ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya
barabara, ujenzi wa malambo na majosho kwa ajili ya kuhudumia mifugo
yao.
Alisema ili kuondoa migogoro kwa
wafugaji na wakulima safari hii Serikali itakayoundwa na CCM imepanga
kupima ardhi yote ya vijiji na Wilaya na kisha kuainisha mipaka ya
wakulima na wafugaji na kuwamilikisha jamii hizo kumaliza migogoro.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
MAMA SALMA KIKWETE AKIONGEA NA WANACHAMA WA UWT WA MKOA WA MARA.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama
Salma Kikwete akiwapungia mkono viongozi na wanachama wa UWT wa Mkoa wa
Mara wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Musoma Community Centre kwa ajili
ya mkutano wa ndani na wanachama hao-Octoba 3, 2015.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanachama wa Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT) wa Mkoa wa Mara wakati alipokutana nao kwenye
ukumbi wa Musoma Community Centre.
Umati
wa wajumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Mara wakimsikiliza kwa
makini Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati alipokuwa
akiongea nao Mjini Musoma.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
WATANZANIA WAASWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KATIKA SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL ILIYOPO CHALIZE MSOLWA MKOANI PWANI
Wanafunzi
wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakielekea
kupandisha bendera ya Taifa wakati wakisherekea mwaka mmoja wa shule
hiyo iliyopo Chalinze Msolwa mkoani Pwani.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakiwa ndani ya darasa la Komputa
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakijibu maswali ya kuhusiana na komputa katika darasa hilo.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial, Ivonne Mnyitafu akitoa ufafanuzi kwa wazazi pamoja na walimu wa shule hiyo.
Mwalimu
wa Taluma wa Shule ya Sekondari ya Imperial, Peter Mwanda akizungumza
katika siku ya Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo iliyopo
Chalinze Msolwa mkoani Pwani.
Wazazi
wakiwasikiliza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakati wa
kusherekea siku ya Impirial iliyofanyika Shuleni hapo leo.
Wazazi
waliowatembelea wanafunzai wa shule ya Sekondari Imperial wakielekea
katika chumba cha masomo ya Sayansi (Laboratory) wakati waliposherekea
siku ya Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo iliyopo
Chalinze-Msolwa mkoani Pwani.
wanafunzai
wa shule ya Sekondari Imperial wakifanya majaribio ya masomo ya Sayansi
ambayo ni Fizikia pamoja na Kemia katika chumba hicho cha majaribio ya
masomo hayo shuleni hapo leo.
Mkuu
wa Shule na Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup
Mukhopadhyay akitolea ufafanuzi moja ya kifaa kinachotumika kuchuja maji
ambayo yamechanganywa na mchanga mbele ya wazazi na walezi waliofika
shuleni hapo kwaajili ya siku ya Imperial iliyofanyika leo shuleni
hapo.
Mwenyekiti
wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial,Buhela Lunogelo akiwapongeza
kuwapongeza wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kufanya majaribio ya
masomo ya Kemia na Fizikia shuleni hapo leo.Kulia ni Mkuu wa Shule na
Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup Mukhopadhyay.
Baadhi
ya wazazi wakichukua kumbukumbu zao (Taswira mbalimbali) wakati
wanafunzi wa shule hiyo wakifanya majaribio ya masomo ya Fizikia na
Kemia katika chumba hicho katika shule ya Sekondari Imperial leo.
Baadhi
ya wanafunzi shule ya Sekondari Imperial wakifafanua somo la hesabu la
pembe zinazoundwa na pembe tatu mbele ya wageni waalikwa na wazazi au
walezi wao (hawapo pichani) waliohudhulia katika siku ya Imperial
iliyofanyika Chalinze Msolwa mkoani Pwani leo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperial wakifanya mdahalo katika siku Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo.
Mwenyekiti
wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial, Buhela Lunogelo akizungumza na
waandishi wa habari leo katika shule hiyo kuhusiana na maendeleo pamoja
na uzuri wa taaluma inayotolewa katika shule hiyo kuwa ni ya kimataifa,
aidha amewaomba wazazi wenye watoto wanataka kusoma kidato cha kwanza
mpaka cha nne wawapeleke watoto wao katika shule hiyo iliyonzishwa Machi
3 Mwaka huu.
Mwenyekiti
wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial, Buhela Lunogelo akiwapa zawadi
wanafunzi wa shule hiyo leo Chalize Msolwa Mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu
wa Shule na Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup
Mukhopadhyay.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperial wakiwa katika picha ya
pamoja wakiwa na vikombe na vyeti vyao walivyozawadiwa leo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperialwakitoa burudani katika siku ya Imperial iliyofanyika leo mkoani Pwani.
