RAIS KIKWETE AFUNGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA NSSF MOSHI

February 11, 2015
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Kazi na ajira Mh.Gaudensia Kabaka(watano kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau(wapili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama(wapili kushoto) pamoja na viongozi na wadau wengine wakikata utepe kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la NSSF Kilimanjaro Commercial Complex mjini Moshi,Mkoani Kilimanjaro.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhan Dau pamoja na wadau wengine wakitazama ramani ya jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi Kilimanjaro Commercial Complex wakati wa hafla ya ufunguzi.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua jengo la upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro muda mfupi baada ya kulifungua leo.Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mawenzi mjini Moshi muda mfupi baada ya kufungua jengo la upasuaji na kuweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa wodi ya mama na watoto katika hospitali hiyo leo.(wanne kulia ni Naibu waziri wa Afya Dkt.Steven Kebwe,wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama,Kushoto ni Mbunge wa Vunjo Agustino Lyatonga Mrema,na wapili kushoto ni Mbunge wa Moshi Vijijini Dkt.Cyril Chami.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na chipikizi wa Tanzania Girl Guides wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi leo.Tanzania Girl Guides,UMATI,Tanzania Red Cross ni wadau wa NSSF katika mradi huo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau baada ya hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la kitega uchumi la NSSF mjini Moshi leo.Katikati ni Waziri wa Kazi na Ajira Mh.Gaudensia Kabaka. Picha na Freddy Maro

WAZEE MWANZA WAMUASA MULONGO KUWEKA NGUVU KWENYE ZAO LA ALIZETI

February 11, 2015

Na: Atley Kuni- Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Magesa Mulongo
Wazee katika Mkoa wa Mwanza, wamemshauri Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kuanza kulima zao la alizeti ili kuuwezesha mkoa huo kuinuka kuichumi kutokana na hali mbaya ya mazao kama pamba kupoteza umaarufu kwenye sekta ya uchumi wa mkoa huo.

Wakizungumza katika kikao kilicho wakutanisha wazee hao na mkuu wa mkoa hivi karibuni katika hoteli ya Mwanza, wazee hao walisema kutokana na hali isiyoridhisha kwa zao kama pamba ambalo ndilo lilikuwa zao kuu la uchumi wa mkoa huu kupoteza umaarufu ni vema sasa jamii ikabadilika na kuhamishia nguvu zake kwenye zao la alizeti.


Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake, aliyekuwa Mkuu wa kwanza  wa wilaya ya Ilemela, Jared John Gachocha, alisema, haoni sababu ya mkoa wa Mwanza kushindwa kutilia mkazo zao la alizeti ambalo gharama zake za uzalishaji ni nafuu zaidi ukilinganisha na pamba.” 

Mh. Mkuu wa mkoa mimi nadhani kipindi hiki tushughulike kufa na kupona kwenye alizeti, sioni kwa nini wenzetu wa Singida watupite katika hili, zao la alizeti ni rahisi mno kulilima halina usumbufu halihitaji mbolea nyingi, haliitaji maji mengi na maandalizi yake kwakweli ni rahisi lakini pia faida yake ni kubwa” alisema na kuongeza kuwa “hali hiyo itasaidia mkoa kujitosheleza kwa mafuta lakini pia kuweza kuuza kwa watu wengine.


Mbali ya zao la alizeti wazee hao pia walimuasa mkuu huyo wa mkoa, kuelekeza nguvu zaidi kwenye masuala ya ufugaji, wakisema kuwa tupo nyuma sana katika masuala ya mifugo huku wakitolea mfano nchi ya Kenya kwamba Ng’ombe anauwezo wakutoa maziwa lita hadi 20 tofauti na Tanzania, hali inayo walazimu wazee hao kumuasa mkuu wa mkoa kuwataka wafugaji kuachana na ufugaji wa kizamani na badala yake watafute mitamba itakayoweza kuleta tija kwa wafugaji. “Ni ukweli usiopingika kwamba hapa kwetu kumpata ng’ombe anayeweza kukupatia lita 10 za maziwa ni nadra sana hivyo tuwashawishi wakulima waweze kutafuta mitamba ambayo itakuwa niya kisasa ili waweze kukuza uchumi wao lakini uchumi wa mkoa kwa ujumla.

