RAIS DK. SHEIN AZINDUA BARAZA LA WAWAKILISHI LA 9 LEO ZANZIBAR

RAIS DK. SHEIN AZINDUA BARAZA LA WAWAKILISHI LA 9 LEO ZANZIBAR

April 05, 2016

shei1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid mara alipowasili katika viwanja vya jengo la Baraza hilo Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar leo kuzinduz Baraza la 9, [Picha na Ikulu.]
shei2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya Heshma ya gwaride la kikosi cha FFU wakati wa Uzinduzi wa Baraza la 9 la Baraza la Wawakilishi  liliopo Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.]
shei3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la  kikosi cha FFU akiongozwa na Kamanda wa FFU Mjini Magharibi S.S.P Anani wakati wa Uzinduzi wa Baraza la 9 la Baraza la Wawakilishi  liliopo Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.]
shei4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Baraza la Wawakilishi alipofika kulizindua Baraza la 9  la Baraza la 9 la Wawakilishi Baraza la  liliopo Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar leo(kulia) Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid,[Picha na Ikulu.]
shei5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akiongoza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid (mbele)na Katibu wa Baraza hilo wakati wakiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbeni nje ya Mji wa Zanzibar leo kabla ya kulizindua baraza hilo la 9,[Picha na Ikulu.]
shei6
Wajumbe wa baraza la Wawakilishi wakisimama wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipoingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi liliopo Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar kabla ya kulizindua baraza la 9 leo, [Picha na Ikulu.]
shei7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika uzinduzi wa Baraza la 9  katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa baraza hilo liliopo Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar, [Picha na Ikulu.]
shei8
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwapungia mkono Wajumbe wakati alipotambulishwa leo akiwa ni miongoni wa Viongozi walioalikwa katika hafla ya uzinduzi wa Baraza la 9 la baraza la Wawakilishi liliopo Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar, [Picha na Ikulu.]
shei9
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika uzinduzi wa Baraza la 9  katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa baraza hilo liliopo Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar, [Picha na Ikulu.]

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) LATOA UFAFANUZI KUHUSU MALIPO YA GHARAMA ZA UMEME NCHINI.

April 05, 2016

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Decklan Mhaiki (kulia) akizungumza na waandishi (hawapo pichani) Dar es Salaam kuhusu malipo ya sasa ya gharama za Umeme nchini.Mwengine ni Kaimu Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Wateja,Leila Muhaji.
 Kaimu Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Wateja,Leila Muhaji.akiwakaribisha waandishi kwenye mkutano.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Decklan Mhaiki (katikati) akizungumza.Wengine ni  Kaimu Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Wateja,Leila Muhaji (kushoto) na Katibu wa Mkurugenzi Mtendaji,Pius Gaspar.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Decklan Mhaiki(kushoto) akizungumza na waandishi.Mwengine ni  Katibu wa Mkurugenzi Mtendaji,Pius Gaspar.
  Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kazini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya pamoja na Baraza la Mji Wete atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kuswekwa rumande

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya pamoja na Baraza la Mji Wete atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kuswekwa rumande

April 05, 2016

????????????????????????????????????
Na Masanja Mabula –Pemba  
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya pamoja na Baraza la Mji Wete  , ambaye atashindwa kutekeleza wajibu wake , atatumia nguvu alizonazo  kisheria  kumuweka rumande masaa 24 , kwani atakuwa ni chanzo cha kukosekana mapato ya Serikali .
 
Aliesema kuwa ni wajibu wa kila mfanyabiashara kukata leseni za biashara yake ili aweze kuchangia mapato ya Serikali Kuu ambayo baadaye hurejea kusaidia miradi ya maendeleo ya wananchi .
 
Alisema kuwa mapato ya Serikali hupotea kutokana na watendaji wanaohusika na ukusanyaji wa mapato kushindwa kuwajibika kutokana na suala la rushwa muhali , jambo ambalo alisema  serikali ya Mkoahaitalivumilia.
 
