WANAFUNZI UTUMISHI WATOA MISAADA KWENYE KITUO CHA KULELEA WAZEE WASIOJIWEZA CHA MWANZANGE

March 29, 2018


Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Jijini Tanga Elibariki Mushi wa pili kutoka k ulia ni akimkabidhi vyakula na vifaa Afisa Mfawidhi Makao ya Wazee Wasiojiweza Mwanzange Jijini Tanga Otilia Chilumba kutoka kwa wanafunzi wa chuo cha utumishiwa Umma tawi la Tanga ikiwa ni mkakati wa kusaidia jamii isiyojiweza kulia ni mratibu wa zoezi hilo Dastan Kingalu

Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Jijini Tanga Elibariki Mushi wa pili kutoka kulia ni akimkabidhi mbuzi mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho kwa niaba ya wenzake


CHUO cha Utumishi wa Umma Tawi la Tanga kimetoa msaada kwenye kituo cha kulelea wazee wasiojiweza cha Mwanzange Jijini Tanga ikiwa ni mpango wao wa kuona namna ya kusaidia jamii inayokabiliwa na changamoto mbalimbali.

Msaada uliokabidhiwa ni mchele kg 500, unga kg 300, sukari mifuko 2 kg100,sabuni ya unga mifuko 3,sabuni ya maji box 10,sabuni ya kuogeakatoni 2,maharagwe kg 100,chumvi katoni 10,mbuzi wawili.

Vitu vyengine ambazo vilikabidhiwa ni majani ua chai katoni 2,dagaa kg10,ngano kg 50,miswaki katoni 5,dawa za meno katoni nne,mafuta yakula ndoo tatu na mafuta ya kupikia katoni 10 vyote vina thamani yash.milioni 2.2.

Akizung umza wakati wakikabidhi msaada huo ,Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma JijiniTanga Elibariki Mushi aliwataka wanafunzi wajifunze taaluma hiyokatika mtazamo mpana ambao utawasaidia kuwajenga katika nyanja yakutatua changamoto zinazozikabili jamiihusika.

Mushi alisema mbali na wanafunzi hao ku jifunza mambo mbalimbali yauga vi na utawala pia wanaowajibu wa kuona umuhimu wa kujali jamii hasazile zinazoishi katika mazingira magumu.

“Tunaimani wanafunzi wetu wanajifunza masuala ya kuutumikia um ma lakini lazima wajikite kuangalia uhalisia halisi katika jamii zetuzinazotuzunguka na tukifanya hivyo tunaweza kuzifikia malengo yakuzisaidia jamii zilizo katika maisha duni”Alisema.

Aidha alisema swala la maadili lipo katika mitaala ya masomo yao hivyolazima wanafunzi hao wajifunze kivitendo kusaidia jamii h itajikaambapo walijitolea kupitia michango yao kwa kujitolea vyakula.

Awali kziungumza mara baada ya kupokea msaada huo,Afisa Mfawidhi Makao ya Wazee Wasiojiweza Mwanzange Jijini Tanga Otilia Chilumba aliwashukuru huku akiwataka kuwa makini kwa kuzingatia masomo ili waweze kupata manufaa kwenye maisha yao
“Ndugu zangu niwaambieni kuwa ujana ni maji ya moto tuutumie vizuri lakini pia acheni kukataa mimba mnazowapa wasichana mtoto utakayemzaandie anaweza kuja kukuokoa baadae “Alisema.

“Wapo baadhi ya wazee walishawahi kunililia walikwisha kuwate lekeza watotowao ndio sababu za kuwepo kwenye kambi za kulea wazee hivyo niwasihiacheni kuwakataa kwani mnaweza kukumbana na changamoto mbeleni

Alieleza pia sababu za baadhi ya wazee wengi kuishi maisha ya t a bu na kulazimika kulelewakwenye vituo maalumu imeelezwa kuchangiwa na baadhi yao kuwakanawatoto wao jambo ambalo linawapelekea kujikuta wakiingia kwenyechangamoto za namna hiyo.

Hatua hiyo inat ajwa kuwapa majukumu mazito wasichana ambao wamekuwaw akikumbana na kadhia hiyo ambao kwa asilimia kubwa wanakuwa wakiishikwa manunguniko.