Awali akizungumza mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kabla yakuanza kupokea maoni ya wazee hao, alisema mkoa wa Mwanza wenye watu Milioni mbili na laki saba na mia saba sabini na mbili mia tano na tisa, huku mkoa ukiwa unachangia Trioni 4.9 katika pato la taifa, Watu wake  milioni moja uchumi wao unategemea zaidi katika Sekta ya Uvuvi, “Wazee wangu nimewaiteni tusaidiane kuongoza mkoa huu, mkoa huu ni mkubwa na changamoto tulizo nazo ni nyingi” alisema Mulongo na kuongeza kuwa, “kati ya watu mil. 2.7, watu Milioni moja wanategemea ziwa kuanzia mvuvi ziwani hadi mparuaji na mchuuzi mdogo mdogo wa mtaani sasa hali ya ziwa letu kwa upande wa uzalishaji sio salama sana, tuna kwendaje lazima tujipange kisawasawa alisema Mulongo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza toka amewasili mkoa wa Mwanza, ameweka utaratibu wakukutana na watu wa makundi mbali mbali mkoani hapa ili kufahamu changamoto ambazo zipo ili waweze kuzitatua kwa kushirikiana kwa pamoja, makundi ambayo tayari yamekutana na mkuu huyo wa mkoa hadi sasa ni pamoja na, Wananchi wa kawaida kwa kuzungumza nao kwenye mikutano ya hadhara na kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi, Wafanya biashara wadogo ambao alifanikisha kufanyika kwa uchaguzi wao, wakuu wa taasisi za umma zilizoko mkoani hapa, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa na asasi zisizo za kiraiya. 

Mkoa wa Mwanza ni mkoa wa pili kwa uchangiaji wa pato la taifa kwa asilimia 9.15%  ukitanguliwa na Mkoa wa Dar Es Salaam, huku wastani wa pato la mwananchi wa kawaida ikiwa ni Tshs. 910,824  kwa mwaka.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI GEORGE SIMBACHAWENE AFUNGUA MKUTANO WA KUJADILI NISHATI ENDELEVU NCHINI KWA WOTE

February 11, 2015
 Waziri wa Nishati na Madini  George Simbachawene akifungua mkutano  kwa ajili ya  kujadili nishati endelevu  nchini kwa wote ( Tanzania Sustainable  Energy for  All)  ulioshirikisha  sekta binfasi,  wataamu  kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na wadau wa nishati nchini.  Mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya   Protea jijini  Dar es Salaam  lengo lake lilikuwa ni kubadilishana uzoefu kwa ajili ya kuboresha  sekta ya umeme  nchini. 
 Meneja   Hifadhi kutoka Shirika la WWF Nchini Dk. Amani Ngusaru  akitoa hotuba ya kumkaribisha  Waziri wa Nishati na Madini George  Simbachawene (hayupo pichani)
Sehemu ya wadau wa mkutano  kwa ajili ya  kujadili nishati endelevu  nchini kwa wote ( Tanzania Sustainable  Energy for  All)  ulioshirikisha  sekta binfasi,  wataamu  kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na wadau wa nishati nchini wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na  Waziri wa Nishati na Madini  George  Simbachawene  ( hayupo pichani)

YONDANI AREJEA YANGA, AANZA MAZOEZI KUWASUBIRI WASWANA

February 11, 2015

Beki wa Yanga, Edward Charles, ametupwa nje  katika kikosi hicho kwa siku kumi, huku mkongwe  Kelvin Yondani akirejea kuivaa BDF XI, siku ya Jumamosi katika raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho.


Charles aliumia katika mchezo wao wa hivi karibuni dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo aliumia kifundo cha mguu, akafungwa bandeji nyepesi.

Yondani yeye aliumia kwenye mchezo kati ya timu yake na Polisi Morogoro, lakini ameshapona na yupo fiti kwa mechi hiyo.

“Wachezaji wanaendelea vizuri kama hivi, Yondani na Dilunga, wameanza mazoezi leo kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi baada ya afya zao kuimarika lakini Edward yeye ataendelea kuwa nje kwa siku kumi mpaka pale afya yake itakapoimarika.

“Upande wa beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’, yeye leo (jana Jumanne), hajafanya mazoezi lakini kesho (leo) ndiyo ataanza rasmi na timu kama kawaida, kwa sababu alipata maumivu kidogo katika mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar na sasa yupo vizuri,” alisema Daktari wa Yanga, Sufiani Juma.
TIPER KUONGEZA UWEZO WA KUHIFADHI MAFUTA KUFIKIA MITA ZA UJAZO 213,000

TIPER KUONGEZA UWEZO WA KUHIFADHI MAFUTA KUFIKIA MITA ZA UJAZO 213,000

February 11, 2015

Mafundi wa kampuni ya kuhifadhi mafuta ya Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER), wakitengeneza paa katika moja ya matanki mapya ya kampuni hiyo, wakati kampuni hiyo ikitarajia kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta maradufu baada ya kukamirika kwa ukarabati wa matanki yake wawili ya mita za ujazo 36,600 kila moja ifikapo machi mwaka huu.
Miongoni mwa matanki ya kampuni ya ya kuhifadhi mafuta ya Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER) yanayofanyiwa marekebisho, wakati kampuni hiyo ikitarajia kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta maradufu baada ya kukamirika kwa ukarabati wa matanki yake wawili ya mita za ujazo 36,600 kila moja ifikapo machi mwaka huu
Zaidi ya watu 200 wahofiwa kufariki kwenye ajali hii ya majini

