MATOKEO VPL: AZAM FC, STAND UNITED ZAANZA KWA KISHINDO....MBEYA CITY FC YAKAZIWA SOKOINE

MATOKEO VPL: AZAM FC, STAND UNITED ZAANZA KWA KISHINDO....MBEYA CITY FC YAKAZIWA SOKOINE

September 20, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara Azam fc wameanza ligi kwa kishindo baada ya kuitandika Polisi Morogoro 3-1 katika mchezo wa ufunguzi wa msimu wa 2014/2015 uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Wagonga nyundo wa Mbeya, Mbeya City kama ilivyokuwa msimu uliopita, wameanza ligi kwa kutoa suluhu pacha ya bila kufungana (0-0) katika dimba lao la Sokoine jijini Mbeya dhidi ya JKT Ruvu.
Afisa habari wa Mbeya City, Dismas Ten amesema mechi ilikuwa ngumu kwa timu zote na matokeo hayo ni ya kawaida katika mpira, lakini benchi la ufundi litakaa chini kufanya marekebisho.
Katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, bao pekee la Ramadhani Pela limetosha kuipa ushindi wa 1-0 Mgambo JKT dhidi ya Kagera Sugar iliyosafiri kutoka Kaitaba.
Kikosi cha Mbeya City fc

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Antony Mgaya amesema kuwa wamefurahishwa na ushindi huo licha ya kupata upinzani wa kutosha, hivyo wanajipanga kwa mechi ijayo ili kuendeleza wimbi la ushindi.
Katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Tanzania Prisons ‘Wajelajela’ wamewatandika wenyeji wa uwanja huo, Ruvu Shootings mabao 2-0.
Huko Kambarage mkoani Shinyanga, Stand United wakiwa nyumbani wametandikwa mabao 4-1 na Ndanda fc kutoka mkoani Mtwara.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Ndanda fc walikuwa mbele kwa mabao 3-1 na kipindi cha pili wakaongeza bao la nne.
Katibu mkuu wa Ndanda fc, Seleman Kachele amesema walitawala mchezo huo na ni mwanzo mzuri kwao.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi moja kupigwa ili kukamilisha mzunguko wa kwanza ambapo wekundu wa Msimbazi Simba watakuwa nyumbani uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuivaa Coastal Union.

KAGERA YACHARAZWA BAKORA HADHARANI.

September 20, 2014


NA SAFARI CHUWA,TANGA.

TIMU ya Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa mkoani Tanga leo wameanza vema michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kuibamiza Kagera Sugar bao 1-0,mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.
 
Mchezo ambao ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa zamu ambapo Mgambo shooting walianza kucheza kwa umakini mkubwa ambao uliwawezesha kufanikiwa kaundika bao la kwenye dakika ya 14 likifungwa na Ramadhani Pera aliyepiga mpira umbali wa mita 40 na kumshinda mlinda mlango wa Kagera Agatony Anthony  na kutinga wavuni.


Baada ya bao hilo Mgambo waliweza kuendeleza wimbi la mashmbulizi langoni mwa Kagera lakini bahati ya mabao ilikuwa sio yao kutokana na wachezaji wake kupata nafasi za wazi na ksuhindwa kuzifanyia kazi.

Mpaka timu zote zinakwenda mapumziko matokeo yalisomeka 1-0 ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake lakini hali haikuweza kubadilika.


Bila shaka Kagera wanapswa kujilaumu kutokana na kutokuwa makini kwenye mechi hiyo hali iliyopelekea kukosa penati ya wazi dakika ya 36 kupitia Abubakari Mtiro baada ya mchezaji wa Mgambo shooting Mohamed Nampokwa kuunawa mpira eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Kenedy Mapunda kutoka dar kuamuru penati.


Ki ujumla mgambo waliweza kuutawala mchezo huo kwa kucheza vema kuanzia mwanzo mpaka mwisho jambo ambalo linaonyesha maandalizi mazuri yaliyoyafanya kuelekea mechi hiyo.

Mwisho.

MGAMBO SHOOTING YAIBAMIZA KAGERA SUGAR BAO 1-0,MKWAKWANI.