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Wete na Micheweni , watendaji wa Baraza ka Mji wete pamoja na watendaji kutoka Serikali za Wilaya juu ya kuimarisha suala la ukusanyaji wa mapato
 
Aidha aliwataka wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya  na Baraza la Mji Wete kuondoa muhali katika suala la ukusanyaji wa mapato kwa kuhakikisha wafanya biashara wanakata leseni za biashara zao.
 
“Ninao uwezo na nguvu kisheria wa kumweka rumande mtumishi wa Serikali masaa 24 , ambaye atashindwa kutekeleza wajibu wake , mimi sitangoja kutumbuliwa jipu nitaanza   na atakaye onyesha uezembe katika agizo hili ”alieleza.
 
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa mapato ya Serikali hupotea kutokana na watendaji wanaohusika na ukusanyaji wa mapato kushindwa kuwajibika kutokana na suala la rushwa muhali , jambo ambalo amesema  haitalivumilia .
 
Pia aliwataka kutumia lugha nzuri kwa wateja wao kwa kuwaelimisha , na wakiendelea kukaidi wawafiishe ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kwa hatua zaidi .
 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Micheweni  Abeid Juma Ali amewasisitiza watendaji wa Halmashauri na baraza la Mji kufuata sheria na miongozo wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi zao
 Alisema kwamba iwapo sheria zitatumika ipasavyo kila mfanyabiashara atakata leseni yake bila ya usumbufu na kuwasisitiza kuwachukulia hatua wanaoendesha biashara bila ya kuwa na leseni .
 
“Sheria zipo lakini hazitumiki , zitumieni kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara abakuwa na leseni na ambaye anakiuka mchukulieni  hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani ”alifahamisha .
 
Akichangia katika Mkutano huo , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Wete Mmanga Juma Ali alisema ili kuzipatiwa ufumbuzi changamoto zinazowakabili wanahitaji kupatiwa askari watakaoongozana nao kupita madukani na kudai leseni .
 
Alisema kuwa kipindi cha vuguvugu la kisiasa , mapato ya Halmashauri yamepungua kutokana na wafanyabiashara wengi kuendesha biashara bila ya kukata leseni .

WAZIRI PROF. MBARAWA AKAGUA DARAJA LA RUSUMO NA VITUO VYA PAMOJA VYA FORODHA KABLA YA UFUNGUZI

April 05, 2016

Muonekano wa barabara ya Nyakahura-Rusumo inayounganisha Tanzania na Rwanda kupitia Daraja la Rusumo wilayani Ngara.
Mtaalam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wa pili kulia akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia), alipotembelea ofisi hizo katika Kituo cha pamoja cha forodha (One Stop Border Post) upande wa Tanzania kilichopo Rusumo wilayani Ngara, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa ufafanuzi kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (mwenye kofia) wakati akikagua maandalizi ya ufunguzi wa Daraja la Rusumo na Vituo vya pamoja vya forodha (One Stop Border Post) wilayani Ngara.
Muonekano wa Daraja la Rusumo linalounganisha Tanzania na Rwanda, kushoto ni daraja la zamani lenye rangi ya njano na kulia ni daraja jipya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale wakati akikagua Daraja la Rusumo wilayani Ngara.
Meneja wa Kituo cha pamoja cha forodha(One Stop Border Post), katika mpaka wa Tanzania na Rwanda upande wa Rwanda Bw. Moses Kalisa akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa na ujumbe wake walipotembelea kituo hicho.

RAIS WA RT,ANTHONY MTAKA AULA SHIRIKISHO LA RIADHA LA DUNIA (IAAF)

April 05, 2016
Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) Lord Sebastian Coe (kushoto) akipeana mkono na Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKISHO la mchezo wa Riadha Duniani (IAAF) limemteua Rais wa Shirikisho la Riadha nchini (RT) Anthony Mtaka kuwa miongoni mwa wajumbe wanaounda kundi la ushauri wa mikakati ya mawasiliano la shirikisho hilo.