Zaidi ya watu 200 wahofiwa kufariki kwenye ajali hii ya majini

February 11, 2015
boat 
Hii ni ajali kubwa ya kwanza kutokea kwa mwaka 2015 ikihusisha vyombo vya majini kupata ajali na kuua watu wengi ambapo zaidi ya wahamiaji 200 wamefariki baada boti mbili walizokuwa wakisafiria kuzama katika bahari ya Mediterrania walipokuwa wakijaribu kuzamia kwenda Ulaya.
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema ni watu nane pekee ndio waliweza kuokolewa baada ya kukaa majini kwa siku nne huku wengine 203 kutojulikana waliko.
Msemaji wa UNHCR Italia, Bi. Carlotta Sami aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa boti mbili zilihusika katika ajali hiyo na zilikuwa zikitokea Libya huku kila moja ikiwa na zaidi ya watu 100.
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
Yote yaliyosikika kuhusu hali ya Bobbi Kristina, hii ni taarifa rasmi iliyotolewa na familia yake

Yote yaliyosikika kuhusu hali ya Bobbi Kristina, hii ni taarifa rasmi iliyotolewa na familia yake

February 11, 2015
bobbi-kristina
Bado kuna utata kuhusu kinaachoendelea juu ya afya ya Bobbi Kristina, mtoto wa pekee wa Marehemu Whitney Houston, mengi yanaendelea kuzungumzwa kuhusu hali yake huku wengine wakisema kuwa leo ni siku ambayo familia hiyo imeruhusu madaktari kumtoa mashine ya kupumulia ambayo aliwekewa toka siku ambayo alifikishwa hospitali baada ya kukutwa akiwa ameanguka ndani ya bafu, Georgia Marekani.
Baada ya yote kusikika familia ya Bobbi imeamua kutumia kampuni ya wanasheria wao kutoa maelezo rasmi kuhusu kila ambacho kimesikika juu ya hali ya mtoto huyo, taarifa hiyo imekanusha uvumi wote uliowahi kusikika ikiwemo ishu ya kumtoa mipira ya kupumulia siku ya leo ambapo ni siku ambayo mama yake alifariki.
Katika taarifa hiyo ya Wanasheria wa familia hiyo wamesema wanaangalia namna ya kuwachukulia hatu wote waliotoa taarifa za uongo ikiwemo waliosema walizungumza na wahusika wa familia hiyo kitu ambacho sio kweli.
whitney-bobbi-kristina
Marehemu Whitney Houston akiwa na mtoto wake Bobbi Kristine wakati akiwa mdogo.
TMZ, The National Enquirer, The Atlanta Journal Constitution na the Daily Mail ni sehemu ya vyombo vya habari ambavyo vimelaumiwa kwa kuandika taarifa za uongo.
ap_bobbi_kristina_oprah_jt_120311_wg
Bobbi Kristina akiwa na Oprah Winfrey
Bado hakuna taarifa rasmi ambayo familia hiyo imetoa kuhusu hali ya mtoto huyo, leo inatimia miaka mitatu tangu afariki Whitney Houston ambaye alikutwa pia ameanguka bafuni.
Hautopitwa na story yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza

Kilimanjaro Marathon 2015 kufanyika Machi 1,mjini Moshi

February 11, 2015

Mbio za 13 za Kilimanjaro Marathon ambazo zimepangwa kufanyika Machi 1, 2015 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro zimepata msisimko mpya baada ya wanariadha nyota wa Tanzania kuthibitisha kushiriki.

Mkurugenzi wa Mbio hizo John Bayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliwataja baadhi ya wanariadha nyota kutoka Tanzania kuwa ni Andrew Sambu, Daudi Joseph, Mashaka Masumbuko, watachuana na wanariadha wengine kutoka nchini na kutoka nje ya nchi katika mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa wanaume za kilometa 42.195.

Kwenye upande wa marathon wanawake Fabiolla William, Sarah Maja and Banuelia  Katesigwa ni miongoni mwa nyota wa Tanzania watakaochuana na wenzao kutoka ndani na nje ya nchi katika kuwania tuzo mbalimbali kwenye Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon kwa wanawake za Kilometa 42.195.

Aidha, wanariadha Fabian Fabian Joseph, Alphonce Felix, Dickson Marwa wamethibitisha kushiriki Tigo Kili Half Marathon wanaume wakati Mary Naali, Natalia Elisante, Catherine Lange na Jacqueline Sakilu ni miongoni mwa majina maarufu katika riadha yaliyothibitisha kushiriki kupitia kundi la wanawake litakalochuana katika Mbio za Tigo Kili Half Marathon.

Katika mbio za nusu marathon ambazo Tanzania ina historia ya kufanya vizuri, Fabian Joseph ana rekodi ya ushinda Kilimajaro Marathon mwaka 2010 ambapo alimaliza mbio katika muda wa 1:3;59 na vilevile ana rekodi ya kushinda Edmonton Marathon mwaka 2005 kwa muda wa 1:01:08.

