KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI ZA JUU MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI ZA JUU MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA

June 14, 2016

KT1 
Gwaride la Maafisa Wahitimu wa kozi ya Uongozi ngazi ya Juu wa Jeshi la Magereza likijiandaa kupita mbele ya Jukwaa la Mgeni kwa heshima kama wanavyoonekana wakiwa wakakamavu katika picha. Sherehe za kufunga Mafunzo hayo zimefanyika leo Juni 14, 2016 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania kilichopo Ukonga, Dar es Salaam.
KT2 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu kama inavyoonekana katika picha.
KT3 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akimvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi za juu aliyefanya vizuri katika masomo ya Medani kwa niaba ya Wahitimu wote wa kozi hiyo(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akishuhudia tukio hilo la uvishaji cheo.
KT4 
Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wageni Waalikwa kutoka Taasisi mbalimbali wakifuatilia kwa karibu Gwaride la Wahitimu.
KT5 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi juu ya Uendeshaji wa Jeshi la Magereza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani).
KT6 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kulia) akimuongoza Mgeni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira kuelekea eneo la hafla ya kufunga rasmi Mafunzo ya Uongozi ngazi za juu wa Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, ACP. Erasmus Kundy(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

PICHA: YANGA WAKIJIFUA NCHINI UTURUKI TAYARI KUWAKABILI MO BEJAIA JUNE 19 NCHINI ALGERIA

June 14, 2016

Kocha wa Yanga Hans van Der Pluijm akitoa maelekezo kwa wachezaji wake. Yanga wapo Uturuki kwa kambi maalum kwa ajli ya mchezo wa Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria utakaochezwa June 19 nchini Algeria.
 Hapa akiendelea kutoa dawa kwa wachezaji wake.
 Wachezaji wakimsikiliza kocha wao.




NAIBU WAZIRI WA NCHI MAZINGIRA NA MUUNGANO AWAZAWADIA WASHINDI WA TAMASHA LA AJIRA NA UJASIRIAMALI

June 14, 2016

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mh Luhanga Mpina Akikabidhi Zawadi kwa Washindi  Wajiojishindia Zawadi Mbalimbali Kutoka Kampuni ya Huawei Kwenye Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Mkoani Mbeya.
Chuo kikuu cha Mzumbe jijini Mbeya kiliendesha kongamano la Ujasiliamali ambalo lilihuishwa na shindano la “badirika kwa vitendo” ambapo Wanafunzi sita walijishindia zawadi mbalimbali zikiwemo simu za mikononi toka kampuni ya Huawei. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mh Luhanga Mpina Katika Picha ya Pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba na Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG group Imani Kajula na washindi waliojinyakulia Zawadi Mbalimbali.Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba  Ambaye naye alitoa Mada Mbalimbali Namna ya Kukabiliana na Changamoto ya Ajira Hapa Nchini
Afisa Mtendaji Mkuu waEAG group Imani Kajula Akitoa Mada kwenye Tamasha La Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Mkoani Mbeya
Katika hafla hiyo ya usiku, Wanafunzi hao sita Elisha Tullo, Nelson Mkolozi, Goodlove Msigwa, Agness Ngusa, Leornard Meshack walieleza walichojifunza na jinsi watakavyotumia ujuzi wao. Mshindi wa kwanza alikuwa ni Elisha Tullo na wa pili alikuwa Goodlove Msigwa.

Washiriki wa Tamasha Hilo wakisikiliza Kwa Makini Mda Mbalimbali Zilizowasilishwa  Kwenye Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya Kuona picha zaidi za washindi na usiku wa wajasiliamali tembelea  Facebook page www.facebook.com/Faharinews

Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar Masjid Loota Kiembesamaki Zanzibar leo

