UKUMBI WA MAZOEZI KIKWAZO NGUMI ZA RIDHAA TANGA.

October 30, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
CHAMA cha Ngumi za Ridhaa mkoa wa Tanga(TBA)kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokuwa na ukumbi wa kufanya mazoezi kwa mabondia kitendo ambacho kinawapa wakati mgumu mabondia wakati wa kufanya mazoezi.


Mwenyekiti wa Chama hicho,Mansour Soud Semfyoa aliiambia Tanga Raha kuwa hali hiyo inawafanya mabondia hao kushindwa kutimiza ndoto zao na kuziomba mamlaka husika ikiwemo uongozi wa serikali ya wilaya kuwasaidia ili kuweza kupatikana ukumbi wa mazoezi.

Soud alisema suala lengine ambalo linawapa changamoto ni uhaba wa vifaa vya kufanyia mazoezi kwa mabondia waliopo mkoani hapa hivyo kuwaomba wadau kuwasaidia ili viweze kupatikana.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA NGUMU ZA RIDHAA MKOA WA TANGA,MANSOUR SOUD SEMFYOA
Mwenyekiti huyo alisema chama hicho kimefanya jitihada mbalimbali ili kuweza kupatikana ukumbi wa Tangamano ambapo uongozi wa chama hicho  tayari umeshaandika barua kwenda kwa mkurugenzi wa Jiji lengo likiwa ni kumuomba wautumia ukumbi wa Tangamano.

Alisema majibu ya barua hiyo iliwajibu wamekubaliwa katika ukumbi wa Communite Centre Makorora ambapo wataungana na vikundi vyengine na kuelezwa kuwa wanatakiwa walipie sh.elfu hamsini ili waweze kupewa eneo hilo.

Aidha alisema mikakati waliokuwa nayo hivi sasa ni kuuendeleza mchezo wa ngumi ambao unaonekana kupotea mkoani hapa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lengo likiwa ni kupata mabondia wazuri ambao watautangaza mkoa huu.

Aliongeza kuwa wanampango wa kuupeleka mchezo huo mashuleni ambapo kwa kuanzia wataanzia katika shule za msingi na sekondari na baadae vyuo vikuu lengo ni kuwapa vijana hao uelewa kuhusu mchezo huo.

Soud alisema pia wanatarajia kuanzisha miradi ambayo itakisaidia chama hicho kujiendesha chenyewe kuliko kutegemea misaada ambao wakati mwengine inaweza kukwamisha malengo yao waliojiwekea.    

CHAMA CHA NGUMI ZA RIDHAA TANGA WALILIA UKUMBI WA MAZOEZI

October 30, 2013
MABONDIA WA MKOA WA TANGA WAKIFANYA MAZOEZI KATIKA UWANJA WA VALLEYBALL MKWAKWANI KUTOKANA NA KUKOSA UKUMBI MAALUMU





A MOSQUE AND 16 HOUSES TORCHED IN VIOLENT STRICKE

October 30, 2013
By Paskal Mbunga, Kilindi    October 30, 2013
AN unknown number of angry residents in Lulago village in Kilindi district have burned down a mosque used by an armed assailants who had tiraken refuge in the forests after killing a militia man last week.

A group of Tanga based journalists who toured the troubled area early this week were informed by the Chairman of Lulago village, Mohamed Waziri Mwariko that all the assailants were of the Ansar Sunni sect and that apart from torching down their mosque, but also 16 houses belonging to the assailants were completely burned to ashes.

The village chairman confirmed that the security atmosphere  was still tense because the main culprits were still at large, though the police has apprehended 18 of them.

Mwariko said there were three main ring leaders in the gang namely, Ayub Idd/a.k.a. Master and his lietnant, known by only one name, Jumanne. He named the third as Yusuf Said.

According to the village chairman, the torching down of the mosque belonging to the Ansar Sunni sect had nothing to do with religion strife or conflict but it was rather they (assailants) to blame for failing to live up according to the law of the land.

‘Let me clarify to you journalists that the torching of the mosque and the burned houses had no connection with religion strife”. 
He said and added that there is no christianity driven agenda or government intervention. It was the Ansar Sunni members whose open agenda was to disobey the government, calling it a kafir one.

The moslem population here is 99.5 per cent against other believers, he said adding that there are two mosques, apart from the torched one which belonged to the Ansar Sunni sect.   

According to residents of the village who talked to reporters, the Ansar Sunni members settled in the village in 20o9 without the consent of the village government. 
 Athumani Bakari and Mariam Abdallah said since they settled in the village, there has more chaos rather than peace in the village.

Another villager,  Mganga Kilimo said after their arrival in two buses  from Dar es Salaam, they singled out themselves from other villagers, saying that they cannot mingle with kafirs.