Akiwa ametengeneza rekodi nyingi, Mary Naali ni kati ya wanariadha bora nchini katika mbio za kilomita 21 maarufu kama Half Marathon. Alishinda Vienna Marathon mwaka 2010 ambapo alimaliza katika muda wa 1:12:16 na baada ya hapo akavunja rekodi kwenye mbio za kilomita 25 za Arusha VIP Race mwaka 2011 ambapo alishinda kwa 1 1:20:52 na kuvunja rekodi ya 1:22:18 iliyokuwa imewekwa na Josephine Deemay mwaka 2006. Mei mwaka 2013 pia alishinda mbio ya Bucharest International Marathonihuko Romania akimaliza katika muda wa 1:16:32.

Naali atachuana vikali na Jacqueline Sakilu ambaye ni bingwa mtetezi kutokana na ushindi wake kwenye 2014 Kilimanjaro Marathon ambapo alimaliza mbio akiwa na 1:12:43 ambayo bado ni rekodi yake katika mbio hizo.

Bayo alisema kwamba Sakilu ni kati ya wanariadha ambao wana mvuto sana kutokana na umahiri na kujituma na anaweza kufanya makubwa kwa mara nyingine tena.

 “Tuna furaha kuwa na kikosi madhubuti kwa wanaume na wanawake,” alisema John Bayo ambaye pia ni kocha maarufu wa riadha. “Uwepo wa wanariadha hawa wazoefu naamini utaifanya mbio hii iwe ya kuvutia.”

John Addison, Mkurugenzi mku wa kampuni ya Wild Frontiers, inayoandaa Mbio za Kilimanjaro Marathon alisema kuwa takribani watu zaidi ya 6000 kutoka mataifa 40 ya mabara sita wanatarajia kushiriki katika maadhimisho ya kumi na tatu ya Mbio za Kilimanjaro Marathon.

Addison alisema kwamba mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuwa na vivutio pamoja na motisha mbalimbali kwa washiriki ambapo medali na tisheti zitatolewa kwa washiriki 500 wa kwanza kumaliza mbio za kilomita 42, washiriki 2,200 na washiriki 80 wa mbio za walemavu za GAPCO watapata tisheti na medali.

Mbio hizo zinaratibiwa na Executive Solutions kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Kilimanjaro, Kilimanjaro Marathon Club chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager, Tigo, GAPCO, Simba Cement, na KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar,  CMC Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, Kibo Palace Hotel, UNFPA na Kilimanjaro Water.
WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO YA UJENZI WA WODI YA WATOTO NA WAZAZI.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YATILIANA SAINI MAKUBALIANO YA UJENZI WA WODI YA WATOTO NA WAZAZI.

February 11, 2015

EA1 
Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Mr. Jaap Frederiks akizungumza na baadhi ya watendaji wakuu wa Wizara ya Afya kabla ya utiaji saini makubaliano ya uboreshwaji wa wodi ya wazazi na watoto Unguja na Pemba, hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Saleh M. Jidawi (wa kulia waliokaa) na Meneja wa Kampuni ya Simed International Services ya Uholanzi Nd. Michor Pleijzer wakitia saini mkataba wa uboreshwaji wa wodi ya wazazi na watoto Unguja na Pemba huku wakishuhudiwa na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Mr. Jaap Frederiks katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar). EA3 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Saleh M. Jidawi  (kulia)na Meneja wa Kampuni ya Simed International Services ya Uholanzi Nd. Michor Pleijzer wakibadilishana hati za makubaliano  ya uboreshwaji wodi ya wazazi na watoto za Unguja na Pemba katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar. EA4 
Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Mr. Jaap Frederiks (wakatikati mbele walio simama)katika picha ya pamoja ya viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman wa mbele kulia. Sherehe hiyo ilifanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
……………………………………………………………………………..
Na Abdulla Ali  Maelezo-Zanzibar    
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuokoa maisha ya Wanawake na Watoto kwa kuimarisha Miundombinu ya Afya.
Hayo ameyaeleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dr. Saleh M. Jidawi wakati akisaini Mkataba kwa ajili ya utekelezaji wa kuanza kwa mradi wa kuimarisha Afya za Mama na Watoto uliyofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo iliyopo Wilaya ya Mjini Unguja.
Mkataba huo uliosainiwa na Wizara ya Afya Zanzibar kupitia Katibu Mkuu Dr. Saleh M. Jidawi kwa pamoja na Meneja wa Kampuni ya Simed International ya Uholanzi Nd. Michor Pleijzier uliofanyika siku ya tarehe 11/02/2015 ni miongoni mwa muendelezo wa utekelezaji wa mradi huo ambao awali ulitiwa saini mnamo tarehe 23/12/2014.
Dr. jidawi amesema kuwa dhamira kuu ya mradi huo ni kuimarisha afya za kina mama na watoto waliozaliwa chini ya mwaka mmoja pamoja na kutoa huduma kwa watoto wengine.
Ametanabahisha kuwa utekelezaji wa mradi huo unakwenda sambamba na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2020 uliotafsiriwa na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA ii).
Amesema kuwa mradi huo unajumuisha maeneo mbalimbali ya utekelezaji ikiwemo upatikanaji wa vifaa, tiba, ukarabati wa vifaa, uboreshaji wa miundombinu pamoja na utoaji wa ushauri elekezi kwa Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Amesema sambamba na hayo mradi huo unakusudia kuviboresha vituo vya Afya 19 vya Unguja na Pemba ili vipate kutoa huduma bora kwa jamii.
Ametanabahisha kuwa kwa upande wa Hospitali ya Mnazi Mmoja mradi huo utajumuisha vitengo mbalimbali vikiwemo chumba cha upasuaji, maabara, duka la dawa, chumba cha wagonjwa mahututi cha watoto na wazazi, kitengo cha huduma za X-ray, wodi za wazazi, kitengo cha kutakasisha vifaa tiba, eneo maalumu la kuteketeza taka za hospitali pamoja na kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD).
Dr. Jidawi ameeleza kuwa mradi huo wa sekta ya Afya unaakisi maazimio ya Serikali zote mbili ambazo ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Uholanzi kwa kufanya kazi pamoja katika nyanja mbalimabali za kimaendeleo ikiwa ni pamoja na uchimabaji wa gesi, uhifadhi wa mwambao wa bahari, uendelezaji wa bandari pamoja na uhifadhi wa Mji Mkongwe.
Nae Balozi mdogo wa Uholanzi Nd. Jaap Frederiks ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuharakisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mradi huo na kazi iliyobakia ni kuanza rasmi kwa maazimio ya mradi huo ambao utachukua takriban Miezi 33 hadi kukamilika kwake.
Mradi huo utagharimu shilingi Bilioni 19.5 Tsh, ambapo asilimia 50% ya fedha hizo zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na 50% zilizobaki zimetolewa na Serikali ya Uholanzi, zaidi ya gharama hizo pia Serikali ya Uholanzi imetoa fedha kwa ajili ya uandaaji wa michoro pamoja na ushauri elekezi uliogharimu shilingi Milioni 720
UONGOZI WAZARA YA AFYA WAKUTANA NA RAIS DK.ALI MOHAMED SHEIN LEO