Rais wa IAAAF ,Lord Sebastian Coe alitangaza uteuzi huo hivi karibuni ambapo wajumbe wengine ni Abrahamson Alan wa Marekani, Rodan Joe Junior ,Sierra  Calixto  ,,Karamarinov  Dobromir  kutoka  Bulgaria na Rochdi Souad  wa Ufaransa.


Akizungumza kuhusu uteuzi huo Mtaka ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Simiyu alisema amepokea uteuzi huo kwa furaha kutokana na kuwa ni nafasi ya juu katika sekta maarufu ya michezo katika ngazi ya kimataifa.


“Nimefurahishwa na uteuzi huu hasa ukizingatia nimeteuliwa nikiwa rais wa shirikisho la riadha mwenye umri mdogo kuliko wote kwa sasa takuwa na fursa ya kujifunza mambo mengi mazuri.”alisema Mtaka.


Alisema uteuzi huo ni faida kubwa kwa maendeleo ya michezo katika taifa letu, hasa kipindi hiki ambapo serikali ya awamu ya tano inapoandaa mkakati wa kuiweka sekta ya michezo kuwa sehemu kubwa ya ajira.


Mtaka alisema Tanzania itapata nafasi pana zaidi ya kuwakilishwa katika mikutano mikubwa ya mchezo wa riadha duniani (Decision Making) eneo ambalo linatoa fursa kubwa kwa maandalizi ya mashindano makubwa yajayo baada ya mashindano ya Olyimpiki yatakayofanyika katika jiji la Rio de Jeneiro mwaka huu.


“Taifa litarajie uwakilishi wenye tija, sababu mimi nimeteuliwa kati ya wajumbe nane  ambao kila mmoja wao anawakilisha eneo kubwa, hivyo kama nimepewa dhamana ya kuiwakilisha bara zima la Africa, kwa vyovyote nitaweka maslahi ya nchi yangu mbele bila kuathiri utendaji wa jukumu nililopewa.”alisema Mtaka.


“ Uteuzi wangu ni sifa kwa taifa zima, sifa ambayo itafufua mtazamo mwema ulioonyeshwa na wanariadha wakongwe walioiletea taifa sifa kama Filbert Bayi, Suleiman Nyambui, Gidamis Shahanga, Juma Ikangaa bila kumsahau Mzee John Stephen Akhwari aliyeshiriki Mexico City Games 1968.”aliongeza Mtaka.


Aidha Mtaka alisema uteuzi huo umeongeza hamasa ya kuwekeza maradufu katika kambi ya timu ya taifa ya riadha iliyopo katika hosteli ya Chuo cha misitu cha FITI kilichopo West Kilimanjaro wilayani Siha na Arusha.

Tigo yawapa wateja wake ofa zaidi kwenye WhatsApp ya bure

April 05, 2016


Mkuu wa  Kitengo Kitengo cha Vifaa vya Intaneti wa Tigo David Zakaria akiongea na  waandishi wa habari  (Hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es salaam., kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha (Picha na Maktaba)


