WATUMISHI OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA WAPIGWA MSASA

November 30, 2016
Mshauri Mwelekezi wa Masuala ya Jinsia kutoka “Women Fund” Profesa Ruth Meena akitoa mada.

 Mshauri Mwelekezi wa Masuala ya Jinsia kutoka “Women Fund” Profesa Ruth Meena (kulia), akiwasilisha mada juu ya jinsi ya kuingiza masuala ya jinsia katika mpango kazi wa taasisi wakati wa kikao kazi cha watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilicho fanyika leo katika Ukumbi wa ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
 Mafunzo yakitolewa.

MUUZA MITUMBA SOKO LA KARUME JIJINI DAR ES SALAAM AFUTIWA LESENI YA BIASHARA KWA KUMDHALILISHA MTEJA WAKE WA KIKE

November 30, 2016

 Diwani wa kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (katikati), akihutubia wakati akizindua kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Shirika la Eguality for Growth (EfG), Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele na kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mchikichini, Charles Kapongo.
TPDC YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOENEZWA NA KAMPUNI YA DANGOTE.

TPDC YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOENEZWA NA KAMPUNI YA DANGOTE.

November 30, 2016
dabg
 Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli  Nchini(TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba akizungumza na waandishi wa habari kukanushaTaarifa zinazoenezwa na kampuni ya Dangote pamoja na washirika wake kupitia mitandao ya Kijamii na vyombo vya Habari kuhusu kushindwa kukiuzia gesi asilia kwa bei rahisi kiwanda hicho.Kulia kwake ni Kaimu Kamishana wa Madini Mhandisi John Shija,Kaimu Meneja manunuzi TPDC Bw.Donal Aponde na Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi.Maria Msellemu.
……………………………..
Na Daudi Manongi-MAELEZO
Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba amekanusha taarifa zinazoenezwa na kampuni ya Dangote kwamba TPDC imeshindwa kukiuzia gesi asilia kwa bei rahisi kiwanda hicho cha Saruji na hivyo kusababisha kusimamisha uzalishaji wa kiwanda hicho.
Mhandisi Musomba ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari akitolea ufafanuzi juu ya suala hilo.
“TPDC imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba kampuni ya Dangote inapata nishati hiyo muhimu kwa ajili ya kuzalisha saruji ikiwemo kufanyika kwa vikao mbalimbali pamoja na makubaliano yaliyofanyika kwa Dangote kuridhia nia yao ya kutumia gesi asilia ili kuzalisha umeme kwa ajili ya kiwanda hicho,”Alisema Mhandisi Musomba.
Aidha amesema TPDC inafuata kanuni na utaratibu wa kupanga bei ya gesi asilia ambapo hupanga bei ya gesi asilia ambapo hupanga kulingana na aina ya wateja waliopo katika makundi mbalimbali ingawa bei elekezi ambayo inapendekezwa na TPDC lazima iridhiwe na ipitishwe na EWURA ndipo ianze kutumika.
Vile vile ameeleza kuwa Kiwanda cha Dangote kimeomba kupewa gesi asilia kwa bei ambayo ni ndogo sana ambacho ni sawa na kiasi kinachonunulia gesi ghafi kutoka kisimani, na hivyo haiwezi kuuza  gesi asilia kwa bei hiyo kwa sababu kuna gharama zinazoongezeka katika kuisafisha na kuisafirisha gesi hiyo.
Mhandisi Musomba anasema kuwa wanategemea ifikapo mwezi Januari 2017 miundombinu ya gesi asilia itakua imeshaunganishwa na mitambo ya kufua umeme utakaotumiwa na kiwanda hicho.
Hata hivyo amesema kuwa TPDC inawajali wawekezaji wake akiwemo Dangote ili wawekeze katika kukuza uchumi wa nchi.
MALINZI AOMBOLEZA VIFO VYA WACHEZAJI WA CHAPECOENSE YA BRAZIL.

MALINZI AOMBOLEZA VIFO VYA WACHEZAJI WA CHAPECOENSE YA BRAZIL.