UONGOZI WAZARA YA AFYA WAKUTANA NA RAIS DK.ALI MOHAMED SHEIN LEO

February 11, 2015

KIF2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiongoza kikao siku moja cha Wizara ya Afya  kilichozungumzia utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.]KIF1 
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Afya na Idara zake mbali mbali  wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo Rashid Seif Suleiman  (hayupo pichani) alipokuwa  akitoa taarifa ya Wizara ya utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,,[Picha na Ikulu.]  KIF3 
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (kulia) akiwa pamoja na watendaji mbali mbali  wakimsikiliza Waziri  Rashid Seif Suleiman  (hayupo pichani) alipokuwa  akitoa taarifa ya Wizara ya utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni mbele ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]    KIF4
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza kikao cha Wizara ya Afya  kilichozungumzia utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni ,[Picha na Ikulu.

KONDAKTA ASHIKILIWA NA POLISI TANGA KWA KUSAFIRISHA MIHADARATI AINA YA MIRUNGI

February 11, 2015
Salim Mohammed,Tanga.

,POLISI Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, wamemkamata kondakta wa basi, Abdalla Kayomba (37) ambaye anasadikiwa kuwa ndie msafirishaji mzoefu wa mihadharati aina ya mirungii kati ya Kilimanjaro na Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Juma Ndaki, alisema tukio hilo lilitokea januari 29 saa 6 usiku kwenye kizuizi cha polisi kijiji cha Chekelei Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe.

Alisema wakati wa kukamatwa kwake  kijana huyo alikutwa na kilo 35 za mirungi ambayo alikuwa ameificha chini ya uvungu wa lori na kuweka katika magunia mawili ya mkaa .

“Kwanza baada ya polisi kumuona tu walimuweka chini ya ulinzi kwani alikuwa akisakwa kwa udi na uvumba----wakati wa mahojiano alifichua siri na kueleza bayana kusafirisha kilo 35 za mirungi” alisema Ndaki na kuongeza

“Polisi walipoiona tu sura yake walimkwida na kumuweka chini ya ulinzi----nae hakufanya shida kwani alikuwa akijua kuwa anawindwa na sasa anahojiwa kutoa taarifa ili kuuzima mtandao wa usafirishaji mihadharati” alisema

Alisema wakati polisi wakifichua mirungi hiyo ambayo ilikuwa imefichwa katika magunia ya mkaa ilikuwa vigumu kuigundua lakini walipatwa na hofu baada ya kusikia harufu kali iliyoasghiria mirungi.

Katika hali nyengine, kaimu kamanda wa polisi aliwataka wananchi wanaoishi kandokando ya milima ya Usambara Wilayani Korogwe na Lushoto kutoa taarifa za watu wanaojishughulisha na kilimo cha bangi.