  • Wateja watafurahia ofa hizo wakinunua kifurushi cha shilling 1,000


Dar es Salaam, Aprili 5, 2016 -Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa maisha ya kidijitali imeboresha ofa yake ya WhatsApp ya bure  kwa kutangaza  kuwanufaisha zaidi wateja wake  pindi wanaponunua kifurushi cha kila siku cha extreme kwa shilingi 1,000.
Faida ya nyongeza  inajumuisha muda wa maongezi wa dakika 50, sms bila kikomo, Mb 8 zitakazotumika ndani ya saa 24 pamoja na kutumia WhatsApp bure. Tigo ilianza kuwapa wateja huduma ya WhatsApp bila malipo kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu kila wanaponunua vifurushi vya wiki au mwezi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari  Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Intaneti wa Tigo, David Zacharia,  kuanzia sasa faida za ziada pamoja na WhatsApp ya bure vitatolewa kwa wateja wote pindi wanaponunua  kifurushi cha extreme  cha shilingi 1,000.
“Ofa hii mpya ni kwa wateja walio na simu zenye uwezo wa kutumia huduma ya Intaneti. Hili linaonesha ni jinsi gani tulivyodhamiria kuleta mabadiliko ya kidijitali katika masisha ya wateja wetu na pia tunavyoongoza kwa ubunifu,” alisema Zacharia.
Kwa mujibu wa Zacharia Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10 na Januari mwaka huu ilikuwa ni kampuni ya kwanza nchini kutangaza upatikanaji wa huduma ya WhatsApp bure klwa wateja wake pindi wanaponunua  vifurushi vya wiki au mwezi au kwa kununua kadi mpya ya simu. Mtandao huo wa kijamii unaopatikana kwa watumiaji wa simu za kisasa za smartphone.
WhatsApp ni mtandao dada wa kijamii kwa Facebook  ambao Tigo ilianza kushirikiana nao tangu mwaka 2014 na mwaka 2015  ilizindua Facebook ya kwanza ya kisasa  ikiwa na menyu ya Kiswahili.
WhatsApp ni  huduma maarufu ya simu ya kutuma ujumbe ambayo ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania  na watumiaji zaidi ya bilioni moja duniani. Huduma ya mitandao ya  kijamii inawawezesha wateja  kubadilishana taarifa, ujumbe, video na miito ya simu kwa sauti.

Hata hivyo, ili kuifurahia huduma hiyo  kwa mujibu wa Zakaria wateja wote wa Tigo wanatakiwa  kwa kadi ya simu ya 3G au 4G kwa ajili ya kununua kifurushi cha etreme cha shilingi 1,000 kwa kupitia *148*00#  ambayo itakupatia maelekezo Tigo-Tigo ExtremeDaily=1000Ths=50min+UNLIMITED SMS+FREE WHATSAPP.

photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"

PRINCE ABUU LEVY AACHIA ALBAMU YAKE IITWAYO "NAKUABUDU".

April 05, 2016
Prince Abuu Levy ni Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, mwenye karama kubwa ya uimbaji hususani uimbaji wa kusifu na kuabudu. Kupitia karama hiyo, anao ujumbe murua kwa ajili yako mwana Mungu kupitia wimbo uliobeba jina la albamu yake uitwao NAKUABUDU.

Ameiambiwa Binagi Blog kwamba "Dvd za Albamu yangu iitwayo Nakuabudu zinapatikana kwa shilingi 5,000 kote nchini ambapo albamu yangu ina nyimbo tano na inasambazwa na Pal Music Service ambao wanapatikana kwa mawasiliano ya simu 0754 742 181 au Email palmusicservice@gmail.com". 
Pakua HAPA Wimbo Uliobeba Albamu au Bonyeza Play Hapa Chini Kusikiliza.
                                                                      Na George Binagi-GB Pazzo

Mambo 9 muhimu ya kufahamu kuhusu Ukatili kwa watoto

April 05, 2016
Afisa wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Asha Sarota akiwasilisha mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.



Mtangazaji Dominic Maro kutoka Redio Huruma akichangia mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.



 Mtangazaji Said Fakhi kutoka Redio Saut ya Quran akichangia mada  katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.

Kutoka kushoto ni Emmanuel Buttorn, Rose Minja (Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto) na Christopher Mushi wote kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.
  .


   Mratibu wa kipindi cha Walinde watoto Neema Kimaro   na Kimela Billa mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto wakizungumza na waandishi wa habari.katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.

 Tabu Salum kutoka redio ya Sauti ya Quran akichangia mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.

 Waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto wakijadiliana mara baada ya mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.