September 20, 2014
WACHEZAJI WAKISALIMIANA

KIKOSI CHA MGAMBO SHOOTING KILICHOIBAMIZA KAGERA SUGAR BA0 1-0 MKWAKWANI LEO BAO LIKIFUNGWA NA RAMADHANI PERA DAKIKA YA 14 BAADA YA KUPIGA SHUTI KALI UMBALI WA MITA 40 NA KUTINGWA WAVUNI.



WACHEZAJI NA MASHABIKI WA MGAMBO SHOOTING WAKISHANGILIA USHINDI HUO.

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AZINDUA BODI MPYA YA USHAURI WA UONGOZI WA HOSPITALI BINAFSI NCHINI

September 20, 2014


                                                                Dotto Mwaibale

SERIKALI imesema itaainisha ukomo wa tozo kwa kila huduma inayotolewa kwa kila ngazi ya kituo cha huduma ili kudhibiti gharama za huduma za afya nchini.

Kauli hiyo ilitolewa  na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid Dar es Salaam wakati akizindua bodi mpya ya ushauri ya Hospitali binafsi nchini.

Dk. Rashid alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kuhusu huduma zinazotolewa na hospitali hizo hivyo hatua hiyo itasaidia kuboresha mfumo na kuwatendea haki wananchi wanaotumia vituo  vya kutolea huduma za afya.

"Malalamiko haya ni pamoja na huduma zisizo na ubora unaotakiwa na gharama zinazotolewa kwa huduma hizo .Sheria iliyopo inatutaka kudhibiti bei ya huduma hizi kwa kuzingatia malalamiko haya pamoja na matakwa ya sheria yenyewe," alisema Dk. Rashid.

Hata hivyo alibainisha kuwa licha ya kuwepo wa changamoto hizo huduma zinazotolewa na hospitali za watu binafsi zimechangia katika mafanikio  yaliyopatikana katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Kuhusu bodi hiyo Dk .Rashid aliwataka wajumbe wapya wa bodi hiyo kufanya vikao vya mara kwa mara vinavyolenga uboreshwaji wa utoaji wa huduma.Na kuwataka kuendeleza utaratibu wa kusajili vituo vipya na kufupisha usajili kwa kutmia muda mfupi  kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Alibainisha kuwa wajumbe wa bodi ya awali iliyosimamiwa na Mwenyekiti Dk. Deo Mtasiwa imesaidia kuboresha uwajibikaji wa wahusika hivyo kuboresha huduma na imeokoa maisha ya wananchi wengi ambayo yangekuwa hatarini endapo bodi isingetekeleza majukumu yake ipasavyo.

Alitaja wajumbe wa bodi mpya kuwa ni Dk.Donan Mbando ambaye ni Mwenyekiti, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa mbeya Dk. Mpoki Ulisubisya, Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando Profesa Chalres Majinge, Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi (NHIF), DK. Frank Lekey.


Wajumbe wengine ni Mkurugenzi Msaidizi- Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba Dk. Sijenunu Aaron, Mkurugenzi wa Association of Private Health Facilities (APHTA), Mwakilishi wa Mkurugenzi, Christian Social Services Comission (CSSC), Dk.Jane Kahabi na Mwanasheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Onorious Njole.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo iliyomaliza muda wake na mpya wakati akizindua bodi hiyo Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa bodi mpya, Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey  akitoa neno la shukurani. Kushoto ni Naibu Msajili Hospitali Binafsi Dk.Mahewa Lusinde na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Mpoki Ulisubisya.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),akimkabidhi cheti cha utumishi wa bodi hiyo,Profesa Bakari Lembariti. Katikati ni Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk.Donan Mmbando. Vyeti hiyo walitunukiwa wajumbe wote waliomaliza muda wao.
 Wajumbe wa Bodi mpya wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Mpoki Ulisubisya, Mwanasheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Onorius Njole, Mkurugenzi Association of Private Health Facilities-APHTA na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi-Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba, Dk.Sijenunu Aaron.
 Wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake. Kutoka kulia ni Profesa .Bakari Lembariti, Profesa Charles Majinge, Dk.Edda Vahahula, Dk.Jane Kahabi na Dk.Eliuter Samky.
 Mkutano ukiendelea.
 Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara hiyo, Dk.Margareth Mhando na Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki na Ubora, Dk.Mohamed wakiwa kwenye mkutano huo.
 Katibu wa Bodi hiyo, Dk.Pamella Sawa akizungumza katika mkutano huo.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi-Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba, Dk.Sijenunu Aaron akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Vituo vya Umama na Binafsi na Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali Binafsi Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Ruth Suza.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya.

