Salaam. Kocha Mkuu wa Simba, Zdavko Logarusic ‘Loga’ ametimiza
mechi 10 za Ligi Kuu Bara akiwa amekusanya pointi 12 lakini amezidiwa
na Abdalah Kibadeni, ambaye aliinoa na timu hiyo kwenye mzunguko wa
kwanza kwani alikusanya pointi 20 katika idadi hiyo ya mechi.
ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA YAKUMBANA NA CHANGAMOTO ZA BARABARA WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimueleza jambo Mbunge wa jimbo
la Nkasi Kaskazini,Mh.Ali Mohammed Kessy,walipokuwa wakitembea kwa miguu
kufuatia msafara huo kukumbana na changamoto ya barabara mapema jana
jioni katikati ya Msitu wa hifadhi ya wilaya ya Nkasi.Ndugu Kinana na
Msafara wake ulikuwa umetoka kijiji cha Namanyere kuelekea kijiji cha
Mwampemba kusikiliza matatizo ya Wananchi na kukagua miradi mbalimbali
ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya mwaka
2010.
Barabara
hiyo yenye urefu wa kilometa 100,lakini iliwachukua zaidi ya masaa 12
kwenda na kurudi kutokana na ubovu wa barabara.Ndugu Kinana yuko Mkoani
Rukwa,Katavi na Kigoma kwa ziara ya siku 21 ya kuimarisha Chama cha
CCM,kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kiwemo na kuzisikiliza kero
mbalimbali za wananchi
Ndugu
Kinana akishiriki kuweka mawe sehemu korofi,angalau kusaidia Lori hilo
pichani lililolala ndani ya msitu huo kwa siku mbili,wapite nae msafara
wake uweze kuendelea na safari.
Sehemu
korofi ya Barabara ikiwekwa sawa ili lori lipite na kisha msafara nao
uweze kupita,lakini hata hivyo zilitumika juhudi kubwa kuvusha msafara
wa Kinana na hatimae kuendelea na safari ya kuelekea kijiji kingine.
SSRA YATOA TAARIFA KUHUSU UANDIKISHWAJI WANACHAMA KATIKA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI
*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA TANZANIA, JIJINI DAR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyeshwa na Mkutubi wa Jiji, Lusekelo Mwalugelo, Gazeti la Mambo Leo la
Mwaka 1923 ambalo ni moja kati ya magazeti ya zamani, wakati alipokuwa
akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka
50 ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya
Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyeshwa baadhi ya vitabu na Ofisa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mture
Educational Publishers Ltd, Bupe Mwasaga, wakati alipokuwa akitembelea katika
mabanda ya maonyesho kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya
Huduma za Maktaba Tanzania, yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya Maktaba Kuu ya
Taifa jijini Dar es Salaam.
*MKUU WA MKOA WA GEITA AZINDUA MCHAKATO WA UANZISHWAJI WA MFUKO WA AFYA YA JAMII WA TIBA KWA KADI (TIKA)
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Magalula Said Magalula
akifungua mkutano wa wadau mkoani Geita unatakaojadili mchakato wa uanzishaji
wa Mfuko wa Afya ya Jamii ujulikanao kama Tiba kwa Kadi (TIKA).
Katibu Tawala wa Mkoa Severine Kahitwa akieleza umuhimu wa kuwa na
utaratibu wa TIKA ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita.
Kesi dhidi ya Rais Kenyatta yaahirishwa
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imehairisha kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta hadi tarehe saba Oktoba mwaka huu.
Rais Kenyatta anatuhumiwa kwa makosa ya jinai
kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi wa mkwaka 2007 - 2008, madai
ambayo ameyakanusha.
Mahakama kuu ya ICC, kupitia
mwendesha mashitaka Fatou Bensouda, imekuwa ikiitaka serikali ya Kenya
kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuendesha kesi zinazowakabili Rais
Kenyatta na naibu wake bwana Ruto.