Mambo 9 muhimu ya kufahamu kuhusu Ukatili kwa watoto

Tatizo la Ukatili dhidi ya watoto, linaongezeka siku hadi siku, na kuleta athari mbalimbali za kimwili, kiakili, (kisaikologia) na kiafya kwa watoto. Watoto wanaumizwa, kubakwa, kunajisiwa, kutelekezwa, kusafirishwa kibiashara na kufanyishwa kazi za hatari zinazoathiri afya zao. Matendo haya ya kikatili hayakubaliki kabisa. 

Yafuatayo ni mambo 9 muhimu ya kufahamu kuhusu ukatili kwa watoto:

1.    Aina za ukatili 
Ukatili dhidi ya watoto upo wa aina nyingi. Ukatili wa Kijinsia, ni vitendo au maneno yanayoweza kusababisha madhara kwa mtu au kundi la watu kutokana na maumbile yao. (Mf: kuguswa bila ridhaa, jaribio la kubaka/kubaka, kulazimisha kufanya ngono n.k). Ukatili wa Kimwili ni kama kupigwa, kusukumwa, au kutishiwa kuuwawa kwa silaha. (Mf: kuonyeshwa kwamba hutakiwi, vipigo vya mara kwa mara) na Ukatili wa Kiakili/Kisaikolojia, kutelekezwa, kubaguliwa, kutishwa. (Mf: kuitwa majina mabaya, kunyimwa huduma za msingi, kufanyishwa kazi ngumu n.k)
2.    Wahusika wa Ukatili dhidi ya watoto 
Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto Tanzania ulifanyika mwaka 2009 na uliongozwa na Kikosi Kazi kinachojumuisha Sekta mbalimbali za Serikali, Asasi za Kiraia na Wadau wa Maendeleo. Katika utafiti huo ilionekana kuwa ndugu  wa karibu kama mjomba, baba, walezi na walimu ndio wanaosababisha ukatili dhidi ya watoto.  Kwa kuona hivyo, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wakaona umuhimu wa kuanzisha mpango wa kuelimisha jamii kuzuia ukatili dhidi ya watoto. 
3.    Nini kifanyike kupunguza ukatili kwa watoto
Wananchi wote kwa ujumla wana jukumu la kuhakikisha kwamba wanawalinda watoto. Wazazi / walezi wanapaswa kujua watoto wao walipo na wanachokifanya kila wakati na kuhakikisha usalama wa mahali watoto wanapopenda kutembea mara kwa mara. Watoto wapewe moyo kuripoti vitendo mbalimbali vya ukatili. 
4.    Umuhimu wa kituo cha huduma ya simu kwa mtoto - namba 116
Kituo cha huduma ya simu kwa mtoto ni muhimu katika mifumo ya ulinzi wa mtoto nchini. Ni sehemu pekee ambayo mtoto au Mzazi/Mlezi anaweza kupiga simu na kutoa taarifa za ukatili kwa siri na kupata huduma ya ushauri nasaha na rufaa kwa msaada zaidi kwa mujibu wa tatizo lolote linalohusu ukatili dhidi ya watoto. PIGA SIMU BURE kwenda namba 116 kutoa taarifa za ukatili dhidi ya watoto. 
5.    Uchumi na Familia
Familia zikiwa na hali ngumu ya kiuchumi husababisha ugomvi kati ya wanafamilia na hii huweza kupelekea kutelekezwa kwa watoto au kuwatenga watoto na familia, jambo ambalo litaongeza hatari ya ukatili na unyanyasaji wa watoto. Vilevile ugumu wa maisha ni kisababishi cha watoto wanaofanya kazi katika umri mdogo, kuchuuza /kufanya biashara ya watoto, mimba zisizotarajiwa na ndoa za utotoni. Hivyo basi ni muhimu wazazi/walezi kujishughulisha na kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa wanachama wa vikundi  ili waweze kuzalisha mapato ya kusaidia mahitaji ya familia.