MIAKA 14 TAJI LA LIGI KUU BARA HALIJANG’OKA ARDHI YA DAR, MSIMU WA 51 MAMBO YATAKUWAJE?

September 20, 2014

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
HATIMAYE michuano mikubwa kabisa ya soka nchini, ijulikanayo kama Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inarejea tena kwa mara ya 51 tangu ilipoanzishwa mwaka 1965 kwa wigo finyu na hali dunia kabisa, ikishirikisha klabu za Dar es Salaam pekee. Naam, msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), unatarajiwa kuanza Jumamosi ya leo, timu 14 zikijitupa dimbani kuwania pointi za mwanzoni, katika mbio za kusaka ubingwa wa ligi, unaoshikiliwa na Wana Jangwani, Yanga SC.  Historia ya ligi hiyo inaanzia mwaka 1929 ilipoanzishwa kifukara, tu kwa sababu ya mapenzi ya watu na soka wakaamua kuungana na kuanzisha michuano ya kutafuta bingwa, ingawa ni timu za Dar es Salaam pekee zilizokuwa zikishiriki wakati huo.
Mabingwa; Azam FC wakiwa na taji lao baada ya kutwaa msimu uliopita. Je, wataweza kulitetea?
Kufika mwaka 1965, ilianzishwa michuano ya Klabu Bingwa Tanzania, ambayo ilikuwa inaanzia ngazi ya Wilaya, ikichezwa kwa mtindo wa mtoano, ingawa pia katika miaka miwili ya mwanzoni, timu za Dar es Salaama pekee ndizo zilizoshiriki. Katika mfumo huo, bingwa wa kwanza ilikuwa ni klabu ya Sunderland ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba SC ya Dar es Salaam, ambayo ilifanikiwa kutetea ubingwa wake msimu uliofuata, kabla ya kuutema kwa Cosmopolitan ya Dar es Salaam pia mwaka 1967.
SERENGETI FIESTA IRINGA JANA USIKU NI SHANGWE ZA KUTOSHA

SERENGETI FIESTA IRINGA JANA USIKU NI SHANGWE ZA KUTOSHA

September 20, 2014

Wakazi wa Iringa usiku wa September 19 walipata burudani ya shangwe za Serengeti Fiesta 2014 iliyofanyika katika viwanja vya Samora mjini humo. Jionee picha za show hiyoMadee aka Rais wa Manzeshe akitumbuiza



Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee wakiimbia kwa hisia hit yao ‘Me and You’



Mshindi wa super diva mkoani Iringa ambaye ni mlemavu wa macho


Makomando wakipiga salute



Linah akijiachia jukwaani


Juma Nature aka Kibra


Backstage: Linah, Juma Nature, Vanessa Mdee na Adam Mchomvu





Backstage: Linah na Edo Boy
HIZI NDIO SALAMU ZA MWIGULU KWA WOTE WALIOHUJUMU FEDHA HIZI ZA UMMA

HIZI NDIO SALAMU ZA MWIGULU KWA WOTE WALIOHUJUMU FEDHA HIZI ZA UMMA

September 20, 2014


Waliosababishia Serikali hasara ya bn 40/- kukiona

Naibu Waziri wa Fedha, Mungulu Nchemba
Wizara ya Fedha imeziagiza taasisi zilizokabidhiwa jukumu la kuchunguza wakuu wa mashirika na taasisi za umma waliojihusisha katika kughushi malipo hewa ya wafanyakazi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 40 kila mwezi wafichuliwe.
Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mungulu Nchemba, akisema wakuu hao pamoja na waajiri wametumia mwanya wa wafanyakazi wao katika  ubadhirifu wa fedha kwa maslahi yao binafsi.
 
