RC Tanga mgeni rasmi Gambo Cup kesho

July 03, 2013


Na Oscar Assenga, Korogwe.

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika fainali ya Mashindano ya Kombe la Vijana ya Gambo Cup itakayofanyika katika uwanja wa Chuo cha Ualimu wilayani hapa.

Akizungumza jana,Mratibu wa Mashindano hayo,Zaina Hassani alisema maandalizi ya hatua hiyo yamekamilika ambapo leo (jana)kutachezwa mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu kati ya Bungu Kibaoni na Kosovo Fc.

Hassani alizitaja timu ambazo zitacheza hatua ya fainali ya mashindano hayo kuwa ni Korogwe United ambao ni mabingwa wa soka wilaya ya Korogwe watakuwa na kibarua kizito dhidi ya Mtonga Fc mchezo unaotazamiwa kuwa na upinzani mkubwa.

 Katibu huyo alisema mshindi wa kwanza katika mashindano hayo anatarajiwa kuondoka na Ng’ombe ,Kombe,Jei seti 1 na mipira 2,mshindi wa pili anatarajiwa kuondoka na Mbuzi wawili,jezi seti moja na mpira mmoja huku mshindi wa tatu akitarajiwa kuondoka na Mbuzi 1,Jezi seti 1 na mpira 1.

Aliongeza kuwa kuanzia mshindi wanne hadi wa nane wanatarajiwa kupata Jezi seti 1 na mpira moja moja kila timu ikiwa ni kuzipa chachu ya kufanya maandalizi ya msimu mpya ambao utaanza mara baada ya kumalizika msimu huu.

Mashindano ya Gambo Cup yalianzishwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo na kufadhiliwa na benki ya NMB lenye lengo la kukuza na kuinua vipaji vya wachezaji wachanga wilayani humo ambapo yalishirikisha timu 85 kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo.

Mwisho.