November 30, 2016
malinziiiiiiiii
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Mpira Brazil (CBF), kutokana na vifo vya wachezaji wa timu ya soka Chapecoense Real ya Brazil.
Rais wa TFF Malinzi, katika salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Brazil (CBF), Lucca Victorelli  amesema ajali hiyo iliyoua watu wengi ni tukio la kusikitisha kwenye familia ya soka duniani na limetokea katika kipindi kigumu.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAREHEMU XAVERY MIZENGO PINDA

November 30, 2016


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kushiriki katika kuaga mwili wa Baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu Marehemu, Xavery Mizengo Pinda kwenye kijiji cha Zuzu, Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete wakiwa nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwenye kijiji cha Zuzu, Manispaa ya Dodoma ambako walishiriki katika kuaga mwili wa baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, marehemu Xavery Mizengo Pinda Novemba 30, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.


Baadhi ya waombolezaji walioshiriki katika kuaga mwili wa marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni Baba mzazi wa Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda akipewa pole na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa wakati awa kuaga mwili wa Baba yake mzazi wa Waziri Mkuu mstaafu, marehemu, Xavery Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akizungumza wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa Marehemu Xavery Mizengo Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakati aliposhiriki katika kuaga mwili wa baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee, Xavery Mizengo Pinda kijijini Zuzu kwenye Manispaa ya Dodoma Novemba 30, 2016.

KIGOMA MJINI WAMPONGEZA LUKUVI KUTATUA MIGOGORO YAO YA ARDHI

November 30, 2016

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi anaendelea na ziara ya siku tatu katika mkoa wa Kigoma ambapo amefungua rasmi Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoa wa Kigoma pamoja na kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa Kigoma. 

Wananchi hao wamempongeza Mhe. Waziri kwa hatua anazozichukua katika kumaliza migogoro yao ya ardhi na kuwajengea Baraza la Ardhi na Nyumba ambalo jipya na lililo na viwango kushinda mengine yote hapa nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akifungua Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma, Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe.Brigedia Jenerali Emanuel Maganga.
Jengo jipya la Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma.
Samani mpya za Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akiongea na wananchi wa Kigoma Mjini na kutatua migogoro yao ya ardhi.
Wananchi wa Kigoma Mjini wakiwasilisha malalamiko yao ya migogoro ya ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi ili yaweze kutatuliwa.
wananchi wa Kigoma mjini wakimsikiliza Waziri wa Ardhi.

Magese apongeza Serikali kwa kumpa ushirikiano, mrembo wake apata nafasi ya tano Afrika

November 30, 2016
Mshiriki wa shindano la Miss Afrika, Julitha Kabete, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili akitokea nchini Nigeria katika shindano la Miss Afrika, Kabete ameshika nafasi ya tano katika shindano hilo.
Mshindi wa nafasi ya tano katika shindano la Miss Afrika Julitha Kabete, akiwa na Mama yake mzazi mara baada ya kumpokea kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akitokea nchini Nigeria katika shindano la Miss Afrika ambalo fainali zake zilifanyika Novemba 26 mwaka huu.

Mwandushi Wetu
MKURUGENZI wa Kampuni ya Millen Magese Group (MMG), Millen Magese  ameishukuru Serikali kupitia kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye, huku akifurahishwa na uwakilishi mzuri wa Miss Tanzania Julitha Kabete (19), aliyeingia kwenye tano bora katika mashindano ya Afrika.


Kabete  alipeperusha vema Bendera ya Tanzania kwa kuingia hatua ya tano bora ya mashindano yaliyofanyika Jumamosi nchini Nigeria na  kuitoa Tanzania kimasomaso.

Akizungumza na waandishi wa habari, Millen alisema ni faraja kubwa kwake na nchi yake kwa  Julitha kuingia hatua ya tano bora, lakini sababu kubwa ikiwa ni ushirikiano iliyoupata.


"Napenda kuchukua fursa hii kwa heshima nyingi na taadhima kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa ushirikiano wa hali ya juu, kupitia Waziri Nape Nnauye kwa ushirikiano na mwongozo wa kipekee, wazazi na familia nzima ya Julitha kwa malezi yenu kwa binti , Kamati nzima ya Miss Tanzania chini ya Mkurugenzi Hashim Lundenga (Tunashukuru sana), kwenu wanahabari hatuna maneno sahihi ya shukrani, asanteni sana," alisema Magese.