MZUKA WA SOKA NA COKA YAWAFIKIA KANDA YA KASKAZINI

March 29, 2018


Baadhi ya shehena ya zawadi za pikipiki watakazojishindia wateja.



Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers, Chris Loiruk akiongea na wafanyakazi wakati wa uzinduzi wa promosheni.

Wafanyakazi wa Bonite wakisherekea kuzinduliwa kwa promosheni.
Baadhi ya wafanyakazi wa Bonite wakiandamana katika mitaa ya mji wa Moshi wakati wa uzinduzi *Kuangalia mashindano ya kombe la Dunia wakiwa majumbani kwao Wakati mashindano makubwa na maarufu ya soka ya Kombe la Dunia 2018 yanakaribia kuanza, kampuni ya Coca-Cola kupitia kampuni kiwanda cha Bonite Bottlers, imezindua promosheni kubwa itakayowawezesha watumiaji wa vinywaji yake kujishindia luninga bafa za kisasa (flat screen TV sets) zinakazowawezesha kufurahia mashindano ya soka ya Kombe la Dunia wakiwa wakiwa na familia zao majumbani kwao. Promosheni hii mpya inajulikana kama “Mzuka wa Soka na Coka” na itanufaisha watumiaji wa vinywaji vinavyotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola ambavyo ni Coca-Cola, Sprite, Fanta, Sparletta, Schweppes Stoney Tangawizi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida. Mbali na kujishindia luninga bapa za kisasa watumiaji wa vinywaji vya Coca-Cola kupitia promosheni hii wanayo fursa ya kujishindia zawadi kubwa ya pikipiki, fedha taslimu kuanzia shilingi 5,000/- hadi shilingi 100,000/- ikiwemo pia kujishindia soda za bure. Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers, Chris Loiruk, amesema kampuni ya Coca-Cola ikiwa ni mdhamini mkuu wa mashindano yajayo ya Kombe la Dunia ,imewaandalia promosheni hii wakazi wa kanda ya Kaskazini ili kuhakikisha wanafurahia “Mzuka wa Soka na Coka” wakiwa majumbani kwao kupitia luninga za kisasa wakati huohuo wakiburudika na vinywaji vya Coca-Cola. “Tukiwa wadhamini wakuu wa mashindano ya Kombe la Dunia yatakayoanza mwezi June mwaka huu tumeona kuna umuhimu wa kuwaletea wateja promosheni itakayowaunganisha na kufurahia mashindano haya makubwa duniani kupitia kunywa zetu.Zawadi za ushindi zitakuwa zinapatikana katika ganda lililopo chini ya kizibo” Kwa upande wa zawadi kubwa za pikipiki,alisema anachotakiwa kufanya mywaji wa soda ni kukusanya maganda matatu ya chini ya vizibo yanayoonyesha sehemu 3 za pikipiki, yapo yanayoonyesha sehemu ya mbele, sehemu ya kati na sehemu ya nyuma ambayo yakiungaishwa yanaonyesha picha halisi ya pikipiki “Katika promosheni hii zawadi ya soda za bure zitatolewa madukani na zawadi za fedha taslimu, luninga na pikipiki zitakabidhiwa kwa washindi kutoka ofisi za kampuni ya Bonite,” Alisema, Chris Loiruk. Meneja wa chapa ya Coca-Cola nchini Tanzania, Sialouise Shayo, alisema promosheni hii imelenga kuwaandaa washabiki wa soka nchini kujiandaa kufurahia mzuka wa kombe la Dunia na kufurahia mashindano haya pindi yatakapoanza.

MAXCOM AFRICA PLC - Maxmalipo Kuendelea kutoa Huduma za Malipo Kielektroniki, kupitia Mfumo wa serikali wa malipo Kielektroniki (GePG) Ikiwamo huduma ya LUKU

March 29, 2018


photo Best Regards Krantz Mwantepele|Managing Director KONCEPT ROGECH ANIMATIONS STUDIO Mikocheni B, House No 58. Adjacent Clouds Media. Dar es Salaam, Tanzania | M: + 255 624053989 / +255 658123310 Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com W: www.koncept.co.tz IMAGINE INSPIRE INFLUENCE

AGPAHI YAKUTANA NA WADAU WA VVU NA UKIMWI MKOA WA MWANZA

March 29, 2018



Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limeendesha kikao cha wadau wanaohusika katika mapambano ya VVU na Ukimwi mkoani Mwanza kwa ajili ya kujadili na kupanga mikakati ya kupambana na Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi mkoani humo.