6.    Madhara ya adhabu kwa watoto

Kuna madhara mengi sana ambayo yanaweza kuwapata watoto kutokana na kupewa adhabu mbalimbali. Adhabu huleta hasira na chuki ambayo haisaidii kuleta mabadiliko ya tabia. Kadri adhabu inapokuwa kali zaidi ndivyo inavyopelekea mtoto kuwa na matatizo ya kutojithamini, kuwa mhalifu, kupata magonjwa ya akili na kuwa na tabia ya ukatili. Adhabu mara nyingi haitoi mchango chanya kwa maendeleo ya mtoto
7.    Ishara ambazo huonyeshwa na watoto waliofanyiwa ukatili
Ni muhimu kwa wazazi/ walezi kutambua ishara mbalimbali zinazoonyeshwa na mtoto aliyefanyiwa ukatili. Ishara hizo ni kama vile mtoto kutojiamini hata kama anafanya kitu sahihi anakua na hofu kwa sababu tu anahisi anaweza kupigwa. Mtoto kukataa kwenda sehemu ambazo amezoea mf. shule, ukifuatilia kwa ukaribu utakuta kuna mtu anamfanyia ukatili huko au njiani.

8.    Wasikilize kwa makini
Ni muhimu kujijengea mazingira ya kumsikiliza mtoto kwa makini. Unapofanya hivyo ni muhimu ajue kuwa unamsikiliza, aidha kwa kutumia ishara bila maneno; kama vile kuashiria kwa kichwa. Mtazame mara kwa mara kwa mtazamo wa kirafiki.  Unaweza pia kurudia aliyokwambia kwa maneno mengine.

9.    Umuhimu wa vyombo vya habari kupambana na ukatili

Kwa mujibu wa mwongozo wa vyombo vya habari wa kuandika habari za watoto uliochapishwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), “Watoto wanahitaji uangalizi maalum wa kuwajali na kuwalinda. Wakati wa kuandika habari za watoto, vyombo vya habari vinapaswa kujenga taswira sahihi kwa watoto ili kuwaepusha katika hatari ya kuadhibiwa au kunyanyapaliwa. Watoto ni binadamu wanaohitaji kutambuliwa, kupewa hadhi, utu, heshima na zaidi ya yote kulindwa. Kutokana na ukweli huo, uelewa, umakini na weledi wa uandishi wa habari zinazowahusu wao kwa kuzingatia hali yao na mahitaji yao ni muhimu. Kimsingi vyombo vya habari vinatakiwa kuboresha uandikaji wa habari za watoto na wakati huo huo kulinda usalama wao kimwili na kihisia/jaziba. “

Mambo haya yameibuka katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro.

Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuriwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.

Redio hizo ni pamoja na Kitulo FM, Radio Maria, Radio Faraja, Boma Hai Radio, Uplands FM, Radio Sauti ya Quran, Kwizera FM na Country FM.

Nyingine ni Bomba FM, Zenji FM, ZBC, Radio Huruma, Ice FM, Radio Jamii Kilosa, TBC Taifa, Dodoma FM, Fadeco Radio, Radio Victoria na Best FM.

Waandishi wa habari wametakiwa kushirikiana na serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa haki za watoto zinatekelezwa hapa nchini.

Ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kuwa anawalinda watoto na kuwasadia kukua na kufikia ndoto zao katika jamii.


fastjet yasitisha safari Kilimanjaro-Nairobi

April 05, 2016




Dar es Salaam, Aprili 4, 2016 -Fastjet Tanzania imesitisha safari zake kati ya Kilimanjaro na Nairobi.

Fastjet ilikuwa  ikifanya safari kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwenda Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi mara mbili kwa wiki siku za Ijumaa na Jumapaili.
Kusitishwa kwa safari kwenye njia hiyo kunatokana na kuwepo mahitaji haba ya abiria kwenye masoko yote mawili ya Kilimanjaro na Nairobi hali iliyosababisha kutokuwa na manufaa kibiashara.
Shirika hilo limeeleza kuwa  lengo lake ni kuhakikisha linarudisha safari hizo kati ya Kilimanjaro- Nairobi pindi tu na wakati ambapo wateja wataihitaji.