Kadhalika, wizara inawataka maafisa utumishi na waajiri kuhakiki upya taarifa wanazoweka katika mfumo ni sahihi ili watumishi wao wawekewe malipo yao katika akaunti kwa wakati mwafaka.
 
“Zoezi hili ni endelevu, hivyo tumebaini tatizo na tunatafuta njia ya kulimaliza na  hii tuliyowaagiza waajiri itakuwa njia ya kutokea, hivyo tutalinganisha taarifa zao na muda wa watumishi wao tuone tatizo lilikuwa wapi,” alisema.
 
Pia, alisema hakuna sababu ya wizara kuendelea kulipa malipo hewa wakati kuna kundi la wafanyakazi katika taasisi na mashirika hayo, ambao kazi yao ni kuhakiki mafaili na wanalipwa mishahara mikubwa huku wale wanaojituma wakiendelea kujaziwa  mishahara hewa.
 
Aliwaagiza waajiri na maafisa hao kufikisha orodha ya majina ya watumishi wakiambatanisha na taarifa sahihi ya mishahara tarehe za mwanzo za kila mwezi zifanyiwe kazi mapema ili kuwepo na uwajibikaji katika sehemu za kazi.
 
Alisema fedha za miradi katika taasisi hizo zitatolewa kulingana na mchanganuo wa malipo yao, “Hatuwezi kuendelea kutoa  malipo hewa kinyemela  tena, hivyo wataalamu wetu watashirikiana na wakuu hao wa maradi kuangalia kama unakidhi kutekelezewa,” alisema.
MASHAMBULIZI MENGINE YA JAMIE CARRAGHER KWA ARSENAL HAYA HAPA...

MASHAMBULIZI MENGINE YA JAMIE CARRAGHER KWA ARSENAL HAYA HAPA...

September 20, 2014


Arsenal were defeated 2-0 in Dortmund on Tuesday, but it could have been much more for the Germans
Arsenal walifungwa 2-0 na Dortmund siku ya jumanne, lakini bado wana imani kubwa ya kufanya vizuri

BADO ni mapema mwa msimu, lakini tayari kuna maswali ya kujiuliza kuhusu Arsenal. Swali kubwa ninalohisi ni hili hapa: Kipi kinabadilika?
Kwa kuwatazama dhidi ya Borrussia Dortmund jumanne usiku, isingewezekana kuhitimisha kwamba, Arsenal hawajifunzi.
Kwa muongo mmoja sasa, Arsenal wamekuwa wakishindwa kupambana na timu inayocheza mpira wa kasi na mpango wa kutumia nguvu. Kila mtu anajua jinsi ya kucheza nao.
Danny Welbeck has been brought in from Manchester United, but is yet to score after a host of chances
Danny Welbeck amesajiliwa kutoka Manchester United, lakini bado amekuwa na ugonjwa wa kukosa nafasi za magoli.

Dortmund wangeweza kufunga mabao kirahisi kama walivyofanya Liverpool (5-1 mwezi februari) na Cheslea (6-0 mwezi machi), lakini kitendo cha kutofungwa mechi 29 za ugenini katika michuano ya UEFA, kiukweli ni rekodi nzuri mno kwa Arsenal.
Ninapoitazama Arsenal kwasasa, ninachanganyikiwa. Wanacheza vilevile kila wanapokwenda- mabeki wao wa pembeni wanapanda juu na kutanuka- na hufungwa kwa mashambulizi ya kushitukiza.
Wao ni wageni! wangekuwa wanafanya hivyo wakiwa nyumbani. Kwanini hawajifunzi?
Nilipokuwa naichezea Liverpool, lengo la kwanza siku zote lilikuwa kutofungwa: Tulijilinda sana na kama nafasi inatokea basi tuliitumia haraka. Kama mashabiki wa nyumbani hawakupenda, maana yake ilikuwa nini?
Bado Arsenal wanaamini wanaweza kuifunga timu yoyote na popote pale wakicheza mpira wao. Ni vibaya sana. Timu pekee iliyoweza kushinda ugenini kwa miaka ya karibuni kwa staili hii ni Barcelona ya Pep Guardiola. Moja ya timu kubwa zaidi miaka ya karibuni, lakini alionekana kuja na mbinu nyingine za kutafuta matokeo.
Angalia mabingwa wa mwaka jana wa UEFA, Real Madrid, walifuzu fainali kwa kushambulia kwa kushitukiza dhidi ya Bayern Munich-na hii ilikuwa katika mchezo wa kwanza Bernabeu. Ilikuwa mbinu nzuri kwao.
Kufanya mambo tofauti ni jambo la msingi.
JOSE MOURINHO AIBUA CHOKOCHOKO CHELSEA IKISAFIRI KUIFUATA MAN CITY ETIHAD

