KATIBU WA CHADEMA TANGA ATEMBELEA SHAMBA LA MKONGE LA KWASHEMSHI NA KUFANYA MIKUTANO NA WANANCHI

February 26, 2014

KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TANGA JONATHAN BAWEJE WA PILI KUTOKA KUSHOTO AKIPANGA JAMBO KABLA YA KUWAHUTUBIA WAKAZI WA KIJIJI CHA KWASHEMSHI KATA YA KWASHEMSHI WILAYANI KOROGWE LEO,


KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TANGA,JONATHAN BAHWEJE KATIKATI AKIISISITIZA JAMBO NA KATIBU WA CHAMA HICHO  KATA YA KWASHEMSHI MARA BAADA YA KUTEMBELEA SHAMBA LA MKONGE LA KWASHEMSHI ESTATE LILILOLIMWA NA WANANCHI IKIWEMO KUPANDA MAZAO LAKINI MWEKEZAJI KUYALIMIA CHINI


HAPA AKISISITIZA HAIWZEKANI LAZIMA ACHUKULIWE HATUA KALI






February 26, 2014
February 26, 2014

UZINDUZI RASMI WA KAMPENI YA TAIFA YA KUSAMBAZA UELEWA WA RASIMU YA PILI YA KATIBA YA TANZANIA KWA WANANCHI WAFANYIKA LEO KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO MLIMANI CITY

Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu  akizindua rasmi vipeperushi vilivyo andikwa , Mambo Saba makubwa ya kuungwa mkono na wananchi katika Rasimu ya Katiba pamoja na mambo makubwa matano yanayokosekana katika Rasimu ya Katiba na Kipeperushi cha pili kinacho sema ‘Taifa ni letu na Katiba ni yetu Husika tupate Katiba Bora.
 Jaji Mkuu Mstaafu Mh. Thomas Mihayo akitoa ufafanuzi wa uzinduzi wa Rasimu ya pili ya Katiba
 Mkurugenzi Mtendaji wa Haki za Binadamu Bi. Helen Simba akieleza kuhusika kwa haki za Binadamu katika Rasimu ya Pili katiba kwa wananchi.
February 26, 2014

MADINI YA TANZANITE YANGA’RA BANGKOK

1Baadhi ya madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana katika mabanda mbalimbali katika maonesho ya 53 ya Kimataifa ya Bangkok Gems and Jewelry Fair. 2Mfanyabiashara  wa madini na Afisa Masoko wa Kampuni ya Tom Gems Tanzania, akimwonesha mgeni aliyefika katika banda la Tanzania kuona madini ghafi ya Tanzanite  yanayozalishwa Tanzania pekee. Wageni wengi wamefika katika banda hilo kuona Tanzanite halisi kutoka Tanzania. 3 (2)Mwenyekiti wa Madini ya Viwandani Bw. Kassim Iddi Pazi, akimwonesha mgeni madini ya Ruby. Kutokana na maelezo ya Bw. Pazi, ameeleza kuwa, madini hayo yametoka katika maeneo ya Winza Dodoma na Matombo Morogoro. 4Mfanyabiashara wa Madini kutoka Kampuni ya Tom Gems Bw.Benjamin Mtalemwa akimwonesha mgeni madini mbalimbali alipotembelea banda la Tanzania. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mthamini wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Edward Rweymamu, Wa pili kulia ni Afisa Madini kutoka Shirika la Madini Tanzania (STAMICO). Bw. Peter Maha, na  wa kwanza kulia  ni Afisa toka Wizarani Bibi. Margareth Muhony.
 …………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Bangkok
Madini ya Tanzanite yamekuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya 53 ya Kimataifa ya‘’Bangkok Gems and Jewelry Fair’’, yanayoendelea katika eneo la kibiashara la ‘Impact Challenger’, jijini Bangkok. 
Madini ya Tanzanite yanayozalishwa nchini Tanzania pekee duniani, yamekuwa kivutio  kikubwa kwa wageni wanaotembelea maonesho hayo ikiwemo  wauzaji, wanunuzi na wafanyabiashara ambao wamefika  katika banda la Tanzania kutaka kuona Tanzanite halisi kutoka Tanzania.
February 26, 2014
Release No. 033
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 26, 2014

SYMBION KUSAIDIA PROGRAMU ZA VIJANA TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Symbion Power Tanzania Limited zimesaini makubaliano ambapo kampuni hiyo itasaidia kwenye maeneo matatu ya mpira wa miguu wa vijana.

Makubaliano hayo yametiwa saini leo (Februari 26 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam. Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesaini kwa niaba ya shirikisho wakati upande wa Symbion aliyesaini ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Peter Gathercoles.

Maeneo ambayo Symbion itasaidia ni ujenzi wa vituo viwili vya kuendeleza vipaji vitakavyojengwa Kidongo Chekundu na Kinondoni mkoani Dar es Salaam, mashindano ya Taifa ya wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 12 (U12) yatakayofanyika mwaka huu na kuisaidia timu ya U17 ya Tanzania (Serengeti Boys).

Serengeti Boys itacheza na Afrika Kusini, Julai mwaka huu katika mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa wachezaji wa umri huo zitakazofanyika mwakani nchini Niger.

Hivyo Symbion imetoa dola 60,000 (zaidi ya sh. milioni 96) kwa ajili ya mashindano ya U12, na dola 50,000 (zaidi ya sh. milioni 80) kwa ajili ya maandalizi ya Serengeti Boys kwa mechi dhidi ya Afrika Kusini.

Rais Malinzi ameishukuru Symbion kwa kukubali kushirikiana na TFF katika mpira wa miguu wa vijana, lakini vilevile amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwani ndiye chachu ya kampuni hiyo kuamua kujishirikisha na mpira wa miguu wa vijana.

ZAMBIA WATUA KUIKABILI TWIGA STARS
Timu ya Taifa ya Zambia (Shepolopolo) inatua nchini kesho mchana (Februari 27 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Tanzania (Twiga Stars) itakayochezwa keshokutwa (Februari 28 mwaka huu).

Shepolopolo yenye msafara wa watu 29 itawasili kwa ndege ya Fastjet ikitokea Lusaka na itafikia kwenye hoteli ya Accomondia kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.

Waamuzi wa mechi hiyo kutoka Burundi wakiongozwa na Ines Niyosaba wamewasili nchini leo asubuhi wakati Kamishna Fran Hilton-Smith kutoka Afrika Kusini atawasili kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South African Airways.

RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari juu ya benchi la ufundi la timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars).

Mkutano huo utafanyika kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya 3 katika Jengo la PPF Tower, mtaa wa Garden na Ohio.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)