June 14, 2016



Mgeni rasmin katika Uzinduzi wa Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qura-an Zanzibar yalioandaliwa na Jumuiya ya Kihifadhi Quran Zanzibar Naibu Kadhi Mkuu Zanzibar Shekh.Hassan Othma Ngwali(katikati) Amiri wa Jumuiya ya Kuhifadhi Quran Zanzibar Mwalim Suleiman Omar Naimi Amiri Kuhifadhisha Quran Zanzibar Shekh. Mohammed Alawi Ally, wakifuatilia mashindano hayo yaliowashirikisha Wanafunzi wa Vyuo vya Quran Zanzibar,Tanga Pwani na Morogoro.
Viongozi wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Zanzibar wakifuatilia mashindano hayo yanayofanyika katika Masjid Loota Kiembesamaki Zanzibar na kuwashirikisha Vijana wa Umri mbali.
Viongozi wa Kamati ya Kuhifadhi Qur-an wakiwa katikac Masjid Loota Kiembesamaki wakifuatilia Wanafunzi wakisoma Qur-an wakati wa mashindano hayo yalioandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Zanzibar.
Washiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar wakiwa katika Masjid Loota wakisubiri zamu zao kushiriki mashindano hayo. yanayoshindanisha Wahifadhi Qur-an Juzuu 5.10,20 na 25.
Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatilia mashindano ya kuhifadhi Qur-an yanayofanyika katika Masjid Loota Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Majaji wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar wakiwa makini kufuatilia usomani wa Wanafunzi hao katika mashindano hayo.
Watoa Aya za Qur-an kwa Washiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar wakitoa Aya kwa Washiriki hao.
Mshinriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Juzuu 10 kutoka Zanzibar Mwanafunzi Khayyam Mohammed mwenye umri wa miaka 13. akisoma Qur-an wakati wa mashindano hayo yanayofanyika katika Masjid Loota Kiembesamaki leo 14/6/2016.
Mwanafunzi kutoka Zanzibar Mussa Hamad mwenye umri wa miaka 9 akishiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Juzuu 10, yanayofanyika katika Masjid Loota kiembesamaki Unguja
Mshiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an kutoka Zanzibar Mwanafunzi Shakir Hamad Juma. akisoma Qur-an katika mashindano hayo yalioandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar. yaliowashirikisha Wanafunzi 27 Kutoka Zanzibar, Tanga, Pwani na Morogoro.Imetayarishwa na Mtandao wa Zanzinews.com.
Profesa Muhongo aelezea mikakati Sekta za Nishati na Madini, Benki ya Dunia yafurahishwa na utekelezaji wake

Profesa Muhongo aelezea mikakati Sekta za Nishati na Madini, Benki ya Dunia yafurahishwa na utekelezaji wake

June 14, 2016

mug1 
Waziri wa Nishati na Madini  Profesa Sospeter Muhongo  akiongoza kikao kilichoshirikisha Watendaji kutoka  Benki ya Dunia pamoja  na watendaji kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini na   taasisi zake ikiwa ni pamoja na  Shirika la  Umeme  Tanzania (TANESCO), Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) na Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA).
mug2 
Mtendaji  Kutoka Benki ya  Dunia anayeshughulikia mazingira  Vladislav Vucetic, akielezea mikakati ya   benki hiyo katika ushirikiano wake  na  Serikali ili  kupanua sekta za nishati na madini.
mug3 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa  Justin Ntalikwa (kushoto waliokaa mbele) na Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Dkt. Juliana Pallangyo ( wa pili kutoka  kushoto waliokaa mbele) wakifuatilia kwa makini maelekezo 
…………………………………………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameelezea mikakati ya   Serikali katika  uboreshaji wa sekta za nishati  na  madini  na kuongeza kuwa  Serikali ipo  tayari kushirikiana na    Benki ya Dunia (WB) katika uboreshaji  wa sekta hizo ili ziwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Profesa Muhongo aliyasema hayo alipokutana na Watendaji kutoka  Benki ya Dunia pamoja  na watendaji kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini na   taasisi zake ikiwa ni pamoja na  Shirika la  Umeme  Tanzania (TANESCO), Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) na Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA)
Akizungumzia Sekta ya Nishati  nchini Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa  Sekta ya nishati inakuwa na mchngo mkubwa katika ukuaji wa uchumi  na kutoka katika kundi la nchi masikini duniani  na kuingia katika kundi la nchi  zenye kipato cha kati ifikapo mwaka  2025 kama Dira ya Maendeleo  ya Taifa ifanvyofafanua
Aliongeza kuwa, Serikali kwa mara ya kwanza imetenga  asilimia  40 ya bajeti yake katika miradi ya  maendeleo  ikiwa ni  pamoja na ya  umeme na kuendelea kufafanua kuwa katika bajeti  ya  Wizara ya  mwaka wa  fedha  2016/17, Wizara imetenga asilimia 94 ya bajeti yake katika miradi ya maendeleo,  ambapo  katika Idara ya Nishati asilimia 98 itakwenda kwenye miradi ya umeme.
Waziri Muhongo alisema  kuwa ili kuimarisha   Sekta ya Nishati,  Wizara imepanga kupanua sekta ya nishati kwa kukaribisha wawekezaji binafsi kuwekeza  katika sekta ya uzalishaji na uuzaji wa umeme pamoja na kuwapo kwa mwongozo utakaowawezesha kuzalisha umeme.
Alindelea kusema kuwa Wizara inatarajia kuimarisha  usambazaji wa umeme vijijini kwa kushirikiana na  Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) na TANESCO.
Profesa Muhongo aliendelea kutaja mikakati mingine kuwa ni pamoja na  kuimarisha mradi wa usambazaji wa umeme  wenye msongo wa kilovolti  400 kupitia  Iringa, Mbeya, Tunduma hadi katika eneo la Kabwe nchini  Zambia  na  kusisitiza kuwa upembuzi  yakinifu unatarajia kukamilika mapema  Desemba mwaka huu kabla ya kuanza kwa mradi.
Aliendelea kutaja miradi mingine kuwa ni pamoja na mradi wa usambazaji  umeme kupitia Mbeya, Sumbawanga, Mpanda, Kigoma, Nyakanazi na kuiomba  Benki ya Dunia kushirikiana na Benki ya Maendeleo  Afrika (AfDB) ili kufanikisha mradi huo.
“Kuna mradi wa kuunganisha  Tanzania  na  Uganda ujulikanao kwa  jila la  Tanzania – Uganda inter-connector unaounganisha Mwanza, Geita,  Nyakanazi, Kyaka- Bukoba hadi  Masaka nchini Uganda.
Akizungumzia  Sekta ya  Gesi  Profesa Muhongo  alieleza kuwa serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha nishati ya  gesi inatumika  ipasavyo katika uzalishaji  umeme pamoja na kusambazwa katika matumizi ya majumbani.
Aliongeza kuwa serikali imeweka mikakati ya kusambaza gesi majumbani kwa ajili ya matumizi ya kupikia katika mikoa ya Dar es salaam, Lindi, Mtwara na katika maeneo mengine ya  Pwani.
Akielezea Sekta ya Madini  Profesa Muhongo aliiomba Benki ya  Dunia kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya madini kwa wachimbaji wadogo pamoja na katika kuwapatia  elimu  kuhusu mazingira, uchenjuaji wa madini  na kuongeza ajira  hususan katika maeneo  ya madini yaliyopo  vijijini
Naye Mtendaji  Kutoka Benki ya  Dunia anayeshughulikia mazingira  Vladislav Vucetic alisema  Benki ya Dunia ipo   tayari kushirikiana na Serikali katika uendelezaji wa sekta za nishati na madini ili kufikia malengo  yaliyokusudiwa.