Safari za fastjet  kutoka Dar es salaam na Kilimanjaro kwenda Nairobi zilianza Januari 11, 2016.
 Mahitaji ya abiria  kwa safari hizo  ambazo kwa kiwango kikubwa ni za kibiashara kati ya majiji  ya Dar es Salaam na Nairobi  ambayo kwa pamoja  yana idadi ya watu ambao ni zaidi ya milioni nane  yamekuwa makubwa na kuifanya fastjet hivi karibuni kuongeza safari zake  kwenye njia  hiyo  ili kukidhi mahitaji makubwa ya abiria.


Fastjet  kwa hivi sasa inafanya safari mbili za kwenda na kurudi kati ya miji hiyo  kila siku ndani ya wiki  na hivyo kufanya  jumla ya safari zake kwa wiki kati ya Uwanja wa Kimataifa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta  kuwa ni 28.
 Mtiririko mpya wa safari unawapatia wateja huduma sahihi mapema nyakati za asubuhi na  jioni  na matokeo ya ratiba hiyo  ni kuwepo kwa takribani  viti 19,000 kila mwezi kwenye safari hizo kati ya majiji hayo mawili na hali kadhalika kuwapatia wateja  mbadala sahihi wa kusafiri kwa nauli wanayoimudu.

 Nauli za fastjet kimsingi ni za chini ikilinganishwa na tozo za mashirika mengine ambayo kwa sasa yanafanya safari zake kati ya Kenya na Tanzania.
Nauli  kutoka Tanzania kwenda Kenya  zinaanzia shilingi 176,000 kwa safari moja, bila kodi ambayo ni shilingi 107,800 kwa kuondokea Tanzania  na dola 40 kwa kuondokea Kenya, na hivyo fastjet kuwashauri abiria kukata tiketi zao mapema kabla ya siku ya kuanza safari ili kutumia fursa hiyo ili kufaidi na nauli ya chini.

 Nauli kutoka Kenya zinaanzia dola za Marekani 120 kwa safari moja zikijumuishwa kodi za serikali ambayo ni dola 40 kwa kuondokea Kenya.
Matokeo ya safari hizi kati ya Nairobi na Dar es Salaam yamekuwa ni makubwa kutokana na ukweli unaojidhihirisha kwamba nauli kwenye mashirika shindani yanayofanya safari kati ya nchi hizi mbili zimeshuka kwa kiwango cha asilimia 40 tangu fastjet ianzishe safari zake.

Fastjet inasisitiza kwamba  kupunguza mtiririko wa safari kwenye njia kati ya Nairobi na Kilimanjaro kunafungua fursa  ya kuongeza uwezo zaidi kwa njia zilizopo kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na hali kadhalika kuwepo uwezekano wa kufungua njia nyingine mpya siku za karibuni. 

Mwisho

photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKI
Taasisi ya Graca Machel yazindua mradi wa kuwasaida watoto walio nje ya shule

