TFF, KTA ZAZINDUA PROGRAMU YA MAENDELEO YA SOKA KWA WANAWAKE

TFF, KTA ZAZINDUA PROGRAMU YA MAENDELEO YA SOKA KWA WANAWAKE

February 23, 2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Taasisi binafasi ya Karibu Tanzania Association (KTA) kwa pamoja wamezindua programu ya maendeleo ya soka kwa wanawake vijana ili kuhamasisha usawa wa kijinsia, uwezeshaji kijamii na kiuchumi kwa wanawake nchini itakayofadhiliwa na Shirika la Forum Syd kutoka nchini Sweden.
Uwekaji saini wa mkataba huo wa ushirikiano umefanywa na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mia Mjengwa Bergdahl, Mratibu wa Programu hiyo kutoka taasisi ya Karibu Tanzania Sweden katika ofisi za TFF zilizopo Karume.
Programu hiyo ni ya aina yake ambayo haijapata kufanyika nchini inalenga kujenga mfumo utakaotumiwa nchi nzima katika kutoa elimu na mafunzo kwa soka la wanawake kwenye maeneo ya ufundi (makocha), waamuzi (refarii), uongozi na tiba kwenye michezo.
Pia itawezesha kuendeleza vipaji kwa wachezaji wanawake vijana na kuongeza hali ya kujitambua na kujiamini kwa walengwa. Lengo ni kuongeza idadi ya wachezaji wenye ubora na viwango kwa soka la wanawake vijana katika ngazi zote, hivyo kuifanya programu hii kuwa nyenzo katika kuwawezesha wanawake.  
Kwa kuanzia kozi 20 za soka la wanawake vijana kwenye Vyuo 20 vya maendeleo ya wananchi zitaanzishwa kwenye kanda saba.  Jumla ya wanawake vijana 600 ikiwamo 30 kutoka katika kila chuo cha Maendeleo ya Wananchi watashiriki.
Katika programu hii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wanashiriki kikamilifu kwa kuwezesha wanafunzi na miundo mbinu ya vyuo vya maendeleo ya wananchi vilivyo chini ya wizara hiyo kutumika katika kufanikisha programu hii.
Mafunzo yatatolewa sambamba na mafunzo mengine ya kawaida yanayotolewa kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi, kama vile maarifa ya jumla na mafunzo ya ufundi.

VODACOM TANZANIA KUPITIA PROGRAMU YA PAMOJA NA VODACOM WATOA MSAADA WA MASHINE YA KUDURUSU KARATASI SHULE YA SEKONDARI SHIMBWE

February 23, 2016
Mkuu wa Shule ya Sekondari Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini,Jacob Costantine akimueleza jambo Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaksakazini,Henry Tzamburakis alipofika shuleni hapo kwa ajili kukabidhi mashine ya kisasa ya kuduru karatasi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom imekabidhi kwa shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilaya ya Moshi vijijini ,msaada wa mashine yenye uwezo wa kufanya kazi zaidi ya tatu ikiwemo kudurusu karatasi.


Msaada wa mashine hiyo (Photocopier) yenye thamani ya zaidi ya sh Mil 12 ni sehemu ya msaada wa vifaa mbalimbali ambavyo kampuni hiyo kupitia mradi wa “Pamoja na Vodacom” imekabidhi shuleni hapo zikiwemo Kompyuta mpakato 30.


Mbali na msaada wa Kompyuta na Mashine hiyo kampuni hiyo pia ilitoa wataalamu kutoka shirika lisilo la kiserikali la Learning  in Sync kwa ajili ya kuweka program maalumu katika kmpyuta za kufundishia na kujifunzia .


Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis alisema kutolewa kwa mashine hiyo ni muendelezo wa msaada ambao Vodacom kupittia mradi wa Pamoja na Vodacom imeendelea kutoa kwa nchi nzima.


“Huu ni muendelezo wa msaada ulitolewa awali ,Kampuni ya Vodacom tunarudisha sehemu ya faida kwa wananchi na wateja wetu,pamoja na hayo ni kusaidia wadogo zetu kuingia katika digitali wakiwa na umri mdogo na kuwaandaa na maisha ya baadae,”alisema Tzamburakis.