JOSE MOURINHO AIBUA CHOKOCHOKO CHELSEA IKISAFIRI KUIFUATA MAN CITY ETIHAD

September 20, 2014


Jose Mourinho claims clubs who fail to comply with FFP should be thrown out of the Champions League
Jose Mourinho amedai kuwa klabu zinazoshindwa kufuata sheria ya matumizi ya fedha ziondolewa katika michuano ya ligi ya mabingwa 

JOSE Mourinho ameibwatukia Manchester City wakati huu Chelsea akijiandaa kusafiri kwenda Etihad, akidai kuwa UEFA lazima ichukue pointi na kuinyang`anya ubingwa timu inayoshindwa kufuata sheria ya matuzimi ya fedha (FFP).
Bosi huyo wa Chelsea alisema adhabu hiyo itakuwa ya haki zaidi kuliko ya sasa ya kutoza faini na kuizuia klabu kusajili  kama ilivyowakumba City.
"Kila mtu anajua kuwa kuna faini, na kama faini zipo, njia za kuzuia zinakuwepo," alisema Mourinho. "Lakini faini hizo ni za haki? sidhani. Kwa maoni yangu, kitu cha kwanza ni kuondoa pointi na kuondoa ubingwa"
James Milner and Martin Demichelis tackle Arjen Robben during Manchester City's defeat at Bayern Munich
James Milner na Martin Demichelis wakimkaba Arjen Robben wakati wa mechi ya UEFA ambapo Manchester City ilitandikwa bao 1-0 na Bayern Munich

"Kama una mtaji ambao unakufanya umalize tatizo la FFP; halafu unashinda makombe na kutozwa faini, utaendelea kufanya kitu hicho hicho".
Mourinho aliongeza kuwa: "Watamtoa mchezaji mmoja au wawili katika orodha ya UEFA. Halafu badala ya wachezaji 24 unakwenda na wachezaji 22. Lakini kama inaelezwa kuwa utaanza msimu ujao wa UEFA ukiwa umekatwa pointi sita au hutacheza michuanoo ijayo ya UEFA na utakwenda michuano ya Europa, itaonekana kuwa na nguvu'
UEFA waliziadhibu City, Paris Saint-German na Zenit St Petersburg kwa kuvunja sheria ya FFP mwaka huu.
City walitozwa faini ya paundi milioni 50 ingawa inaweza kupunguzwa kama wataifuata baadaye na kikosi chao kinachocheza UEFA mwaka huu kimepunguzwa mpaka wachezaji 21.

KIVUMBI CHA LIGI KUU TANZANIA BARA NI LEO....YANGA WATAFANYA NINI MORO?

September 20, 2014


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

PAZIA la ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 linafunguliwa leo kwa mechi sita kupigwa viwanja mbalimbali nchini.
Macho na masikio ya mashabiki wengi wa soka nchini yatanarajia kuwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ambapo Mtibwa Sugar watakuwa nyumbani kuikaribisha Yanga ya Dar es salaam.
Homa ya pambano hilo ni kubwa mjini humo na tayari majina ya Wabrazil wawili, Genilson Santos Santana ‘Jaja’ na Andrey Coutinho yamekuwa gumzo huku jezi zao zikiongoza kuuzwa.
Mechi nyingine leo hii ni baina ya mabingwa watetezi, Azam fc ambao watakuwa uwanja wa nyumbani wa Azam Complex kuchuana na Polisi Morogoro.
Stand United itakuwa uwanja wa nyumbani wa Kambarage mjini Shinyinga kuoneshana kazi na wageni wenzao, Ndanda fc kutoka mkoani Mtwara.
Katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga, wenyeji Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera.
Maafande wa Ruvu Shootings watasaka pointi tatu muhimu mbele ya Tanzania Prisons ‘Wajelajela’ katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani.
Mechi nyingine kali itapigwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ambapo wenyeji Mbeya City wanaikaribisha JKT Ruvu ya Pwani.