Taasisi ya Graca Machel yazindua mradi wa kuwasaida watoto walio nje ya shule

April 05, 2016

DSC_0296
Na Rabi Hume, Modewjiblog, Mara
Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto, Taasisi ya Graca Machel kwa kushirikiana na serikali imefanya uzinduzi wa mradi ulio na malengo ya kuwarudisha shule watoto 20,000 waishio mkoa wa Mara ambao hawakupata nafasi ya kuwa shuleni.
Akizungumzia mradi huo, Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel alisema taasisi yake imeanzisha mradi huo kwa kutambua kuwa kuna idadi kubwa ya watoto walio nje ya shule kwa sababu mbalimbali hivyo kupitia mradi huo ni matarajio yao kuona watoto wakirudi shule ili kupata elimu ambayo itawasaidia kwa maisha yao ya baadae.
Aliongeza kuwa anatambua kazi aliyoifanya Mwalimu Nyerere kwa kuacha msingi bora wa elimu kwa watu wa aina zote na kuwataka wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha wanafanikisha mradi kwa kuweka usawa baina ya watoto wa kike na watoto wa kiume ili wote wapate nafasi ya kurudi shule.
“Watoto wanatakiwa wawepo shuleni na wapate elimu bora bila kufanya upendeleo kwa watoto wa kike na watoto wa kiume ili wamalize pamoja elimu ya shule ya msingi na kuendelea na masomo wote wafikie malengo yao,
“Tunataka watoto wasio chini ya 20,000 warudi shule natambua Mwalimu (Nyerere) aliweka msingi bora wa elimu na ni haki ya watoto wote kupata elimu,” alisema Bi. Machel.
DSC_0188
Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel akizungumza jambo kuhusu mradi huo. (Picha zote na Rabi Hume wa Modewjiblog )
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo aliishukuru Taasisi ya Graca Machel kwa kupeleka mradi huo mkoa wa Mara na kuahidi kuwa atakuwa kiongozi kufanikisha mradi huo ambao utafanyika kwa kipindi cha miaka miwili.
Pia alitumia fursa hiyo kutoa maagizo kwa watumishi walio chini yake kufanya kazi kwa juhudi katika maeneo yao pindi wanapohitajika kusaidia ili kufanikisha mradi huo ambao una malengo ya kuwasaidia watoto wa mkoa wa Mara kurudi shuleni.
“Nina shukuru sana kwa kuletewa mradi huu na Taasisi ya Graca Machel na nitashiriki kwa asilimia 100 kufanikisha mradi, na nitoe rai kwa watumishi wenzangu kuwa wafanye kazi kwa bidii kuanzia sasa tufanikishe mradi kama umevyopangwa,” alisema Mulongo.
DSC_0208
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo akimshukuru mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel kwa kupeleka mradi huo mkoani kwake.
Aidha pamoja na kuzinduliwa kwa mradi huo, pia kunataraji kufanyika utafiti kutazama ni changamoto gani ambazo zilikuwa zinasababisha watoto wa mkoa huo kuwa nje ya shule, utafiti ambao utafanywa na Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF).
Akizungumzia utafiti huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema wanataraji kuanza kufanya utafiti kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itafanyika mwezi huu Aprili na awamu ya pili itafanyika mwezi Julai.
DSC_0114
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida akizungumzia utafiti unatarajiwa kufanywa na ESRF kuhusu changamoto ambazo zilikuwa zinasababisha watoto wa mkoa wa Mara kuwa nje ya shule wakati wa uzinduzi wa mradi ulio na malengo ya kuwarudisha shuleni watoto 20,000.
“Utafiti huu ambao unamalengo ya kufanikisha watoto 20,000 wa mkoa wa Mara kurudi shuleni utafanyika kwa awamu mbili, unaanza Aprili kwa maeneo ya Musoma, Bunda, Rorya, Butiama na Wilaya ya Tarime,
“Awamu ya pili itafanyika kuanzia mwezi Julai kwa eneo la Manispaa ya Musoma, Bunda Mjini, Tarime Mjini, Serengeti na Magumu,” alisema Dkt. Kida.
DSC_0290
Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel akiweka saini ya kuashiria kufanyika kwa mradi huo.
DSC_0296
Watiliaji saini ya makubaliano ya mradi huo wakiwa katika picha ya pamoja.
DSC_0397
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo.
DSC_0385
Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
DSC_0378
Baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa mradi huo, Wa kwanza Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida, Mwanzilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel, Askofu Michael Msongazira wa Kanisa la Roman, Musoma na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa ESRF, Prof. Fortunata Makene.