Kikao hicho cha siku mbili kilichoandaliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC), kimefanyika Machi 27,2018 hadi Machi 28,2018 katika ukumbi wa Gold Crest jijini Mwanza.

Miongoni mwa wadau waliohudhuria kikao hicho ni waratibu wa Ukimwi ngazi ya mkoa na wilaya,wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri,waganga wakuu wa wilaya,waratibu wa afya ya uzazi na mtoto,waratibu wa kifua kikuu,mashirika,taasisi na wadau mbalimbali wanaofanya shughuli za kupambana na VVU na Ukimwi.

Akifungua kikao hicho,Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella alisema mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi yatafanikiwa tu endapo kila mdau atashiriki

“Sisi kama mkoa wa Mwanza ni wa pili kwa idadi kubwa ya watu baada ya Dar es salaam,lakini pia tupo wa pili kwa shughuli za uchumi, takwimu za mwaka 2011/2012 zinaonesha kuwa tulikuwa na maambukizi ya asilimia 4.2 lakini mwaka 2016/2017 maambukizi yamepanda hadi kufikia asilimia 7.2”,alieleza.

“Ili tushushe asilimia hizi kubwa za maambukizi lazima wadau wote tushirikiane katika mapambano dhidi ya Ukimwi kwa kuelekeza nguvu zaidi katika kundi la vijana ambalo linapata maambukizi ya VVU kwa kasi”,aliongeza Mongella.

Aidha alisema teknolojia na utandawazi inachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa maambukizi kwani vijana wanatumia vibaya mitandao ya mawasiliano na kusababisha kujiingiza katika tabia hatarishi zinazochongia kuwepo kwa maambukizi.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wadau wa afya mkoani humo likiwemo shirika la AGPAHI ambalo limekuwa msaada mkubwa katika sekta ya afya nchini,kuendelea kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema mkoa huo una takribani watu 90,000 wanaokisiwa kuwa na maambukizi ya VVU na bado hawajafikiwa.
Aliongeza kuwa shirika hilo lina mpango wa kuwafikia watu wapatao 37,900 kwa ajili ya kuwapatia huduma za tiba na matunzo watu wanaoishi na maambukizi ya VVU na Ukimwi (kutokana na takwimu za utafiti wa Tanzania HIV Impact Survey (THIS) 2016 – 2017).
ANGALIA PICHA WAKATI WA KIKAO



Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella akizungumza katika kikao cha wadau wa mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa. Kushoto ni Kaimu Mganga mkuu mkoa wa Mwanza Dk. Sylas Wambura. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella akiwasisitiza wadau wa afya kuungana katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella akilishukuru shirika la AGPAHI na Watu wa Marekani kupitia CDC kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.



Kaimu Mganga mkuu mkoa wa Mwanza Dk. Sylas Wambura akizungumza wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.

Wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya mkoa wa Mwanza wakiwa ukumbini.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akizungumza wakati wa kikao hicho na kueleza kuwa shirika hilo litaendelea kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU.


Mwakilishi wa Centres for Disease Control (CDC) nchini, Eva Matiko akizungumza katika kikao hicho. Wadau wa masuala ya VVU na Ukimwi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa kikao hicho.


Wadau wakiwa ukumbini.

Wafanyakazi wa shirika la AGPAHI mkoa wa Mwanza wakiwa ukumbini.

Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza, Dk. Pius Masele akizungumza katika kikao hicho.

Mkuu wa wilaya ya Magu, Hadija Nyembu akichangia hoja wakati wa kikao hicho kuhusu namna ya kupambana na maambukizi ya VVU.




Mratibu wa Ukimwi,Kifua Kikuu na Malaria kutoka TAMISEMI, Mbuuni akichangia hoja wakati wa kikao hicho.



Kikao kinaendelea...