Alisema Mashine hiyo ya kisasa itasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zikiikabili shule hiyo hususani katika maandalizi ya mitihani pamoja na machapisho mengine ambayo shule ili lazimika kuingia gharama kubwa kuchapisha.


Katika kuhakikisha walimu wa shule hiyo wanaweza kutumia vyema mashine hiyo Tzamburakis alisema ofisi ya Vodacom kanda ya Kaskazini itatoa mtaalamu kwa ajili ya kufundisha namna ya kuitumia.


“Ofisi ya kanda ya Vodacom ina wataalamu wa IT ambao watasaidia katika kutoa mafunzo kwa walimu ya namna ya kutumia mashine hizi na tutaweka utaratibu wa kufika mara moja kwa mwezi katika shule hii ili waweze kubadilishana uzoefu na walimu wa masomo hayo.”alisema Tzamburakis.


Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Shimbwe,Jacob Costantine aliishikuru kampuni ya Vodacom kwa msaada huo huku akieleza changamoto zilizoikabili shule hiyo ikiwemo ya kuchapisha mitihani kwa gharama kubwa .


“Tumepewa mashine ya Photocopy ikiwa ni ahadi ya mgeni rasmi kutoka Vodacom baada ya kumueleza kuwa tumekuwa tukitumia gharama kubwa hasa kipindi cha mitihani ,kuchapisha mitihani yetu ya mihula na ile ya mwisho wa mwaka”alisema Costantine.


Alisema kupatikana kwa mashine hiyo ,sasa shule itakuwa na uwezo mkubwa wa kuchapisha machapisho mbalimbali vikiwemo vitabu ambavyo upatikanaji wake umekuwa mgumu kwa ajili ya wanafunzi hao kujifunzia.


Mkuu huyo wa shule alisema wamekuwa wakitumia zaidi ya shilingi Milioni nne kwa ajili ya maandalizi ya mitihani shulebi hapo na kwamba kwa sasa adha ya kuandika ubaoni mitihani ya majaribio itatoweka.


Mwisho.

HILI NALO NI JIPU LASUBIRIWA KUTUMBULIWA:: TANESCO YAPUUZIA WITO WA WANANCHI, KUHUSIANA NA NGUZO HATARISHI

February 23, 2016
Wananchi wa Eneo la Tegeta Nyuki Jijini Dar es Salaam wamelilalamikia Shirika la TANESCO kushindwa kutatua Kero ya Nguzo ambayo inahatarisha Maisha ya wakazi Hao katika eneo hilo kwa zaidi ya Miaka 8 hivi sasa, nguzo hiyo imesogelea Kibanda cha Biashara na kusababisha hali ya Sinto fahamu kufuatia usalama wao.

Uzembe wa Nani?

Wakizungumza na Mtandao huu wakazi wa Eneo hilo wamedai yakuwa Taarifa walisha peleka katika sehemu husika lakini Hadi leo hii ni mwaka wa Nane Bila ya Mafanikio.
Uzembe wa Nani?
Mwaka 2008 wakazi hao waliiandikia Tanesco Barua ya kufanya Marekebisho ya Kuomba Kuondoa Mstimu huo lakini hadi leo Mamlaka hiyo haijafanya hivyo, Ila Mwaka 2015 mwishoni Tanesco ilifika eneo la tukio na kuangalia tu na kuondoka bila ya kufanya Marekebisho yoyote.
Uzembe wa Nani?
Je kwa hali hii Tunangojea Maafa au Hasara Itokee Ndio tukimbilie? Tunaiomba Mamlaka Husika Iweze Kuchukua Hatua za Haraka kurekebisha hili kabla ya Maafa hayajaweza Kutokea.
Fungwa S.Kilozo Founder of Lindiyetu.com & Kickzacelebrity.blogspot.com P.o.Box 285, Lindi, Tanzania Mob.+255787572019 OR +255713572019 Email: fkilozo@gmail.com or lindiyetu@gmail.com