Alisema kilimo hicho kimekuwa kikishamiri katika Wilaya hizo na hivyo kutoa wito kwa wakulima waliobadilisha aina ya kilimo na badala yake kulima bangi kuwa msako wa kuwasaka uko karibu.

“Natoa wito kwa wakazi wanaoishi karibu na milima ambayo yunadhani kuna watu wamebadilisha aina ya kilimo na kulima bangi kuwafichua na kutupa taarifa----polisi imejipanga kufanya msako usiku na mchana” alisema Ndaki

Alisema tabia ya watu kulima bangi badala kilimo cha chakula kunaifadhaisha jamii kwani eneo hilo kila mwaka hukumbwa na njaa huku chanzo kikiwa ni wakulima kubadilisha kilimo.

Meli Kubwa yenye Urefu wa Mita 244 yatia nanga Bandari ya Dar

Meli Kubwa yenye Urefu wa Mita 244 yatia nanga Bandari ya Dar

February 11, 2015

unnamed 
Meli kubwa MSC Martina yenye urefu wa mita 244 na upana wa mita 32.2 ikiwa na uwezo wa kubeba makontena 2,411 imefanikiwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka, Mhandisi Madeni Kipande amesema, mafanikio hayo ni juhudi zilizofanywa na Mamlaka kuzitangaza bandari zake pamoja na uboreshwaji wa huduma.
“Ujio huu wa meli kubwa za mizigo kama hizi ni faraja kubwa sana kwetu kwani pia utaongeza uingiaji wa mizigo kwa wingi na hatimaye kuleta unafuu kwa mtumiaji wa mwisho,” alisema Mhandisi Kipande.
MSC Martina Kampuni ya Mediterranean Shipping Company (MSC) ni miongoni mwa meli kubwa na za kisasa ambazo zimefanikiwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam na kupakia na kupakua mzigo.
Meli nyingine kubwa na ya kisasa kuja nchini kwa mara ya kwanza ilikuwa ni Maersk Cubango mali ya Maersk Line iliyokuwa na urefu wa mita 250 na upana wa mita 38 ikiwa na uwezo wa kubeba kontena 4,500.
Mhandishi Kipande ameomba ushirikiano uliopo kati ya Mamlaka na mawakala wa meli uendelee ili kuleta ufanisi zaidi na amewataka mawakala wengine kuleta meli kubwa kama walivyofanya, Maersk and Mediterranean.
Kwa upande wake Nahodha aliyeingiza meli hiyo ndani ya Bandari ya Dar es Salaam, Abdulah Mwingamno alisema mabadiliko ya teknolojia yameongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia meli kubwa zaidi.
“Tuliweza kuingiza meli yenye urefu wa mita 250 ya kampuni ya Maersk iitwayo Maersk Cubango na sasa tumeingiza meli nyingine kubwa ya kampuni ya MSC iiitwayo MSC Martina yenye urefu wa mita 244, haya ni mafakio makubwa kwetu,” alisema.
Nahodha Mwingamno aliongeza kwamba meli hiyo ya mizigo iliingia salama katika lango la Bandari ya Dar es Salaam bila tatizo lolote kama ziingiavyo meli nyingine.
Alisema kwamba ujio wa meli hiyo na kufanikiwa kutia nanga katika bandari yetu bila tatizo lolote ndio kumefungua milango kwa meli hiyo na nyingine za aina hiyo kuanza safari zake kuja Dar es Salaam.
“Tunatarajia ujio wa meli kubwa zaidi ya hii yenye urefu wa mita zipatazo 260 katika bandari yetu kwenye miezi ya Machi na Aprili mwaka huu,” alisema.
Naye mwakilishi wa kampuni ya meli hiyo ya MSC nchini, Ndugu Ahmed Kamal alisema kwamba wanatarajia kuleta meli kubwa zaidi nchini, kwani kampuni yao ina meli kubwa zaidi zinazotia nanga katika bandari nyingine Duniani.
“Hii ni meli kubwa ya kwanza ya kampuni yetu kuja nchini lakini lengo letu ni kuleta meli kubwa zaidi ya hii nchini,” amesema Kamal.
Meli nyingine kubwa zaidi zilizowahi kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam zilikuwa na urefu wa mita 220 na mita 234, zikiwa na uwezo wa kubeba makontena kati ya 2800 na 3000. Awali meli zilizokuwa zinaruhusiwa kuingia katika bandari ya Dar es Salaam hazikutakiwa kuzidi urefu wa mita 234.

