WATOTO WAUAWA KWA BOMU SUDANI YA KUSINI.

October 17, 2013
Watoto watano wameuawa kwa bomu wakati walipokuwa wakichimba chuma chakavu katika eneo la mji mkuu wa Juba, Sudan Kusini.
 
Watoto hao walikuwa wakitafuta vyuma hivyo katika eneo la makazi ya zamani wanajeshi, msemaji wa Jeshi ameiambia BBC.
 
Mwandishi wa Habari wa BBC James Copnall amesema baruti ambazo hazijalipuka kwenye migodi bado ni tatizo kubwa Sudan Kusini kufuatia miongo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kuna operesheni maalum ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Sudan Kusini, lakini milipuko imekuwa ikiua watu kila mwaka.

Watoto wenye umri kati ya miaka 10 na 14 wameuawa katika eneo la makazi ya wanajeshi ya zamani katika wilaya ya Souk Sita katika mji wa Juba, msemaji wa Jeshi Kanali Philip Aguer amesema.
Amesema raia wa Uganda aliyekuwa pamoja watoto hao akitarajia kununua vyuma hivyo chakavu naye amejeruhiwa.

Sudan Kusini ilipata uhuru mwaka 2011 baada ya muda mrefu wa migogoro na Sudan na kubakia miongoni mwa mataifa maskini sana duniani.

USAFIRI KIKWAZO KITUO CHA KUTUNZIA WAZEE CHA MWANZANGE.

October 17, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga. 
UKOSEFU wa Usafiri katika makao kwa ajili ya kuwapeleka wazee sehemu mbalimbali ikiwemo hospitalini ni miongoni mwa changamoto zinazokikabili kituo cha kutunzia wazee cha Mwanzange jijini Tanga.
 
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii katika kituo hicho,Clara Kibanga wakati akisoma taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Tanga ,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa ambaye alikwenda kituo hapo kukabidhi zawadi za sikuu ya Eid Al Hajj kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanga,Jakaya Mrisho Kikwete.

Kibanga licha ya kukabiliwa na changamoto hiyo lakini pia kuna ukosefu mkubwa wa madawa katika kituo hicho hasa pale wanapopata dharura kwa mgonjwa anayehitaji huduma ya haraka au dawa zinapokosekana katika hospitali za serikali na hivyo hulazimika kuzinunua.

Ameongeza kuwa changamoto nyingine ni uhaba wa vitanda kutokana na kuwa vilivyopo vimechakaa na ni vya muda mrefu.

Akizungumzia mafanikio ya kituo hicho,Kibanga amesema wamefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa ombaomba kwa wazee licha ya kutofanikiwa kulimaliza kabisa.

Kituo hicho cha kuwahudumia wazee Mwanzange  kilianzishwa mwaka 1950 na wakoloni wa kiingereza kwa ajili ya kuwatunza wazee ambao walikuwa wafanyakazi (manamba)katika mashamba ya mkonge na chai.

AMUUA MKEWE NAYE KUJIUA.

October 17, 2013
Na Oscar Assenga,Handeni.
MKAZI wa Kijiji cha Kwedichocho wilayani Handeni mkoani Tanga Aweso Athumani (38) amemuua mkewe Saumu Athumani (24) kwa risasi naye kujiua kwa kujipiga risasi kisongoni kwa kutumia bunduki aina ya Gobole tukio ambalo limeacha simanzi kwa wakazi wa eneo hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constatine Massawe alisema tukio hilo limetokea octoba 16 mwaka huu majira ya saa kumi na moja asubuhi wakati wakiwa nyumbani kwao ndipo alipofanya tukio hilo na kukimbilia msituni.
Massawe alisema baada ya kukimbia msituni na ndipo alipofanya tukio hilo la kujiua mwenyewe kwa kujipiga risasi shingoni na baadae wananchi walipokwenda eneo hilo waliuona mwili wake na kutoa taarifa kuhusu tukio hilo.
Kamanda Massawe alisema baada ya polisi kufika eneo la tukio wakauchukua mwili huo na kuufanyia uchunguzi wakagundua wamepigwa risasi na kuwakabidhi ndugu zao kwa ajili ya taratibu za mazishi.

WAHAMIAJI HARAMU 32 WAKAMATWA TANGA.

October 17, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Tanga imewataka wahamiaji haramu 32 ndani ya kipindi cha wiki mbili ambao waliingia mkoani hapa kinyume cha sheria
 

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Sixtus Nyaki amesema tukio la kwanza lilitokea septemba 25 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili asubuhi wakati maafisa wa idara hiyo wakiwa kwenye doria walikamata wahamiaji haramu kumi raia wa Ethiopia.