Wadau wakiwa ukumbini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

JUMIA KUWAWEZESHA WATANZANIA KUMILIKI SIMU ZA KISASA KWA BEI NAFUU

March 29, 2018



Yapunguza bei za simu mpaka 60%!


Mteja kuunganishwa na kifurushi cha internet ya bure kutoka Tigo mpaka GB 18

Na Jumia Tanzania

Katika kuhakikisha kwamba kila mtanzania anamiliki simu za kisasa na kwa bei nafuu, Jumia inaendesha kampeni ya ‘Mobile Week’ ambayo itadumu mpaka Machi 30. Tofauti na kampeni zake zingine kama vile ‘Black Friday’ ambayo huwa inajumuisha mauzo ya bidhaa tofauti, wiki hii ni maalum kwa ajili ya mauzo ya simu pekee kwa gharama nafuu, ukizingatia sikukuu ya Pasaka ikikaribia.




Jumia inaamini kwamba sekta ya simu ina mchango mkubwa katika maendeleo ya watanzania kwa upande wa kijamii na kiuchumi. Kwenye karne hii yenye maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia, simu sio kifaa cha anasa tena kama ilivyokuwa awali bali ni nyenzo muhimu inayorahisisha maisha na shughuli za kila siku. Kwa mfano, hivi sasa simu hazitumiki tu kupata, kusambaza na kupashana habari bali pia hutumika kutuma na kupokea fedha, pamoja na kufanya malipo ya huduma mbalimbali kama vile umeme, maji, karo za shule, biashara, na hata uuzaji na manunuzi ya bidhaa.

Akielezea umuhimu wa kampeni hiyo kwa wateja na sekta nzima ya mawasiliano ya simu nchini, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Zadok Prescott amesema kuwa maendeleo ya ukuaji wa kasi ya kiuchumi nchini yameifanya sekta hiyo kuwa ni muhimu na yenye mchango mkubwa kwa ukuaji wa sekta nyinginezo pia.





“Hii ni kampeni ya kipekee kutokea nchini hususani katika mauzo ya bidhaa moja. Soko la simu limekuwa kubwa Tanzania likichochewa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa makampuni ya mitandao ya simu na yanayouza bidhaa hii. Changamoto kubwa ambayo Jumia tumeigundua na tungependa kuitafutia ufumbuzi ni upatikanaji wake kuwa wa ghali jambo ambalo si watanzania wote wanaweza kumudu. Lakini kupitia ‘Mobile Week’ wateja watajipatia simu za kisasa na mpya kabisa kwa bei iliyopunguzwa karibuni nusu yake. Bei ambayo ni nafuu na hauwezi kuipata hata ukienda kwenye maduka ya kawaida isipokuwa kwenye mtandao wetu pekee,” alifafanua Bw. Prescott.

“Lengo kuu la Jumia ni kubadili mtazamo na kujenga tabia ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao miongoni mwa watanzania wengi. Bado kuna idadi kubwa ya watanzania wanaamini kwamba manunuzi kwa njia ya mtandao sio salama. Tunataka kubadili dhana hiyo kwa sababu dunia ndipo ipo huko kwa sasa, ulimwengu wote umehamia kwenye mifumo ya mtandaoni. Kupitia njia hii wateja wataweza kuokoa muda na gharama ambazo wanaweza kuziwekeza katika shughuli zingine za kujenga taifa. Tunataka pia kubadili dhana kwamba kufanya manunuzi lazima iwe mwisho wa wiki. Kupitia mtandao wa Jumia sasa mtu yoyote anaweza kufanya manunuzi ya bidhaa anazozipenda na kuletewa mahali popote alipo bila ya kuathiri shughuli zake,” aliendelea kufafanua zaidi.




Katika ripoti iliyowasilishwa na Jumia siku za hivi karibuni ilibainisha kuwa watumiaji wa simu za mkononi pamoja na ueneaji wa mtandao wa intaneti inakuwa kwa kasi kubwa. Hivi sasa Tanzania, watumiaji wa simu za mkononi ni zaidi ya milioni 40, idadi ambayo ni sawa na asilimia 72 kwa ueneaji wake nchini. Kuongezeka kwa watumiaji hao kunaenda sambamba na ongezeko la watumiaji wa mtandao wa intaneti ambao kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya kuingia kwa simu za mkononi za kisasa. Watanzania wanaotumia intaneti kwa sasa wanafikia takribani milioni 23.