TANZANIA BLOGGER'S NETWORK (TBN) YATOA UBANI KWA WAHANGA AJALI YA MOTO DAR

February 11, 2015
Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi (kulia) akikabidhi ubani wa fedha shilingi laki tano (500,000) jana zilizotolewa kwa mwanahabari wa Kitulo FM kama pole baada ya kupoteza ndugu watano wa familia moja katika ajali ya moto iliyotokea hivi karibuni na kuua watu sita eneo la Kipunguni jijini Dar es Salaam. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa TBN, Dotto Mwaibale aliyeshiriki tukio hilo. TBN ilishiriki katika mazishi ya marehemu hao sita waliozikwa jana katika makaburi ya Airwing Dar es Salaam. Picha na Francis Dande.
wakibadilishana mawazo kabla ya kukabidhi mchango
Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi (kulia) akikabidhi ubani wa fedha shilingi laki tano (500,000) jana zilizotolewa kwa mwanahabari wa Kitulo FM kama pole baada ya kupoteza ndugu watano wa familia moja katika ajali ya moto iliyotokea hivi karibuni na kuua watu sita eneo la Kipunguni jijini Dar es Salaam. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa TBN, Dotto Mwaibale aliyeshiriki tukio hilo. TBN ilishiriki katika mazishi ya marehemu hao sita waliozikwa jana katika makaburi ya Airwing Dar es Salaam. Picha na Francis Dande.
Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi (kulia) akikabidhi ubani wa fedha shilingi laki tano (500,000) jana zilizotolewa kwa mwanahabari wa Kitulo FM kama pole baada ya kupoteza ndugu watano wa familia moja katika ajali ya moto iliyotokea hivi karibuni na kuua watu sita eneo la Kipunguni jijini Dar es Salaam. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa TBN, Dotto Mwaibale aliyeshiriki tukio hilo. TBN ilishiriki katika mazishi ya marehemu hao sita waliozikwa jana katika makaburi ya Airwing Dar es Salaam. Picha na Francis Dande.

MH. MAKALLA AZINDUA MRADI WA MAJI HANANG

February 11, 2015

Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme na Inj. Salum Chusi wa Wizara ya Maji (nyuma) wakiangalia pampu ya maji ya mradi wa Simbay katika ziara yake ya kukagua utekelezaji na uzinduzi wa miradi ya maji mkoani Manyara jana.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akiwa kwenye tanki la maji la mradi wa maji wa Simbay, wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akizindua rasmi mradi wa maji wa kijiji cha Simbay, Wilaya ya Hanang, mkoani Manyara katika ziara yake aliyoanza mkoa wa Manyara jana, akiwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu na Mbunge wa Hanang, Dk. Mary Nagu na Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme.
Mradi wa maji wa Simbay mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla.
Mwenyeji wa Kijiji cha Simbay akisoma ripoti ya maji ya kijiji cha Simbay, wilaya ya Hanang, mkoani Manyara kwa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla kati.

MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA LINDI KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

February 11, 2015

Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi

Wakazi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye zoezi la kuipigia kura Katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Mwito huo umetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika tawi la Msinjahili wilayani humo.

Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema zoezi la uandikishaji litafanyika kwa muda wa wiki moja na katika mkoa huo litaanza tarehe 16 hadi 22 mwezi huu  hivyo basi ni muhimu wananchi wakajitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya msingi ya kujiandikisha.

“Mkoa wetu ni mmoja kati ya mikoa minne ya mwanzo itakayoanza zoezi hili, mikoa mingine ni Mtwara, Ruvuma na Njombe. Ni muhimu wananchi mkajitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani uandikishaji utafanyika kwa njia ya mashine na baada ya wiki moja mashine hizi  zitahamia katika mkoa mwingine”, alisema Mama Kikwete.

Kuhusu Katiba inayopendekezwa alisema ni ya watanzania wote kwa maendeleo yao kwa kuwa inamgusa kila mtu. Ili wananchi waweze kuipigia kura ni muhimu wakajiandikishe katika daftari la kudumu la wapiga kura na ifikapo tarehe 30 ya mwezi wa nne mwaka huu wakaipigie kura ya Ndiyo. 

Aidha MNEC huyo alisema Tanzania yenye neema inawezekana kwani maisha bora ni kuhakikisha binadamu anafunguka kiakili kwa kupata elimu kwa kuona umuhimu wa hayo yote Serikali imejenga shule nyingi za Sekondari za Kata ambazo zimeweza kuwasaidia watoto wengi kutoka  familia maskini kupata elimu jambo ambalo halikuwepo katika miaka ya nyuma.

Mama Kikwete anasema, “Hivi sasa huduma za afya zimeboreshwa na zinapatikana kirahisi ukilinganisha na miaka ya nyumba kwani Serikali imejenga Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali, idadi ya wafanyakazi katika sekta hii imeongezeka na vifaa tiba pamoja na madawa vinapatikana.

“Barabara zimejengwa kwa kiwango cha lami katika maeneo mengi nchini na hivyo kurahisisha usafiri, wananchi wanasafirisha bidhaa zao kutoa eneo moja hadi lingine haya ndiyo maendeleo kwani mkulima analima mazao yake na kuwa na uhakika wa kuyafikisha sokoni kwa mnunuzi na walaji”,.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi Mzee Alli Mtopa aliwasihi wanachama wa Chama hicho  kuondoa tofauti zao za makundi ya wagombea waliyokuwa nayo katika uchaguzi uliopita bali  waungane na kuwa kitu kimoja  na kufanya kazi za chama kwa kufanya hivyo watapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao.