Naye mshindi huyo wa tano wa Miss Afrika, Julitha Kabete, alisema anashukuru kwa ushirikiano aliupata, lakini pia nchi yake kupata thamani ya kipekee katika shindano hilo kupata nafasi tano za juu.

Kabete alisema kuwa licha kutopata nafasi ya kwanza, lakini ameweza kuiwakilisha vema nchi katika shindano hilo, kwa sababu ushindani ulikuwa mkali sana.

"Kwangu ni faraja kubwa kwa kuwa balozi mzuri wa Tanzania na kuweza kuwashinda wenzangu wengi ikiwemo na mwenyeji wetu ambaye hakuingia katika hatua ya tano kama ambayo mimi nimeipata nina furaha kubwa sana,"alisema Kabete.


Alisema kuna mkataba mpya ambao utaingiwa kati ya Tanzania na waandaaji wa shindano hilo la Miss Africa katika kutoa ushirikiano wa ushiriki wa shindano hilo.

Katika shindano hilo lililofanyika Novemba 26, mwaka huu nchini Nigeria, taji la shindano hilo lilienda kwa mnyange Neurite Mendes (23) wa Angola, aliyenyakua kitita cha dola za Marekani 25,000 sawa na sh.milioni 52 ya Kitanzania na  gari jipya (brand new 2016 Ford Escape), safari maalum ya mafunzo nchini Uingereza na Ubalozi wa Mazingira– Afrika.

Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Refilwe Mthimunye wa Afrika Kusini alipata dola za Kimarekani 15, 000 ni sawa na zaidi ya sh. milioni 32, na Jencey Anwifoje kutoka nchini Cameroon, akiibuka wa tatu na kupata dola za kimarekani 10,000 sawa na zaidi ya  sh.milioni 20.



Shindano la Miss Afrika 2016 lilichagizwa kwa heshima ya mji wa Calabar na jimbo la Cross River, chini ya Gavana wa Cross River Profesa Ben Ayade.

Kampuni tanzu ya Millen Magese (MMG) imeanzishwa kwalengo la kuibua, kuinua, kutambua na kukuza vipaji katika Bara la Afrika na ngazi ya Kimataifa.

MMG imeweza kufika nchi mbalimbali barani Afrika na mwaka 2012 iliweza kuendesha shindano la kwanza ya aina yake ambapo wanamitindo wawili kutoka Tanzania walipata nafasi ya kupata mikataba nchini Afrika Kusini.

Wanamitindo kutoka mashindano hayo wameweza kuendelea kufanya vizuri maonesho mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Mwaka huo huo wa 2012 MMG kupitia mradi wa TIFEX iliwezesha wabunifu kutoka nchini kupata uzoefu na uelewa wa wiki za mitindo duniani.

DC STAKI AZINDUA HUDUMA YA UPANDAJI MITI MAENEO OEVU KWENYE VYANZO VYA MAJI

November 30, 2016
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki amezindua shughuli ya kupanda miti maeneo oevu/ kwenye vyanzo vya Maji katika Kata ya Bwambo. Zoezi hilo limefanyika kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la Floresta.





MOBISOL NA ZUKU TV WAZINDUA HUDUMA ZA TELEVISHENI YA SATELITE YA NISHATI YA JUA

November 30, 2016

 Meneja Mkuu wa Zuku Tv Tanzania  , Bw.Omari Zuberi akiongea na waandishi wa habari juu ya huduma mpya ya TV ya nishati ya jua ambayo ina channel za Zuku Tv
 katikati ni Afisa masoko wa Mobisol Sjors Martens akiwa na wafanyakazi wa mobiso l katika uzinduzi huo hii leo jijini Arusha
 mmoja wa mmteja wa mobisol ambaye akutaka kutaja jina lake akiongea wakati wa uzinduzia ambapo aliisifia kampuni ya mobisol nakusema ni mtetezi wa wananchi wanaoishi vijijini ambapo umeme haujafika
 Meneja wa zuku Tanzania wa kwanza kushoto akibadilishana mawazo na wa kwanza kulia ni afisa usiano wa Zuku  dada Yasta pamoja na  mwakilishi wa zuku  Jack Karanja katika uzinduzi
 wafanyakazi wa zuku wakifurahia mara baada ya uzinduzi



            
 Na Woinde Shizza,Arusha

 KAMPUNI inayoongoza kwa utowaji wa huduma za nishati ya jua majumbani ,Mobisol na Kampuni ya Zuku Tv inayotoa burudani za satellite wameungana  pamoja kwa ajili kuwanufaisha watanzania wasiounganishwa na nishati ya umeme. 