RAIS DKT. SHEIN AMKARIBISHA IKULU YA ZANZIBAR WAZIRI CHIKAWE
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
(kulia) akimkaribisha ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar, Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe. Waziri Chikawe alifika
ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais huyo baada ya
kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia
walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa
Tanzania Bara na Visiwani. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,
Pereira Ame Silima. (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi).
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
(kulia) akimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.
Mathias Chikawe (katikati) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa
mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu ya Zanzibar leo. Waziri Chikawe
alifika ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais huyo baada ya
kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia
walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa
Tanzania Bara na Visiwani. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,
Pereira Ame Silima. (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi).
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
(watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (watatu kushoto), Naibu Waziri wa wizara
hiyo, Pereira Ame Silima (wapili kulia), Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (wapili kushoto). Kulia ni Mkurugenzi wa
Vitambulisho vya Taifa, Ofisi ya Zanzibar, Vuai Suleiman. Kushoto ni
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omary Makame. Waziri
Chikawe alifika Ikulu ya Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais
Shein baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi
hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na
usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara
hiyo, Pereira Ame Silima. (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi).
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
SERIKALI ITAHAMISHA NA KUWONDOKA WANANCHI WAISHIO KANDO KANDO YA BONDE LA MTO MKOMAZI-JK
NA OSCAR ASSENGA,KOROGWE
SERIKALI
imesema itahamisha makaburi na itawaondoa wananchi wote wanaoishi kando
kando ya bonde la mto mkomazi kwa kuwalipa fidia za makazi na mimea yao ili kupisha
ujenzi wa bwawa kwa ajili kuinua na kuendeleza kilimo
cha umwagiliaji.
Rai
hiyo ilitolewa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Mrisho
Kikwete wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika viwanja vya mamlaka ya mji wa mombo wakati wa ziara yake ya
kukagua shughuli za maendeleo ya wananchi wilayani korogwe.
BARAZA LA MADIWANI LA MJI KOROGWE LAUPOKEA KWA MIKONO MIWILI MPANGO
Afisa
Utumishi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, ambaye alimwakilisha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna
akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani katika kupitisha sheria ndogo ya
Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini
wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha mwisho kimefanyika Machi 29,
2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni
Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya
Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kulia), Makamu Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa
Francis Komba (kushoto).
Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally
Mwakababu akitoa maelezo machache juu ya TIKA. Pembeni ni Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga,
Mheshimiwa Francis Komba na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe
ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera.
WAZIRI CHIKAWE ATUA ZANZIBAR KUTEMBELEA IKULU, NIDA NA UHAMIAJI LEO
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kushoto) akipokelewa
na Naibu Waziri wa wizara yake, Pereira Ame Silima, wakati alipotua
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo.
Kulia ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omary Makame.
Waziri Chikawe amewasili Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kikazi. (Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kushoto) akimsalimia
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu
wakati alipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani
Karume Zanzibar leo. Waziri Chikawe amewasili Zanzibar kwa ajili ya
ziara ya kikazi. (Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi).
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (wa pili kushoto) akiwa
na NaibuWaziri wa wizara yake, Pereira Ame Silima (kushoto), Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu na Kamishna
wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omary Makame, katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo Waziri Chikawe
amewasili Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kikazi. (Picha zote na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
TUESDAY, APRIL 01, 2014
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.compress@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA UMMA
Uingereza inajivunia kuwa nchi inayoongoza katika uwekezaji nchini Tanzania na itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kiuchumi na kuleta maendeleo .
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amemuambia Rais Kikwete wakati wa mazungumzo yaliyofanyika 10 Downing Street, Leo tarehe 31 March, 14, ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Waziri Mkuu wa Uingereza.
"Tunafurahia sana uhusiano wetu na kujivunia kuwa tunaongoza katika Uwekezaji nchini Tanzania" Bw. Cameron amesema na kumhakikishia Rais Kikwete kuwa Uingereza iko tayari kutoa misaada zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)