Mzee Mtopa alisema vyama vya upinzani vinaona maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya CCM lakini havitaki kukubali ukweli bali wanapita mitaani na kuwarubuni watu kuwa hakuna maendeleo yoyote yaliyofanyika jambo ambalo siyo sahihi na kuwataka wananchi hao kuwapuuza na kuendelea kufanya  kazi ili wajiletee maendeleo.

Mama Kikwete pia alifanya vikao na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama hicho  katika matawi ya Sheikh Badi, Msonobari na Msinjahili  alizungumza nao  mambo mbalimbali yanayohusu kazi za chama hicho na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.

Akiwa katika tawi la Msonobari alikipatia kikundi cha utengenezaji batiki cha wanawake wa mtaa wa Msonobari juu na chini shilingi laki tano ili ziweze kuwasaidia kununua vitendea kazi na malighafi kwa ajili ya uzalishaji wa batiki.
 MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. BILAL AONGOZA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KWENYE MAZISHI YA FAMILIA KAPTEN DAVID MPILA LEO

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. BILAL AONGOZA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KWENYE MAZISHI YA FAMILIA KAPTEN DAVID MPILA LEO

February 11, 2015
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwenye majeneza yenye miili ya Familia ya marehemu Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto nyumbani kwao Kipunguni, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga Dar es salaam. BIL2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji mama mzazi wa marehemu bibi Celina Mpila mke wa marehem Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga Dar es salaam.             (Picha na OMR)

TANZANIA YAKANUSHA RIPOTI KUHUSU FDLR

February 11, 2015


Tanzania imekanusha vikali tuhuma kwamba imekuwa ikiwaruhusu viongozi wa kundi la waasi la FDLR kufanya mikutano nchini humo.
Hapo jana kulikuwa na taarifa ambazo zilitangazwa na vyombo mbali mbali vya habari duniani kuhusu ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa umoja mataifa kuhusu Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwamba iilituhumu Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi FDLR kuandaa mikutano nchini humo.
Katika ripoti hiyo pia wanajeshi wa Burundi wanatuhumiwa kuwa walitekeleza unyanyasaji wa kingono.

BARAZA LA UJENZI ENDELEVU NA MAZINGIRA TANZANIA (TANZANIA GREEN BUILDING COUNCIL ) LATAMBULISHA SHUGHULI ZAKE NCHINI

February 11, 2015
Rais wa Baraza la Ujenzi Endelevu na Mazingira Tanzania (Tanzania Green Building Council ), Ngwisa Mpembe (wa pili kulia) akilitambulisha baraza hilo la kitaalamu ambalo Shirika la Nyumba la Taifa ni mmoja wa waasisi wake kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) mojawapo wa majukumu ya Baraza hilo ni kushawishi, kuratibu na kusimamia ujenzi wa nyumba za kisasa zilizo rafiki wa mazingira. Baraza lina wadau wengi wakiwamo Wasanifu Majenzi , Wakadiriaji majengo, wahandisi watengenezaji vifaa na watumiaji wa vifaa. Machi 19-20 mwaka huu, Baraza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali litafanya Kongamano la Kwanza la Ujenzi Endelevu na Mazingira jijini Arusha litakaloshirikisha wadau zaidi ya 400 kutoka pembe mbalimbali za Dunia. Kushoto ni Ipyana Moses Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Green Building Council, Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Farizan d’Avezac de Moran na Mike T’chawi wa Chama cha Wasanifu Majengo.
 Bango lililoonyesha maandalizi ya mkutano utakaofanyika Machi 19-20 mwaka huu huko Arusha
Viongozi wa Tanzania Green Building Council wakijadiliana jambo kwenye  mkutano na waandishi wa habari kulitambulisha baraza hilo la kitaalamu ambalo Shirika la Nyumba la Taifa ni mmoja wa waasisi wake kwa waandishi wa Habari.

Viongozi wa Tanzania Green Building Council wakijadiliana jambo kwenye  mkutano na waandishi wa habari kulitambulisha baraza hilo la kitaalamu ambalo Shirika la Nyumba la Taifa ni mmoja wa waasisi wake kwa waandishi wa Habari.
Ipyana Moses Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Green Building Council akizungumza kwenye  mkutano na waandishi wa habari kulitambulisha baraza hilo la kitaalamu ambalo Shirika la Nyumba la Taifa ni mmoja wa waasisi wake kwa waandishi wa Habari kulia kwake ni Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Farizan d’Avezac de MoranRais wa Baraza la Ujenzi Endelevu na Mazingira Tanzania (Tanzania Green Building Council ), Rais wa Baraza la Ujenzi Endelevu na Mazingira Tanzania (Tanzania Green Building Council ) Ngwisa Mpembe na Mike T’chawi wa Chama cha Wasanifu Majengo.