Kwa pamoja kampuni hizi zimezindua kwa mara ya kwanza TV ya nishati ya jua ambayo ina channel za Zuku Tv  huduma inayowalenga wale ambao hawajafikiwa na umeme wa gridi ya Taifa.



Huduma hii huunganisha mfumo  wa nishati jua, televisheni ya hadi inchi 32 ya nishati jua, ungo wa satellite, na huduma ya ya kifurushi cha Zuku Smart Plus chenye chanelli 47 and 18 za redio. Mobisol wanalenga  kutoa huduma hii kwa watanzania ambao hawajafikiwa na huduma ya nishati ya umeme, kwa  kutoa nashati safi na ya kuaminika kwa bei nafuu popote ulipo katika mfumo moja mkamilifu.



Mobisol inatoa vifurushi mbalimbali vya nishati ya jua ya majumbani, vilivyo na uwezo wa kutoa nguvu ya umeme hadi 200W,  unaotosha matumizi ya kaya nzima. Kila kifurushi kintaota paneli ya PV, betri ya nishati ya jua, taa nne za mwanga mkali,TV kubwa ya kioo cha  bapa, tochi, chagi ya simu na redio ambayo unaweza kuichagi. Vifaa hivi vinapatikana na waranti, huduma ya kufungiwa bure, huduma ya wateja na huduma ya marekebisho kwa miaka 3.  Pia, Kwa kuongezaTsh 8,999 kwamwezikwakifurushi, watejawatawezakupatahudumazaZuku TV kwamudawamasaasabakwasiku .



Akizungumza katika uzinduzi  huo   Afisa masoko wa Mobisol Sjors Martens alisema kuwa wao wanania ya kuleta maisha mazuri kwa wateja wao nchini Tanzania. 
Alisema Huduma yao  ya kifurushi cha televisheni ya satellite kitawezesha wateja  kufurahia habari , michezo, burudani na maudhui ya elimu wakati wowote hata wakiwa wanaishi  mjini au vijijini.



Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Zuku Tv Tanzania  , Bw.Omari Zuberi alisema ubunifu wa huduma hii itatuwezesha kufikia zaidi ya watanzania million 8 ambao hawajawa na nishati ya umeme wa grid ya Taifa na kutuwezesha kuchangia kwa asilimia kubwa ongezeko la televesheni nchini. 

  “Hii ni fursa ya kipekee na ya kuleta hamasa  kwa wateja wa Mobisol kuwa na uwanja mpana zaidi  wa kuchagua na kufurahia zaidi ya chaneli 40 za Zuku TV inayotambulika kama huduma bora ya bei nafuu inayotoa burudani kwa  familia kwa kuhamasisha  maudhui ya kinyumbani zaidi,” alisema Zuberi.



Aliongeza kuwa Ingawa asilimia 70 ya watanzania hawajafikiwa na huduma ya nishati ya umeme na asilimia kubwa ya watanzania bado hawana Televisheni, Mobisol na Zuku wametumia fursa hii na kuungana pamoja kwa ajili ya kutoa huduma ya umeme wa jua na kutoa burudani ya TV Satellite yenye ubora wa kimataifa



 Aidha alisema kuwa Huduma hii ya PayTV  iliozinduliwa mkoani hapa itapatikana katika mikoa ambayo Mobisol inatoa huduma ambapo ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Singida, Tabora, Dodoma, Mwanza, Shinyanga, Geita, Mara, Kagera, Simiyu, Mbeya, Songwe na Njombe - na baadaye kote nchini mwaka ujao



Alibainisha kuwa Kupitia Zuku TV, watanzania wanaweza kufurahia idadi ya channel  za kusisimua ikiwa ni pamoja na channel  za nyumbani  FTA, channel  za kimataifa na channel za  Zuku asili; Zuku Sports, hivi karibuni ilizindua tena  Zuku Swahili, Zuku Kids, Zuku Life Glam na Zuku Nolly.