N/WAZIRI MAKAMBA AVIPA CHANGAMOTO VIWANDA VYA CHAI BUMBULI.

October 30, 2013
Na Raisa Said, Bumbuli.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amevipa changamoto  viwanda vya chai vya Hekulu na Dindira kuongeza uzalishaji ili kuweza kuchukua majani ya chai kutoka kwa wakulima wa zao la chai wa Bumbuli ambao walikuwa wakihudumiwa na Kiwanda cha Mponde.

Hatua hiyo inatokana na kiwanda cha chai cha Mponde kufungwa kutokana na mgogoro baina yawakulima wa chai na Chama cha Wakulima wa Chai cha Usambara (UTEGA) na mwekezaji.

Makamba, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Bumbuli aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wakulima katika kijiji cha Tamota, kilichopo kata ya Tamota jimboni hapo, alisema hatua hiyo ni muhimu kwa kiwanda cha Mponde kilivyofungwa na viwanda hivyo viwili vikiongeza uzalishaji wakulima watapata mahali pa kuuzia majani ya chai na kujipatia kipato.

Alisema kuwa hivi sasa majani ya chai ni mengi hivyo hatua ya viwanda hivyo kuongeza uzalishaji ni nafuu kwa wakulima ikiwemo kuchangia kasi ya maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo.

Makamba alisema kuwa alikwisha kuzungumza na menejimenti za viwanda hivyo ili viongeze uzalishaji na vifaa vya kusafirishia chai kutoka mashambani hadi kwenye viwanda.

Alisema kuwa atavishauri viwanda hivyo kuweka utaratibu wa kuchukua majani ya chai mara tatu kila wiki kwa wakulima hao ili kukabiliana ongezeko hilo la majaniya chai.

Aliwataka wakulima kuwa wavumilivu wakati huu ambapo kuna mpango wa kuweka menejimenti ya muda kama ilivyokubaliwa na serikali ili kiwanda hicho kianze kazi ya kusindika majani ya chai.

Aliwataka viongozi wa UTEGA kuacha kuwatisha wakulima kwa kuwaambia kuwa watawakomesha kipindi hiki cha majani mengi ya chai na kwamba watahakikisha wanawapigia magoti ili kiwanda kifunguliwe.

PAMBANO LA YANGA, MGAMBO SHOOTING LAINGIZA MIL 37/-

October 30, 2013
Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mgambo Shooting lililochezwa jana (Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 37,915,000.

Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 46 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 walikuwa 6,515 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 5,783,644.07, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,145,790 wakati kila klabu ilipata sh. 8,550,741.95.

Wamiliki wa uwanja walipata sh. 4,347,834.89, gharama za mchezo sh. 2,608,700.93, Bodi ya Ligi sh. 2,608,700.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,304,350.47, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,014,494.81.

SIMBA, KAGERA SUGAR KUUMANA KESHO

October 30, 2013
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 kesho (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.

Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MWIDAU ATAKA KASI YA MAENDELEO TANGA.

October 30, 2013

Na Mwandishi Wetu, Tanga
MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kubadilika kwa kuwa na ari ya kujiletea maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa mjini hapa leo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (Tanga Press Club).

Alisema kuwa ili maendeleo ya haraka yaweze kupatikana katika mkoa huo ni lazima jamii kubadili kwa kuwa na mawazo chanya.

“Maendeleo ni jambo muhimu sana na katika hili ni lazima tushirikiane kwa dhati. 

Binafsi ninapenda kupongeza juhudi za chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya katika kutangaza mkoa wetu.

“Nilikuwa nasoma na sasa kila wakati tutakuwa pamoja na wanahabari pamoja na wananchi wa mkoa wetu ili kuweza kuungana kwa pamoja katika juhudi za maendeleo za mkoa,” alisema Mwidau
October 30, 2013
Mbunge Amina Mwidau akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga, kulia ni Mratibu wa chama hicho Neema Hatibu.

Mbunge Mwidau, akipata ufafanuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga, Hassan Hashimu.

ZIARA YA MBUNGE AMINA MWIDAU WILAYANI PANGANI.

October 30, 2013
Mbunge Amina Mwidau, akihutubia wanannchi wa Wilaya ya Pangani katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Mkoa wa Tanga.

Mbunge Mwidau akiwa na Ofisa Utamaduni na Michezo wa Wilaya ya Pangani, Kemmy Anatory mara baada ya kuzindua mashindano ya Mwidau CUP.




Mbunge Amina Mwidau, akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa Timu ya soka ya wanawake ya Spin Sister, Habiba Hamisi. Timu hiyo ipo Marizala Pongwe jijini Tanga.