Nyaki alisema raia hao walikamatiwa katika eneo la kange nje kidogo ya jiji la Tanga na kufanyiwa mahojiano ambapo ilibainika kwamba waethiopia hao waliingia nchini wakitokea nchi jirani ya Kenya na walisafiri kwa kutumia boti lililopita bahari ya hindi mpaka maeneo ya sahare jijini hapa.
 

Ofisa uhamiaji huyo aliwataja wahamiaji haramu hao kuwa ni Ayano Tamrat Shanko,Abraham Tafara Dobuse,Yonas Ayala Dolaso,Salamu Zalaka Wondu,Tamasgen Yohans Herano,Tasfahun Qalbiso Angore na Dababa Dante Handiso ambao wote kwa pamoja wanatuhumiwa kwa kosa la kuingia nchini kinyume na sheria ya uhamiaji.
 

Nyaki alisema uchunguzi bado unaendelea ili kubaini boti lililotumika na watu waliohusika kuwasaidia wahamiaji haramu kuingia nchini.

Hata hivyo alieleza taratibu za kuwafikisha mahakamani zitachukuliwa dhidi ya wahamiaji haramu waliokamatwa ambapo alisema zoezi hilo litakuwa endelevu na kutoa wito kwa wananchi na raia wema kutoa taarifa pindi wanapowaona au kuwatilia mashaka watu wa namna hiyo.
 

Alisema wahamiaji haramu wengine 22 walikamatwa Octoba 9 mwaka huu eneo la kisiwa cha kirui kilichopo kilomita 10 kutoka kijiji cha jasini wilayani Mkinga majira ya saa kumi na mbili jioni.

Alieleza wahamiaji haramu hao walitokea Mombasa, Kenya kwa kutumia njia ya majini wakiwa na lengo la kwenda Afrika kusini ambapo taratibu wa kuwafikisha mahakamani zinaendelea.

MASHABIKI WAWATAKA VIONGOZI WA VILABU VYA JAMHURI NA KIZIMBANI KUBAKI LIGI KUU

October 17, 2013
Na Masanja Mabula -Pemba .
Hatimaye mashabiki wa vilabu vya Jamhuri na Kizimbani zote za mjini Wete, wamevunja ukimiya na kuuomba uongozi wa timu hizo kupanga mikakati itakayoziwezesha timu hizo kubakia kwenye michuano ya ligi kuu ya Zanzibar msimu ujao .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti , wamesema kuwa mwenendo wa timu hizo kwenye ligi kuu ya Zanzibar inayoendelea sio wa kuridhisha , jambo ambalo limezifanya timu hizo kushika nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi hiyo .

Aidha wameongeza kwamba huwenda  Mji wa Wete kukosa timu inayoshiriki ligi kuu msimu ujao  , endapo hatua za makusudi hazitrachukuliwa na viongozi wa timu hizo kwa kuweka mikakati madhubuti pamoja na kufanya usajili wakati wa dirisha dogo .

" Hii itakuwa ni aibu kwa Mji wa Wete kukosa timu ya kushiriki ligi kuu , na lwamba viongozi wa vilabu hivyo wanapaswa kufanya usajili wakati wa dirisha dogo litakapofunguliwa " alisisitiza shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina Omar Juma .

Wameeleza kwamba klabu hizo ambazo zinawawakilisha wananchi wa Mji wa Wete na Wilaya hiyo kwa ujumla , ambapo mikakati ya makusudi inahitajika ili kunusuri timu hizo kushuka daraja .

Kombo Said shabiki wa Timu ya Jamhuri alisema kuwa wanashangaa kuona timu yao imekuwa kichwa cha mwendawazimu tofauti na ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma ambapo ilikuwa tishio kwa vilabu vya ligi kuu Zanzibar .

"Matatizo ya timu yetu kufanya vibaya yamechangiwa na viongozi wetu kwa kukubali kuwatoa wachezaji zaidi ya sita wa kikosi cha kwanza na wao kushindwa kusajili wachezaji wa kuweza kuziba nafasi hizo " alieleza Kombo  .

Hata mmoja wa Viongozi wa Klabu ya Jamhuri ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema kuwa uongozi umekusudia kuvunja benki na kufanya usajili wa kutisha wakati wa dirisa dogo pindi likifunmguliwa .

Aliwatoa hofu mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo ,kuondoa wasiwasi na kwamba timu itaendelea kubaki kwenye ligi kuu Zanzibar kwani mapengo yalijitokeza katika kipindi hichi tayari wamo katika kuyapatia ufumbuzi.