NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

January 05, 2018

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mbarali wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua shughuli za maendeleo, Jana Januari 4, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe Reuben Mfune mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Jana Januari 4, 2018. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbarali mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Jana Januari 4, 2018. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mbarali wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua shughuli za maendeleo, Jana Januari 4, 2018

Na Mathias Canal, Mbeya

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa amemuagiza Mrajis Mkuu wa Maendeleo ya Ushirika nchini kuanza uchunguzi mara moja kwenye SACCOS ya Wakulima wa mpunga Madibila iliyoko Wilayani Mbarali, Mkoani Mbeya ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Watendaji waliohusika na upotevu wa fedha pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

Mhe Mwanjelwa alitoa agizo hilo Jana Disemba 4, 2018 wakati akipokea taarifa ya kilimo ya Wilaya ya Mbarali akiwa katika ziara yake ya kikazi Wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe Reuben Mfune alimueleza Mhe Mwanjelwa kuwa katika SACCOS ya Madibila kumekuwa na hasara kubwa kutokana na matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika.

Hivyo alimuomba Naibu Waziri kuwachukulia hatua za kinidhamu haraka viongozi wote waliosababisha hasara kwenye vyama hivyo vya ushirika baada ya uchunguzi kufanyika katika kipindi cha siku 14.

Aliongeza kuwa taarifa ya ukaguzi iliwasilishwa kwa Mrajis wa vyama vya ushirika kwa barua Kumb Na. MDC/C.20/10/89 tarehe 23/01/2017 lakini mpaka sasa hazijachukuliwa hatua zozote za kinidhamu jambo ambalo linafifihisha shughuli za wananchi kujipatia maendeleo endelevu.

Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa ametoa wiki mbili (siku 14) kwa Mrajis kufika katika SACCOS hiyo ya Madibira na kutoa majibu haraka ya matokeo ya uchunguzi huo katika kipindi tajwa.

Mhe Mwanjelwa alisema kuwa sekta ya ushirika ni moja kati ya sekta muhimu katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, Vikundi, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla katika kukuza pato la mwananchi na kupunguza umasikini hivyo ni lazima kuwa na majibu ya haraka pindi kunapobainika uhujumu wa vyama hivyo.

Alisema kuwa Viongozi wa Wilaya zote nchini wana jukumu muhimu la kuhamasisha na kuhiza wanachama kuongeza thamani ya mitaji yao ili kuviwezesha vyama kukuza mitaji ya ndani badala ya kuwa tegemezi kwenye Taasisi zingine za kifedha.

Aidha, Kuendelea kutoa elimu juu ya mfumo wa stakabadhi ya Mazao ghalani ili mkulima apate bei stahiki ya Mazao yake.

TIGO YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA TUMIA TIGO PESA NA USHINDE

January 05, 2018
Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tigo, Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde. Amezingirwa na baadhi ya washindi 153 wa promosheni hiyo waliojinyakulia vitita vya shilingi milioni 15, TZS milioni 10, TZS milioni 5, TZS milioni moja na TZS 500,000 kila mmoja.




Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (kushoto) pamoja na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Hussein Sayed (katikati) wakikabidhi mfano wa hundi ya TZS 5 milioni kwa Mariam Maligisa, mkulima kutoka Nagangu mkoani Lindi, aliyekuwa moja wa washindi katika promosheni ya 'Tumia Tigo  Pesa na Ushinde'. Jumla ya washindi 153 kutoka maeneo mbali mbali nchini walijinyakulia zawadi za TZS 500,000 hadi TZS 15 milioni katika promosheni hiyo. 


Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (kushoto) pamoja na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Hussein Sayed (katikati) wakikabidhi mfano wa hundi ya TZS 10 milioni kwa Kulthum Salim , mkulima kutoka Tunduru mkoani Ruvuma, aliyekuwa moja wa washindi katika promosheni ya 'Tumia Tigo  Pesa na Ushinde'. Jumla ya washindi 153 kutoka maeneo mbali mbali nchini walijinyakulia zawadi za TZS 500,000 hadi TZS 15 milioni katika promosheni hiyo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (kushoto) pamoja na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Hussein Sayed (katikati) wakikabidhi mfano wa hundi ya TZS 15 milioni kwa Lugano Thomas , ambaye ni dereva na mkaazi wa Mbezi Makonde aliyekuwa mshindi katika promosheni ya 'Tumia Tigo  Pesa na Ushinde'. Jumla ya washindi 153 kutoka maeneo mbali mbali nchini walijinyakulia zawadi za TZS 500,000 hadi TZS 15 milioni katika promosheni hiyo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (aliyeketi wa pili kushoto) akiwa pamoja na baadhi washindi wa promosheni ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde' ambapo jumla ya wateja 153 walijishindia zawadi tofauti za  TZS 15 milioni, TZS 10 milioni, TZS tano milioni na zawadi za kila siku za TZS milioni moja na TZS  500,000 kila mmoja.


WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DK. HAMISI KIGWANGALLA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA TFS

January 05, 2018
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pilia kulia) akisalimiana na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya mamlaka hiyo mkoani Morogoro jana.


...................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameugiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kukabidhi eneo la Kilomita za mraba 25,000 kutoka kwenye Hifadhi ya Msitu wa Morogoro unaosimamiwa na wakala huyo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Ametoa agizo hilo jana akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Morogoro ambapo alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mej. Jen. Gaudence Milanzi kuzikutanisha taasisi hizo ndani ya siku saba zijazo ili kukamilisha mchakato wa kumega eneo hilo na kukabidhiwa kwa Mamlaka hiyo ili taratibu za ujenzi ziweze kuanza.

Aidha, ameuagiza uongozi huo wa TFS kuweka vigingi vya mpaka katika eneo la hifadhi hiyo ya msitu ndani ya siku 30 zijazo huku akitoa muda huo huo kwa wananchi wote waliovamia eneo hilo kuondoka mara moja kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Prof. Dos Santos Silayo kukabidhi mbao zaidi ya 400 zilizokamatwa hivi karibuni mkoani Morogoro baada kuvunwa kinyume cha Sheria kwa uongozi wa Mkoa huo ili zisaidie kutengeneza madawati ya shule za msingi.

Pamoja na mbao hizo amemuagiza pia mtendaji huyo kukabidhi kwa uongozi wa mkoa huo magunia 350 ya mkaa yaliyokamatwa katika kituo cha Tazara yakiwa yanasafirishwa kinyume cha Sheria ili yasambazwe kwenye shule za Sekondari mkoani humo.

Dk. Kigwangalla alitoa maagizo hayo jana wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Steven Kebwe, ambapo alimuomba kusimamia zoezi hilo la ugawaji kikamilifu ili walengwa waweze kufikiwa.

Katika ziara hiyo ametembelea pia bonde la Kilombero ambalo ni chanzo kikubwa cha maji yanayotengeneza Stieglers Gorge ambapo Serikali ya awamu ya tano itajenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa megawatts 2100.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pilia kulia) akisalimiana na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya mamlaka hiyo mkoani Morogoro jana.
Dk. Kigwangalla akizungumza na watumishi wa TAWA wakati wa ziara hiyo.