Alisema kuwa Bei ya kifurishi cha Zuku smart pack kitakuwa kikiongezwa kwa awamu katika mfumo nishati ya  jua  ya Mobisol, ambayo wateja hulipa kupitia  simu  kwa kipindi cha miaka mitatu.

Alifafanua kuwa  Baada ya miaka mitatu, wateja watamili hivyo vifaa  na kupata ofa ya kuvutia kwa kulipa tena huduma hiyo mpya

MD KAYOMBO AFANIKISHA MRADI SHULE YA MATOSA

November 30, 2016
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amepongezwa na walimu pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Matosa iliyopo Kata ya Goba , Manispaa ya Ubungo kwa kufanikisha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa mradi wa SEDP II.

Mradi huo unaohusisha ujenzi wa vyumba viwili vya darasa, nyumba za walimu, kisima cha maji, tanki la kuhifadhia maji pamoja na vyoo upo katika hatua nzuri ya kukamailika kutokana na juhudi pamoja na utendaji kazi uliotukuka wa Mkurugenzi Kayombo akishirikiana na watumishi wa Manispaa hiyo.

Akizungumza na mtandao wetu mwalimu Mkuu wa shule hiyo alisema amefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo za kuleta maendeleo kwa wananchi na kwenda sambamba na kauli mbiu ya Rais John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

"Napenda kutoa shukrani Kwa Serikali kwa kuuleta mradi wa SEDP II katika shule yetu, pia napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo kwa juhudi zake anazozifanya mpaka mradi umefika hatua hii, kwa kweli ametusaidia sana, mungu ambariki", alisema Mwalimu mkuu.

Wakati huo huo wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wamempongeza Mkurugenzi Kayombo kwa kazi nzuri aliyofanya mpaka kuweza kufanikisha kupatikana kwa maji pamoja na madarasa, vyoo, tanki la maji na nyumba za walimu.

MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA WAINGIA MTAANI KUKUSANYA MAPATO

November 30, 2016
Meya wa jiji la Mbeya David Mwasilindi


 Na JamiiMojablog,Mbeya
Halmashauri ya jiji la Mbeya imebuni njia mpya ya ukusanyaji wa mapato  ili kufikia malengo yake ya ukusanyaji wa kiasi cha shilingi bilioni  11 katika  mwaka wa fedha wa  2016/17 .

Katika kufanikisha mpango huo halmashauri imewashirikisha madiwani na wataalmu wake katika kufanya kazi ya ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vyake vya ndani .


Moja ya njia hiyo halmshauri imeanza kuwatumia Madiwani pamoja na wenyeviti wa mitaa katika ukusanyaji wa fedha kupitia vyanzo vyake vya ndani vya mapato .

Akielezea mkakati huo  Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Ndugu David Mwashilindi amesema katika kuhakikisha halmshauri inafikia lengo lake la ukusanyaji wa mapato imeamua kuongeza nguvu kazi kwa kuwaingiza madiwani na wenyeviti ambao wapo karibu na wananchi.


Kazi kubwa  wanayo ifanya madiwani na wenyeviti kwa kushirikiana na wataalam ni kuhakikisha wanavitambua vyanzo vyote vya mapato vinavyostahili kuingia katika mapato ya halmashauri  ikiwa na kubaini mianya iliyokuwa ikitumiwa na wahusika kukwepa kulipa kodi,”amesema Mwasilindi.


Amesema kuziendesha halimamshauri hizi inategemea sana mapato ya ndani hivyo lazima kuweka jitahada za makusudi katika kufikia malengo husika .


Amesema katika kipindi cha nyuma halmasahuri hiyo hali ilikuwa katika hali mbaya kwani kwa mwezi walikuwa wanakusanya kiasi cha shilingi milioni 120 hadi 200 lakini mara baada ya kuanza kwa jitihada hizo imesaidia kupandisha mapato ambapo kwa sasa imefikia kiasi cha shilingi milioni 700 kwa mwezi.


Amesema zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo sanjali na kukusanya mapato pia kuna sauala la utoaji wa elimu kwa wananchi ili kuelewa namna ya kulipa  tozo zilizo wekwa kisheria.


Amesema zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku tano na mara baada ya hapo kutafanyika kwa tahimini ya pamoja ili kubaini changamoto zilizopo katika zoezi.