PUNTLAND WAJA NCHINI KUJINOA MASUALA YA UTUMISHI WA UMMA

June 14, 2016

Picha ya pamoja , ujumbe wa serikali ya Puntiland wakiwa na wenyeji wao TPSC,waliokaa wa tatu kutoka kushoto Waziri wa Kazi,Vijanana Michezo wa Puntiland, Abdurahman Ahmed Abdulle na wa nne kutoka kushoto (waliokaa) Kaimu Mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Dkt.Henry Mambo , Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kupata uzoefu katika masuala mbalimbali ya Utumishi
Kaimu Mkuu ya wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania(TPSC), Dkt. Henry Mambo (kushoto) akibadilishana mawazo na  Waziri wa Kazi,Vijana na Michezo wa Puntiland, Abdurahman Ahmed Abdulle kando ya kikao cha pamoja baina ya ujumbe wake na TPSC.                    

ZAIDI YA WAKAZI 4000 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI PANGANI

June 14, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martine Shigella katikati akipata maelezo ya mradi wa maji Boza-Kimang’a kutoka kwa Meneja wa Maji Wilaya ya Pangani,Mohamed Seif wakati alipofanya ziara wilayani humo kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani,Esteria Kilasi

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martine Shigella mwenye suti katikati akitazama mradi wa Maji  wa Boza-Kimang’a wa kwanza kushoto ni Mhandisi wa Maji Wilaya ya Pangani,Mohamed Seif na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Ahmed
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martine Shigella mwenye suti akiingia kwenye tanki la kuhifadhia maji

ZAIDI ya wakazi 4009 wa Kijiji cha Boza Kimang’a wilayani Pangani Mkoani Tanga watanufaika na mradi wa huduma ya maji kupitia program ya maji na usafi wa mazingira vijijini (NRWSSP) katika mpango wa vijiji vya nyongeza.

Hayo yalisemwa juzi na Mhandisi wa Maji wilaya ya Pangani, Mohamed Seif wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji Boza-Kimang’a kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella aliyefanya ziara ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo.

Alisema kuwahadi sasa kisima kirefu kimekwisha kuchimbwa na usanifu wa mradi huo umefanyika na mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji Saxon Building Contractor na kusimamiwa na Mtaalamu mshauri Don Consult Limited.

Mhandisi huyo alisema mradi huo ambao umeanza February 19 mwaka huu na kutarajiwa kukamilika Novemba 19 ukigharimu kiasi cha sh.milioni 884.4 ambapo shughuli zitakazofanyika ni uchimbaji wa kisima kirefu,ujenzi wa nyumba ya kuhifadhia mashine,ujenzi wa matenki mawili ya kuhifadhia maji.

Aliongeza kazi nyengine ni ujenzi wa vituo 16 vya kuchotea
maji,kununua na kufunga mashine za kusukuma maji,kununua na kufunga mabomba ya viungio ikiwemo kuvuta umeme kwenye eneo hilo la mradi.

Akizungumza wakati akizundua mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella aliwataka wananchi kuhakikisha  wanautunza vema ili uweze kuwasaidia wao na vizazi vijavyo ikiwemo kuacha kuharibu vyanzo vya maji.