ZIARA YA MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA UBUNGO, JANA

January 05, 2018

 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya UbungoLucas Mgonja akizungumza na viongozi wa Wilaya hiyo katika Mkutano wa ndani uliofanyika jana katika Kata ya Msigani wilayani humo, ikiwa ni sehemmu ya ziara yake ya kuimarisha uhai wa Chama. Kushoto ni Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Salum Kally
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akishauriana jambo na Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Salum Kally wakati wa kikao hicho
 Katibu wa UVCCM Kata ya Msigani Reinhard Chicano akisalimia baada ya kutambulishwa
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Msigani Godlove Mondo akifungua kikao hicho
 Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ubungo Mbarouk Masoud akifanya utambulisho wa viongozi waliofuatana na Mwenyekiti Mgonja kwenye kikao hicho
 Wajumbe kwenye kikao hicho wakishangilia jambo kuliunga mkono.
 Diwani wa CCM Kata ya Manzese Manumbu Magafu akisalimia katika kikao hicho
 Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ubungo Pili Mustafa, akiimba wimbo wa hamasa alipopewa nafasi ya kusalimia
 Wajumbe wakiwa wamesimama kuimba wimbo huo 
 Mbunge wa Mbinga Vijijini ambaye pia ni Mweneyekiti wa Mtaa wa Msingwa Kata ya Msigani Martin Msuha akisalimia
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na kamati ya Siasa mkoa wa Dar es Salaam Issa Mtemvu akisalimia kwenye kikao hicho  katibu wa CCM wilaya ya Ubungo Salum Kally akiimbisha wimbo wa hamasa kwenye kikao hicho
 Viongozi wa meza kuu wakishiriki kuimba wimbo huo wa hamasa. 
 Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo akihutubia kikao hicho kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti Mgonja kuhutubia.Mgonja akihutubia.
 Mgonja akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa Chadema Gatto John, ambaye alitangaza kuhamia CCM wakati wa kikao hicho
 Mgonja akimpa kadi ya CCM
 Gatto akionyesha kadi ya CCM baada ya kukabiodhiwa
 Mgonja akimpokea kadi kutoka kwa aliyekuwa katibu Mwenezi wa Chadema Kata ya msigani Kerned Odera baada ya kutangaza kuhamia CCM wakati wa kikao hicho
Mgonja akimpokea kadi kutoka kwa aliyekuwa katibu Mwekiti wa Chadema Tawi la Msigani Benedict Mumbi baada ya kutangaza kuhamia CCM wakati wa kikao hicho
 Waliokuwa wanachama wa Chadema wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za CCM
 Kinamama wajasiriamali wakishangilia wakati wakipeleka zawadi na kujinadi kwa viongozi wa meza kuu kuhusu shughuli zao 
 Kiongozi wa Kinamama hao akitoa maelezo
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akikabidhiwa zawadi kutoka kwa Kinamama hao wajasiriamali
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akitazama bidhaa za kinamama wajasiriamali waliozkuwa wakionyesha nje ya ukumbi
 Mgonja akinunua bidhaa kwa kinamama hao wajasiriamali
 Mwenyekiti wa CCM Lucas Mgonja akiwa na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mbezi Othman Shaibu baada ya kuwasili katika kata hiyo kuendelea na ziara yake. 
 Wajumbe wakiwa wamesheheni ukumbini kwenye mkutano huo wa Kata ya Mbezi
 Wakiomba dua kabla ya kikao kuanza
 Baadhi ya vijana wa CCM waliofika kwenye kikao hicho Mbezi
 Baadhi ya vijana waliofika kwenye kikao hicho wakiwa nje ya ukumbi kwa kuwa siyo wajumbe.
 Vijana wakipata chakula nje ya ukumbi
 Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo Salum Kally akimkaribisha Mwenyekiti kuzungumza kwenye kikao hicho cha kata ya Mbezi 
 Baadhi ya wajumbe ukumbini 
Mwenyekiyi wa CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akihutubia wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika Kata ya Mbezi Wilayani humo jana.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

“WAZIRI UMMY AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA KLABU YA AFRICAN SPORTS”

January 05, 2018


 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu katikati akimkabidhi vifaa vya michezo ambavyo ni viatu Mwenyekiti wa timu ya African Sports
Awadhi Salehe Pamba ikiwa ni kuipa motisha timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano wanayoshiriki ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kuweza kurejea daraja la kwanza na Ligi kuu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja Hamisi Mkoba
                   WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu   kushoto akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo
    WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu   kushoto akiteta jambo na  Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kushoto ni  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja Hamisi Mkoba
 Halfa ya makabidhiano ikiendelea
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu   kushoto akimkabidhi viatu hivyo Nahodha wa timu ya African Sports Mohamed Kidiwa
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu ametoa vifaa vya michezo kwa timu ya African Sports ya Tanga yenye thamani ya zaidi ya milioni 1.5 ikiwa ni mkakati kabambe wa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki na hatimaye kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati wa ufunguzi wa timu ya wanawake ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya wilaya ya Tanga ambapo alisema vifaa hivyo vitakuwa ni chachu ya timu hiyo kuweza kufikia malengo yao.
Aliyasema hayo mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa timu hiyo katika halfa iliyoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa klabu ya African Sports ambapo alisema dhamira yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inarejea ligi daraja la kwanza na ile ya Coastal Union ihakikisha msimu ujao inarudi Ligi kuu.
“Niseme tu sisi tumejipanga kuhakikisha tunazirejesha timu hizi kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara tukianzia na timu ya Coastal Union lakini ndugu zangu African Sports mhakikishe mnarudi ligi daraja la kqwanza na baadae ligi kuu “Alisema
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo,Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports,Awadhi Salehe Pamba alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia msaada huo ambao utakuwa ni chachu kwao kuweza kufikia malengo yao kutokana na changamoto hiyo kwisha.
Alisema msaada uliotolewa na Waziri utakuwa chachu kubwa kwao kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea ya kuhakikisha wanarudi ligi kuu kwani ndio ndoto yao kubwa ambayo wamekuwa wakiiwaza kila wakati.
“Mh Waziri tukushukuru sana katika hili umetupa nguvu ya kuweza kupambana na tuna kuhaidia kuhakikisha tunairudisha timu Ligi daraja la kwanza na hatimaye ligi kuu.