WANANCHI WA KIJIJI CHA KENYAMANYORI WILAYANI TARIME WANASTAHILI PONGEZI.
Kwa
mbali kabisa, Kamera ya Binagi Media Group-BMG ikapata fursa ya kunasa
picha za Shule ya Sekondari Kenyamanyori ambayo ilijengwa kwa nguvu za
Wananchi miaka michache iliyopita na kuanza kupokea wanafunzi mwaka 2013
baada ya kukamilika ambapo wanafunzi waliokuwa kidato cha pili katika
shule zilizokuwa mbali walihamia shuleni hapo na kuendelea na kidato cha
pili huku wengine walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka
huo.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Ni
ukweli usiopingika kuwa uongozi wa kijiji hicho pamoja na wananchi wake
ambao asilimia kubwa ni wakulima, wanastahili pongezi kwani wazo lao la
kujenga shule ya sekondari ni wazo bora na limewasaidia watoto wa
kijiji hicho na wale wanaotoka vijiji jirani kupata elimu karibu zaidi
hivyo ni vyema wakaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wahisani
wengi katika kuhakikisha kwamba wanaiboresha zaidi shule hiyo ili iweze
kuwa mkombozi kwa ajili ya watoto wao kielimu.
Kulia ni jengo la Utawala na Majengo mengine matatu kushoto ni majengo ya maabara tatu za Sayansi
Majengo mawili ya Maabara
Jengo moja la Maabara
Jengo la Utawala
Madarasa
Vyoo
Kuna majengo mawili ya nyumba za waalimu ambayo yamefikia hatua hii na moja limekamilika.
Shamba la Shule
NHC YAZINDUA UUZAJI WA NYUMBA ZA BIASHARA NA MAKAZI ZA MOROCCO SQUARE,WAZIRI KIRUKI AIPONGEZA NHC KWA UFANISI
Na Francis Dande
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela
Kairuki, amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mpango wake wa
kujenga nyumba bora na kuwauzia wananchi kwa ajili ya makazi na biashara.
Waziri Kairuki aliyasema
hayo juzi jijini Dar es Salaam
alipokuwa akizindua mauzo ya nyumba za biashara
na makazi zilizojengwa eneo la Morocco Square, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Aliwapongeza Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu na
wenzake kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa
kiasi kikubwa katika kuleta uhai na
taswira nzuri ya shirika hilo.
Alisema kuwa serikali inatambua kuwa makazi
ni jambo muhimu kwa maendeleo ya
taifa, ndiyo maana imekuwa ikichukua
hatua mbalimbali ili kuwezersha
sekta ya nyumba kuwa endelevu na
yenye tija kwa wananchi na uchumi wa nchi.
Alibainisha kuwa moja ya mambo yaliyofanyika katika kukuza
sekta hii ni kuwa na Sheria ya Mikopo ya
nyumba (The Mortgage Financing (Special Provision Act) ya mwaka
2008, iliyoanzishwa kuweza kuwafanya wadau wa sekta ya nyumba wakiwemo waendelezaji, wanunuzi wa
nyumba na taasisi za fedha kushiriki kikamilifu katika kukukuza sekta
hii muhimu.
Aidha , alisema tangu kuwapo kwa sheria
hiyo, tangu mwaka 2008 kumeshuhudiwa benki 19 kati ya zaidi ya benki 50 zilizopo nchini
zikitoa mikopo ya nyumba kwa Watanzania, 16 kati ya
hizo zikiwa zimesaini makubaliano na
na Shirika la Nyumba la Taifa ili kuweza
kutoa mikopo kwa Watanzania wanao nunua nyumba zinazojengwa na NHC.
Naibu waziri huyo alisema kuwa kutokana na
kuwepo kwa changamoto ya riba kubwa
ya mikopo ya nyumbva inayotozwa na benki mbalimbali ambayo ni kati ya
asilimia 18 na 25, serikali
itaendelea kushirikiana na wadau
mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania ili kuona namna bora ya
kuewezesha benki kupunguza riba katika
mikopo ya nyumba ili Watanzania wengi waweze kukopa na kununua nyumba.
Aliwahimiza Watanzania
kutumia fursa zilizopo za mikopo
ya Benki kununua nyumba zinazojengwa na
NHC, ikiwamo kujitokeza kwa wingi
kununua nyumba hizo za za mradi wa Morocco Square ambao una nyumba za ofisi
hoteli, makzi na maduka makubwa.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki
akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mauzo ya nyumba za biashara na
makazi-Morocco Square uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa
wiki. (Picha na Francis Dande)
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu
Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiwa
na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia
Mchechu.
Wageni waalikwa.
Naibu
Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia
Mchechu.
Burudani ya muziki.
Burudani ikiendelea.
Naibu
Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia
Mchechu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)