Miongoni mwa sababu za ukuaji huo ni pamoja na uwepo wa ushindani wa bei sokoni hivyo kupelekea bei kuwa nafuu. Kwa kuongezea, maboresho na ofa zinazotolewa na kampuni za mitandao ya simu kama vile huduma za intaneti zimekuwa ni kichocheo kikubwa kwa watanzania kumiliki simu za mkononi.




Akitoa wito kwa watanzania kuichangamkia ofa ya ‘Mobile Week,’ bosi wa kampuni hiyo inayojihusisha na manunuzi na uuzaji wa bidhaa mtandaoni, alihitimisha kwa kusema, “lengo la kampeni hii ni kuhakikisha kuwa watanzania wanaomiliki simu za mkononi wanaongezeka zaidi. Katika kulihakikisha hilo, tunawasihi wateja kuitumia wiki hii ipasavyo kwa sababu punguzo ni kubwa na kuna ofa kemkem kwenye mtandao wetu.”

MAONYESHO YA YOUNG SCIENTISTS TANZANIA (YST) 2018 KUFANYIKA MWEZI AGOSTI

March 29, 2018



Mwanzilishi Mwenza wa Young Scientists Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland.

Meza Kuu pamoja na wadhamini wa maonyesho hayo.


Mkurugenzi wa Karimjee Jinanjee Foundation (KJF), Yusuf Karimjee akizungumzia udhamini wao


Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) akizungumza kwenye mkutano huo.


Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland akizungumzia kazi za ubunifu na jinsi nchi yao inavyowawezesha wanafunzi waliofanya vizuri katika miradi yao.


Muonekano wa chumba cha mkutano huo.


Na Dotto Mwaibale

MAONYESHO ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatafanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwanzilishi Mwenza wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha alisema maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe moja hadi mbili mwezi huo.

"Wanafunzi wote wanaopenda kushiriki wanashauriwa kutuma kazi za miradi yao kwenda YST kabla ya tarehe 21 Aprili 2018" alisema Kamugisha.

Kamugisha alisema wanafunzi 200 watakaochaguliwa wataonyesha kazi za teknolojia na ugunduzi wa kisayansi kwenye onesho hilo la mwaka huu na kuwa na wanafunzi watakaochaguliwa watapewa mafunzo kutoka kwa washauri wa sayansi wa YST kuhusu namna ya kutengeneza kazi zao za kisayansi.

Alisema onesho hilo pamoja na mpango wa kuzitembelea shule na wanafunzi kuwapatia ushauri wa kisayansi vinawezeshwa na wadhamini wakuu wa YST ambao ni Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Karimjee Jinanjee Foundation (KJF)

"Tunapenda kuwashukuru wadhamini wetu tangu mwaka 2012. Mwaka huu wa 2018 KJF wameongeza kiwango cha udhamini na kuwa mmoja wapo wa wadhamini wakuu wa YST kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Alisema udhamini huo utaiwezesha programu ya YST kuwa endelevu na kuwawezesha vijana kufanya ubunifu na kufanya tafiti za kisayansi ili kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kamugusha aliongeza kuwa wanasayansi chipukizi wakaoshiriki onesho la YST mwaka huu kwa sasa wanaendelea kutengeneza kazi za miradi yao katika nyanja mbalimbali za kisayansi kama kemia, fizikia na hesabu, biolojia na ekolojia, saynsi ya jamii na teknolojia na kuwa kazi miradi nyingi zimejikita katika sekta ya afya,kilimo na usalama wa chakula, mawasiliano na usafirishaji, nishati,elimu, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema wanafunzi watakajituma na kufanya ugunduzi mzuri watazawadiwa pesa taslimu, medali, vikombe na uimarishaji wa maktaba ya shule yao kama ambavyo wamefanya kwa miaka sita iliyopita KJF watawazadia wanafunzi wenye ugunduzi mzuri zaidi zawadi za udhamini wa masomo ya chuo kikuu ili kuwawezesha kusoma masomo ya sayansi na teknolojia katika ngazi ya chuo kikuu.