Ligi hiyo itaendelea kwa mechi moja kupigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa kuwakutanisha Simba sc dhidi ya Coastal Union.

PPF YAWANOA WAAJIRI KUHUSIANA NA HUDUMA ZAKE MPYA IKIWEMO PPF TAARIFA APP.

September 20, 2014
Prof. Betria Mapunda ambae amemwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es salaam akifungua semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa Waajiri kwa lengo la Kutoa elimu juu ya huduma zitolewazo na mfuko huo wa Pensheni wa PPF katika ukumbi wa Seaescape, Uliopo Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam.
Meneja wa Kanda ya Kinondoni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahara Kayugwa akitoa mada wakati wa semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Penhsheni wa PPF kwaa Waajiri wa Makampuni na mashirika mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Seaescape, Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam leo.
Mgeni Rasmi Prof Betria Mapunda akiwa katika picha ya Pamoja na Waajiri pamoja na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF leo katika Semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika Katika Ukumbi wa Seascape Hotel Mbezi Beach Jijini Dar.
Baadhi ya Waajiri kutoka Mashirika na makampuni mbalimbali wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wafanayakazi wa Mfuko Wa Pensheni wa PPF.
Majaliwa E Mkinga, Mchambuzi na Mtengenezaji wa Mifumo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akielezea jinsi PPF ilivyotengeneza mfumo wa kupata taarifa za wanachama kupitia simu aina za Smartphone na kuutaja mfumo huo kuwa ni PPF TAARIFA App ambayo mteja ataweza kuiweka katika simu yake ya mkononi.
Baadhi ya waajiri wakielekeza kuhusu jinsi ya kuweka mfumo wa PPF Taarifa katika simu zao za Smartphone leo katika semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Seascape hotel Mbezi beach Jijini Dar Es Salaam.
Meneja wa Kanda ya Kinondoni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahara Kayugwa akiwaelezea waajiri waliohudhuria semina iliyoandiliwa na mfuko wa pensheni wa PPF leo jinsi kanuni mpya inavyofanya kazi kwa wanachama ili kuweza kupata mafao yao kutoka mfuko wa pensheni wa PPF.
 
Mmoja wa waajiri akiuliza swali kwa Meneja wa Kanda ya Kinondoni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Zahara Kayugwa (hayupo pichani) wakati wa semina iliyoandaliwa na mfuko wa pensheni wa PPF iliyokuwa na lengo la kuwaelimisha waajiri kuhusiana na huduma mbalimbali za PPF ikiwemo huduma mpya ya PPF Taarifa App.Picha zote Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

KINANA , NAPE WAITEKA KIBAHA

September 20, 2014

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwasalimia wakazi wa Kibaha mjini wakati wakiwasili kwenye uwanja wa mkutano .
 Kikundi cha ngoma cha Kisamamwe kikitumbuiza ngoma ya Afrika kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara ambapo Katibu Mkuu wa CCM alihutubia wananchi wa Kibaha mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibaha mjini ambapo aliwaambia wapinzani wamekosa hoja ya msingi kiasi cha kuamua kufanya maandamano ya kuleta vurugu nchini.
 Sehemu ya Umati wa watu wakisikiliza mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Wana CCM wakiwa kwenye mkutano
 Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Francis Koka akihutubia wakazi wake na kuwaambia kuwa pamoja na jitihada zote anazofanya maji bado ni donda sugu ila ufumbuzi upo njiani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibaha mjini wakati wa mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia viongozi wa halmashauri hawana budi kukaa na wafanya biashara ndogo ndogo kujadili kodi kabla ya kuwapangia kuona kama wana uwezo wa kulipa ama hapana hii itasaidia kupunguza lawama na mikingamo baina ya wafanya biashara na halmashauri.